Anguko kuu la Kikwete na CCM, dalili zimeanza

Anguko kuu la Kikwete na CCM, dalili zimeanza

Status
Not open for further replies.
Nao wababaishaji!!! Kama wana list si wangeitoa tu ili kama wanafungiwa tuchademe tena na polisi. Kwa nini ku alert? Au ni mbinu ya kutaka mhariri avutwe pembeni alambishwe halafu hatutasikia tena kitu!!!!!! Mbwembwe za magazeti nazo zinatukinaisha. We need names now sio kesho!!!! FYA!!!
 
wakuu hili gazeti sijawahi kulisoma. Ni huru au la ccm. Yawezekana huyu jamaa analinadi

nimeona tangazo lake itv nikaiandika kama nilivyoisikia, cha msingi likitoka tulisome maana heading yake ni kuwa watataja majina
 
Kukosekana kwa utashi wa dhati wa kusimamia maslahi ya nchi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiko kulikosababisha Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) likashindwa kesi na kuamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi Migogoro ya Kibiashara (ICC) iilipe kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans Sh. bilioni 94.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) kilichopo jijini Mwanza, Profesa Mwesiga Baregu.
Baregu alitoa kauli hiyo alipoombwa kutoa maoni yake kuhusiana uamuzi wa serikali kukubali Tanesco ilipe fedha hizo, ambao umeibua mjadala mkubwa nchini.
“Ninachoweza kusema ni kwamba tumeshindwa kesi hii kutokana na ukosefu wa utashi wa dhati aliouonyesha Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kitendo cha kusema hukumu iko sawa na hakuna kinachoweza kufanyika dhidi ya hukumu hiyo kinaonyesha kuwa ofisi hiyo imeipokea hukumu kwa mikono miwili,” alisema Profesa Baregu ambaye ni msomi aliyebobea katika masuala ya uhusiano wa kimataifa.
Profesa Baregu alifafanua kwamba ofisi hiyo ilikuwa na mambo mengi ya kufanya ili kushinda kesi hiyo, tangu kwenye usikilizaji wa kesi yenyewe na hata baada ya hukumu kutolewa na ICC.
Alisema ofisi ya Mwanasheria Mkuu ndiyo inayowajibika kutoa utetezi wa nchi pale serikali inaposhitaki au kushitakiwa.
“Lakini historia inaonyesha kwamba kesi nyingi ambazo nchi yetu ilishitakiwa kwenye mahakama hiyo ilishindwa. Unaposhindwa kesi mara nyingi maana yake utakuwa na haki ya kuwatilia mashaka watetezi wenu,” alisema Profesa Baregu.
Aidha, Profesa Baregu alieleza kusikitishwa na kitendo cha Mwanasheria Mkuu cha kutochukua juhudi za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, alisema kitendo hicho ni dosari isiyokubalika.
Alipotakiwa kueleza ni athari zipi zinaweza kuipata nchi ikiwa serikali itakataa kutekeleza hukumu ya ICC kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Profesa Baregu alifafanua kuwa hiyo inategemeana kama nchi itaweza kuhimili maamuzi yatakayofanywa na vyombo vya kimataifa.
“Mahakama hii ya Kimataifa ya Usuluhishi inatambulika na kufadhiliwa na mashirika makubwa ya fedha duniani kama Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia. Hivyo kama tutakataa bila ya kuwa na sababu za msingi, ni lazima wakubwa hawa watatuadhibu,” alisema.
Profesa Baregu alifafanua kwamba adhabu zinazoweza kutolewa ni pamoja na kunyimwa misaada na mikopo kutoka kwenye vyombo hivyo ambavyo ndivyo Tanzania inavitegemea kwa maendeleo ya wananchi wake.
Alihitimisha kwa kusema kuwa njia pekee anayoitegemea kuokoa fedha ambazo serikali inatakiwa kulipa ni kwenye kesi iliyofunguliwa wiki hii na mashirika 17 ya wanaharakati katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Biashara kupinga hukumu ya ICC isisajiliwe.
“Pengine pale ndipo mambo mengi yanaweza kufahamika ikiwa ni pamoja na mkataba tulioingia na kampuni hiyo (Dowans) unavyoeleza, majina ya wanaotudai na mambo mengi ya kisheria yatajulikana huko,” alisema Profesa Baregu.
Juzi Mahakama hiyo iliipanga kesi hiyo namba 14 ya mwala 2011 kusikilizwa na Jaji Robert Makaramba.
Katika kesi hiyo, wanaharakati wa mashirika hayo wanaitaka Mahakama Kuu ikatae kusajili hukumu ya ICC ili kuzuia malipo hayo yasifanyike.
Kadhalika, mashirika hayo yameitaka serikali kuonyesha hadharani picha za wamiliki wa kampuni za Dowans kwa kuwa yanaamini wamiliki waliotajwa ni majina hewa na hayapo na ni wajanja wachache wanaotaka kuchota fedha za walipa kodi na kuzigawana.
CHANZO: NIPASHE
 
SUALA la malipo ya fidia kwa Kampuni ya Dowans, limeingia sura mpya baada ya wanaharakati na wanasheria kuwataka wananchi wawashinikize wabunge wao kwenda kupinga suala hilo bungeni.

Mbali na wito huo, wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuvunja ukimya na kuzungumzia suala hilo.

Wadau hao walitoa wito huo juzi
katika kipindi cha ‘Kipima Joto’ kilichorushwa hewani na Kituo cha Independent Televisheni (ITV) jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Shirika la linalojishughulisha na Utawala Bora na Haki za Binadamu la (Afdp), Renatus Mkinga alisema bunge sasa linatakiwa kuingilia kati na kupinga malipo hayo.

“Wananchi wawashinikize wabunge kwenda bungeni kupinga uamuzi uliofikiwa na serikali wa kuilipa Dowans,’’ alisema Mkinga.

Kauli ya Mkinga iliungwa mkono na Wakili wa Kujitegemea, Harold Sungusia aliyeitaka serikali pamoja na mambo mengine, kuacha usiri katika mikataba mbalimbali.

Sungusia aliwataka wananchi kuunga mkono uamuzi wa kituo cha LHRC na wanaharakati wa haki za kijinsia wa kufungua kesi mahakamani kupinga malipo hayo kwa kuwa sio halali.

“Njia nyingine ambayo wananchi wanatakiwa kufanya ni kuwataka wabunge wao, kupitia Bunge kupinga uamuzi uliofikiwa na serikali,’’ alisema Sungusia.

Mwanaharakati mwingine, Deus Kibamba alisema, nchi inaingizwa katika matatizo na kikundi cha watu wachache ambao hujibadilisha majina ya umiliki.

“Nchi inayumbishwa na kikundi cha watu wachache, waroho wa madaraka, wabinafsi, wasiojali maslahi ya taifa na ambao wanajiita ni Watanzania,’’ alisema Kibamba.

Kibamba ambaye ni mwanasheria alimshauri Rais Kikwete kuzungumzia suala hilo na si kukaa kimya kama anavyofanya kwa kuwa Watanzania wana haki ya kujua sababu na umuhimu wa malipo hayo.

“Sakata hili la Dowans, limezungumzwa na viongozi wengi akiwemo Waziri mwenye dhamana wa wizara husika na wengineo lakini, cha ajabu Rais Kikwete amekaa kimya hadi leo na wananchi wanahoji ni kwa nini asitoe uamuzi wa kampuni hii feki ya Dowans isilipwe fedha?’’ alihoji Kibamba.

Kwa mujibu wa Kibamba, Rais Kikwete asiridhike na ujanja unaotaka kufanyika, badala yake ahoji na kutilia mkazo fedha zisilipwe kwanza mpaka tujiridhishe kuwa wanasheria wetu wameshindwa kulitetea suala hilo.

Mwakilishi kutoka Agenda Participartion 2000, Michael Dalali, aliitaka serikali kutoharakisha kuilipa Dowans na badala yake ihakikishe suala hilo linajadiliwa na Bunge.

“Kabla ya yote, Bunge lipewe nafasi ya kujadili sakata hili la Dowans, kinyume na hapo ni kutaka kuwanyima haki wabunge na wananchi kwa ujumla,’’ alisema Dalali.

Dalali alikwenda mbali na kusema utashi wa kisiasa umesababisha wasomi na wananchi wa kada mbalimbali kutoshirikishwa katika maamuzi ya nchi na kwamba mambo yakiharibika, wananchi hubebeshwa mzigo.

