Nyani Ngabu mbona unalitaja taja jina langu!
Lekaga gete nkoyi!
Kuna baadhi ya watu hawafahamu kuwa wakati ndege za ATC zinapishana kwenye anga la Ulaya, sisi hapa Ng'wamapalala hatukuwa hata na uwanja wa mpira achilia mbali uwanja wa ndege.
Shuleni tulikuwa tunakaa kwenye mawe tuliyoenda kutafuta na kuyapata mlimani achilia mbali madawati.
Angalau huduma ya afya tulikuwa tunapata kwenye dispensary ya kanisa katoliki ambayo ilikuwa inahudumia zaidi ya kata nzima ya Ng'wamapalala.
Unga tulikuwa tunanunua kwenye duka la kijiji kwa kupanga foleni.
Basi la kutoka Bariadi kwenda Shinyanga lilikuwa linapita mara moja baada ya siku mbili au wiki.
Usafiri wa uhakika wa kwenda Bariadi ilikuwa ni baiskeli.
Kupanga ni kuchagua!