Ananunua ndege wakati hiki na kile hatuna...

Ubaya unaongezeka pale vipaumbele vyenyewe anaamua mtu mmoja!! Kwa ubora gani aliokuwa nao? (ni rahisi kuhoji hivyo)
Kumbe shida yako wewe ni humpendi magufuli basiii....
 
Kutokuridhika kwa binadamu ni jambo la kiasili.

Kunung'unika nako ni ada ya mja.

Bila ya kupoteza sana muda ngoja nizame moja kwa moja kwenye hoja.

Baada ya ununuzi wa hizi ndege za shirika letu la ndege, kumekuwepo na hoja kadha wa kadha zinazohoji eti kwa nini mheshimiwa MTUKUFU rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali yake wananunua ndege ilhali sehemu nyingi za Tanzania hazina viwanja vya ndege, eti hatuna sukari ya kutosha, hatuna sijui mashine gani mahospitalini, na kadhalika na kadhalika.

Sasa nami hebu ngoja niulize [maswali] yangu:

Hivi, kwani wakati ule tulipokuwa na zile ndege zetu za ATC, tulikuwa na viwanja vingapi vya ndege huko mikoani na wilayani?

Je, wakati ule hospitali zetu za serikali zilikuwa na kila kitu? Bugando ilikuwa na mashine zote zilizokuwa zinahitajika? Muhimbili nayo ilikuwa imejitosheleza kwa kila kitu?

Sukari, unga, sabuni, na mahitaji mengine nayo tulikuwa tumejitosheleza nayo vizuri tu?

Hizo Fokker Friendship [nadhani walikuwa nazo mbili au zaidi] za ATC ziliweza kutua hata huku kwetu Ikungulyabashashi, Ng'wamapalala, Lamadi, Madale, na Nyangokolwa?

Nchi zingine zilizo na mashirika yao ya ndege zenyewe zimetatua matatizo yake yote kabla ya kuamua kuwa na ndege zake zenyewe?

Huko Kenya kwa mfano, wao kila hospitali yao ina kila kifaa kilicho cha muhimu?

Sasa labda mimi kwa vile ni mbeba maboksi tu nisiye na elimu yoyote ile kubwa [niliishia kidato cha nne ambapo nilipata daraja la nne na pointi 30] ndo maana labda kwa kiasi fulani sizielewi hizo hoja za baadhi ya hao vipanga wanaozitoa.

Lakini nadhani mtu unaweza ukawa unatafuna jojo huku ukitembea na kuongea kwenye simu yako ukiwa unaelekea kwa Joji kwenda kula kiti moto au chipsi vumbi.

duh, kumbe mara moja moja akili unazo ila unafanyaga kusudi tu kutoona uchapa kazi wa Magu.
 
Ndio mkuu, nimeshikiwa na mbaya zaidi aliyevishika ni "Juma Pombe Maharagwe".
Sijaongelea ukamilifu wa Jaji Warioba, ila nimependa usome alichoongelea kuhusu Taifa kukosa dira katika uongozi.
Kama ambavyo anakosea, na ndivyo hivyo ambavyo na wewe unatakiwa kuchanganya na zako katika kusoma ilani ya Magufuli.
Sasa kama Taifa halina Sera ya kuliongoza, na inategemea ilani ya Chama, tutafika?
Maana kama ndio hivyo kila chama au uongozi utakaokuwa unaingia madaraka ni utakuwa unaingia na mdundo wake, yule kama aliacha hajamaliza ujenzi wa barabara, basi atakayefuata hawezi kumalizia, vile tu halipo kwenye ilani yake. Na ndio haya tunayoyaona.
Kichwani mwako ni kutupu kabisa... Waulize chadema wangeshinda wangeongoza jwa kutumia nini!
 
Umeingia kichwa kichwa/Mzima Mzima...thread kama hz sio saizi yenu...subirini zile za kutafuniwa kila kitu ndo mchangie...hz piteni tu.

Mkuu kama kweli umefika kidato cha nne kwa jinsi ulivyoanalyse mambo hapo ni dalili tosha kwamba umepata elimu na umeelimika,unayaona mambo ambayo "wanaojifanya"wameenda shule wanashindwa kuyaona.
 