Hoja za wasomi na wanaharakati hao kuhusu sakata la malipo kwa Kampuni ya Dowans, zimekuja wakati ambao Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na wanaharakati wa haki za kijinsia tayari wamewasilisha pingamizi Mahakama Kuu kuzuia malipo hayo.

Serikali imetakiwa kuilipa kampuni ya Dowans baada ya hukumu ya Mahakama ya Usuluhishi ya Biashara ya Kimataifa (ICC), kuitia hatiani Tanesco, kwamba ilikiuka mkataba baina yake na kampuni hiyo iliyokuwa ikizalisha umeme wa dharura.

Suala hili la Dowans limezua mjadala mzito hadi kufikia mahali pa kuligawa baraza la mawaziri.

Tayari mawaziri wawili wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harisson Mwakyembe kwa nyakati tofauti wamepinga Dowans kulipwa fedha hizo.

Hata hivyo, kauli hiyo inapigana na kauli ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema wanaotaka Dowans ilipwe.

Lakini Alhamisi iliyopita, LHRC kwa kushirikiana na wanaharakati wa haki za kijinsia nchini, waliwasilisha pingamizi Mahakama Kuu kupinga hukumu na malipo hayo ya Sh97 bilioni.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Francis Kiwanga alieleza kuwa kituo hicho kimeamua kupinga malipo hayo kutokana na mikataba ya awali ya kampuni ya Dowans, kupatikana kwa rushwa na hivyo kukiuka maslahi ya umma.

“Kituo kinafungua shauri Mahakama Kuu kupinga uhalali wa tuzo iliyotolewa kwa Dowans isisajiliwe na kuwa tuzo ya kimataifa kwa sababu mikataba ya awali ilipatikana kwa rushwa na kukiuka maslahi ya umma,” alisema Kiwanga.

Wakili wa Kujitegemea na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Dk Sengondo Mvungi ndiye wakili aliyeteuliwa kusimamia shauri hilo.
 
sasa wabunge wakisema lipigiwe kura ccm wengi watasema deni lilipwe
 
Kuna mambo matatu ambayo hayajaelezwa vizuri katika hili sakata la Dowans; Kwanza,mkataba ulioridhishwa kwa Dowans kutoka kwa Richmond ulikuwa uishe muda wake mwaka 2007, hiki kipindi cha mwaka mmoja zaidi kiliongezwa kinyemela baadaye; kwa maoni yangu ya kubadirisha hicho kipengere cha uhai wa mkataba, kinaondoa dhana ya Dowans kuridhishwa mkataba wa Richmond. Jambo la pili, linahusu "timing" ya uvunjaji wa mkataba husika; uhai wa mkataba husika ulikuwa unafikia hatma yake mwisho wa mwaka 2008. Hii ina maana, wakati unavunjwa ulikuwa umebakiza miezi mitatu tu ya uhai wake. Sasa tujiulize, kulikuwepo na uharaka gani wa kuvunja mkataba ambao ulikuwa karibu kufikia hatma yake. Tatu, inasemekana wakati mkataba unavunjwa TANESCO haikuwa na madai yeyote kwa kampuni hiyo, katika hali hiyo kwanini ilizuia mitambo yake. Kama ni suala la kodi kwanini lisishughulikiwe na idara husika. Kwa kujumulisha pamoja mambo hayo yote na mengine mengi ambayo yamekuwa yakitajwa ni dhairi kulisukwa njama za kuvunja mkataba wa Dowans kwa lengo la kuinufaisha visivyo halali kampuni hiyo.
 
sikiliza radio one deo kibamba na dr lwaitama wanajadili kutofautiana kwa serikali ktk katiba na dowmans. wanasema ni moja ya serikali dhaifu na ya kihuni
 
Walianzia kukinzana kwa kauli ya Katiba mpya.. Sasa ndio inajadiliwa Dowans..
 
Mchango wa vyombo vya habari kwa kuwaelimisha watanzania kuhusu kinachoendelea katika nchi yao ni mkubwa sana.Mwamko wa watanzania kujua jinsi nchi inavyoendeshwa uko juu sana kiasi cha hata wazee kujua chanzo cha matatizo ya watanzania.

Pamoja na baadhi watu kujitokeza kuitetea Dowans lakini wananchi huko Hai wamekataa Dowans isilipwe na kuamua kumtuma mbunge wao Bw.Freeman Mbowe akauwashe moto bungeni ili Dowans isilipwe na umeme upatikane.Ngeleja awa bubu kuongelea Dowans kwa kuwa suala lipo mahakamani na Sitta naye amekosa uwajibikaji wa pamoja kwa kuendelea kuwa mwiba mchungu kwa Dowans...Swali la kujiuliza je Dowans italipwa?


Source : Tanzania Daima : Dowans yatua CHADEMA
 
Nchi yeyote yenye wananchi makini na uongozi makini haiwezi lipa pesa kama za dowans. sana sana kitu ambacho kingekuwa kinaongelewa hapa ni kuwajibishwa kwa viongozi wote waliohusika na hii mikataba ya kijinga kama ya Dowans.
 
My advice is for CDM to just sit and watch as CCM is already doing a very good job of discrediting themselves on this issue.
 
Dowans yatua CHADEMA
• Wananchi wamtuma Mbowe akawashe moto bungeni

na Waandishi wetu


amka2.gif
WIMBI la wananchi kutokubaliana na uamuzi wa serikali kuilipa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans (T) LTD limezidi kushika kasi baada ya wananchi wa Jimbo la Hai kumwagiza Mbunge wao, Freeman Mbowe, aende bungeni kuhakikisha fedha hizo hazilipwi.
Msimamo huo ulitangazwa jana kwenye Kijiji cha Nronga wakati mbunge huyo ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alipokwenda kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge wao pamoja na kuchukua mawazo yao kwa ajili ya kuwasilisha bungeni.
Akiongea kwenye mkutano huo, Rowland Lema (77), alisema kwa sasa taifa linakabiliwa na tatizo kubwa la uhaba wa huduma ya nishati ya umeme, ambayo licha ya kuwa ghali, lakini haipatikani kwa uhakika na kwenye maeneo mengine hupatikana kwa mgawo.
Mzee huyo alisema jambo la kusikitisha ni kuona serikali inataka kutumia kiasi kikubwa cha fedha za wananchi kwa kampuni hiyo ambayo ilipewa jukumu la kuzalisha umeme na kushindwa.
“Kero ambayo tunataka uende ukaizungumzie bungeni na uisimamie kisawasawa ni hili la kupanda kwa gharama za umeme na kuna hiki kitu… sijui mtu anaitwa Dowans anataka serikali imlipe bilioni 96 …fedha hizi ni nyingi na Watanzania tuna hali ngumu. Tunataka uhakikishe fedha hizi halipwi, labda kutokana na uzee wangu huku kijijini sielewi lakini sioni sababu ya serikali kulipa fedha hizo,” alisema Lema huku wananchi wenzake wakipiga makofi kuonyesha kumuunga mkono.
Akijibu hoja hiyo, Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliwaeleza wananchi hao kuwa atalishughulikia suala hilo kupitia Bunge kwani tayari walishaiambia serikali kutolifanyia mchezo suala hilo kutokana na ukweli kuwa linagusa masilahi ya wananchi wote wa Tanzania.
“Suala la umeme nimelisikia na huyo mdudu anayeitwa Dowans tumeshaambiwa serikali wasicheze naye na mtalisikia tukilishughulikia bungeni Dodoma na endapo serikali haitakuwa sikivu, basi mtalisikia nchi nzima,” alisema Mbowe huku wananchi hao wakimshangilia.
Tayari CHADEMA ilishatangaza kuwa itafanya maandamano nchi nzima kupinga kuongezeka kwa gharama za umeme hapa nchini zilizopanda kuanzia mwezi Januari mwaka huu.
Aidha, wananchi hao walimweleza mbunge huyo kuwa kero nyingine inayowakabili ni uhaba wa masoko kwa ajili ya mazao yao, hasa mahindi, ambapo licha ya kutumia gharama kubwa katika kulima lakini wamekuwa wakipata mapato duni ambayo hayarudishi hata gharama za uzalishaji.
“Serikali inasema kuwa kilimo ni uti wa mgongo lakini haitilii maanani utekelezaji wa kauli hiyo. Tunalima mahindi lakini tukienda sokoni tunauza bei ndogo sana gunia shilingi 20,000 lakini kama wangeruhusu Wakenya kama walivyokuwa wakija walikuwa wakinunua gunia mpaka shilingi 45,000, tunaomba utusaidie hili,” alisema Martin Mfuru.
Pia wananchi hao walisema kuna umuhimu kwa serikali kuanza kutoa ruzuku ya pembejeo kwa wafugaji, kwani wanakabiliwa na hali ngumu katika utunzaji na uzalishaji wa mazao yanayotokana na mifugo, hasa kutokana na ughali wa pembejeo hizo.
“Hapa tunategemea ufugaji kwa ajili ya kujiingizia kipato lakini tatizo hatuna mbegu nzuri na ng’ombe wetu wamepata kwashakoo kutokana na kula chakula ambacho hakitoshelezi na kutokana na uhaba wa malisho hata vyakula vya mifugo vinavyosindikwa tunavyonunua havina ubora,” alisema Hellen Usiri.
Pia walimtaka mbunge huyo kuendelea kuhamasisha utaratibu wa wanafunzi kupatiwa maziwa shuleni ili kuwaongezea soko kama alivyoanzisha utaratibu huo mwaka 2001 akiwa mbunge wa jimbo hilo.
Walisema utaratibu huo ulisaidia kuboresha afya za watoto pamoja na kuwaongezea soko la maziwa yao.
Wakati huo huo Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema suala zima linalohusu Dowans kulipwa fidia litaamuliwa na mahakama na kwamba hataki tena kulizungumzia zaidi suala hilo kwani anahofia kufungua mjadala mpya kutoka kwa wanasiasa nchini.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa uendelezaji endelevu wa biofuel kimiminika nchini, iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kusisitiza kauli yake aliyoitoa awali haijabadilika.
Alisema suala la hukumu dhidi ya Dowans ni la kisheria na kwa kuwa hivi sasa tayari limeshafika mahakamani ni vizuri ukaachiwa mhimili huo, kwani ndio wenye uwezo kisheria kuhusu hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC).
“Sina maoni katika suala la Dowans, ila kauli niliyotoa awali inatosha na naogopa kufungua mjadala mpya kutoka kwa wanasiasa kwa kuwa suala hili lipo mahakamani na kuendelea kulisema ni kuingilia uhuru wa mahakama, kwa kweli inatosha turidhike na hayo,” alisema Waziri Ngeleja.
Aidha, alisema umefika wakati kwa Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kumaliza suala la mgawo wa umeme kwa kuibua miradi mbalimbali ambayo itasaidia kuleta ufanisi na kuondoa kero hiyo inayolikabili taifa.
Hata hivyo kauli hiyo ya Waziri Ngeleja ilipingwa vikali na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambapo alisema kuilipa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans sh bilioni 94 ni makosa, kwani suala hilo nyeti lilihitaji kwanza kujadiliwa na kuamuliwa na baraza la mawaziri.
Sitta alisema Dowans ni Kampuni ya wajanja watatu waliocheza ujanja kwenye karatasi na serikali kuingia ‘mkenge’ kulipa kitu ambacho alikielezea kuwa hakina sababu za msingi.
Waziri huyo alisema Kampuni ya Richmond iligunduliwa na Kamati ya Uchunguzi ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, kuwa haikuwa halali, lakini inasikitisha kuona na kusikia mbia wake Dowans amehalalishwa.
Akizungumzia mwongozo wa uendelezaji wa biofueli, Ngeleja alisema serikali inatambua manufaa yanayopatikana kutokana na uendelezaji huo, hususan ajira na kuongezeka kipato katika sekta ya viwanda na kilimo.
Alisema katika kuwezesha uendelezaji wa biofueli, sheria ya mafuta ya mwaka 2008, inatambua bidhaa zinazozalishwa na nishati hiyo hata kama zitachakachuliwa na wajanja kwa kutumia mafuta ya petroli.
“Mwongozo huu utasaidia kuinua kipato cha Watanzania hasa kwa kuunda vyama vya ushirika ambapo watanufaika na mpango huu kwa kuandaa mikataba mizuri iliyoandaliwa kisheria,” alisema Ngeleja.
Alisema jambo la uzalishaji wa nishati mbadala Tanzania si nchi ya kwanza na hivi sasa dunia nzima inahamasisha uzalishaji huo katika kila mikutano mikubwa ya kimataifa.
Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hosea Mbise, alisema lengo la kuzindua mwongozo huo ni kutoa taarifa kwa umma ili watambue jinsi inavyotumika kwa mujibu wa sheria na kanuni.
Alisema kuzalishwa kwa nishati ya biofueli kumezingatia sheria za uwekezaji ambao hautaliingiza taifa kwenye janga la njaa huku wawekezaji katika sekta hiyo wakitakiwa kuwekeza kwa kipindi cha miaka 25.
“Tunaamini uzinduzi huu utasaidia kutoa taarifa kwa wananchi jinsi inavyotumika na kutambua matumizi yake kisheria kwa kuzingatia sheria ya uwekezaji nchini ambapo wawekezaji hupewa muda wa miaka 25,” alisema Mhandisi Mbise.










A man who won't die for something is not fit to live
 
"Taifa Halina Imani na CCM Popote Serikalini"Ukisoma Maneno ya Kigaidi Kutoka Kamati Kuu ya CCM iliyofanya kikao katika Ofisi Yetu Kuu ya Taifa Ikulu, utaona jinsi gani Jk na CCM wanataka kutulaghai kwa kupitia Mahakama kuu. Kitu gani kinaharakisha malipo ya Dowans? Wananchi tunataka kuundwa kwa Katiba mpya na hii inamaanisha tunataka shughuli zote za serikali ya Tanzania zisimame mpaka Katiba Mpya Iundwe, Hii inasisha Dowans na mikataba yote Tanzania. Hili jambo la Uteuzi wa Jaji Mkuu bila wananchi kumjua na kuchujwa na Vyombo vya Kisheria ni Tumeukataa. Haiwezekani na inaonekana kabisa Jaji Ramadhani asinge kubali hili jambo la Dowans kulipwa bila uchunguzi wa kina...Warema na Judicial system yenyewe inaonekana wameshakubalina JK, Nini Tunakifuata Mahakama Kuu? Kama Sheria na Case Tunaweza Kuunda tuhakikishe tunafuata kila angles kujua Dowans chanzo chake ni Nini na Uhusiano na Richmond sio Kujadili Uhalali wa ICC, itakuwa ni Ujinga na Upotofu...Kwanini Tunaharakisha kuwalipa Dowans? Swala sio shilingi ngapi tuwalipe ni more than that...Dowans ni uongo na wizi wa hali ya juu ndio maana limewaamsha Watanzania wote kwa maamuvu. Bunge limejadili na lilisha toa maamuzi kuwa Richmond ni Kampuni Fake na Ingawa CCM imefanya Cover up ya hali ya juu bila Lowasa na wenzie kuchukuliwa hatua yeyote ile. Kama Richmond haikuwa Fake kwa nini Lowasa alijiuzuru? Dowans linatakiwa kujadiliwa Bungeni na Kamati maalumu iiundwe kwanini Pesa nyingi hivi zinalipwa bila Chombo Chochote kile kujua isipokuwa Kikwete, Makamba, Rostam, Ngereja, Warema na Viongozi wa CCM
Haiwezekani nchi maskini hivi inatoa pesa nyingi kirahisi hivi kwa milango ya nyuma na kutumia Ofisi Kubwa ya Taifa, Ikulu.

uapisho5.gif


High Court Of Tanzania
The High Court was first established by Article 17 (1) of the Tanganyika Order-in-Council, 1920, the High Court now derives its establishment from Article 108 (1) of the 1977 Union Constitution as the High Court of the United Republic.
Administratively, the High Court is headed by the Jaji Kiongozi (Principal Judge), a special assistant to the Chief Justice. Like other Judges of the High Court, the President appoints the Jaji Kiongozi. Since its establishment, the High Court has been headed by a total of six Principal Judges namely:

1) The Hon. Mr.Judge Nassor Suleiman Mzavas -31/08/1979 – 17/06/1989
2) The Hon. Mr. Judge Barnabas Albert Samatta -17/06/1989 – 16/06/1997
3) The Hon. Mr. Judge Hamisi Amiri Msumi -17/06/1997 – 14/07/2004
4) The Hon. Mr. Judge Amir. R. Manento -14/09/2004 - 31/01/2008
5) The Hon. Mr. Judge Salum. A. Massati -02/02/2008 – 18/12/2008
6) The Hon. Mr. Judge Fakihi. A. R. Jundu -14/02/2009 To date.

Apart from Jaji Kiongozi, there are other Judges of the High Court who were appointed by the President after consultation with the Judicial Service Commission. These are 62 Judges, among them 26 are Ladies. Hon. Mr. Justice Frederick Mwita Werema was later appointed by the President as The Attorney General, the position that he holds to date.

