Anguko kuu la Kikwete na CCM, dalili zimeanza

Anguko kuu la Kikwete na CCM, dalili zimeanza

Status
Not open for further replies.

Sir R

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2009
Posts
2,175
Reaction score
300
Kadri siku zinavykwenda naona dalili zote za CCM kuanguka. Hakuna atakayeweza kuiokoa chama hiki kongwe. Naona anguko hilo litatokea ndani ya miaka kumi na tano (15). Watakaokingusha CCM ni wana CCM wenyewe, si vyama vya upinzani.

Zifuatazo ni dalili ya kuanguka kwa CCM
1. Upendo kati ya wanachama umekwisha, ni ugomvi usiokwisha ( Sitta camp Vs Rostam camp)

2. Fedha ni kipaumbele siyo Sera au hoja.

3. Wasemaji wa chama ni wapayukaji ( makamba, Hiza Tambwe, Sofia simba)

4. Wazee wenye busara wamesusa chama ( Warioba, Salim, Butiku, Sumaye)

5. Familia ya viongozi wamekiteka chama ( Makamba's, JK's, )

6. Kampeni zimebadilika kuwa concert ( wanamuziki kibao)

7. Kununua wapinzani

8. Kukataa midahalo ( mchakato majimboni- TBC)

9. Ahadi nyingi wakati huu wakati za mwaka 2005 hazijatekelezwa ( Mikopo ya wanafunzi maisha bora kwa kila mtz n.k)

10. Chama kujadili issue binafsi zaidi badala ya maslahi ya wananchi.

CCM kwa sasa ina uwoga sana kuliko cha chama chochote hapa nchini. Wanaelewa wanakoelekea.
 
Nina imani kubwa kwamba wafanyakazi wengi hawatampa kura JK. Lakini pia nina wasiwasi kwamba waislamu wengi hawana msimamo, kwa kuwa wana kasumba za udini, hivyo wanaweza kumpigia JK kwa minajili ya udini. Au wanaweza kumpigia Lipumba. Kwa kufanya hivyo watapunguza kura za wapinzani (kwa kuwa zitagawanywa kati yao) wakati zile za wanachama wa CCM na wale asilimia 75 ambao ni fuata upepo, zinaweza kurudi kwa JK. Na hivyo kumpa ushindi.

Kuna haja ya kuharmonize uwepo wa kampeni safi zisizoingiza itikadi za kidini. Hili litatusaidia sana katika kuwa na uchuguzi huru na wa haki.
 
Ili kuweza kuwapata Waislamu ni lazima CHADEMA Ihubiri zaidi HAKI na kukubali UAMINIFU na USAWA kwani siku zote Muislamu anaziamini hizi kuwa ni sifa za kiongozi bora bila kujali katokea upande gani.

Endapo mahubiri hayo katika kampeni yataonesha dalili za ukweli na wala siyo danganya TOTO basi kura nyingi za Waislamu zitakuwa CHADEMA.
 
Una habari mishahara imeongezwa kinyemela???

Karibu mkuu, sijakusoma siku nyingi nikadhania pengine ulikwenda kugombea ubunge Makongolosi!! Hata wakiongeza mishahara kinyemela wafanyakazi wengi wanaishi kwa dhiki na most likely hawatampa kura Jakaya!! Ushindi wake utakuwa wa wizi wa kura. He might ascend to the office but he will be illegitemate!!
 
4. Wazee wenye busara wamesusa chama ( Warioba, Salim, Butiku, Sumaye)

huyu sumaye naye anabusara ?,
 
4. Wazee wenye busara wamesusa chama ( Warioba, Salim, Butiku, Sumaye)

huyu sumaye naye anabusara ?,
Busara alikuwa nayo Kambarage tu ambaye mambo yalipokuwa yakienda vibaya alikuwa anawashukia live. Sio hawa waliokaa kimya nchi ikiuzwa kwa familia ya Kikwete.
 
4. Wazee wenye busara wamesusa chama ( Warioba, Salim, Butiku, Sumaye)

huyu sumaye naye anabusara ?,

Nikifanya comparison ndani ya CCM naona anaonekana nafuu kuliko kina Makamba
 
kwa kweli i feel like crying kuona watanzania wanaziba masikio na kuwa na shingo ngumu. yaani hawataki kuelewa jinsi wakijani walivyoibomoa nchi yetu nzuri na kuwafanya watanzania kuishi maisha ya umasikini wa kutupwa huku wenyewe na familia zako wakitumbua mali za walalahoi bila huruma. Enyi watanzania wenzangu ni nani aliyewalogaaaaa??? mbona tunakuwa waoga namna hiyo kufanya mabadiliko? kwa nini tunapenda kukumbatia mazoea ati kwa kuilinda amani tuliyonayo, je hiyo amani ya kinafiki inamaana gani wakati watu wanalala na njaa, watoto wanakwenda shule peku na kukalia matofali darasani? umevunjika mguu unekwenda hospital unapewa panado then bado mwanang'angania amani ya maneno wakati huo wenyewe wakiendelea kuitumbua nchi na kuvimbisha mavitambi yao kama mimba ya miezi tisa. Inauma sanaaa tena inauma sanaaa, jamani shime watanzania tuamke tufanye mabadiliko mwaka wa ukombozi ni huu, tumpe Dr. Slaa miaka 5 then tumpime tuone atatufanyia nini, ni bora kujaribu kitu kipya kuliko kung'ang'ania dudu pruf lisilokuwa na msaada wowote zaidi ya kutunyonya tu. Amkeni watanzaniaaaaaaaaaaaaaaa
 
Asante Sir R lakini mbona unakataa tamaa? Ina maana huamini kuwa anguko la CCM linawezekana mwaka huu? Kwa nini huamini? Kama unaamini mbona unataja miaka 15? Kama una nia ya kuleta mabadiliko Tz yanawezekana. Ni mwaka huu. Ni wewe tu kuamua.

Sasa kama wewe umeshakata tamaa hivyo utawaeleza nini mababu zako huko kijijini ulikotoka? Utamshawishi mtu kweli akaleta mabadiliko Tz kwa kutumia kura yake? Huu sio wakati wa kukaa chini na kulalama, au kulia. ni wakati wa kufanya kazi. Kwa sasa kazi ni moja tu: kuondoa CCM madarakani sio kwa sababu tunaichukia, bali kwa sababu imeingiliwa na genge la majambazi wanaoipora nchi yetu. Tukisubiri miaka 15 kama unavyona wewe wala hatutakuwa na kitu cha kukomboa. Watakuwa wameuza nchi kwa mafisadi tayari. Watakuwa wametuachia mashimo ya madini. Watakuwa wanaponda maisha labda huko ughaibuni.
 
Kadri siku zinavykwenda naona dalili zote za CCM kuanguka. Hakuna atakayeweza kuiokoa chama hiki kongwe. Naona anguko hilo litatokea ndani ya miaka kumi na tano (15). Watakaokingusha CCM ni wana CCM wenyewe, si vyama vya upinzani.

Zifuatazo ni dalili ya kuanguka kwa CCM
1. Upendo kati ya wanachama umekwisha, ni ugomvi usiokwisha ( Sitta camp Vs Rostam camp)

2. Fedha ni kipaumbele siyo Sera au hoja.

3. Wasemaji wa chama ni wapayukaji ( makamba, Hiza Tambwe, Sofia simba)

4. Wazee wenye busara wamesusa chama ( Warioba, Salim, Butiku, Sumaye)

5. Familia ya viongozi wamekiteka chama ( Makamba's, JK's, )

6. Kampeni zimebadilika kuwa concert ( wanamuziki kibao)

7. Kununua wapinzani

8. Kukataa midahalo ( mchakato majimboni- TBC)

9. Ahadi nyingi wakati huu wakati za mwaka 2005 hazijatekelezwa ( Mikopo ya wanafunzi maisha bora kwa kila mtz n.k)

10. Chama kujadili issue binafsi zaidi badala ya maslahi ya wananchi.

CCM kwa sasa ina uwoga sana kuliko cha chama chochote hapa nchini. Wanaelewa wanakoelekea.

Nafkiri haya ni Maono yako wewe Binafsi... CCM BADO IMESIMAMA NA ITAENDELEA KUSIMAMA! ...
 
Asante Sir R lakini mbona unakataa tamaa? Ina maana huamini kuwa anguko la CCM linawezekana mwaka huu? Kwa nini huamini? Kama unaamini mbona unataja miaka 15? Kama una nia ya kuleta mabadiliko Tz yanawezekana. Ni mwaka huu. Ni wewe tu kuamua.

Sasa kama wewe umeshakata tamaa hivyo utawaeleza nini mababu zako huko kijijini ulikotoka? Utamshawishi mtu kweli akaleta mabadiliko Tz kwa kutumia kura yake? Huu sio wakati wa kukaa chini na kulalama, au kulia. ni wakati wa kufanya kazi. Kwa sasa kazi ni moja tu: kuondoa CCM madarakani sio kwa sababu tunaichukia, bali kwa sababu imeingiliwa na genge la majambazi wanaoipora nchi yetu. Tukisubiri miaka 15 kama unavyona wewe wala hatutakuwa na kitu cha kukomboa. Watakuwa wameuza nchi kwa mafisadi tayari. Watakuwa wametuachia mashimo ya madini. Watakuwa wanaponda maisha labda huko ughaibuni.

Stop dreaming and drink KoolAid!
CCM will win by a landslide on October 31st.
Love it hate it, CCM is the people's choice.
Let's vote CCM and help JK finishing what he has started. Go CCM
 
Stop dreaming and drink KoolAid!
CCM will win by a landslide on October 31st.
Love it hate it, CCM is the people's choice.
Let's vote CCM and help JK finishing what he has started. Go CCM
Finish what he started? Selling our country? God forbid!
 
Asante Sir R lakini mbona unakataa tamaa? Ina maana huamini kuwa anguko la CCM linawezekana mwaka huu? Kwa nini huamini? Kama unaamini mbona unataja miaka 15? Kama una nia ya kuleta mabadiliko Tz yanawezekana. Ni mwaka huu. Ni wewe tu kuamua.

Sasa kama wewe umeshakata tamaa hivyo utawaeleza nini mababu zako huko kijijini ulikotoka? Utamshawishi mtu kweli akaleta mabadiliko Tz kwa kutumia kura yake? Huu sio wakati wa kukaa chini na kulalama, au kulia. ni wakati wa kufanya kazi. Kwa sasa kazi ni moja tu: kuondoa CCM madarakani sio kwa sababu tunaichukia, bali kwa sababu imeingiliwa na genge la majambazi wanaoipora nchi yetu. Tukisubiri miaka 15 kama unavyona wewe wala hatutakuwa na kitu cha kukomboa. Watakuwa wameuza nchi kwa mafisadi tayari. Watakuwa wametuachia mashimo ya madini. Watakuwa wanaponda maisha labda huko ughaibuni.

Niliposema anguko la CCM nina maana kuvunjika vipande vipande naitafika mahali ikashindwa kushiriki uchaguzi. Kuangusha katika uchaguzi sijaipa muda huo wote maana naelewa kuanzia sasa inaweza kuangushwa. Pia sijakata tamaa, binafsi nimekuwa nikiwahamasisha ndugu zangu waliko kijiji kuleta mabadiliko mwaka huu. Na mafanikio nayaona, mama yangu juzi kwa mara ya kwanza kaniambia ataipigia kura upinzani badala ya CCM;

Katika jimbo nilikozaliwa mimi dalili ziko wazi kuwa CHADEMA wanachukua jimbo. Siwezi kukata tamaa mimi;

Mwezi wa mumi nategemea kutembelea kijiji nilikozaliwa, kazi nitakayo fanya nipamoja nakuwaelimisha wananchi namna ya kuhamasisha kumchagua Dr Slaa na CHADEMA.
 
Nafkiri haya ni Maono yako wewe Binafsi... CCM BADO IMESIMAMA NA ITAENDELEA KUSIMAMA! ...
Siku yakitimia utanikumbuka, CCM imesini mama juu ya ufisadi na haiwezi kendelea kusimamia hapo. Kuanguka ni lazima kwani misingi ni mibovu.

Nakushauri kama unakipenda sana CCM chukua hatua ya kukiokoa ila naona too late to do so. Soma dalili.
 
Dalili za anguko ni mwanzo wa hujuma kwa demokrasia

Gud one!!!!!!!!!

Source: Raia mwema

DALILI ya anguko la chama cha siasa huanza kwa mambo makuu kadhaa yakiwamo makuu manne. Kwanza, kwa kuanzisha na kuenzi hujuma za ndani ya chama chenyewe pale mtu anapokuwa bora kuliko chama na chama kuwa bora kuliko taifa. Hii hufanyika kwa kutelekeza maadili na misingi ya uadilifu katika utumishi wa umma.

Pili, kwa kukabidhi mustakabali wa chama mikononi mwa mgombea urais. Hii hufanyika kwa kumrundikia mgombea urais madaraka makubwa ya kichama na kidola.

Tatu, kwa juhudi za kutafuta ushindi kwa gharama yoyote bila kujali njia gani zinatumika; bali kujali matokeo tu. Katika hili, hujuma, wizi wa kura na hata kutumia nguvu za dola hutumika kuhakikisha ushindi unapatikana kwa chama hicho.
Matokeo ya dhana hii ndani ya chama tawala ni ulevi unaoonekana kwa njia ya kauli mbiu kama zile zinazosikika katika taifa letu “CCM itatawala milele”, “wapinzani tuwachane chane”, “wapinzani ni fotokopi”, n.k.

Nne, anguko la chama huanza kutabiriwa kutokea ndani ya chama chenyewe badala ya wapinzani wa chama kutabiri anguko la chama hicho. Linapotokea hili, viongozi wa chama huanza kuwatishia na “kuwashughulikia” wanaodhaniwa ni maadui wa ndani ya chama, badala ya kushughulikia sera na mapambano dhidi ya vyama vingine.

Kwa bahati mbaya nadharia hiyo hapo juu inakihusu chama tawala kuliko chama pinzani; hata kama dalili hizi zaweza pia kuonekana ndani ya vyama visivyo madarakani.

Tofauti ya pande hizi mbili ni kuwa, zinapoonekana katika chama tawala huonekana ni utaratibu uliokubaliwa, wakati zikionekana katika vyama vya upinzani hulaaniwa kuwa ni uhalifu dhidi ya demokrasia.
Niliwahi kusema huko nyuma kuwa CCM ni chama cha viongozi, na kwa hiyo haya yanapotokea ni vigumu kupatiwa ufumbuzi kwa sababu ya utamaduni uliojengeka ndani ya chama wa kuabudu na kulindana kwa gharama ya kuangamiza chama.

Waliodiriki kuvunja kimya hicho kwa kusema ndani ya vikao au kuandika maoni yao hadharani, wanajutia uamuzi wao huo kwa sababu wameonekana ni ‘wahaini’ na wasiokitakia mema Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika kampeni zinazoendelea kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kuna dalili zimeanza kujitokeza kuonyesha usahihi wa nadharia nilizozitaja hapo juu. Chama Cha Mapinduzi, kwa mara ya kwanza katika historia yake, kimelazimika kujitokeza hadharani kutetea na kutoa maelezo juu ya masuala yaliyoibuliwa na wapinzani. Tumemwona Mwenyekiti wa Kampeni, Abdulrahman Kinana akitolea maelezo juu ya tuhuma za ufisadi wa EPA baada ya CHADEMA kuuzumgumzia katika uzinduzi wa kampeni zake.

Tumemwona tena akitolea maelezo juu ya mwenendo wa mke wa mgombea wao urais kujihusisha na kampeni kwa gaharama za serikali. Tumewaona makada wa CCM wakitumia hoja nyepesi kuzuia au kuchelewesha wapinzani wasiendelee kufanya kampeni.

Mathalan tumeona mapingamizi ya ajabu dhidi ya wapinzani; tumeona hoja ya Makongoro Nyerere akizuia matumizi ya jina la ukoo wao (Nyerere); tumeona mgombea wa CCM akimkwida mgombea wa CHADEMA na kujichukulia sheria mkononi; tumeona CCM ikiwazuia wagombea wake wasishiriki midahalo; tumewaona CCM wakiibua siasa zinazoitwa za “maji taka” dhidi ya maisha binafsi ya mgombea wa CHADEMA; tumesikia kuwa ufisadi ni wa mtu binafsi na si wa chama wakati chama ni watu na si majengo!
Tumeona CCM ikibadili ratiba ya mgombea urais na kumnyima kabisa muda wa kupumzika kama walivyoahidi hapo awali; tumeshuhudia CCM ikitumia raslimali nyingi kupita kiasi kumnadi mgombea wao kana kwamba anagombea kwa mara ya kwanza; tumeona mgombea akilazimika “kulamba” matapishi ya chama hicho pale alipolazimika kuwanadi makada wanaotuhumiwa kwa tuhuma chafu za rushwa wakati CCM ikihubiri kuwa rushwa ni adui wa haki. Orodha ya dalili za anguko ni nyingi na zimeenea nchi nzima.
Liko suala na malalamiko ya kampeni za udini zinazolalamikiwa na mgombea urais wa CCM. Katika tangazo la biashara linalorushwa na ITV kila siku, mgombea anawatahadharisha Watanzania wasigawanywe kwa msingi ya dini, kabila wala rangi.

Maneno haya ni matamu kuyatamka lakini ni magumu sana kuyatekeleza; hasa pale anguko linapokuwa limeanza kuonyesha dalili. Kampeni za udini zimeshamiri sana ndani ya CCM yenyewe!
Kuna wagombea wengi katika kura za maoni walioshinda au kushindwa kwa matumizi ya udini, kabila na hata rangi. Kamati ya maadili ya chama ilishindwa kabisa kuyashughulikia na hatimaye NEC ikaamua kura nyingi za maoni ziwe ndicho kigezo kikuu cha kuteuliwa bila kujali hizo kura zimepatikana vipi.
Wapo Wakiristo waliokaangwa na Waislam na hali kadhalika wapo Waislam waliokaangwa na Wakiristo kupitia kampeni za udini. Wiki iliyopita, mgombea wa CCM jimboni Nyamagana alitamka hadharani kuwataka wapiga kura wasimpigie mpinzani wake kwa sababu tu, ni mkazi wa Nyamagana, utadhani Nyamagana haiko Tanzania!

Katika chama ambacho kinachukia ubaguzi wa aina yoyote, hii ingetosha kwa CCM kumuondoa, na hata kuacha jimbo lichukuliwe na chama kingine ili kulinda misingi na imani yake.
Wako wagombea wanawake ambao kwa sababu za ndoa wanajikuta wanakataliwa kila mahali – walikozaliwa na wanakoolewa!

Malalamiko ya udini yamesikika hata katika mazungumzo binafsi ya mgombea urais wa CCM pale anapowatuhumu viongozi wa dini hadharani na nyuma ya pazia kuwa hawampendi. Kudhihirisha hilo, ameteua kikosi kazi cha kuwashughulikia mmoja baada ya mwingine au kwa kuwatuma wajumbe hao kuwaona viongozi hao au kuwatisha kwa kupitia viongozi wa dola walio karibu nao.

Baadhi ya viongozi wa dola huko mikoani na wilayani wameagizwa kuwaona viongozi hao na tayari baadhi yao kwa kulinda vibarua vyao wameonekana kuwasiliana na mgombea wakimweleza kuwa endapo majimbo ya maeneo yao yatachukuliwa na upinzani, ni kwa sababu ya viongozi wa dini.
Uchonganishi wa namna hii, hauna tija hata kidogo na utamtenga mgombea huyo na viongozi hawa wa kijamii. Utengano huu hauwezi kuisaidia CCM hata ikishinda kwa sababu ushindi wa vitisho na ghilba hauchochei maendeleo yoyote yaliyoanishwa katika ilani yake.

Sasa pazia limefunguka na CCM inaonekana wazi mbele ya wapiga kura. Uko udhaifu mkubwa wa chama chenyewe, lakini lililo kubwa ni udhaifu wa wagombea wake akiwamo mgombea urais. Udhaifu wake ambao niliuzungumzia wiki iliyopita hauwezi kutetewa kwa hoja nyepesi kama ambavyo makada wa CCM wanavyojaribu kufanya.

Udhaifu wake umekuwa ni mtaji mkubwa kwa wapinzani kwa kuutumia kujenga hoja nzito zenye kuvutia wasikilizaji hata kama kuna uwezekano wa kuzijibu, lakini kwa sasa hakuna mtu makini ndani ya chama aliye na uwezo wa kujieleza na kujielekeza katika kujibu hoja hizo.

Wapo wanaosema kuwa wapo makada wenye uwezo wa kukitetea chama na wakakubalika, lakini hatari ni pale inapoonekana wakifanya hivyo watakuwa wanamfunika mgombea urais wao.

Dhima na hatima ya chama katika uchaguzi imekabidhiwa mikononi mwa mgombea ambaye hata wanachama wake wana mashaka naye kuhusu uwezo wa kukitetea chama hicho.
Siyo siri tena kuwa makundi yaliyoshamiri ndani ya chama yanamtazama kwa makini mgombea huyo kuona kama atakiokoa chama hicho.

Kundi kuu lililomwingiza madarakani mwaka 2005 limeonekana ama kutengwa na kampeni za mwaka huu, au limejitenga lenyewe na nyuma ya pazia linasubiri kuwaambia Watanzania kuwa bila kundi hilo CCM ni dhaifu sana mbele ya wapiga kura.

Kama anguko linalotabiriwa na wanachama wenyewe litatokea, tuwe tayari kuyaona na kuyasikia ambayo baada ya kuyaona na kuyasikia, tutadhani hatukuwa tunaishi Tanzania wakati haya yanatokea!
hs3.gif
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom