Andrew Nyerere on Mwalimu humble children!

Andrew Nyerere on Mwalimu humble children!

Hii si kweli kwamba siku zote huwa wanatatua matatizo yao bila kuingiza mtu wa nje. Wakati familia inafarakana kuhusu mahala pa kumzika marehemu Mwalimu, ilibidi Waziri Kimiti ndio aingilie kati kuwasuluhisha, na Nyerere akazikwa mahala ambapo hakuna aliyetaka baina ya pande zilizogawanyika katika mvutano.

Na si kweli kwamba hawaombi misaada. Andrew hukimbilia ubalozini kupewa misaada na pia kutunzwa kwenye majengo ya serikali, Usalama. Na sitashangaa familia kupokea misaada maana hata Mwalimu alifanya. Alisaidiwa nyumba mpya na TANU mwaka 1974, alisaidiwa nyumba mpya na Jeshi mwaka 1999, alisaidiwa rehani ya nyumba ya Msasani na ukarabati na utunzaji wake kuanzia mwaka 1985. Tuseme yote, sio kuwasafisha tu.

Dilunga,
Nilikuwepo Butiama kwa siku sita za maombolezi kuelekea maziko ya Mwalimu. Si kweli kwamba kulikuwa na mfarakano wa mahali atakapozikwa. Suala lililojitokeza ni Wanamaombi wa Padri Nkwera (?) walitaka wapewe nao nafasi maalumu ya kuuombea dua mwili wa marehemu wakiamini kuwa wana uwezo wa kumfufua. It was a foregone conclusion kuwa Mwalimu angezikwa Mwitongo.
 
1.

- Mwalimu hakupenda kuona watoto wake wanatajirika, huo ni uongo wa mchana, kama unaamini ni ukweli weka source yake mkuu!

2.

- Ni wapi uliposoma ambapo Mwalimu alisema hataki watoto wake kujilimbikizia mali? Na ni wapi ambapo hakutaka viongozi wake kutojilimbikizia mali? Mwalimu alichokuwa hataki ilikuwa ufisadi kujilimbikizia mali kwa ufisadi, lakini sio kwa njia za halali, hebu nitajie m-Tanzania yoyote unayemjua aliyekuwa na utajiri wake under Mwalimu na akamnyanga'anya mali zake bila sababu?

- Mzee Mbowe hakuwa tajiri wakati wa Mwalimu? Ndesamburo hakuwa tajiri under Mwalimu? Mzee Kanyamala hakuwa tajiri under Mwalimu? Kurgisi hakuwa tajiri under Mwalimu? Komanya hakua tajiri under Mwalimu? Mengi hakuwa tajiri under Mwalimu? Sasa kama alikuwa hataki wananchi kujilimbikizia mali ilikuwaje akawaacha hawa? Sasa what is your point kuhusu watoto wake? Ni lini uliwahi kusikia mtoto wake mmoja amekwua tajiri akamnyanga'anya mali zake?

- Hivi unajua kua Mwalimu akiwa kwenye power mtoto wake Madaraka, alikuwa akimiliki malori ya mchanga mengi tu, na kwamba Magige alikua ni Engineeer mkubwa sana kiwanda cha Sukari Kilombero tena akila kuku zake ile mbaya sana! Na kwamba Anna alikuwa Italy akisoma na kuishi huko kwa muda mrefu sana! Rosemary akaja kuwa mbunge wa kupewa na Mkapa, Makongoro akawa mbunge na sasa ni Mwenyekiti wa CCM Musoma, sasa ni nini kosa la Mwalimu hapa? Wewe huwezi kuona kwamba hapa ndipo uwezo wa akili zao kimaisha zilipoishia, sasa Mwalimu ulitaka afanye nini?

3.

- Elimu kubwa inatakiwa kuku-guarantee maisha mazuri au utajiri, sasa kama huna akili za darasani basi uwe na akili za maisha, kama huna zote hakuna msaaada na hakuna wa kulaumiwa, wewe ulitaka Mwalimu afanye nini hasa? Achukue hela hazina awape ndio ungefurahi? Kama hawana akili ya kuzitunza then what?

4.

- Ulitaka Mwalimu awape madaraka watoto wake are you serious au unatania? Mkapa si aliwapa then what happened? Yaani mkuu kilio chako chote hapa ni kwa sababu ulitaka Mwalimu awape madaraka watoto wake bila sababu kwa kuwa yeye ni rais tu?

5.

- Hapa unasema nini eti watoto wa Mwalimu walikuwa hawapewi hela za matumizi ndio maana leo hawana maisha mazuri? I s that so? Hela za matuimizi kwa watoto ndio guarantee ya maisha mazuri wakikua? Hebu rudia tena hii point mkuu!

6.

- Wewe mkuu ndio hujui source ya unachokiongea, je unawafahamu vizuri hawa watoto wa Mwalimu, au na wewe unarukia tu habari za mtaani? Madaraka alioa mtoto wa waziri mmoja then Mageni, ambaye alikua Hotel Manager pale Twiga Hotel huyu demu alikua opportunists na wote pale mjini tulikuwa tunamshitukia jamaa yangu akaupanda mkenge akaishia kuachwa malori yote miguu juu, sasa wewe unasema ninaongea habari za mtaani wakati ninaongea habari nilizozionai, sasa kama huyajui si uulize, hao kina Magambo, Steven Kiboko, Milton na Matare wanaokula kuku sasa hivi kwa jina la Mwalimu wewe unawafahamu mkuu? Huna hoja hapa mkuu!

7.

- Sasa eti unasema kwamba watoto wote waliopewa malezi mazuri na wazazi wao duniani ndio peke yao wanaokula kuku? Una maana wananchi wote walioko kwenye majela ni kwa sababu hawakupewa malezi mazuri na wazazi wao? Mbona mkuu huna hoja?

8.

- Good point, sasa ilikuwaje ndugu wa pembeni wa Mwalimu wakalitumia jina na kutajirika wakati watoto wenyewe wakishindwa? Unasema hili ni kosa la Mwalimu? Utamlinganisha Bush aliyekua akimiliki timu ya Baseball ya Texas Rangers na watoto wa Mwalimu aliyekua hamiliki anything? Watoto wa Mwalimu walikwua na kila kitu on their hands ni matatizo yao wenyewe wakashindwa kutumia nafasi, DK. Hussein asingesota Turkey leo asingekua waziri period.

Respect.

FMES

Mkuu inabidi turudi kwenye darasa la ujamaa...Kwa taarifa yako ujamaa ulikuwa ni kama ugaidi kwa mataifa ya west,tena kipindi hicho ilikuwa worst kuliko sasa.
Mwalimu kama muumini wa ujamaa alipata shida hiyo,lakini cha msingi ni kwamba alipractice ujamaa,sasa kama matunda yake hayawezi kuoenekana hususan kutokana na familia yake na Taifa kwa ujumla then tunaweza tukawa tunajadili kwa ushabiki.
Ningependelea wataalam wa sociology watusaidie,wakisaidiwa na wa saikolojia....Sasa mkuu wewe ni bingwa wa kusema viongozi ni reflection ya sisi wananchi,sasa mkuu umesahahu kuwa ngazi ya mwanzo kabisa ya jamii ni familia?
Mkuu product ya generation inategemea sana na culture na norms jamii inazopractice na pia what the believe...Again rejea ujamaa.
Sitopenda kuendelea kulumbana kwasababu muda haupo...Hata hivyo napenda nikusisitizie kuwa mjadala huu ni mpana na ndio maana umefikia hapa ulipo,kuna issue ya kumtunukia mwalimu "Utakatifu" Kuna wanaosema he could have done better in regard to raising his own kids..Chini ya ujamaa hayo yote niliyoyataja huwa affected.
Mkuu hapo kwenye matumizi kwa kumalizia pia ni jambo la msingi. Ni wazi hakuwa na communication ya kutosha na watoto...Kwasababu kama ni mtoto anataka kuongea na baba yake mzazi labda kuhusu pocket money ya shule nk...Yani kweli aende akaongee na mtu mwingine we unaona hiyo sawa? Mtoto ni mtoto na sina shaka mwalimu alitaka ku watreat kama watanzania wengine tu,hilo linawezekana chini ya ujamaa,lakini consequences zake pia zipo...Kabla hatujaenda mbele zaidi ni muhimu tuakakumbushana maana halisi ya ujamaa.
Ahnsante.
 
Dilunga,
Nilikuwepo Butiama kwa siku sita za maombolezi kuelekea maziko ya Mwalimu. Si kweli kwamba kulikuwa na mfarakano wa mahali atakapozikwa...It was a foregone conclusion kuwa Mwalimu angezikwa Mwitongo.

Unasema ilikuwa inajulikana bila kupingwa kwamba Mwalimu atazikwa Mwitongo.

Mwitongo ni wapi?
 
duh! mbona tupo tulioishi hayo mazingira na sasa tunavinjari kwenye intaneti! au maana yake ni kwamba nilikuwa avereji na sasa nipo juu ya avereji lol

Naam, Mkuu. Umejitoa kwenye maisha ya mtanzania wa kawaida. Wewe ni above aveleji na una wajibu kuwasaidia uliowaacha nyuma yako! Tatizo ni kudhani kuwa kwa vile wote wametoka kama wewe na kupandisha kiwango cha average Tanzanian. Average Tanzanian bado ni maskini wa kutupwa!
 
Watoto wa Nyerere wameruhusiwa vipi kuingia air force wakati wana historia ya kuwa lunatics?

Unamchukua lunatic unamuweka kwenye mizinga na midege ya vita unategemea nini kitatokea kama siyo kummaliza kabisa kisaikolojia?

I am using the term lunatic in its medical dimension and not as a derogative one.

Walianza kuwa maluuni kabla au baada ya kujiunga na jeshi??
je kuna ushahidi kuwa huo uafriti wa akili walizaliwa nao au ndo zile fastresheni za maisha?? au ulitaka nao wangepewa chansi za kufungia ndoa zao ikulu au tungekuwa tunawaona wanapigana vikumbo na mafisadi kuwania tenda serikalini??
Nadhani tuwaache na maisha yao kwani kila mmoja wetu hapa anapaswa sasa kujifunza kuwa kuainisha anayoyaona na kuyafahamu ili kuzuia makosa yasitokee mbeleni.
Jenga familia yako kwani ukishupalia sana familia ya Mwalimu sidhani kama kuna faida yeyote unayovuna hapo au labda.....!
 
- Dosa Azizi aliyekuwa muanzilishi wa TAA ndiye aliyemuomba Mwalimu kushika usukani w a chama, na priviledges zake zikawa ni pamoja na kupewa nyumba, sasa unaona unachanganya priviledges za uongozi na kuomba ni vitu viwili tofauti, nyumba ya Mkapa kule Lushoto amejengewa na serikali kwa muijbu wa sheria sio ameomba.

Respect.

FMES. Haujajibu hoja. Dilunga anadai Mwalimu alisaidiwa nyumba na TANU mwaka 1974. Hili la TAA linatoka wapi? Waanzilishi wa TAA walikuwa Mzee Bin Sudi na Kleist Sykes katika miaka ya 1930s. Dossa Aziz,John Rupia, Abdulwahid Sukes ( aliyemtangulia Mwalimu katika urais wa TAA mwaka 1952) na Ally Sykes walikuwa wafadhili wakubwa wa TAA. Dossa Aziz aliinunulia TANU (sio TAA) gari lake la kwanza, Land Rover, ambayo mwalimu aliitumia kuzungukia nchi. Wakati wa TAA na miaka ya mwanzoni mwa TANU hawakuwa na hizi privileges unazodai. Kambona alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa TANU aliambiwa bayana kuwa mshahara wake utatokana na ada za wanachama. Nyumba ya Mwalimu ya Magomeni ilikuwa yake na hakupewa na mtu. Nyumba ya Msasani alijenga kwa mkopo. Mkopo ambao inadaiwa alisamehewa.

Mzee Dossa Aziz, huyu shujaa wa mapigano ya uhuru wetu, alikufa katika hali duni Mlandizi. Ni wengi tu kama yeye ambao taifa hili liliwasahau na linaendelea kuwasahau. Tunabaki kuwaenzi watoto na wake wa wale walioshika usukani tukisahau wale waliokuwa nyuma yao wakisukumiza gari ili lisikwame!

Nyumba ya Mkapa ya Lushoto ni ya kwake mwenyewe, hakujengewa na serikali. Aliyopewa na serikali kama stahili yake iko Masaki.

Amandla........
 
Yatasemwa mengi humu
Nabugia biwi la mahindi mkononi nina bilauri ya maji natizama hii muvi
 
- Ahsante kwa historia, lakini Mwalimu alipewa nyumba kama priviledge ya nafasi yake kikazi sio kuomba, Mwalimu alisindwa kuwaomba wa-German sasa leo itakuwaje awaombe TANU? Vipi ukiweka source za jinsi maelezo yote uliyoyatoa yalivyofanyika maana umeenda deep sana sasa hapo panahitajika source kwanza mkuu!

- Mkapa, aliikataa nyumba ya Masaki hivyo serikali ikajenga nyingine Lushoto, kama vile usalama ilivyoikataa ile ya Sea View, ulikuwa ni ushauri wa rafiki yake Ngwilizi ambaye sasa ni jirani yake kule Lushoto.

Unachanganya vitu tena. Baada ya uhuru TANU wasingeweza kumpa nyumba maana wakati ule chama na serikali vilikuwa kitu kimoja. Na Mwalimu asingeweza kuwaomba wajerumani maana alizaliwa baada ya utawala wao kuisha.

Source zangu ni humu humu kwenye mtandao. Google utapata habari zote.

Nyumba ya Lushoto Mkapa aliijenga kabla ya ile ya Masaki hata kufikiriwa. Nyumba ya Lushoto haikuwa mpya bali ilikuwa ni mabadiliko kwenye nyumba iliyokuwa kwenye shamba alilonunua. Serikali haikuhusika kabisa katika ukarabati na mabadiliko ya nyumba ile. Ni ya kwake in the full sense of the word.

Nyumba ya Masaki imejengwa baada ya yeye kustaafu. Hii ni mpya kabisa na hajaikataa.

Amandla..............
 
John jameni ni chapombe saana, anakunywa gongo kama hana akili nzuri, na that white thing in his head you call it brain, network ndivyo sivyo. Ila gongo mhh Butiama Msasani wanalijua hilo midomo myekunduuuuuuuuuuu
 
Mwalim was more than a politician, he was just a normal JOE. Mimi sikuwa kupata nafasi ya kumuona ana kwa ana. Lakini kadri nilivyokuwa nikikua niliona umuhimu wa kumjua mwalimu ni nani.

Nadhani Tanzania kuna kila haki ya kufanya intensive research about who is real Julius Nyerere. I spent more than 2 years collecting every peace that i can find ambazo zimetaja jina la mwalimu. I will tell you kwamba Mwalim was a leader, a father and motivated speaker. His Ghost will never go away.
 
Tofauti na ninavyosoma humu, nasikia wengi wa watoto wa Mwalimu walikuwa vitu wanavipata. Kuna kijana alisoma na Magige nae aliniambia kuwa alikuwa mkali darasani huko Chuo Kikuu. Rosemary nae hivyo hivyo. Na wale waliongea na John nae walikuwa wakimsifia uelewa wake. Kwenye mambo ya darasani, hawakupendelewa na mtu. Tusiwanyang'anye hata hiki kwa vile tu sasa hivi wako walipo! Wakali wengi mbona wanakuwa na personal issues. Maprofesa wangapi ni chapombe? Hii haiondoi ukali wao.

Amandla.......
 
acha kumtetea ni fisadi, anafanya kazi IMMA na cheo chake ni legal officer amepata wapi hela ya kunua hiyo BMW.
usione watu hawana akili humu ndani, you dont have to be a rocket scientiest .......

Jamani hee mtot wa muungwana alipiga deal la Deep Green na Mhe Masha hapo IMMMA sasa mgao hautoshi kupata BMW na nyingine kusomea Masters UK?
 
Unachanganya vitu tena. Baada ya uhuru TANU wasingeweza kumpa nyumba maana wakati ule chama na serikali vilikuwa kitu kimoja. Na Mwalimu asingeweza kuwaomba wajerumani maana alizaliwa baada ya utawala wao kuisha.

Source zangu ni humu humu kwenye mtandao. Google utapata habari zote.

Nyumba ya Lushoto Mkapa aliijenga kabla ya ile ya Masaki hata kufikiriwa. Nyumba ya Lushoto haikuwa mpya bali ilikuwa ni mabadiliko kwenye nyumba iliyokuwa kwenye shamba alilonunua. Serikali haikuhusika kabisa katika ukarabati na mabadiliko ya nyumba ile. Ni ya kwake in the full sense of the word.

Nyumba ya Masaki imejengwa baada ya yeye kustaafu. Hii ni mpya kabisa na hajaikataa.

Amandla..............

Mkuu kwenye hutuba yako moja. Mwalimu alisema kuwa alichukua mkopo kutoka NBC au benki ya nyumba (sikumbuki sawasawa ni benki gani) hili kujenga nyumba yake ya Msasani.

Lakini siku zilivyokuwa zinakwenda aliona kuwa kwa mshahara wake asingeweza kulipa.

Hivyo mwenyewe alikwenda benki na kuwaambia kuwa wachukue nyumba. Wakurugenzi wa Benki, wakaona si vizuri kwa mwasisi wa benki kunyang'anywa nyumba. Hivyo kwa lugha ya sasa wakam-bailout. Hiyo ndio source ya yeye kuwa na nyumba Msasani.

Kwa upande mmoja tunaweza kusema alikuwa mfuata maadili na kile alichosema.

Kwa upande mwingine anathibitisha fikra zangu sahihi kuwa UJAMAA SUCKS. Kiongozi ambaye sio aveleji katika mishahara na marupurupu kama atashindwa kulipa mikopo kutoka katika mabenki aliyoanzisha mwenyewe, je kabwela na mlalahoi anaweza vipi?
 
..Mkuu analisisi zako zinaniacha hoi kweli. unamulika pande zote za shilingi nakupa kudos
 
Unasema ilikuwa inajulikana bila kupingwa kwamba Mwalimu atazikwa Mwitongo.

Mwitongo ni wapi?
Mwitongo ni pale ambapo wamejenga nyumba mpya ya Mwalimu. Mwitongo ni pale ambapo wazazi wake Mwalimu wamezikwa. Mwitongo ni pale alipozikwa Mwalimu. The debate was whether to bury Mwalimu in Dar as some people had suggested. Mwalimu himself requested that he be buried in Mwitongo.
 
Mkuu kwenye hutuba yako moja. Mwalimu alisema kuwa alichukua mkopo kutoka NBC au benki ya nyumba (sikumbuki sawasawa ni benki gani) hili kujenga nyumba yake ya Msasani.

Lakini siku zilivyokuwa zinakwenda aliona kuwa kwa mshahara wake asingeweza kulipa.

Hivyo mwenyewe alikwenda benki na kuwaambia kuwa wachukue nyumba. Wakurugenzi wa Benki, wakaona si vizuri kwa mwasisi wa benki kunyang'anywa nyumba. Hivyo kwa lugha ya sasa wakam-bailout. Hiyo ndio source ya yeye kuwa na nyumba Msasani.

Kwa upande mmoja tunaweza kusema alikuwa mfuata maadili na kile alichosema.

Kwa upande mwingine anathibitisha fikra zangu sahihi kuwa UJAMAA SUCKS. Kiongozi ambaye sio aveleji katika mishahara na marupurupu kama atashindwa kulipa mikopo kutoka katika mabenki aliyoanzisha mwenyewe, je kabwela na mlalahoi anaweza vipi?

Lakini kweli Mwalimu aliamini kuwa wakati ule wa chama kimoja na hicho hicho kimeshika hatamu kuna mtu aliyekuwa na ubavu wa kunyang'anya nyumba yake? Au ilikuwa danganya toto tuu akijua kuwa watamsamehe tu?
 
Mwitongo ni pale ambapo wamejenga nyumba mpya ya Mwalimu. Mwitongo ni pale ambapo wazazi wake Mwalimu wamezikwa. Mwitongo ni pale alipozikwa Mwalimu. The debate was whether to bury Mwalimu in Dar as some people had suggested. Mwalimu himself requested that he be buried in Mwitongo.

Jasusi:

Naona tone yako imebadilika katika hii post (with an emphatic). Je wewe sio Godfrey Mwakikagile in disguise.
 
Jasusi:

Naona tone yako imebadilika katika hii post (with an emphatic). Je wewe sio Godfrey Mwakikagile in disguise.
kwi!kwi!kwi!
Mwakikagile is a friend of mine ingawa tumepoteana muda mrefu sasa. Kama unazo contacts zake nitapenda kuwasiliana naye.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom