Andrew Nyerere on Mwalimu humble children!

Andrew Nyerere on Mwalimu humble children!

Na Mwalimu asingeweza kuwaomba wajerumani maana alizaliwa baada ya utawala wao kuisha.

Hiyo kali. Naona huyu mtu aliteleza kidogo, au alipindisha habari makusudi. Juzi kadai watumwa walikuwa wanafungiwa kwenye mabweni mashambani halafu wanasikilizwa wakibishana kuhusu ni nani ambae mwinyi wake ana mali nyingi zaidi. Nimemkumbusha kwamba hili jamvi lina wanachama elfu nane. Utakamata elfu saba mia tisa tisini, lakini kuna wengine watashtuka unapoleta tenzi zako.

Tuachane nae. Historia ya TAA, TANU, Nyerere na Ukoloni ulotoa ni nzuri sana, shukrani.

Kuhusu nyumba ya Msasani, nilitaka kuongeza kitu kimoja kuhusu "msamaha" wa ule mkopo. Kilichofanyika ni kwamba, alipostaafu mwaka 1985 akaigawa ile nyumba kwa serikali, lakini akawaambia hii nyumba ina deni. Serikali ikachukua, ikalilipa lile deni, ikaikarabati, ikamrudishia. Nyerere akapokea.

Sasa, Nyerere hakuwa tapeli mjanja mjanja. Hili dili ni safi, nina hakika. Lakini kwa nchi za Magharibi ambapo Mbunge akipewa kazawadi ka kupakiwa rangi nyumba bure ( Alaska ) au kupewa msaada wa lifti ya kuendeshwa kwenye taxi bubu bure ( Dakota Kusini) itabidi mpaka wakusanya kodi wajue, umeokoa kiasi gani kwenye hiyo misaada manake ni kama mapato. Katika nchi ya "kinoko" kama hiyo, ndugu yetu Nyerere angeambiwa, wait a minute now Mister Integrity, say that again, you gave the house away, got the mortgage paid off, by public money, then got the house kicked back to you, took it with clean deed. Who authorized the goverment payoff, from what funds, whose budget allocation? That's not fishy to you? Geraaare here...

Kwa viwango vyetu Nyerere ni "mtakatifu." Kwingine, anaweza kuwa sio. Magharibi ambapo toka mdogo nilikuwa nasikia huko kwa wadhungu ni Sodoma na Gomora, hakuna maadili, hakuna utu. Uhuni mtupu. Ufisadi na machukizo. Sisi ndio tunajisifu tuna maadili ya Kiafrika. Wanasema, nenda kafikiri zaidi, go figure.

Nyerere alimiliki, alijenga, alipewa misaada ya majumba yanafika matano. Jana Warioba alihojiwa na waandishi wakati wa mhadhara wa Soyinka Chuo Kikuu, amenukuliwa akisema Nyerere alikufa na nyumba moja tu ya kujengewa na Chama. Si sahihi. Tena Warioba ni mtoto wa kisiasa wa Nyerere, angejua ukweli. Nyerere alikuwa na majumba, alimiliki matreka mengi kuliko mmoja wa wenye mashamba makubwa kuliko wote Afrika, Olusegun Obasanjo. Warioba anajiweka kama hajui haya, hajali hajali facts, jaji wa kimataifa.

Southern African Research and Documentation Centre
28 October 1999


He called in his commercial bank manager and asked for a loan. Nyerere later nationalised the bank but kept up his payments. When he retired as Tanzania's first President in 1985, he gave the Msasani house he had built to the state. He waived all the payments he had made leaving the state with the balance. Somewhat to his chagrin, the state paid off the mortgage and gave him the house back; including all the upkeep costs that went with it.

Whenever he could, Nyerere went back to his village. There he had a farm - of sorts. Olusegun Obasanjo, then a farmer and now Nigeria's President, once observed that although Nyerere had more tractors than he did, the Tanzanian would never be a commercial farmer.

October 29, 1999
The East African.
By Mike Okema

Of the four houses he possessed - one in Msasani, Dar-es-Salaam and three in Butiama, his native village - two were gifts. He built the first house before joining politics. In 1974, the party decided the house was no longer worthy of his status and built him another one.

On April 13, 1999, which was taken to be Mwalimu's 77th birthday, the army gave him another house in Butiama as a birthday present, mainly because his library was getting larger by the day and there was no longer enough space in his Butiama village houses for his books.

