Anataka mchukua mwanangu kinyemela

Anataka mchukua mwanangu kinyemela

sijakuelewa hapo unaposema huna mpango wa kuzaa tena ingawa uko kwenye mahusiano na mwanaume mwingine au yeye pia hana mpango wa kuzaa na wewe.

kuhusu huyo ex wako muogope kama ukoma kwa kuwa lengo lake ni kukuharibia baada ya kuona umuulizi lolote kuhusiana na malezi ya mtoto.
Niliye naye kwenye mahusiano naye ana mtoto mmoja alozaa na mwanamke mwingine.So naweka jitahada kuandaa future ya mwanangu kwani maisha saivi yako magumu,kama unataka mtoto apate malezi bora pamoja na elimu nzuri lazima kujipanga.
 
Anayelia hapo ni mama au baba aliyemtekeza mtoto. Acha ujinga we kuku!
Sina tatizo na mtoa mada, naongea na we ajuza unae quote quote tu mambo usiyoelewa.
 
Tatizo unapanic. All the best
No ur wrong,we done and we good.tatizo wengi mlitegemea nionyeshe kumchukia na bifu,for what?mie nina bifu na maisha,mwanangu,ale vizuri,alale pazuri na aje apate elimu bora.

Muda wa kuweka chuki moyoni nautumia kutafuta shilingi na kuwekeza for my Prince.
 
Kuna danga fulani lilimimbisha mdogo wangu.baada ya mimba lilikata mawasiliano. Nikasema isiwe taabu.

Dogo nikamkodishia chumba hapo niko chuo najisomesha sina mkopo wa bodi aiseeee niliteseka balaa, pamoja na usumbufu wa mtu mjamzito nililea mimba vizuri tu.

Mtoto alizaliwa nzuri balaa. jamani kulea mtoto sikia kwa mtu mara aumwe Mara nn yaan nimeteseka na mtoto mpaka sasa hivi. Ana 4yrs sasa; She is extremely cute. Namuona kama mwanangu Kila kitu ni mm hadi mfanyakazi.

Jina tulimuita tunalojua sisi. Jamani nalisubiri kwa hamu Mara siku lije kufata mtoto aiseee atatamani aridhi immeze. Sheria itafata mkondo wake.

Dada usife moyo huwezi kulea kwa shida afu mtoto ampeleke kirahisi hivyo.
Hakuna kitu kinachoshindikana.
 
Kaa uelewane na mwenzio. Pia elewa unaweza mzuia sasa huyo mtoto baadae akamfuata baba yake. Kila mtoto anapenda kumuona baba na mama yake.Usimkatalie jamaa ila mueleze nini atekeleze ili machungu ya kumlea mtoto peke yako yapungue.
Sina ugomvi naye,nachopinga ni kuchukua mtoto wa under 5years,akalelewe bila malezi ya mama yake,ilhali sijashindwa kumlea.sasa hata kazi nafanya ili iweje?ninunue mawigi na mavazi ama?i work for my boy.
 
Nilivyoelewa si kwamba amemzuia baba mtoto asimuone mwanae ila hataki mtoto wake achukuliwe kwake akiwa bado mdogo na wkt alimtelekeza.
.
.
Aendelee na msimamo wake huo huo. Jamaa aruhusiwe kumuona mtoto, mtoto akikua anaweza akaenda kwa baba yake. Why amchukue sasa hivi?
Exactly my point
Waweza mkabidh mtu mtoto halafu baada ya muda ukipata nafasi ya kumwona unaishia mwaga chozi.
 
Sawa hatujui na ndio sababu,tunabeba mimba miezi 9,tunazaa kwa uchungu then tunakubali kulea mtoto hata kina baba mkijiweka pembeni.Tunajikana na kubeba msalaba wetu,hatukimbii jukumu la malezi kwani mtu mzima ni kuwajibika kwa maamuzi uliyofanya.
Pole ndugu.Tena ningekuwa mimi ndo amekimbia toka mimba wallah! Hata jina nisingemwita la baba ake bora niongeze ukoo wa baba yngu.
 
Mbona kaongea kauli ya kibwege eti "kama shida mtoto nitakupa mwingine.." mwambie akamchukue yeye huyo mwingine. Hapo hazungimzii kuhusu kukuoa ili mtoto apate malezi ya baba na mama! Komaa mtoto haendi kwake hadi afikishe miaka 7 tena alipie gharama za matunzo ya mimba na mtoto. Mruhusu kumtembelea mtoto wake chini ya uangalizi asijemtorosha siku moja.
Hawezi mtorosha kwangu kuna ulinzi na watu wa kutosha.Ndio nimemweleza azae tu mwingine kwa mwanamke mwingne.
 
Kwendraaaaaaa! Ukute wewe ndo umetelekeza unakuja kujishaua hapa.
Mtoto hupewi ng'o!
Mimi ni ajuza ndio umri umeenda sana lazima niwashauri wadogo zangu.
Mwanaume toa hoja za maana!
Nimetelekeza wengi sana, inawezekana hata huyo unaelea mi ndio baba nimekuachia ulee maana hatujuani humu
 
Yani huyo usithubutu kumpa mtoto kabisa coz hutomuona tena, amekumbuka shuka kumekucha, ulifanya kosa kuendelea kumu entertain, kama uliamua kuendelea na maisha yako, hukuwa na sababu ya kuendeleza na mawasiliano naye.
Je ungetoa mimba? angekuwa anakubembelezea nini sasa hivi?
 
Hata hivyo Dada una roho ya kibinadamu sana. Kama alitelekeza mimba basi alinikana mimba sio yake hivyo sioni haja ya kumpa mtoto asie na uchungu nae mn atamlea kimazoea.
Hata mahakamani unaweza kumkatalia kuwa sie mwanae kwaani kama mwanae angemlea.

Na usikute hata jina la mtoto ulichagua pekee yako
 
Atammiss je wakati alimkimbia, mwambie hata mawasiliano na wewe sitaki, achana nae kabisa. Huyo si binadamu .
 
Hii thread ni kama kikao cha masingo maza,

Sio kwa mapovu hayo
 
Kwendraaaaaaa! Ukute wewe ndo umetelekeza unakuja kujishaua hapa.
Mtoto hupewi ng'o!
Mimi ni ajuza ndio umri umeenda sana lazima niwashauri wadogo zangu.
Mwanaume toa hoja za maana!
Hahaha umenifurahisha
 
Huu ndio tunauita ubinafsi, mtoto mlitafuta wote alafu unatumia neno my prince inamaana ye hamhusu? Kukataa kulea haitoi uhalisia wa ubaba wake na umiliki wa huyo mtoto.

Ushauri wangu tafuteni sehemu tuliivu mkiwa wawili mjadili hatma ya huyo mtoto na jinsi ya kumlea nina imani hakita haribika kitu
Alivyo mtelekeza mtoto hakuwa mbinafsi? Au alikuwa sahihi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom