kwi!kwi!kwi!
Mwakikagile is a friend of mine ingawa tumepoteana muda mrefu sasa. Kama unazo contacts zake nitapenda kuwasiliana naye.
Jasusi,
Kama ulivyosema, ulisoma shule H.H. The Aga Khan (Tambaza) kabla ya mimi na wanafunzi wenzangu kama kina George Mazula (marehemu), Andrew Nyerere, Mohammed Chande Othman (High Court Judge), Msafiri Abdallah, Godfrey Mwakikagile, Celestine Mwinula, Walter Mallya (kaka ya High Court Judge Willie Mallya), Rashid Hemed (mwanasheria)i, James Maugo (pia mwanasheria), Balinagwe Mwambungu, Hamisi Kasanga, Abdallah Yakuti, Geoffrey Mbogo, Suleiman Kazema, Mlozi, Chinja, Omari Mangosongo, Dodo Dafi, Swai, Nkya, wasichana na classmate wangu Pili (kutoka Tabora) na Flora (kutoka Handeni), msichana mwingine Tecla Chando (kutoka Moshi) na wengineo hatujaenda hapo.
Kwa sababu ulitutangulia pale Tambaza, unawafahamu kina Juma Penza na Reginald Mhango? Wao pia wlisoma shule Aga Khan (Tambaza) kabla ya sisi, na nimeambiwa kwamba ni marafiki sana wa Godfrey Mwakikagile. Pia walifanya kazi pamoja na Godfrey Mwakikagile kama waandishi wa habari pale Daily News kati ya 1969 na 1972 mwaka ambao Mwakikagile aliondoka kwenda shule USA. Kama wanavyojua, Godfrey alianza kufanya kazi pale gazetini alipokuwa bado mwanafunzi Tambaza, Form V, wakati wa likizo, mwezi wa June. Namkumbuka sana kwa sababu alikuwa ni classmate wangu na tuliishi pamoja pale H.H. The Aga Khan Hostel 1969 - 1970.
Nimewataja hao wawili, Juma Penza ambaye baadaye akawa national publicity secretary wa chama cha utawala CCM (pamoja na Paul Sozigwa), halafu director wa Radio Uhuru, na Reginald Mhango ambaye alikuwa editor wa Daily News na baadaye managing editor wa Guardian (na kazi zingine serikalini) kwa sababu wanaweza kukusaidia kuwasiliana na Godfrey Mwakikagile.
Pia muulize Charles Kizigha, Daily News, na Kassim Mpenda, Director of Information Services, Ministry of Information, ambao walifanya kazi pamoja na Mwakikagile kama news reporters pale Daily News pamoja na Juma Penza na Reginald Mhango na wengineo. Hao wawili, Kizigha na Mpenda, walikuwa na mawasiliano na Mwakikagile kupitia kwa Andrew Nyerere miaka ya karibuni. Unaweza kuwauliza kuthibitisha jambo hilo. Nina uhakika kwa sababu nilikuwa na Andrew Nyerere kwa muda mrefu Dar es Salaam Godfrey Mwakikagile alipokuwa anaandika kitabu kuhusu Mwalimu, "Nyerere and Africa: End of an Era." Andrew aliwasiliana na Mwakikagile kwa muda mrefu kati ya 1999 na 2004 alipokuwa anaandika kitabu hicho na kabla ya second edition kuchapishwa mwanzoni mwa 2005. Edition ya kwanza ilichapishwa 2002, ya pili 2005, ya tatu 2006, na ya nne 2008.
Godfrey alimwambia Andrew aende kwa Kizigha na Mpenda ili wamtafutie picha anazohitaji kitabuni. Andrew alikwenda kuonana na Kizigha na Mpenda kwa niaba ya Mwakikagile kuhusu project hiyo ili wamtumie Godfrey picha mbali mbali za Mwalimu. Andrew alipewa picha hizo kutoka kwenye archives na alimtumia Godfrey pamoja na picha chache kutoka nyumbani kwa Mwalimu ili azitumie katika kitabu alichokuwa anaandika na ambamo amemtaja Kizigha na Mpenda na kuwapa shukrani kwa msaada wao ingawa amesema pia hakuweza kuzitumia picha zote katika kitabu hicho. Na Andrew aliwahi kuniambia kwamba anawasiliana na Godfrey Mwakikagile kwa email na simu nyakati hizo. Pia barua za mawasiliano hayo ziko katika kitabu hicho ambacho kwa sasa kimesomwa na watu mbali mbali pamoja na Watanzania kama Mzee Butiku na Salim Ahmed Salim kama inavyoelezwa kitabuni kutokana na mawasiliano kati ya Andrew na Godfrey. Hivi sasa nasoma Fourth Edition ya kitabu hicho, 740 pages, and I'm really plodding through since it's a tome with small print (font size 10). Ingekuwa print ya kawaida ( 12 point font size), kitabu hicho kingekuwa zaidi ya 1,000 pages.
Ningeweza kumuuliza Andrew kama anaweza kukupa contact za Mwakikagile lakini kutokana na hali yake, haiwezekani. Na sijamwona Dar kwa muda mrefu. Kwahiyo jaribu kuwauliza kina Juma Penza, Reginald Mhango, Charles Kizigha na Kassim Mpenda. Inawezekana watakusaidia kuwasiliana na rafiki yako huyo.
Kwa upande wangu, nitajaribu kukusaidia kwa sababu Mwakikagile na mimi tuna mutual friend, Professor Emmanuel Sendezera, Physics, kule Afrika Kusini. Amewasiliana na Mwakikagile kwa miaka mingi tangu walipokuwa pamoja USA - walisoma shule pamoja USA - na ninadhani bado anawasiliana naye hata sasa. Kuna wakati aliniambia kuna Mtanzania anayemfahamu sana ambaye ameandika vitabu, na aliponiambia jina, nilimwambia kwamba Godfrey Mwakikagile alikuwa ni classmate wangu Tanzania. Mimi pia bado nawasiliana na Sendezera. Alikuwa head of Physics Department, University of Malawi, na pia alifundisha Wits (University of Witwatersrand) na vyuo vikuu vingine kule South Africa. Na bado anafundisha huko. Yuko KwaZulu/Natal sasa. Nitamuuliza kama anaweza kunipa contact hizo na nitakujilisha kwa njia ya private message.