Angalieni hii ramani ya nyumba alafu mnishauri kitu

Angalieni hii ramani ya nyumba alafu mnishauri kitu

Bila vipimo ni ngumu kukadiria

Tuseme kwa mchoro jinsi ulivyo tukadirie kila chumba kina m3×m3, sebule m5×m3, dining m4×m2.5, vyoo kila kimoja m2×m2.5, kitchen, kibaraza cha jikoni na store m5×m2.5

  • Hapo unapata usable space jumla ya sqm 73.5

(Hiyo ni usable space haijajumuisha corridor, upana wa kuta na veranda)

Tuje kwenye makadirio ya upana na urefu wa hiyo nyumba

  • Hapo upana wa nyumba ni kama m10 na urefu ni m11 (m10×m11) = sqm 121

(Kiwanja cha sqm 72-81 hakitatosha kujenga hiyo nyumba ya ndoto yako)

Hautapata hata sehemu ya kupark gari, kabustani kakishikaji, watoto pa kucheza au pa kukaa watu siku ukifa
Ni za kukopi kwenye mtandao
 
Ndugu

Je hii ramani inaenea kwenye eneo la aquare mita 150 na kubakiza sehemu ya kupaki kagari na kuanika nguo.... Naombeni mawazo yenu ikibidi sana naombeni na vipimo

Mimi nilikuwa na waza icheze kwenye square mita 72 au 81 square meter...

Naombeni mawazo yenu na vipimo vizuri kadiri muwezavyoView attachment 3564803
Hii ninayo njoo nikupe vipimo na gharama zake na nikupe ushauri BURE wa kuanza ujenzi wa Nyumba nzuri
 
TUMPE USHAURI MTU ANAYETAKA KUJENGA NYUMBA YA KWANZA YA KUISHI

(1) Anza na bajeti halisi
Andika pesa uliyonayo mkononi.
Jua gharama za ramani, vibali, vifaa, fundi, finishing, umeme, maji na fence.
Ongeza akiba ya dharura angalau asilimia 10 hadi 15.
Watu wengi hukwama si kwa kukosa pesa, bali kwa kupanga chini ya uhalisia.

(2) Chagua ramani inayolingana na kipato chako
Usijenge kwa presha ya kuonyesha uwezo.
Nyumba ndogo lakini imara na iliyopangiliwa vizuri ni bora kuliko kubwa isiyoisha.
Kama ni familia changa, vyumba 2 hadi 3 vinatosha.
Pendelea mpangilio unaoruhusu kupanua baadaye.

(3) Eneo ni muhimu kuliko ukubwa
Hakikisha kiwanja hakina mgogoro wa umiliki.
Kuna upatikanaji wa maji na umeme.
Barabara ipo au ina mpango wa kupatikana.
Nyumba nzuri kwenye eneo baya ni hasara ya muda mrefu.

(4) Tafuta mafundi na mkandarasi kwa umakini
Usichague kwa bei ndogo tu.
Angalia kazi walizowahi kufanya.
Angalia uaminifu wao.
Fanya mkataba wa maandishi, hii ni muhimu sana.

(5) Usikimbilie finishing za kifahari
Marble, gypsum, milango ya gharama kubwa vinaweza kusubiri.
Kipaumbele kiwe msingi imara, kuta na paa bora, umeme na mabomba yaliyofanywa kwa viwango.
Finishing unaweza kuboresha kidogo kidogo baadaye.

(6) Simamia mwenyewe au uwe na msimamizi unayemuamini
Usipotee site kwa muda mrefu bila kufuatilia.
Vifaa huibiwa na kazi huharibika bila uangalizi.

(7) Epuka mikopo mikubwa bila mpango wa uhakika
Usijenge nyumba itakayokunyima amani ya kifedha miaka mingi ijayo.
Jenga kwa hatua kama ni lazima: msingi, kuta, paa, kisha malizia taratibu.

(8) Fikiria maisha ya baadaye
Je, familia itaongezeka?
Je, unahitaji chumba cha wageni au biashara ndogo mbele?
Je, kuna nafasi ya maegesho?
Jenga kwa mtazamo wa miaka 10 hadi 20 mbele.

Ukweli muhimu
Nyumba ya kwanza si lazima iwe ya ndoto zako zote.
Ni msingi wa safari. Bora iwe imara, halali na inayokupa amani.

Muhimu Bado tunatoa ramani za ujenzi Bure na tunakushauri kuhusu ujenzi Bure kabisa....

Unachotakitakiwa kufanya ni kubofya hii link kuja Whatsapp

Wa.me//255789005562

Au jiunge na group la ujenzi wa gharama nafuu na ramani Bure

 

Attachments

  • 591bd52ca8b41b5fcb3b895269a89391 (1).jpg
    591bd52ca8b41b5fcb3b895269a89391 (1).jpg
    54.6 KB · Views: 9
  • 6217e05806d1a5620935fd16cdb746b2 (1).jpg
    6217e05806d1a5620935fd16cdb746b2 (1).jpg
    69.1 KB · Views: 8
  • 6217e05806d1a5620935fd16cdb746b2.jpg
    6217e05806d1a5620935fd16cdb746b2.jpg
    69.1 KB · Views: 11
  • b3cc10dd028289ea72e9bc7cbd06aad8 (1).jpg
    b3cc10dd028289ea72e9bc7cbd06aad8 (1).jpg
    61.4 KB · Views: 12
  • 976dc24794382c5589bfc68caeaa1956 (2).jpg
    976dc24794382c5589bfc68caeaa1956 (2).jpg
    94.9 KB · Views: 12
  • 1cd904e456cfb0f4e5dc2acab3b1923a (2).jpg
    1cd904e456cfb0f4e5dc2acab3b1923a (2).jpg
    138.7 KB · Views: 13
  • 0616af66cd66fef820ca87f4e4fe6eea.jpg
    0616af66cd66fef820ca87f4e4fe6eea.jpg
    59 KB · Views: 11
  • dcfb3416c6051a21c6da926599997714 (2).jpg
    dcfb3416c6051a21c6da926599997714 (2).jpg
    105.4 KB · Views: 12
  • 29d2be5337a90fd772ad80a348c7c271.jpg
    29d2be5337a90fd772ad80a348c7c271.jpg
    119.4 KB · Views: 13
  • 6c5eecff5b75a53487dde61d9def4bb3 (1).jpg
    6c5eecff5b75a53487dde61d9def4bb3 (1).jpg
    72 KB · Views: 8
  • 58364aeb353339da426c620c0ecb5324 (1).jpg
    58364aeb353339da426c620c0ecb5324 (1).jpg
    82.1 KB · Views: 16
  • d8071fef2fe0bd4785f7ae75fb0d49da (4).jpg
    d8071fef2fe0bd4785f7ae75fb0d49da (4).jpg
    116.1 KB · Views: 13
  • d8071fef2fe0bd4785f7ae75fb0d49da (2).jpg
    d8071fef2fe0bd4785f7ae75fb0d49da (2).jpg
    116.1 KB · Views: 9
  • 394596328132fe21c8db029597366900 (1).jpg
    394596328132fe21c8db029597366900 (1).jpg
    55.6 KB · Views: 9
  • d8071fef2fe0bd4785f7ae75fb0d49da (1).jpg
    d8071fef2fe0bd4785f7ae75fb0d49da (1).jpg
    116.1 KB · Views: 17
  • d966cc981b6b3a85a08747f825a9682f.jpg
    d966cc981b6b3a85a08747f825a9682f.jpg
    68.6 KB · Views: 13
Ndugu

Je hii ramani inaenea kwenye eneo la aquare mita 150 na kubakiza sehemu ya kupaki kagari na kuanika nguo.... Naombeni mawazo yenu ikibidi sana naombeni na vipimo

Mimi nilikuwa na waza icheze kwenye square mita 72 au 81 square meter...

Naombeni mawazo yenu na vipimo vizuri kadiri muwezavyoView attachment 3564803
Hakuna anayejua
- barabara ipo upande gani
-mfumo wa maji taka upo wapi
-upepo unavuma kutoka wapi..
-Jua linachomoza na kuzama kutokea wapi
-eneo tambarale au
-Kiwanja kina regular shape au irregular

Aina yoyote ta ushauri mtakao peana hapo ni itakuwa Mzaha tu.
Tafuta fundi wako nenda naye site upate kitu cha uhakika...
Unataka matibabu bila kwenda Hospital.
 
Ndugu

Je hii ramani inaenea kwenye eneo la aquare mita 150 na kubakiza sehemu ya kupaki kagari na kuanika nguo.... Naombeni mawazo yenu ikibidi sana naombeni na vipimo

Mimi nilikuwa na waza icheze kwenye square mita 72 au 81 square meter...

Naombeni mawazo yenu na vipimo vizuri kadiri muwezavyoView attachment 3564803
Unatoka Master unakutana na choo mbili watu wanatoka chooni. Hapo usiri wako uko compromised . Haifai, rekebisha hapo
 
Mgeni akienda chooni anapata nafasi ya kuchungulia ndani kwenu wote. Public toilet imekaa pabaya sana inaweza kuleta immorality ukipata wageni wahuni
 
Back
Top Bottom