Sijui ni picha gani inayozungumziwa hapo. Lakini kama ni ile ya zamani iliyopigwa katika viwanja vya Ikulu, Manyerere hakuwepo pale,ambapo Madaraka alikuwa amepakatwa, Manyerere alikuwa hajazaliwa. Mambo mawili watu wanapaswa kujua kuhusu John. Kwanza ni jinsi alivyofukuzwa shule Mazengo Dodoma. Yeye na wenzake watatu waligombana na mlevi mmoja mjini Dodoma. Wakampiga,yule baadaye,akafa. Kwa hiyo manslaughter wakafukuzwa shule. Jambo la pili ni jinsi alivyokuwa anaishi Ikulu baada ya kufukuzwa shule. Siku moja usiku alimleta msichana kutaka aingie naye ndani. Mlinzi wa Usalama wa Taifa akamzuia. John akajaribu kupanda ukuta aingie,akateleza,akaanguka. Kama umeiöna Ikulu,kutoka ghorofa ya kwanza akaanguka kwenye sakafu. Jambo la tatu ni jinsi alivyougua. Muda aliougua ni takriban nusu ya maisha yake. Halafu,it gets worse, John amefukuzwa shule,amekwenda Air Force,alipofika. Ngerengere Air Force Base,. C. O., Commanding Officer,alikuwa ndugu yake yule headmaster aliyemfukuza Mazengo.