IPP MEDIA
July 19th, 2007
By Pascal Shao
and Beatha Hyera


Speaking on behalf of her mother, Mama Maria Nyerere at the late walimu's residence in Msasani in the city yesterday Makongoro Nyerere said that the house his father lived in [at Magomeni] was owned by the colonial government and that his late father was only a tenant.

Makongoro said that in 1959, the late Nyerere built his own house next to the disputed one where he lived in for a period of six months before shifting to another government house located at Sea View also in the city.

He sold the house he had built at Magomeni to Ambassador Mzee ibandebage. Therefore the family has no claim on any of the two houses, including the one at Maduka Sita, he clarified.
 
Lakini kweli Mwalimu aliamini kuwa wakati ule wa chama kimoja na hicho hicho kimeshika hatamu kuna mtu aliyekuwa na ubavu wa kunyang'anya nyumba yake? Au ilikuwa danganya toto tuu akijua kuwa watamsamehe tu?

Duuuh,

Nimebandika tundiko langu, nikakuta na wewe ushabandika hicho kitu hapo, tena inaonekana kama mwanzo wala ulikuwa hujui undani wa lile dili la ule msamaha, na bado ukaweza kufikiria hicho kitu. Kwamba msamaha ulikuwa kama umeshajulikana toka awali, kama umepangwa hivi.

Duu, nilichoandika na mimi ni kama hicho hicho, kwamba kwa wengine, ule msamaha unaweza kuonekana ni danganya toto kukwepa deni. Aligawa nyumba kwa serikali, ikalipiwa deni, akarudishiwa, akapokea. Mtakatifu.
 
Lakini kweli Mwalimu aliamini kuwa wakati ule wa chama kimoja na hicho hicho kimeshika hatamu kuna mtu aliyekuwa na ubavu wa kunyang'anya nyumba yake? Au ilikuwa danganya toto tuu akijua kuwa watamsamehe tu?

FM

Msamaha ungekuwa unatokea hata kwa watu aveleji, basi kusingekuwa na matatizo. Lakini wanakijiji wa Mvomero wakishindwa kulipa trekta, mashamba yao yanauzwa. Na mnunuzi ni Sumaye.
 
Asante Dilunga kwa ufafanuzi. Hayo ya nyumba ya Magomeni sikuyajua wala hilo la kujengewa nyumba na TANU mwaka 1974. Alijengewa wapi maana zaidi ya ile ya Magomeni, Msasani na Butiama hamna nyingine inayotajwa tajwa! Hiyo nyumba ya TANU ilijengwa Dar es Salaam au Butiama? Au ndiyo ile ya Butiama tunayoijua?

Amandla........
 
FM

Msamaha ungekuwa unatokea hata kwa watu aveleji, basi kusingekuwa na matatizo. Lakini wanakijiji wa Mvomero wakishindwa kulipa trekta, mashamba yao yanauzwa. Na mnunuzi ni Sumaye.


Hivi hii ni kweli? Sumaye aliyekuwa PM ndie aliyenunua? Ndiyo maana watu aveleji wanakimbilia DECI!
 
Dilunga,
Ile nyumba ya Magomeni TANU iliinunua kutoka kwa balozi Tibandebage. Bado ipo pale kama mali ya CCM. Nadhani wanataka kuifanya kama ukumbusho. Ile ya Msasani, ingawa serikali ilimrudishia, Mwalimu aliasa kuwa ataitumia mama Maria and when she is gone it will revert to govt ownership. Kuna mpango wa kuifanya museum of some sort.
 
kwi!kwi!kwi!
Mwakikagile is a friend of mine ingawa tumepoteana muda mrefu sasa. Kama unazo contacts zake nitapenda kuwasiliana naye.

Mkuu sina contacts zake na wala simjuhi. Lakini, nilisoma excerpts zake kuhusu kitabu alichoandika kuhusu Nyerere. Kutokana na posti zako nikawa naunganisha dots. Unajua tena profiling.

Kwikwikwi
 
Hivi hii ni kweli? Sumaye aliyekuwa PM ndie aliyenunua? Ndiyo maana watu aveleji wanakimbilia DECI![/SIZE][/FONT]


Kama kumbukumbu zangu zitakuwa bado ni nzuri, hii ni kweli. Na Lowasa naye kanunua Ranch ya Mkata. Ranch hii haikutoa manufaa kwa taifa lakini wafugaji wa Kimasai waliruhusiwa kuishi na kuitumia.

Ranch sasa imepigwa uzio na wamasai wamefukuzwa. Kuchunga kwao mifugo ni trespass katika private property.
 
Dilunga,
Ile nyumba ya Magomeni TANU iliinunua kutoka kwa balozi Tibandebage. Bado ipo pale kama mali ya CCM. Nadhani wanataka kuifanya kama ukumbusho. Ile ya Msasani, ingawa serikali ilimrudishia, Mwalimu aliasa kuwa ataitumia mama Maria and when she is gone it will revert to govt ownership. Kuna mpango wa kuifanya museum of some sort.

Asante, Mkuu. Sasa ni nyumba ipi ya Magomeni iliyouzwa kwa jamaa anaekusudia kuibomoa na kujenga ghorofa? Au ndiyo mambo ya redio mbao tena?

Hayo ya Msasani, ndugu na jamaa wanayajua? Title iko kwa nani? Itakuwa heri kama aliandika hivyo ama sivyo huko mbeleni patatokea ugomvi tu!
 
Asante, Mkuu. Sasa ni nyumba ipi ya Magomeni iliyouzwa kwa jamaa anaekusudia kuibomoa na kujenga ghorofa? Au ndiyo mambo ya redio mbao tena?

Hayo ya Msasani, ndugu na jamaa wanayajua? Title iko kwa nani? Itakuwa heri kama aliandika hivyo ama sivyo huko mbeleni patatokea ugomvi tu!
Nijuavyo Magomeni Mwalimu alikuwa na nyumba moja tu. Labda hiyo wanayosema ni ile aliyopangisha kabla ya nyumba yake kumalizika. Na kuhusu nyumba ya Msasani wana familia wanajua hilo. Kuna wakati Rose Nyerere alifuatana na waziri mmoja (nimemsahau jina) walitembelea majumba ya marais wa zamani kama vile jumba la Jefferson na Washington pale Mt. Vernon kuona jinsi yanavyotunzwa na serikali. Kwa hiyo hilo linajulikana.
 
Ninavyojua Mwitongo ni makazi ya Mwalimu pale Butiama.

Mwitongo ni pale ambapo wamejenga nyumba mpya ya Mwalimu. Mwitongo ni pale ambapo wazazi wake Mwalimu wamezikwa. Mwitongo ni pale alipozikwa Mwalimu. The debate was whether to bury Mwalimu in Dar as some people had suggested. Mwalimu himself requested that he be buried in Mwitongo.


Nyerere hakuwahi kusema azikwe wapi. Na hakuna sehemu inaitwa Mwitongo.

Sio hapa tu, ila nimeona na sehemu nyingine pia kama kwa Michuzi, anasema Madaraka alimkaribisha mgeni wake Jaffar Amini nyumbani, akapigwa picha wanakula kwa kina Madaraka, Mwitongo. Upotoshaji. Dunia inajua Nyerere alizikwa Butiama, sio Mwitongo, hakuna Mwitongo.

Kwa jiografia ya Tanzania, kijiji ndio kisehemu cha mwisho kabisa katika ngazi ya mpangilio wa mahala za dunia ya Tanzania, zaidi ya mtaa. You don't get any more local than kijiji, other than mtaa, kama kijiji kina mitaa. Ukoo, familia, jamaa ni unit ndogo kuliko kijiji lakini hayo ni mahusiano, sio jiografia.

Jasusi, ukisema ilikuwa inajulikana kwamba Mwalimu atazikwa Mwitongo unakuwa kama huelewi maana ya Mwitongo. Kana kwamba kuna sehemu inaitwa Mwitongo ndani ya Butima. La hasha.

Mwitongo, kwa watu wa kule, ni kwenye "tongo," neno la lugha ya watu wale, ikamaanisha makazi, mahame, mahala, nyumba ulipozaliwa haswa haswa na ambapo unategemewa kuzikwa. Mwitongo ni ujumla wa "yika," nyumbani, na makaburi, "mbihira." Nyumbani kwao, pembeni ya makaburi wanapolazwa na babu zao ndio mwitongo. Kila mtu, kila, kila familia, kila ukoo, una tongo lake. Hakuna sehemu inaitwa Mwitongo, Butiama. Again, kwenye jiografia ya Tanzania, you don't get any more local than Kijiji, zaidi ya mtaa, kama kijiji kina mitaa.

Neno mwitongo lilikua sana baada ya kuanzishwa vijiji vya Ujamaa ambapo watu walihamishiwa "mjini," kwenye vijiji vya ujamaa. Mkitaka kutembelea kule mlikofukuzwa na serikali, kwenye mahame, mlipozaliwa, walikolaza mifupa ya babu zenu wanasema tunakwenda kwenye tongo, mwi-tongo, mwitongo. Kwa Butiama, kijiji cha ujamaa kilikuwa hapo hapo Butiama. Watyama hawakuhamishwa. Matongo yao yapo hapo hapo. Tongo ni ujumla wa eneo lililozungukwa na nyumba, kiwanja, makaburi, bustani, ua.

Mtafaruku wa mazishi ya Nyerere ulihusiana na sehemu ya kumzika Nyerere ndani ya maeneo hayo ya kwao. Ilijulikana atazikwa Mwitongo, unasema. Mwitongo wapi?

Ni hivi. Kuna waliotaka alale na baba yake, pembeni ya kaburi la Babu Burito. Na kuna waliotaka alazwe nyuma ya nyumba yake. Kwa watu wa kule, Jasusi sikiliza vizuri hapa, maana umenisikitisha, nilikuchulia wewe una undani mwingi wa Nyerere, mpaka kumzika ulimzika, ukakaa Butiama siku sita unalia machozi, lakini unalegalega na details za mila za tongo, umeni dissapoint vibaya mno. Katika mila za watu wa kule, mtu akifa kama alikuwa na nyumba, anazikwa kwake. Hivyo, kundi moja la mfarakano likapinga Nyerere kuzikwa pembeni ya kaburi la Babu Burito, maana Nyerere ana kwake. Azikwe nyuma ya nyumba yake, kwake.

Serikali ikaingilia kati. Waziri Kimiti akiwa mwenyekiti wa kamati ya mazishi, (sio mwakilishi wa Mkapa, kama alivyo potosha yule mleta nyeti Field Marshall, aliyedai kwamba watwana walikuwa wanafungiwa mabwenini mashambani kusikilizwa wanabishana kuhusu mali za mabwana wao) Waziri Kimiti akaingilia kati, na hatimae Mwalimu Nyerere akazikwa mbele ya nyumba yake.

Hizi sehemu zote ni mwitongo. Huwezi kusema "it was a foregone conclusion kwamba atazikwa Mwitongo." Mwitongo wapi? Nyumba ya nyumba yako, pembeni ya kaburi la baba yako, mbele ya nyumba, katikati ya kaburi la Mama na kaka yako, ndani ya nyumba yenu, kote humo ni mwitongo. Sasa ukisema "ilijulikana atazikwa Mwitongo," mwitongo wapi?

Baadaa ya msuguano wa kifamilia ulioingiliwa na serikali, Julius Nyerere alizikwa kijijiji cha Butiama, kata ya Butiama, wilaya ya Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara, nchini Tanzania.

The East African.
October 29, 1999
By Mike Okema


Makongoro has acted as the family spokesman ever since his father was taken ill. He has, however, made it clear to the press that he is not the new chief of the clan, pointing out that he is only the fifth child.

This lack of leadership has affected the whole funeral procedure. Tanzanians had taken it for granted that Mwalimu's funeral and burial would be public, not private, and it was generally assumed he would be buried somewhere in Dar-es-Salaam or Dodoma, the new capital. Mwalimu had not indicated where he wanted his final resting place to be. So his relatives argued that since, upon retirement, Mwalimu had returned to his native village, he would have preferred a private burial in Butiama.

Within the clan, there was another wrangle going on as to the exact spot where Mwalimu would be buried. Elders, led by Chief Wanzagi, wanted Nyerere to be laid to rest next to his parents. Emil Magige, Nyerere's son, on the other hand wanted his father to have the back of the new house for a resting place. Digging the grave was thus delayed for a few days.

It took the intervention of the Minister for Labour and Youth Development, Paul Kimiti, in his capacity as a member of the official burial committee, to strike a compromise: Nyerere was to be buried in front of the new house where his statue stands.

It would be idle to ponder what Nyerere himself would have preferred.
 
Last edited:
Dilunga unatisha! Kumbe Mwitongo ni generic term na si sehemu particular! Mimi kila siku nilikuwa nadhani Mwitongo ni jina lililopewa mahali alipojenga Mwalimu. Kwamba ilikuwa particular to the place yaani hakuna Mwitongo nyingine. Sasa unatuambia kuwa sote tuna Mwitongo zetu, kule tulikotokea, walikozikwa waliotutangulia katika ukoo!

Asante kwa shule. Ila usimlaumu Jasusi maana naamini alisema in good faith. Pengine yeye naye ni mgeni kwa hiyo maana ya neno hilo lilimpiga chenga. In his defense, sijawahi kumsikia akitumia uongo au upotoshaji ili ashinde argument. Naamini kabisa amesema anayoamini na anayojua. Pengine na yeye ana tafsiri nyingine ya neno hili " Mwitongo".

Asanteni wote wawili kwa shule.

Amandla...........
 
Fundi Mchundo said:
Asante kwa shule. Ila usimlaumu Jasusi maana naamini alisema in good faith. Pengine yeye naye ni mgeni kwa hiyo maana ya neno hilo lilimpiga chenga. In his defense, sijawahi kumsikia akitumia uongo au upotoshaji ili ashinde argument. Naamini kabisa amesema anayoamini na anayojua. Pengine na yeye ana tafsiri nyingine ya neno hili " Mwitongo".

Asanteni wote wawili kwa shule.

Fundi,

..hata mimi namheshimu sana Jasusi.

..pia namshukuru sana Dilunga kwa maelezo yake kuhusu neno Mwitongo.

..nadhani itakuwa vizuri kama Jasusi atatueleza alikuwa akimaanisha Mwitongo ipi, maana ziko nyingi hizi.
 
Wakati sisi na wanafunzi wengine wa Mkwawa tuliongeza hela ili tupande basi kutoka Iringa kwenda Dar moja kwa moja (mwaka 1970) wakati wa likizo ya shule, Andrew Nyerere aliendelea kutumia safari warrant ya shule ambaye ililazimisha wanafunzi kwenda na basi mpaka Dodoma na kuendelea na safari ya treni katika 3rd class kwenda Dar.
 
attachment.php

Hivi hawa wote ni watoto wa mwalimu? kumbe ana watoto wengi

Mnaweza kuwataja......
 

Attachments

  • family nyerere..jpg
    family nyerere..jpg
    29.4 KB · Views: 247
Fundi Mchundo,
Pale ilipojengwa nyumba mpya ya Mwalimu panaitwa Mwitongo. Mwitongo kwa Wazanaki ni eneo la mazishi. Zamani Wazanaki walikuwa na tabia ya kuzika mtu na kuhama. Mwitongo ni mahali walipozikwa wazazi wake Mwalimu. Yeye alikataa kuhama. Hata kina Madaraka wanapaita pale Mwitongo.
 

Sasa akili zetu zimekumbwa na agenda za uzazi wa mpango! Kumbe tatizo ni uzalishaji mali na uchumi mbovu!

Heshima mbele kwa wanaoendelea kuzaa watoto zaidi ya watatu maana miaka ya mbele watu watakuwa ni rasilimali muhimu katika uchumi hasa kwa africa.
 
Mwitongo kwa Wazanaki ni eneo la mazishi.

Kumbe unajua. Ndio maana, kabla sijakukurupukia, nikakuuliza, Mwitongo ni wapi? Jibu lako likalenga kuonyesha kwamba kuna mahala halisi panaitwa Mwitongo alipozikwa Nyerere. Sasa hivi unakuja na jibu bora zaidi. Nilijua unajua, na nasumbuliwa sana na mtu kulegalega na facts ambazo anazijua au anatakiwa azijue. Kama Warioba kudai jana kwamba Nyerere alikufa na nyumba moja, thenashara wa Nyerere unapindisha nyeti za Nyerere.


In his defense, sijawahi kumsikia akitumia uongo au upotoshaji ili ashinde argument.
..hata mimi namheshimu sana Jasusi.

Nimelisoma hili jamvi muda mrefu, hakuna mtu mstaarabu humu ndani kama huyo Jasusi, pembeni yako mtaua Jokakuu, nawe Fundi Mchundo. Jasusi ninamheshimu sana. Tena, ili mtu yeyote aweze kutathmini au kuhukumu wastaarabu kama ninavyojifanyisha hapa, inabidi na yeye awe na ustaarab, kitu ambacho mimi sina, siwezi kufunga kamba za viatu vyenu, najua.

Sasa basi, japokuwa nina mapungufu ya ustaarabu (majuzi nimeripotiwa kwa kumtukana Mzungu Koko mmoja humu anaekuja kutukana watu weusi halafu tanaambiwa tumtafsirie lugha yetu ya Kiswahili, na ninatubu), japo mimi mwenyewe sio Gabrieli wa Bwana, lakini hapa sikukurupuka kumshutumu Jasusi kwa uongo. Hana kawaida ya uongo, sijamwona. Isitoshe si wengi wanaongopa humu jamvini, zaidi ya wahalifu waleta nyeti sugu fulani fulani mmoja, wawili, kama wote wawili si taswira ya mmoja huyo huyo, au tunajua ni huyo huyo, ila stahi yetu inatufanya tujifanyishe hatujui, na yeye anajua tunamjua, ila kwa usahihi wa kisiasa tunasema tunawajua, badala ya tunamjua. Simuongelei Jasusi.

Ila, tukirudi kwa Nyerere, mwitongo na Jasusi, Jasusi aliombwa aeleze maana ya mwitongo, akaiweka kama ni neno la ki Nyerere, Nyerere hivi. Kumbe maelezo bora zaidi anayajua, kayaleta baadae.

Sasa Jokakuu na Fundi Mchundo msianze kumsafisha Jasusi. Hahahahaaaaaaaaaaa


Sasa unatuambia kuwa sote tuna Mwitongo zetu, kule tulikotokea, walikozikwa waliotutangulia katika ukoo!

Fundi Mchundo, wa kwanza kati ya walio sawa.

Si wote wanaweza kusema wana mwitongo yao. Ukizaliwa hospitali, ukakulia mbali na matongo ya babu zako, ukaishi kwenye sehemu zenye mitandao na nishati, ukifa unaweza kuzikwa Kinondoni makaburini, sio mwitongo. Hukuzaliwa kwenye tongo, hukukulia kwenye tongo, hukurudi kwenye tongo, hukumiliki eneo kwenye tongo, hukufia kwenye tongo, hukuwa na chako kwenu. Huna mwitongo.

Baba wa Taifa inabidi tuzidi kumchambua. Tumjue zaidi. Tukisema ni Mtakatifu na madhambi yake tuyaseme pia, kama mwenye madhambi anaweza kuwa mtakatifu. Wengine tunaposema Nyerere katenda ovu hili na lile, sio kwamba hatumfahamu, au tumekosa leo hela ya pombe tukaanza kulaumu Ujamaa wa Nyerere na vizuizi vya mateso vya Nyerere. La hasha. Tena kuna wengine tunajaribu kuwa na uhuru wa uwiano wa mawazo (objectivity) kiasi cha kusema inawezekana zile jela za mateso, vile vifungo vya majasusi wa Nyerere kuminya kende za wapinzani wa Nyerere mpaka wafe, inawezekana vile vifo ndio vilifanya nchi iwe na amani. Ni halali kutesa watano kutunza amani ya tisini na tano? Ni swali la siku nyingine.
 
Last edited:


Unachanganya vitu tena. Baada ya uhuru TANU wasingeweza kumpa nyumba maana wakati ule chama na serikali vilikuwa kitu kimoja. Na Mwalimu asingeweza kuwaomba wajerumani maana alizaliwa baada ya utawala wao kuisha.

Source zangu ni humu humu kwenye mtandao. Google utapata habari zote.

Nyumba ya Lushoto Mkapa aliijenga kabla ya ile ya Masaki hata kufikiriwa. Nyumba ya Lushoto haikuwa mpya bali ilikuwa ni mabadiliko kwenye nyumba iliyokuwa kwenye shamba alilonunua. Serikali haikuhusika kabisa katika ukarabati na mabadiliko ya nyumba ile. Ni ya kwake in the full sense of the word.

Nyumba ya Masaki imejengwa baada ya yeye kustaafu. Hii ni mpya kabisa na hajaikataa.

Amandla..............

- Mkuu Fundi ahsante sana kwa ufahamisho wako kwamba source yako ni humu humu Google, sina la kuongeza zaidi mkuu, labda kidogo tu!.

FMES!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom