Mkuu PM, samahani sana nilikuwa sijaiona hii topic, pole sana mkuu naona unabishana na wasioelewa vizuri ukweli,
- Ni kwamba Mwalimu aliwapeleka watoto wake shule kama vile wazazi wetu, sasa kilichojalisha zaidi ilikuwa either akili ya maisha au ya shule, watoto wa Mwalimu hawakuwa na vyote sio siri kwa wale tunaowafahamu, sasa what else Mwalimu alitakiwa kufanya? Hivi unafikiri DK. Hussein asingesota na shule kule Turkey sasa hivi angekua waziri? Hivi unajua maisha ya Turkey yalivyo mkuu kwa mtoto wa rais kusoma kule mpaka kua Doctor?
- Hebu tizama watoto wa Joseph, yaani Matare na Milton, hawa walikuwa na akili ya shule na maisha pia, sasa hivi hawalali njaa na wala hawana shida, pamoja na kwamba wao ni Joseph tu, sasa ndio iwe Mwalimu?
- Watoto wa Mwalimu ni wa kulaumiwa wenyewe and they know that, wewe tizama mtu kama Magambo alivyotajirika kwa jina la Mwalimu na ni ndugu tu, the real Mwalimus wanasota eti wa kulaumu ni Mwalimu? Steven Kiboko anakula kuku ile mbaya tena longtime, na yeye ni Kiboko tu sasa ndio iwe watoto wa Mwalimu?
Mwalimu kwenye watoto wake hana lawama kabisaa, ni noma lao wenyewe!
FMES!