Ananunua ndege wakati hiki na kile hatuna...

Leta hiyo ilani tuone vipaumbele vya
Ndege
Kuwakamata wapinzani
Kuwatukana wafanya biashara
Na kuzuia siasa mpaka 2020
Kukwamisha Ajira
Kukagua wafanya kazi hewa

Hivi ndio vipaumbele vya ilani?
Kuna watu kibao sasaivi wameachishwa kazi kutokana na mdororo wa uchumi. Ni vile tu ni marufuku siasa mpk 2020.
 
Watapanda watoto wa matajiri...huku kantamba hatuna madawati tutapandaje ndege na vijihela vya dagaa
 
Nchi haina vipaumbele tuliambiwa kipaumbele ni viwanda lakini kuchekesho wizara ya viwanda ikatengewa bilioni 88....

Tukabadili gia angani na kununua ndege za bilioni 61....

Wakati huo tunategemea kumwaga pesa kununua zingine......

Sijui viwanda na ndege ni kipi kitatoa Ajira za kutosha na kulipa kodi kubwa....

# only in black continent....
Wewe kipaumbele Chako ni kipi?

Mijitu ya nchi hii sijui nani kawalaan?

Yaani hamna jema kabisa
 
Kama unafata mtu, na sio chama na itikadi zake, jiandae kuruka ruka sana.
Bora mimi nirukeruke kuliko kuwa mwanachadema ya mashabiki wa hovyo kama wewe yaani nyie jamaa mliokuja na mamvi hamna akili kabisa kumbe nyie ndo mlikuwa mnavuruga kile chama kikongwe
 
Kutokuridhika kwa binadamu ni jambo la kiasili.

Lakini nadhani mtu unaweza ukawa unatafuna jojo huku ukitembea na kuongea kwenye simu yako ukiwa unaelekea kwa Joji kwenda kula kiti moto au chipsi vumbi.
kuna jambo moja ambalo ni baya kuliko yote kwenye siasa ambalo ni 'kuombeana mabaya',yaani hadi inakera mtu anajenga nchi kwa ajili ya watz wote ila wengine wanaomba aboronge ili wapate cha kusema.Wengine nao "wenye madaraka" wakipewa ushauri wanakataa eti waonekane hawajui kukopy ya wengine!!
Ngoja niende kwa Joji nikapate kidogo!!
 
Kutokuridhika kwa binadamu ni jambo la kiasili.

Kunung'unika nako ni ada ya mja.

Bila ya kupoteza sana muda ngoja nizame moja kwa moja kwenye hoja.

Baada ya ununuzi wa hizi ndege za shirika letu la ndege, kumekuwepo na hoja kadha wa kadha zinazohoji eti kwa nini mheshimiwa MTUKUFU rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali yake wananunua ndege ilhali sehemu nyingi za Tanzania hazina viwanja vya ndege, eti hatuna sukari ya kutosha, hatuna sijui mashine gani mahospitalini, na kadhalika na kadhalika.

Sasa nami hebu ngoja niulize [maswali] yangu:

Hivi, kwani wakati ule tulipokuwa na zile ndege zetu za ATC, tulikuwa na viwanja vingapi vya ndege huko mikoani na wilayani?

Je, wakati ule hospitali zetu za serikali zilikuwa na kila kitu? Bugando ilikuwa na mashine zote zilizokuwa zinahitajika? Muhimbili nayo ilikuwa imejitosheleza kwa kila kitu?

Sukari, unga, sabuni, na mahitaji mengine nayo tulikuwa tumejitosheleza nayo vizuri tu?

Hizo Fokker Friendship [nadhani walikuwa nazo mbili au zaidi] za ATC ziliweza kutua hata huku kwetu Ikungulyabashashi, Ng'wamapalala, Lamadi, Madale, na Nyangokolwa?

Nchi zingine zilizo na mashirika yao ya ndege zenyewe zimetatua matatizo yake yote kabla ya kuamua kuwa na ndege zake zenyewe?

Huko Kenya kwa mfano, wao kila hospitali yao ina kila kifaa kilicho cha muhimu?

Sasa labda mimi kwa vile ni mbeba maboksi tu nisiye na elimu yoyote ile kubwa [niliishia kidato cha nne ambapo nilipata daraja la nne na pointi 30] ndo maana labda kwa kiasi fulani sizielewi hizo hoja za baadhi ya hao vipanga wanaozitoa.

Lakini nadhani mtu unaweza ukawa unatafuna jojo huku ukitembea na kuongea kwenye simu yako ukiwa unaelekea kwa Joji kwenda kula kiti moto au chipsi vumbi.

Nyani Ngabu ,kwanza nikupongeze kwa kuanzisha mada nzuri sana na wakati muafaka lakini nasikitika kuwa kwa standard ya JF ya sasa hii mada itaonekana haina maana lakini ingekuwa mada nzuri sana kama tungepunguza ushabiki wa kisiasa ambao umestawi kwenye vichwa vya watanzania wengi.

Nchi yetu ina matatizo mengi mno (yanaweza fika bilioni) sidhani kama kuna sekta ambayo tumefanikiwa tunaweza kujivunia (elimu,afya,kilimo,miundombinu,ufugaji,uvuvi,uchumi,utalii,michezo,habari,teknolojia) sidhani kama tukitatua tatizo moja watu wataunga mkono,bado tutaendelea kulalamika kwa nini hakuanza na C tumeanza na A.Kuna matatizo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu na tunaweza kuyamaliza sisi wenyewe ndani ya muda mfupi.

Haya matatizo ni ngumu sana kuisha ndani ya miaka 10/20 na hakuna mwanasiasa ambaye anaweza kuyamaliza ndani ya miaka 20 kama viongozi wetu na wananchi kwa ujumla hatutabadilika.Kibaya zaidi mambo yanabadilika kwa kasi sana tukiendelea kuzubaa tunazidi kuachwa nyuma licha ya rasilimali tulizonazo,kwa sasa hatuna kipaumbele .Tatizo kubwa lilitufikisha hapa lilikuwa ni rushwa na ufisadi tukijitahidi kulipunguza/kulimaliza hili una haja ya kuhamia kwenye vipaumbele kwenye sekta ya afya,elimu,kilimo,ufugaji,utalii na teknolojia
 
Okay, sina kabisa tatizo na valid criticism.

Lakini kwa wanaohoji eti mwanakijiji wa Busanda atafaidika vipi na ndege mpya nami nawauliza, kwani watu wa Dumila walifaidika vipi na ATC?
Tunakusudia huyo mwanakijiji wa Busanda awe biashara kwenye hiyo ndege ili tupate hela, ndege sio mapambo wala chombo cha kuwapakia wahalifu uchwara (wachochezi) tunakusudia kufanya biasharaa jamanii!!
 
Nyani Ngabu ,kwanza nikupongeze kwa kuanzisha mada nzuri sana na wakati muafaka lakini nasikitika kuwa kwa standard ya JF ya sasa hii mada itaonekana haina maana lakini ingekuwa mada nzuri sana kama tungepunguza ushabiki wa kisiasa ambao umestawi kwenye vichwa vya watanzania wengi.

Nchi yetu ina matatizo mengi mno (yanaweza fika bilioni) sidhani kama kuna sekta ambayo tumefanikiwa tunaweza kujivunia (elimu,afya,kilimo,miundombinu,ufugaji,uvuvi,uchumi,utalii,michezo,habari,teknolojia) sidhani kama tukitatua tatizo moja watu wataunga mkono,bado tutaendelea kulalamika kwa nini hakuanza na C tumeanza na A.Kuna matatizo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu na tunaweza kuyamaliza sisi wenyewe ndani ya muda mfupi.

Haya matatizo ni ngumu sana kuisha ndani ya miaka 10/20 na hakuna mwanasiasa ambaye anaweza kuyamaliza ndani ya miaka 20 kama viongozi wetu na wananchi kwa ujumla hatutabadilika.Kibaya zaidi mambo yanabadilika kwa kasi sana tukiendelea kuzubaa tunazidi kuachwa nyuma licha ya rasilimali tulizonazo,kwa sasa hatuna kipaumbele .Tatizo kubwa lilitufikisha hapa lilikuwa ni rushwa na ufisadi tukijitahidi kulipunguza/kulimaliza hili una haja ya kuhamia kwenye vipaumbele kwenye sekta ya afya,elimu,kilimo,ufugaji,utalii na teknolojia

Shukran sana ndugu Belo.

Hakika vichwa vikongwe utavitambua tu.
 
Hilo la uwiano kati ya mahitaji ya msingi na ununuzi wa ndege vinahusianaje?

Unataka kuniambia kipindi kile uwiano ulikuwa ni mzuri/ bora zaidi kuliko ilivyo hivi sasa?

Kwani enzi za ATC watu hawakupanga foleni? Watu walipanga foleni hadi kwenye maduka ya ugawaji nini hii kupanga foleni kwenye ofisi za RITA, kwa mfano?

Hayo matatizo makubwa hayakuwepo enzi za ATC?

Na kwa mwendo huu wa kuponda tu kila kitu pasipo hata na sababu ya/za msingi basi kweli tutaishia kukwamishana hata kwenye shughuli chanya zenye zilizo na tija ya kimaendeleo.

Kazi kuponda tu kila kitu.
Usiumize kichwa hawa jamaa wamepeana mikakati na wameamua kwamba watapinga kila kitu kinachofanywa na serikali hii.Walianzia kwa baba lao kwamba kama angeupata urais kwenye sector ya elimu angeanza na walimu na sio madawati kama alivyofanya mkulu wetu,so onaaaaaaa.
 
Anachokifanya Rais JPM ni cha kuungwa mkono ni wajinga tu na wapenda siasa za kipumbafu ndo watapinga no wonder Kenya wanatupiga daflao kwa sababu ya kuendekeza siasa kwenye kila jambo go JPM
 
Kutokuridhika kwa binadamu ni jambo la kiasili.

Kunung'unika nako ni ada ya mja.

Bila ya kupoteza sana muda ngoja nizame moja kwa moja kwenye hoja.

Baada ya ununuzi wa hizi ndege za shirika letu la ndege, kumekuwepo na hoja kadha wa kadha zinazohoji eti kwa nini mheshimiwa MTUKUFU rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali yake wananunua ndege ilhali sehemu nyingi za Tanzania hazina viwanja vya ndege, eti hatuna sukari ya kutosha, hatuna sijui mashine gani mahospitalini, na kadhalika na kadhalika.

Sasa nami hebu ngoja niulize [maswali] yangu:

Hivi, kwani wakati ule tulipokuwa na zile ndege zetu za ATC, tulikuwa na viwanja vingapi vya ndege huko mikoani na wilayani?

Je, wakati ule hospitali zetu za serikali zilikuwa na kila kitu? Bugando ilikuwa na mashine zote zilizokuwa zinahitajika? Muhimbili nayo ilikuwa imejitosheleza kwa kila kitu?

Sukari, unga, sabuni, na mahitaji mengine nayo tulikuwa tumejitosheleza nayo vizuri tu?

Hizo Fokker Friendship [nadhani walikuwa nazo mbili au zaidi] za ATC ziliweza kutua hata huku kwetu Ikungulyabashashi, Ng'wamapalala, Lamadi, Madale, na Nyangokolwa?

Nchi zingine zilizo na mashirika yao ya ndege zenyewe zimetatua matatizo yake yote kabla ya kuamua kuwa na ndege zake zenyewe?

Huko Kenya kwa mfano, wao kila hospitali yao ina kila kifaa kilicho cha muhimu?

Sasa labda mimi kwa vile ni mbeba maboksi tu nisiye na elimu yoyote ile kubwa [niliishia kidato cha nne ambapo nilipata daraja la nne na pointi 30] ndo maana labda kwa kiasi fulani sizielewi hizo hoja za baadhi ya hao vipanga wanaozitoa.

Lakini nadhani mtu unaweza ukawa unatafuna jojo huku ukitembea na kuongea kwenye simu yako ukiwa unaelekea kwa Joji kwenda kula kiti moto au chipsi vumbi.

Kaka fatilia vizuri, MSD hakuna dawa kabisa, shelf ni nyeupe
Chanzo za watoto nchi nzima hakuna,
 
Back
Top Bottom