Anataka mchukua mwanangu kinyemela

Anataka mchukua mwanangu kinyemela

Kaa uelewane na mwenzio. Pia elewa unaweza mzuia sasa huyo mtoto baadae akamfuata baba yake. Kila mtoto anapenda kumuona baba na mama yake.Usimkatalie jamaa ila mueleze nini atekeleze ili machungu ya kumlea mtoto peke yako yapungue.
 
Kuna sababu nyingi nyuma ya pazia you never know, tatizo lenu akina mama wagumu kuelewa mnataka kila mnachokitaka kifanyike kwa wakati huo, mtu akikuambia kafulia ujue kafulia kweli.
That's why alipokataa kuonyesha ushirikiano katika kutoa matumizi,nikaamua kujikalia kimya,nikifanya kazi kwa juhudi na kumlea mwanangu.
 
Tatizo lenu jambo dogo tu mnalikuuuuza, kwahyo ikitokea baba leo hana hela ya matumizi hata kesho hutamuomba?

Kipindi hicho hakua na kitu lakini sasa Kapata mwacheni atumie na mwanae
Sijaelewa hata ulichoandika. Hakuwa na hela kivipi? Kwani mama mtoto alipata wapi hela ya kumlea mtoto mpk amefika hapo?
.
.
Kama huna hela ya kulea usifanye ngono zembe. Umetia mtu mimba wajibika kwa makosa yako. Matangazo ya condom huwa hamyaoni au? Acha kutetea ujinga basi, wangapi hawana maisha mazuri lkn wanalea watoto wao kishidashida? Mwanaume wajibika kwa makosa yako!
 
Bibie naona bado unampenda jamaa ndo maana anahangaisha serikali ya kichwa chao,una mahusiano na mtu mwingine kisha unabembelezana na baby dady wako eti uumpe mtoto atakupa mwingine na unakuja kuomba ushauri humu aiseeeee pole kwa mwanaume wako wa sasa

Mara malezi yakikushinda utampa ooh asubiri ifike miaka saba aje amchukue be serious mtoto sio jojo kusema ikiisha utamu utaitupa. Hakukuoa kiasi cha kuwa na haki zote za kujichukulia mtoto.
No ur wrong,we done and we good.tatizo wengi mlitegemea nionyeshe kumchukia na bifu,for what?mie nina bifu na maisha,mwanangu,ale vizuri,alale pazuri na aje apate elimu bora.

Muda wa kuweka chuki moyoni nautumia kutafuta shilingi na kuwekeza for my Prince.
 
Tatizo lenu jambo dogo tu mnalikuuuuza, kwahyo ikitokea baba leo hana hela ya matumizi hata kesho hutamuomba?

Kipindi hicho hakua na kitu lakini sasa Kapata mwacheni atumie na mwanae
Sijashindwa mlea isitoshe bado mdogo,kama ni watoto si atafute wengine huko aliko ale nao hizo good times.
 
Kaa uelewane na mwenzio. Pia elewa unaweza mzuia sasa huyo mtoto baadae akamfuata baba yake. Kila mtoto anapenda kumuona baba na mama yake.Usimkatalie jamaa ila mueleze nini atekeleze ili machungu ya kumlea mtoto peke yako yapungue.
Nilivyoelewa si kwamba amemzuia baba mtoto asimuone mwanae ila hataki mtoto wake achukuliwe kwake akiwa bado mdogo na wkt alimtelekeza.
.
.
Aendelee na msimamo wake huo huo. Jamaa aruhusiwe kumuona mtoto, mtoto akikua anaweza akaenda kwa baba yake. Why amchukue sasa hivi?
 
Sijaelewa hata ulichoandika. Hakuwa na hela kivipi? Kwani mama mtoto alipata wapi hela ya kumlea mtoto mpk amefika hapo?
.
.
Kama huna hela ya kulea usifanye ngono zembe. Umetia mtu mimba wajibika kwa makosa yako. Matangazo ya condom huwa hamyaoni au? Acha kutetea ujinga basi, wangapi hawana maisha mazuri lkn wanalea watoto wao kishidashida? Mwanaume wajibika kwa makosa yako!

Umelazimishwa kujibu kitu usichokielewa?
 
Mbona kaongea kauli ya kibwege eti "kama shida mtoto nitakupa mwingine.." mwambie akamchukue yeye huyo mwingine. Hapo hazungimzii kuhusu kukuoa ili mtoto apate malezi ya baba na mama! Komaa mtoto haendi kwake hadi afikishe miaka 7 tena alipie gharama za matunzo ya mimba na mtoto. Mruhusu kumtembelea mtoto wake chini ya uangalizi asijemtorosha siku moja.
 
Kama hakutoa mahari na hakuoa mwanasheria hatasaidia.
.
.
Bidada shikilia msimamo wako. Tena mwambie mtoto si wake, na kama ulimpa mtoto jina la baba yake badilisha mpe jina lako. Wajinga sana hawa vidume sometimes.
Nilishamwambia mtoto si wake,akasema hata hakimu mwenyewe atanishangaa jinsi walivyofanana.
 
Kwahiyo wakati we umefulia mi ndo nakua cjafulia au?...kwa unavyoonekana tu ww ni baba unaetelekezaga watoto
Hata wewe unaweza ukawa mwanangu nilimtelekezea mwingine, muulize vizuri mama ako
 
Atakua mwanao cku ambayo pia mm mamaake nilikufa....mnasubirigi Watoto wawe wakubwa na maisha mazuri aliyoyatengeneza mama ake halafu muanze kuomba misaada
Kwahiyo mtoto wa miaka mitatu ana maisha mazuri? LOOOOOOOOOL
 
Kuna danga fulani lilimimbisha mdogo wangu.baada ya mimba lilikata mawasiliano. Nikasema isiwe taabu.

Dogo nikamkodishia chumba hapo niko chuo najisomesha sina mkopo wa bodi aiseeee niliteseka balaa, pamoja na usumbufu wa mtu mjamzito nililea mimba vizuri tu.

Mtoto alizaliwa nzuri balaa. jamani kulea mtoto sikia kwa mtu mara aumwe Mara nn yaan nimeteseka na mtoto mpaka sasa hivi. Ana 4yrs sasa; She is extremely cute. Namuona kama mwanangu Kila kitu ni mm hadi mfanyakazi.

Jina tulimuita tunalojua sisi. Jamani nalisubiri kwa hamu Mara siku lije kufata mtoto aiseee atatamani aridhi immeze. Sheria itafata mkondo wake.

Dada usife moyo huwezi kulea kwa shida afu mtoto ampeleke kirahisi hivyo.
 
Tatizo lenu jambo dogo tu mnalikuuuuza, kwahyo ikitokea baba leo hana hela ya matumizi hata kesho hutamuomba?

Kipindi hicho hakua na kitu lakini sasa Kapata mwacheni atumie na mwanae
Yaani hela ya matumizi ya mwanao mpaka nikuombe,we hujui kwamba mtoto huhitaji matunzo...
Nyie wanaume tumewaendekeza mda mrefu sasa hv mtaisoma no
 
Huyu nae Maelezo yake hayajitoshelezi, kasema jamaa hatoi Hata kumi mara huwa anakuja kumona mwanae simkataliagi,, anakujaje kumona mtoto nakuondoka asitoe hata mia???
Kwa mwaka anakuja kama mara moja na hamlei chochote wala hatoi hata senti,Mungu ni shahidi.mwanzo nilikuwa namwambia kuhusu matumizi akasema atatoa,ila hatoi,so nikaacha kumwomba.kwani anaahidi tu ila hatoi hata senti.alishauri tumfungulie mtoto akaunti atakuwa anamwekea kiasi fulani kila mwezi,ni mwaka wa pili sasa mimi ndo namsevia mwanangu visenti nikipata.hajawahi weka hata mia kwenye hio akaunti.
 
Nilishamwambia mtoto si wake,akasema hata hakimu mwenyewe atanishangaa jinsi walivyofanana.
Hakimu mwenyewe atamshangaa kwa jinsi alivyomtelekeza mtoto wake miaka yote hiyo. Akienda mahakamani hatashinda zaidi ya kupata aibu. Kama hukuolewa nae just relax..mtoto ni wako na uamuzi unao wewe mwenyewe asikutishe. Lea mtoto wako...babake aje kumuona.
.
.
Mtoto ataenda kwa baba yake akiwa mkubwa na akipenda mwenyewe. Ila maamuzi ni yako sie tunabaki kuwa washauri tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom