ndugu zangu,
..binafsi nimem-criticize Mwalimu sana tu kutokana na utekelezaji wake wa sera mbalimbali Tanzania. nasisitiza utekelezaji. lakini kuanza kumkosoa kwasababu wanawe wako hivi au vile nadhani tumekwenda mbali kidogo.
Shwari,
..inawezekana kuna mtoto wa Mwalimu, siyo Andrew Nyerere, aliyesoma sekondari Mkwawa.
..halafu mbona urafiki wako na Andrew Nyerere ulikuwa wa michezo-michezo tu? unasimulia mlivyokuwa mkipanda juu ya dari, ua kwenda baharini, au kusikiliza redio. when were you guyz studying, if you did at all?
..sasa na nyinyi mnaomsimanga Mwalimu kwa malezi ya watoto wake nadhani mmeusoma vizuri ushuhuda wa Shwari. Mwalimu kapeleka mwanae akasome, kina Shwari wanampandisha juu ya dari, na kumpeleka baharini kupunga upepo.
..mara nyingine wazazi wanajitahidi kwelikweli, lakini watoto nao wanakwenda wanapata waalimu wengine mitaani.