Mel James
JF-Expert Member
- Jun 23, 2015
- 344
- 241
Kama kichwa cha habari kinavyosema,
Kuna jambo binafsi limenishangaza sana nilivyoenda kwenye kikao cha wazazi cha hii likizo. Moja ya shule ya msingi maarufu hapa Mbeya, nakusikia mkuu wa Shule akisema wazazi waache tabia ya kutongoza walimu wake. Ni kero walimu wanasumbuliwa sana. Mzazi anachukua simu kwa lengo la kuwasiliana na mwalimu kuhusu maendeleo ya mtoto wake anaishia kumtaka mwalimu kimapenzi. Binafsi nimeona kama sio hekima na busara kumtongoza mwalimu anayekufundishia mtoto wako.
Mtoto anaweza kukosea kawaida tu ila mwalimu akaona amechukua tabia za mzazi.
Pia mzazi ukikataliwa na mwalimu unaweka mazingira magumu kwako kuwasiliana na mwalimu, pia mazingira magumu kati ya mwanao na mwalimu. Mwalimu anaweza kukudharau wewe na mwanao. Maana hadi mtoto anapelekwa shule ana wazazi wawili. Pia mzazi hasa wa kiume fahamu kwamba wamama wanafuatulia sana watoto wao wakiwa shuleni kwa mambo mbalimbali hivyo ni rahisi sana walimu kufahamiana na mama wa mtoto.
Tujitahidi wazazi kuweka mazingira mazuri watoto wasome kwa amani na furaha.