Mkuu, ebu fikiria vizuri. OK, umeongelea kwa kipindi kile, je unakumbuka idadi ya watu na uwiano wa mahitaji yao ya msingi.?
Leo Tanzania ina watu si chini ya milioni 45, je unahisi kuna uwiano wa mahitaji yao ya msingi, mfano kupata huduma bora za Afya, Malazi bora na Elimu bora.
Watu wanapanga foleni kila mahali siku hizi, sio hospital, kwenye mabenki, barabrani, baadhi ya maofisi ya umma.
Tuna matatizo mengi, sana na makubwa kuliko hata hilo la ndege.
Kwa mwando huu wa kuchagua vipaumbele vya maendeleo pasipo kufanya tafiti za kina na kutosha, tutabaki tunaruka sarakasi wakati bado tupo kwenye vazi la kanzu na msuli, kufaidisha wengine.
Denoo49, umeusemea moyo wangu na ninakushukuru. Binafsi mawazo yangu yameenda mbali zaidi nikawaza na kuwafikiria walio wengi katika nchi yetu ambao ni masikini sana.

Kuna sehemu huku umang'atini na umbuluni ambako watu wanaishi hadi km 10 toka zahanati iliyo karibu zaidi. Natafakari mazao yanayooea shambani (nyanya na vingine vingi) na kutamani viwanda ili kuchakata mazao ya kilimo.

Nafikiria akina mama katika sehemu nyingi nchini ambao hata ndoa zao na maisha ya kifamilia yako katika hali tete sababu lazima waamke saa tisa alfajiri kwenda kuteka maji na kusafirisha kwa punda au vichwa vyao na kufika majumbani kwa masaa sita hadi nane baadaye!

Nafikiria mtandao wa njia ya reli nchi nzima kama namna nzuri ya kuwapatia walio wengi njia rahisi ya kusafiria na kusahirisha bidhaa mbalimbali; kufanya hata barabara zetu zidumu kwa muda mrefu zaidi.

Kiongozi anayejali masikini natarajia vipaumbele vyake viendane na hali halisi.

Kwa bahati mbaya awamu hii uongozi unataka kufanya yale ambayo yatashangiliwa haraka haraka; yale ambao yanawezekana kukamilika mapema mapema ili by 2020 iwe rahisi kuwaonyesha wapiga kura wachache mafanikio huku walio wengi (wa loolera na balangdalalu) wakishangilia na kupiga kura bila kufikiri.

Ngoja tuone labda kabla ya 2020 focus itabadilika na kuwalenga walio wengi. Vinginevyo Tanzania ya viwanda itabakia kuwa ndoto.
 
Hakuna plan na sera maalum,
Sera,mpangaji na mchepuaji fedha hazina ni mkulu peke yake kulingana na vipaumbele vyake.
Tatizo akili zetu hazijishughulishi na kusoma na kujua. Mfano mtu anasema hatuma mpango hivi kweli tumekuwa wajinga kiasi hiki. Mpango wa maendeleo uliopitishwa na bunge tumeusoma kweli. Mpango na bajeti wa kila mwaka wa fedha je. Mipango ya kisekta je tumesoma. Mfano agricultural sector development program two je. Hivi tutafika kwa uzembe huu wa kuto kusoma
 
Kutokuridhika kwa binadamu ni jambo la kiasili.

Kunung'unika nako ni ada ya mja.

Bila ya kupoteza sana muda ngoja nizame moja kwa moja kwenye hoja.

Baada ya ununuzi wa hizi ndege za shirika letu la ndege, kumekuwepo na hoja kadha wa kadha zinazohoji eti kwa nini mheshimiwa MTUKUFU rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali yake wananunua ndege ilhali sehemu nyingi za Tanzania hazina viwanja vya ndege, eti hatuna sukari ya kutosha, hatuna sijui mashine gani mahospitalini, na kadhalika na kadhalika.

Sasa nami hebu ngoja niulize [maswali] yangu:

Hivi, kwani wakati ule tulipokuwa na zile ndege zetu za ATC, tulikuwa na viwanja vingapi vya ndege huko mikoani na wilayani?

Je, wakati ule hospitali zetu za serikali zilikuwa na kila kitu? Bugando ilikuwa na mashine zote zilizokuwa zinahitajika? Muhimbili nayo ilikuwa imejitosheleza kwa kila kitu?

Sukari, unga, sabuni, na mahitaji mengine nayo tulikuwa tumejitosheleza nayo vizuri tu?

Hizo Fokker Friendship [nadhani walikuwa nazo mbili au zaidi] za ATC ziliweza kutua hata huku kwetu Ikungulyabashashi, Ng'wamapalala, Lamadi, Madale, na Nyangokolwa?

Nchi zingine zilizo na mashirika yao ya ndege zenyewe zimetatua matatizo yake yote kabla ya kuamua kuwa na ndege zake zenyewe?

Huko Kenya kwa mfano, wao kila hospitali yao ina kila kifaa kilicho cha muhimu?

Sasa labda mimi kwa vile ni mbeba maboksi tu nisiye na elimu yoyote ile kubwa [niliishia kidato cha nne ambapo nilipata daraja la nne na pointi 30] ndo maana labda kwa kiasi fulani sizielewi hizo hoja za baadhi ya hao vipanga wanaozitoa.

Lakini nadhani mtu unaweza ukawa unatafuna jojo huku ukitembea na kuongea kwenye simu yako ukiwa unaelekea kwa Joji kwenda kula kiti moto au chipsi vumbi.
Asante Mkuu nimekuelewa na nyakati zilizopita niliwahi kujiuliza; hivi sasa hatuna vipaumbele?, na je tunaweza kufikia mahala tunaamua kununua vitu visivyowanufaisha walio wengi kwa matamko ya jukwaani. Wangapi kwa nauli ya ndege kutoka Dar mpaka Kwanza wanaweza kuimudu?! Sasa hivi huduma za afya zipo hoi (wana lumumba nendeni muhimbili mkaone maana hamchelewi kubisha) hata dawa hakuna, leo wanaoshangilia kwenye uzinduzi wa "panga boy" wanajua kama bunge lilipewa nafasi kujadili ununuzi wa ndege hizi? (Silaumu sababu mtukufu malaika kupitia vuvuzela alipiga marufuku wananchi kupata matangazo ya moja kwa moja ya bunge lao ). Ngoja niondoke ntarudi kesho na ntaanzia hapa nilipoishia
 
Na ndio sababu hilo shirika lilishindwa kutoboa. Maana hata enzi hizo ndege ilikua kwa ajili ya pride na sio hitaji halisi.

Kenya airways uliotaja ni hasara tupu inaendeshwa na pesa za walipa kodi. Slogan yake ni 'pride of Africa'. Ni ufahari tu ndo maana wanaendelea kulihudumia.

Ndio NN unaeza kula jojo na unachat kwenye smartphone ukiwa unafata chips dume. Kama starehw au staftahi.

La kama huna namna ya kula na ukaamua kununua smartphone badala ya walau chakula na kuwekeza, utaendelea kuwa fukara na ombaomba maisha yote na kubaki kujiuliza umelaaniwa na nani?

So ndege hata kwa sasa haipaswi kwa kipaumbele cha serikali. Serikali iwekeze kwenye yale yanayozalisha na kujumuisha wengi, ndege zitaongezeka zenyewe hasa kama serikali inaweka mazingira wezeshi kwa mashirika binafsj ya ndege.

Kikubwa hapa ni kwamba serikali haina sababu kuendesha biashara ya ndege. Waachiwe sekta binafsi watapambana nayo vizuri tu. Mind you kama nchi tuna ndege.

Sitashangaa hii ATCL ikifa tena. Kama si leo basi utawala huu ukitoka ujao lazima ifeli tena. Ukikosea kupanga hata utekeleze vizuri vipi, hutapata matokeo tarajali.
 
Tatizo akili zetu hazijishughulishi na kusoma na kujua. Mfano mtu anasema hatuma mpango hivi kweli tumekuwa wajinga kiasi hiki. Mpango wa maendeleo uliopitishwa na bunge tumeusoma kweli. Mpango na bajeti wa kila mwaka wa fedha je. Mipango ya kisekta je tumesoma. Mfano agricultural sector development program two je. Hivi tutafika kwa uzembe huu wa kuto kusoma
We umesoma hayo? Upi unazungumzia ndege 2 kufikia sept 2016? Je sera ya afya inasemaje? Sera ya elimu au mpango wa elimu unasemaje kuhusu madawati? Mi sijui bali kama zipo nna uhakika hazifuatwi.

Haiwezekani nchi haina chanjo ya pepopunda wala madawati ya kutosha halafu unanunua ndege cash bilioni 120 unanambia unatekeleza mpango wa maendeleo. Yapi hayo wakati watu wanakuza pepopunda na watoto hawana pa kukaa shule?
 
Denoo49, umeusemea moyo wangu na ninakushukuru. Binafsi mawazo yangu yameenda mbali zaidi nikawaza na kuwafikiria walio wengi katika nchi yetu ambao ni masikini sana.

Kuna sehemu huku umang'atini na umbuluni ambako watu wanaishi hadi km 10 toka zahanati iliyo karibu zaidi. Natafakari mazao yanayooea shambani (nyanya na vingine vingi) na kutamani viwanda ili kuchakata mazao ya kilimo.

Nafikiria akina mama katika sehemu nyingi nchini ambao hata ndoa zao na maisha ya kifamilia yako katika hali tete sababu lazima waamke saa tisa alfajiri kwenda kuteka maji na kusafirisha kwa punda au vichwa vyao na kufika majumbani kwa masaa sita hadi nane baadaye!

Nafikiria mtandao wa njia ya reli nchi nzima kama namna nzuri ya kuwapatia walio wengi njia rahisi ya kusafiria na kusahirisha bidhaa mbalimbali; kufanya hata barabara zetu zidumu kwa muda mrefu zaidi.

Kiongozi anayejali masikini natarajia vipaumbele vyake viendane na hali halisi.

Kwa bahati mbaya awamu hii uongozi unataka kufanya yale ambayo yatashangiliwa haraka haraka; yale ambao yanawezekana kukamilika mapema mapema ili by 2020 iwe rahisi kuwaonyesha wapiga kura wachache mafanikio huku walio wengi (wa loolera na balangdalalu) wakishangilia na kupiga kura bila kufikiri.

Ngoja tuone labda kabla ya 2020 focus itabadilika na kuwalenga walio wengi. Vinginevyo Tanzania ya viwanda itabakia kuwa ndoto.
Mkuu leo, nilikuwa natazama ITV kipindi cha Haki Elimu, walikuwa shule moja hivi inaitwa Muungano(sikuweza kupata details haraka ipo wilaya na mkoa gani tz). Kiukweli kidogo nidondokwe na chozi muda wote niliokuwa natazama hicho kipindi, hilo darasa hata zizi la ng'ombe linanafuu. Wanafunzi wanakalia mawe, choo kimejengwa kwa kuta za nyazi, mbaya zaidi kuna darasa wamechanganyika wanafunzi wa Darasa la 2,3 na 4, kila Mwalimu husika wa Darasa lake anapoingia darasani, inawalazimu wanafunzi wengine kumsikiliza.

Alafu leo anakuja mtu anaelezwa hali halisi ya nchi ilivyo anakuja na siasa uchwara.
Haki ya Mungu nahapa, kama tusipokuwa makini katika kuangalia vipaumbele vya maendeleo na uwiano wa mahitaji, katu hatutokaa tutoke hapa tulipo zaidi ya kuongengeza gap la walio nacho na wasiokiwanacho.

Hata hizo ndege zenyewe kuna siku zitapotea kama zilivyopotea zilizokuwepo, na shirika kufa kama lilivyokufa mwanzo. Tumekuwa mazuzu ndani ya nchi yetu na rasilimali zetu.

Nini tunapata viongozi wa kuacha kumbukumbu za kufutika haraka kama upepo, kosa lipo wapi kwa hao viongozi. Leo hii katika hawamu zote ni Nyerere na Sokoine, sijui waliopita walishindwa nini, au kukosea wapi.?
 
Tatizo akili zetu hazijishughulishi na kusoma na kujua. Mfano mtu anasema hatuma mpango hivi kweli tumekuwa wajinga kiasi hiki. Mpango wa maendeleo uliopitishwa na bunge tumeusoma kweli. Mpango na bajeti wa kila mwaka wa fedha je. Mipango ya kisekta je tumesoma. Mfano agricultural sector development program two je. Hivi tutafika kwa uzembe huu wa kuto kusoma
Majibu yangu yangekuwa sawa na haya chini
1
Asante Mkuu nimekuelewa na nyakati zilizopita niliwahi kujiuliza; hivi sasa hatuna vipaumbele?, na je tunaweza kufikia mahala tunaamua kununua vitu visivyowanufaisha walio wengi kwa matamko ya jukwaani. Wangapi kwa nauli ya ndege kutoka Dar mpaka Kwanza wanaweza kuimudu?! Sasa hivi huduma za afya zipo hoi (wana lumumba nendeni muhimbili mkaone maana hamchelewi kubisha) hata dawa hakuna, leo wanaoshangilia kwenye uzinduzi wa "panga boy" wanajua kama bunge lilipewa nafasi kujadili ununuzi wa ndege hizi? (Silaumu sababu mtukufu malaika kupitia vuvuzela alipiga marufuku wananchi kupata matangazo ya moja kwa moja ya bunge lao ). Ngoja niondoke ntarudi kesho na ntaanzia hapa nilipoishia

2
We umesoma hayo? Upi unazungumzia ndege 2 kufikia sept 2016? Je sera ya afya inasemaje? Sera ya elimu au mpango wa elimu unasemaje kuhusu madawati? Mi sijui bali kama zipo nna uhakika hazifuatwi.

Haiwezekani nchi haina chanjo ya pepopunda wala madawati ya kutosha halafu unanunua ndege cash bilioni 120 unanambia unatekeleza mpango wa maendeleo. Yapi hayo wakati watu wanakuza pepopunda na watoto hawana pa kukaa shule?
 
Tatizo akili zetu hazijishughulishi na kusoma na kujua. Mfano mtu anasema hatuma mpango hivi kweli tumekuwa wajinga kiasi hiki. Mpango wa maendeleo uliopitishwa na bunge tumeusoma kweli. Mpango na bajeti wa kila mwaka wa fedha je. Mipango ya kisekta je tumesoma. Mfano agricultural sector development program two je. Hivi tutafika kwa uzembe huu wa kuto kusoma
Mipango inabaki kwenye makaratasi, ila utekelezwaji wa dira ya Taifa ni ilani ya chama, ambayo kila baada ya miaka 5, imabadilishwa haijalishi iliyopita ilikamilika au haikukamilika.
 
Kwa hiyo hatuwezi kununua ndege zetu wenyewe kwa sababu hospitali hazina vifaa vya kutosha?
Hizo ndege zitabeba wagonjwa si ndio maana hospitali hazina chanjo vijana wengi wako mitaani wslioko ajiran baadh yao wapo majumban kwa uhakiki zaid jee hizo ndege zinajiendesha bila kuwa na watu wenye afya bora kukiwemo na mahtaj muhimu au zitasafirisha buree
 
Kutokuridhika kwa binadamu ni jambo la kiasili.

Kunung'unika nako ni ada ya mja.

Bila ya kupoteza sana muda ngoja nizame moja kwa moja kwenye hoja.

Baada ya ununuzi wa hizi ndege za shirika letu la ndege, kumekuwepo na hoja kadha wa kadha zinazohoji eti kwa nini mheshimiwa MTUKUFU rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali yake wananunua ndege ilhali sehemu nyingi za Tanzania hazina viwanja vya ndege, eti hatuna sukari ya kutosha, hatuna sijui mashine gani mahospitalini, na kadhalika na kadhalika.

Sasa nami hebu ngoja niulize [maswali] yangu:

Hivi, kwani wakati ule tulipokuwa na zile ndege zetu za ATC, tulikuwa na viwanja vingapi vya ndege huko mikoani na wilayani?

Je, wakati ule hospitali zetu za serikali zilikuwa na kila kitu? Bugando ilikuwa na mashine zote zilizokuwa zinahitajika? Muhimbili nayo ilikuwa imejitosheleza kwa kila kitu?

Sukari, unga, sabuni, na mahitaji mengine nayo tulikuwa tumejitosheleza nayo vizuri tu?

Hizo Fokker Friendship [nadhani walikuwa nazo mbili au zaidi] za ATC ziliweza kutua hata huku kwetu Ikungulyabashashi, Ng'wamapalala, Lamadi, Madale, na Nyangokolwa?

Nchi zingine zilizo na mashirika yao ya ndege zenyewe zimetatua matatizo yake yote kabla ya kuamua kuwa na ndege zake zenyewe?

Huko Kenya kwa mfano, wao kila hospitali yao ina kila kifaa kilicho cha muhimu?

Sasa labda mimi kwa vile ni mbeba maboksi tu nisiye na elimu yoyote ile kubwa [niliishia kidato cha nne ambapo nilipata daraja la nne na pointi 30] ndo maana labda kwa kiasi fulani sizielewi hizo hoja za baadhi ya hao vipanga wanaozitoa.

Lakini nadhani mtu unaweza ukawa unatafuna jojo huku ukitembea na kuongea kwenye simu yako ukiwa unaelekea kwa Joji kwenda kula kiti moto au chipsi vumbi.
Nadhani mkulu sasa atafanya ziara za nnje kwavile amenunua ndege zake!!!!
 
Back
Top Bottom