2. JURISDICTION OF THE HIGH COURT OF TANZANIA.
The Court has unlimited Jurisdiction on both Civil and Criminal matters within Tanzania. In addition to the said original and jurisdiction, the High Court of Tanzania has an appellate, extended, revision and supervisory jurisdiction over subordinate Courts.
Appeals from the High Court are preferred to the Court of Appeal of Tanzania which is vested with powers, authority and jurisdiction of confirming, reversing or varying any decision made by the High Court.


Tunauhakika na Upeo wa kujua Vibaraka na watumishi wa CCM Akiwemo Jaji Mkuu wa Tanzania Alieteuliwa na Kiongozi Alieba Uchaguzi atakubali Dowans ilipwa kwani lazima atetee sera na maamuzi ya CCM. Kitakacho fuata ni Nini. Wengi tumesikia Checks za kuwalipa Dowans zipo tayari Tanesco kudeposit account ya Dowans. Tunacho takiwa sasa hivi ni kuonyesha Watanzania hautegemei na kusubiri Maamuzi ya Mahakama Kuu. Bunge ni Venue nyingine ya kutumia na kama Makinda Akileta kelele zake za kutoka kwa JK tutafute njia ya kumkabili..
Jk anapigania kuwalipa Dowans kwa sababu kubwa Rostam alisimamia vizuri uchaguzi na kumwezesha kuiba kura, hakuna sababu zozote za kumlipa Rostam na CCM kujilipa mwenyewe. Tutachokifanya baada ya Dowans kulipa ni an Imaginable na Jk na familia yake itawabidi wakimbie haraka sana na boti huko Saudi kama Ben Ali wa Tunisia..
 
WATANZANIA NI WANGAPI HADI SASA (2005 - 2010) WENYE MAISHA BORA NA HADI HIVI SASA (2010 -2015) WAO WANAJIBIDISHA TU KUTAFUTA KIADA CHAKE NCHINI????

Watanzania wenzangu tuambizane ukweli hapa na tusifichane hali halisi ndani ya mifuko yetu. Mpaka hivi sasa wengi wetu HATUZUNGUMZII TENAUCHUMI wa maisha yetuTanzania bali hali halisi ni UCHUMA wa maisha yetu nchini. Je, wewe????

Baya zaidi, ajabu ninayoiona nkule bado CCM na JOPO LA MAFISADI wangependa Watanzania wote tukaseme tu YOTE NI MAISHA na kukimbilia kitanndani, baada kucheka na Masanja TBC, huku CC ya CCM wakibariki Dowans walimpwe.

Huku waliosbobea katika uchumi nchini wanatutahadharisha KIAMA DOWANS WAKILIPWA na kuongeza kuongeza kwamba tunachoona mpaka sasa kwa gharama ya maisha eti hapo bado ni mwanzo tu wa mapinduzi ya sinema nzima wa ahadi ya Maisha BORA ZAIDI kwa kila Mtanzania; na katika kutimiza hilo Mhe Kikwete na CCM wametuhakikishia dhamira zao za kutufikisha huko kwa Nguvu Zaidi, Ari Zaidi na Kasi Zaidi.

Sasa Mtu endapo utakuwa hauoni MAISHA BORA ZAIDI basi wala usisubiri kuambiwa na mtu, Wenye kuona UGUMU ZAIDI KWA KILA NAFSI YAKE huyu si Mtanzania tena maana WATANZANIA WOTE waliopata ahadi hizo tangu siku nyingi tu (2005 - 2010) maisha yao ni bora kabisa hivi sasa (2010 - 2015) wanacho kitafu kiukweli ni Uziada wa UBORA HUO WA MAISHA.
HOJA YANGU:

Kwa mantki hiyo Mhe Kikwete na CCM, watu wa Takwimu nchini acheni kutu fikicha ukweli, Watanzania ni wastani wa watu wangapi nchini maana hili la watu milioni 46 wala sihitaji tafsiri ya mtaalamu kubani kwamba si kweli.
 
Kutapatapa kwa jk (ccm), na kufananisha na kipindi cha bush na anguko la ( Republican)
Kuliibuka maswali na hata kuwatia hatiani waliyo daiwa kuwa ni magaindi kumbe ndivyo sivyo lili kuwa ni anguko la kisiasa,

Kwa Tanzania sasa shutuma zinatupiwa kwa Slaa tunaambiwa ni mchochezi wa vurungu, ana udini,(CHADEMA)

Hapa mimi nakataa SLAA kuingizwa kwenyeshtuma zisizo muhusu, shutuma hizi zina muhusu JK na serikali yake,

Kwanza kukamatwa kwa Mtanzania Ahmed Ghailani na siasa za marekani, na kukamatwa kwa Dr slaa na siasa za Tanzania.

Hadi kukamatwa kwake, kufunguliwa mashtaka kwa kosa la kuharibu majengo na mali za marekani kumeibuka maswali mengi,

Miongoni ni haya ambayao yalipata kujadiwa katika siku za nyuma ambayo nadharia yake imeonekana wakati wauendeshaji wakesi, kwa SLAA nadharia yake itaonekana kipindi cha uendeshwaji wa kesi pamoja na viongozi wenzake, ambayo mimi ninaiita kesi ya kishujaa juu ya ukombozi wa mtanzania.

Mwaka 2004 wakati Ghailani akikamatwa serikali iliyokuwa madarakani chini ya G.Bush, ilikosolewa vikali na wapinzani wao wa Democract, ambayo sasa ipo madarakani, ndivyo ilivyo sasa kwa serikali ya jk na CCM yake, imebanwa vyakutosha na CHADEMA, inaonekana yakuwa CHADEMA sasa inajiandaa kushika uongozi.

Democrat walioonya wakisema kuwa hatua ya kukamatwa kwa Ghailani zilikuwa ni mbinu za kisiasa ambazo zilikuwa na nia ya kubadili mwelekeo na mawazo ya wamarekani ili waache kujadili maswala muhimu yaliyokuwa yakitokea wakati huwo, kama uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi uliyomuweka madarakani rais Bush.

Naufananisha mchezo huwo na huu uliyo muweka madarakani Jk, na sasa walimkamata SLAA ilikuwasahaulisha watanzania maswala kama, DOWANS,MAISHA YA MTANZANIA, KATIBA MPYA, sasa wameibuka tena na hoja ya UDINI ilitusahau kujadili maswala nyeti ya kitaifa.

Democrat walidaikuwa Republican walifanya mchezo huwo baada ya kuona wameelemewa na hoja ya kudaiwa kuiba kura za mgombea wa DEMOCRAT, JOHN KERRY. Kwa TANZANIA haya yanayoibuka ni dalili za Uchakachuaji wa matokeo yaliyo muweka madarakani JK na CCM yake, ndiyo maana wanaibuka na hoja zisizokuwa na maana katika taifa letu, nakuandaa makundi ya kidini kuleta uchochezi usiyokuwa natija.

Wakati huwo pia, suala la serikali y BUSH kuivamia Iraq ilikuwa ni mada kubwa iliyokuwa ikijadiliwa kila kona. Hivyo kuchomekwa kwa hoja ya ugaidi (udini) wa Ghailani ilikuwa ni kuwafanya watu waachekuishutumu serikali ya BUSH,(ccm. Julai 25,2004 baada ya masaa nane ya mapambano katika mji wa GUJRAT katikati ya pakistani, (serikali ya ccm na wataka mabadiliko katika ya jiji la ARUSHA january 5,2011 watu walipambana). Ghailani na watu wengine 15 akiwamo mke na watoto wake walikamatwa( SLAA na mke wake na VIONGOZI wenzake pamoja na wafuasi wengine walikamatwa kinyume na sheria kwakuwa walikuwa na kibali halali)

Waziri wa mambo ya ndani wa pakistani alitangaza kukamatwa kwa Ghailani,( waziri wa mambo ya ndani alikaa kimya mpaka midia zilipo anza kumghasi ndipo akatoka hadharani na hoja potofu za kulifumba taifa macho, waonekane wao ni wasafi na wanafuata taratibu na sheria juu ya kile kilichotokea ARUSHA)

Hili nianguko kubwa kwa serikali ya CCM, na hawawezi kufika 2015 wakiwa pamoja kwani kwahali halisi ilivyo sasa kuna ccm mbili zenye dira tofauti,
VIVA CHADEMA na harakati za ukombozi.
Naomba kuwasilisha hoja
Ahsante
Kilewo next mp of MWANGA 2015
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom