Ananunua ndege wakati hiki na kile hatuna...

Ananunua ndege wakati hiki na kile hatuna...

Kutokuridhika kwa binadamu ni jambo la kiasili.

Kunung'unika nako ni ada ya mja.

Bila ya kupoteza sana muda ngoja nizame moja kwa moja kwenye hoja.

Baada ya ununuzi wa hizi ndege za shirika letu la ndege, kumekuwepo na hoja kadha wa kadha zinazohoji eti kwa nini mheshimiwa MTUKUFU rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali yake wananunua ndege ilhali sehemu nyingi za Tanzania hazina viwanja vya ndege, eti hatuna sukari ya kutosha, hatuna sijui mashine gani mahospitalini, na kadhalika na kadhalika.

Sasa nami hebu ngoja niulize [maswali] yangu:

Hivi, kwani wakati ule tulipokuwa na zile ndege zetu za ATC, tulikuwa na viwanja vingapi vya ndege huko mikoani na wilayani?

Je, wakati ule hospitali zetu za serikali zilikuwa na kila kitu? Bugando ilikuwa na mashine zote zilizokuwa zinahitajika? Muhimbili nayo ilikuwa imejitosheleza kwa kila kitu?

Sukari, unga, sabuni, na mahitaji mengine nayo tulikuwa tumejitosheleza nayo vizuri tu?

Hizo Fokker Friendship [nadhani walikuwa nazo mbili au zaidi] za ATC ziliweza kutua hata huku kwetu Ikungulyabashashi, Ng'wamapalala, Lamadi, Madale, na Nyangokolwa?

Nchi zingine zilizo na mashirika yao ya ndege zenyewe zimetatua matatizo yake yote kabla ya kuamua kuwa na ndege zake zenyewe?

Huko Kenya kwa mfano, wao kila hospitali yao ina kila kifaa kilicho cha muhimu?

Sasa labda mimi kwa vile ni mbeba maboksi tu nisiye na elimu yoyote ile kubwa [niliishia kidato cha nne ambapo nilipata daraja la nne na pointi 30] ndo maana labda kwa kiasi fulani sizielewi hizo hoja za baadhi ya hao vipanga wanaozitoa.

Lakini nadhani mtu unaweza ukawa unatafuna jojo huku ukitembea na kuongea kwenye simu yako ukiwa unaelekea kwa Joji kwenda kula kiti moto au chipsi vumbi.

Mimi binafsi nafikiria hivi,
Badhi ya wizara hazina kipato maalum cha kujiendesha kwa hiyo asilimia kubwa ya budget yao anategemea kodi zetu, mfano elimu, afya, ulinzi na jeshi lapolisi na kadhalikia. Ili hela za serikali au hazina ziongezeke inabidi serikali itafute njia nyinyi za kuongeza kipato. Utalii ni mmoja yapo ya kipato hapa nchini, kwa hiyo ili ili kuboresha Utalii inabidi kuboresha na usafiri. Na pia wafanya biashara wanahitaji usafiri bora ili biashara zao ziende kiurahisi. Kwa hiyo usafiri wa anga ni muhimu sana kwa wafanya biashara.
Kwa hiyo kufufuliwa hili shirika ni muhimu sana. Si lazima tuwe na ndege zinazo kwenda international. Mbona hapa Sweden hawana ndege za nje na hakuna anayepiga kelele na kukashifu kwamba hawana hizo ndege kubwa za kwenda nje.
 
Logic za watu wengine mimi sizielewi kabisa.

Unakuta mtu anauliza eti ndege zitamsaidiaje au zitamnufaishaje bibi yake aliyeko kijijini!

Wengine ni wa kuwaacha tu kwa kweli.

..mimi ni mmoja wa wanaopinga ununuzi wa ndege hizo, na mpango wa serekali wa kufufua shirika la ndege atcl.

..sababu zangu ni kwamba biashara ya usafiri wa anga/ndege ni biashara ya HASARA.

..katika bara zima la Afrika ni shirika moja tu, Ethiopia, ambalo linaendeshwa kwa faida. Rwanda ambao tunataka kuwaiga shirika lao linaendeshwa kwa hasara. Kenya nako ni hasara tupu.

..mashirika ya ndege yanayofanya vizuri duniani ni yale ya nchi za Kiarabu ambayo nayo inasemekana yanabebwa kwa kiasi kikubwa na serekali zao ambazo zina utajiri wa fedha za mafuta na gesi.

..Kwa hapa Tz tayari tumeshapata taarifa za ATCL kuendeshwa kwa HASARA tangu ndege mbili mpya za JPM ziletwe.

..Sababu nyingine ni kwamba fedha tulizoelekeza kwenye manunuzi ya ndege ni nyingi mno kuziwekeza nje. Na matumizi yake hayapitii hata kidogo ktk mikono/mifuko ya wa Tz.

..Watengenezaji wa hizo ndege hawatumii malighafi toka Tz. Pia hawaajiri waTz ktk hatua yoyote ile. Wao wako Canada, na wanalipa kodi huko.

..Kwa hiyo fedha hizo ambazo ni mabilioni ya shilingi ni fedha za masikini wa Tz tumewapa zote waCanada. Baada ya hapo wanatuletea ndege ambazo zitatutia hasara kwa kipindi kirefu ktk matumizi yake.

..Kwa hiyo mimi siafiki nchi yetu masikini kuwekeza ktk nchi tajiri kwa jambo ambalo hata halitakuja kutusaidia. T

..Uwekezaji ambao mimi nitauunga mkono ni ule ambao tuna uhakika kwamba utakuja kutuletea faida ktk kipindi kifupi au hata kirefu.

..Uwekezaji tunaopaswa kufanya ni ule ambao utatuwezesha kuzalisha mali zaidi na kuwa jamii inayojitegemea.

..Serekali ingeelekeza fedha hizo kufufua mazao kama Pamba, Korosho, Chikichi, Alizeti,.. ningeunga mkono kwa moyo mmoja. Kwanza uwekezaji wa aina hiyo unawagusa waTz wengi. Pili ungeongeza mapato yetu ya ndani na kutusaidia tusonge mbele ktk jitihada zetu za kujitegemea.

..Mwisho, nikirudi sasa ktk hoja yako, ni kweli tunanunua ndege huku hatuna maji, madawa, etc. JE, uwekezaji ktk ndege utatupatia faida na mapato ambayo yataongeza uwezo wetu wa kugharamia miradi ya maji, afya, na huduma nyingine za kijaamii? Kwa maoni yangu, jibu ni HAPANA.

Cc mkolosai
 
Back
Top Bottom