Anayewadhalilisha Walimu ni matendo ya baadhi ya walimu wao wenyewe

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Itoshe kusema kada ya walimu imeingiliwa na mamluki!

Zamani ilikuwa rahisi sana kuwachambua walimu kwenye kundi la watu pasipo hata kujitambulisha, lakini sasa hivi kwenye kikundi cha watu mtaani wakichanganyika wa kike na kiume huwezi kutofauti uvaaji wa mwalimu na muimba singeli, wote utawaona wameshikilia dera, kofia za kitozi, mavazi ya kitozi, maongezi ya kihuni huni, umbeya ndio usiseme n.k. Hapo zamani mwalimu alitambulika kuanzia staha ya mavazi hadi uongeaji wa hekima.

Tabia za ajabu mashuleni

1. Ni kawaida sana sasa hivi kuambiwa mwalimu fulani huwa anatuuzia visheti na vipipi wakati wa vipindi darasani. Tabia kama hizi mwalimu anapozifanya darasani wakati wa vipindi zinadhihilisha, hajali tena heshima yake, hajali tena taaluma ya watoto n.k.

2. Tabia za kumsengenya mwalimu mwenzake darasani au kuwaonyesha watoto kwamba walimu fulani na fulani hawapatani, ni moja ya tabia ya ajabu sana.

3. Upigaji wa hovyo wa watoto wadogo pasipo kuzingatia utaratibu wa utoaji adhabu. Watoto wadogo wanapigwa kila sehemu ya mwili hadi kichwani wakati mwingine hata kwa mateke na ngumi. Huu siyo ufindishaji ni uuaji.

4. Utongozaji wa kishamba wa watoto na ubakaji, yaani takwimu za makadirio kwasasa katika walimu 100, asilimia 5% wanajihusisha kimapenzi na wanafunzi. Hivyo tukiamua kupiga kura ya siri shuleni ni aibu tupu kwa walimu, tena wengine ni walimu wakuu.

5. Kushiriki kuiba mali za shule, vitendea kazi, vifaa vya usafi au mali iliyopo kwenye himaya ya shule.

6. Michezo ya upatu na makundi yasiyoeleweka n.k.

Kiufupi shuleni imekuwa ni biashara na mapenzi halafu taaluma bora liende. Anaewadhalilisha walimu ni matendo yao, Serikali isichoke kuwafanyia semina walimu mara kwa mara.

Pia kwa wale walimu wanaofanya vizuri wapongezwe, siyo kila siku taarifa mbaya tu mwalimu kaua, kabaka n.k.
 
Pumba tupu, nilidhani kuna hoja kumbe mwalimu tu mmoja kaandika uharo wake. Unapoongelea maadili,kwani jamii nzima inayo maadili? Hujui huyo mwalimu naye ni zao la jamii hii hii iliyokengeuka?
Hii ndiyo akili ya baadhi ya walimu tuliowapa dhamana!
Huna tofauti na mwalimu aliyepiga mtoto wa darasa la nine huko Moshi kwa ngumi na mateke hadi kumuua...kwa kosa la kupiga kelele darasani
 
Jinga moja,na huko Polisi kuna nini? Bank je? TRA? Wapi unaona ni kada safi hapa Tanzania?
Acha unafki hakuna kazi yoyote nchi hii isiyo na watu waovu
Unaandika kutafuta umaarufu kupitia walimu kama yule mpuuzi mwenzio
Kwahiyo unaona ni ruksa hayo kufanywa na walimu siku hizi shuleni
 
Kwahiyo unaona ni ruksa hayo kufanywa na walimu siku hizi shuleni
Usiseme walimu peke yao ss sema jamii nzima imekengeuka hao wazaz wanaowalawiti watt wao wazazi wanaovaa mavaz ya ovyo kwa watt wao au kada gani yenye afadhali kwenye dunia ya ss daktar juzi sikonge tabora kabaka mama mjamzito hao wapo vzur au sio we sema jamii nzima ya tz imebadilika tufanyeje sio useme walimu kwan hakuna walimu wenye maadili mazuri kama hao wazaman
 
Kwamba ni sawa mwalimu kula mwanafunzi
Ni kama tu zile kesi za wale wauguzi na madaktari wachache wanaokiuka maadili ya kazi zao, na hivyo kujikuta wanatafuna wagonjwa!

Ni sawa tu na Askari magereza kutafuna/kutafunwa na mfungwa, Mchungaji/Padre/Sheikh kutafuna muumini, nk. Kwa hiyo jibu jepesi tu siyo sawa. Ila kutokana na madhaifu ya kibinadamu kwa baadhi yao, wanajikuta wametenda hayo makosa.
 
Ni kama tu zile kesi za wale wauguzi na madaktari wachache wanakiuka maadili ya kazi zao, na hivyo kujikita wanatafuna wagonjwa!

Ni sawa tu na Askari magereza kutafuna/kutafunwa na mfungwa, nk.
Huyo hana akili vzuri ndo wale kuwasema walimu ivi kwa ss kuna kada gani ambayo haina mambo ya ajabu ivo mana hospital wanabaka polisi ndo mahabusu wanawaua kabisa mahakaman watu wanaliwa si mchezo ss waseme watumishi wote wa serikal n ovyo sn sio kusema walimu
 
Polisi akiua sawa,kada nyingine zikifanya hivi sawa,ila aliekufundisha kuandika na kukutoa makamasi Leo unamtukana,hivi wangekuacha ungejua kuandika weye? Hisani Yao ya kukufundisha kushika kalamu na kujua kusoma na kuandika unawaona hawana maana sio?.dogo wape heshma walikua wako.
 
Polisi akiua sawa,kada nyingine zikifanya hivi sawa,ila aliekufundisha kuandika na kukutoa makamasi Leo unamtukana,hivi wangekuacha ungejua kuandika weye? Hisani Yao ya kukufundisha kushika kalamu na kujua kusoma na kuandika unawaona hawana maana sio?.dogo wape heshma walikua wako.
Huna uelewa kaa kimya
 
Usiseme walimu peke yao ss sema jamii nzima imekengeuka hao wazaz wanaowalawiti watt wao wazazi wanaovaa mavaz ya ovyo kwa watt wao au kada gani yenye afadhali kwenye dunia ya ss daktar juzi sikonge tabora kabaka mama mjamzito hao wapo vzur au sio we sema jamii nzima ya tz imebadilika tufanyeje sio useme walimu kwan hakuna walimu wenye maadili mazuri kama hao wazaman
Point
 
Back
Top Bottom