Capacity Nursery and Primary School: Ni shule nzuri lakini baadhi ya Walimu ni wanatesa watoto.

affinitytz

JF-Expert Member
Feb 10, 2020
206
983
Wasalam,

Kwa mkuu wa shule,

Awali ya yote nipongeze uongozi wa Capacity Building Trust kwa namna ambavyo unajitahidi kuboresha mazingira ya shule na kukuza maendeleo ya kitaaluma ya shule hii.
Kwa wasiofahamu Capacity Building Nursery and Primary School ni shule ya mtaala wa kiingereza iliyopo eneo la Kisiwani huko Kigamboni.

Ni shule nzuri na Ina matokeo mazuri kitaaluma.

Leo nataka kufikisha ujumbe kutoka kwa wazazi ambao wamechoshwa na baadhi ya tabia za Walimu ( ni baadhi ya Walimu, zingatia hilo) ambao wamekuwa na tabia ya kunyanyasa na kupiga watoto bila kufuata utaratibu wa adhabu.

Zingatia, wazazi hawana tatizo na adhabu ila zufuate utaratibu na kwa kiwango stahiki.

Baadhi ya Walimu wanapiga watoto mpaka wanavimba mikono, viwiko , wengine wanapiga watoto migongoni. Na wengine imekuwa ni kawaida kumchapa mtoto kila anapokosea kwenye homework.
Na wengine wanatumia mikono kufinya, kusukuma kupiga makofi na hata mateke kupiga wanafunzi

Wazazi wengi wamepokea malalamiko kwa Walimu wa darasa la tatu, nne na tano.

Mkuu wa shule ndugu Abraham Ntengwi , kaa na Walimu wako na uwaelekeza namna bora ya kutoa adhanbu na sio kuwaonea watoto.

Mnawapa tabu wazazi maana watoto mpaka wanagoma kuja shule kwa sababu ya baadhi ya Walimu kuwa wakali na kutoa adhabu zisizofa.

Zingatia: Hali ya Walimu wako ikiendelea hivi tutawataja majina ili kila mtu ajue.

Tunathamini kazi ya ualimu lakini sio kutesa watoto kwa bakora na kuwapiga tena bila kuzingatia muongozo wa kutoa adhabu.

Wazazi wana group la Whatsapp na wanajadili haya mambo, ni suala la muda tu kabla makubwa hajaibuka, huwezi kupiga mtoto wa miaka 9 mgongoni mpaka ukaacha alama za bakora. Wengine mnawapiga mpaka mikono inavimba.

Zungumza na Walimu wako wafanye kazi kwa weredi na kwa kuzingatia muongozo.

Ukicheka nao wataipa shule sifa mbovu na litakuwa jambo baya sana.

Wako katika ujenzi wa taifa.
 
Hizi sio tuhuma ngeni kwa hiyo shule, nyie kama wazazi waambieni ukweli.

Walimu wasilete hasira za nyumbani kwa watoto wenu.

Wanawapa watoto msongo wa mawazo na kuwapa woga.

Yaani afrika hata elimu ya shule ya msingi nayo ni mapambano.

Ujumbe ufike kwa Headmaster na mwenye shule.
 
Shule nzuri ila baadhi Walimu wanachanganya hasira za maisha na masuala ya shule.

Sio sawa kupiga watoto kwa hasira na kutumia viungo vya mwili wako.

Unampigaje mtoto makofi, ngumi na mateke?

Sio sawa,pazeni sauti kwa nguvu watawaumizia watoto hao na kuwatia ulemavu.
 
Kama ni kweli naomba mnipatie mawasiliano ya mkuu wa shule pamoja na mmiliki wa shule.

Haiwezekani walimu watoe adhabu zilizo nje ya waraka wa elimu na adhabu mashuleni halafu tuwachekee tu hao wanywa gongo.

Pia wazazi msikae kimya lifikisheni kwa mkuu wa shule na kama naye hawajibiki ipasavyo lifikisheni kwa mmiliki kisha kwa afisa elimu wilaya hadi ngazi za juu.
 
Kwani lazima kusoma hapo. Acha kulalamika na peleka shule ambao unadhani ni nzuri. Acha kudekeza watoto
 
Wengine mnawapiga mpaka mikono inavimba.
Kama una ushahidi wa aina hii unakuja kulialia nini huku Jf....huu ni ufala!
Shida hapa iko kwa mzazi zaidi kuliko kwa hao waalimu wanaotuhumiwa.

Kwa mbali naona kama unaisagia kunguni hiyo shule, kama sivyo basi nenda kawaone wenye shule ana kwa ana.
 
Back
Top Bottom