jogi
JF-Expert Member
- Sep 25, 2010
- 25,556
- 25,369
Ubaya unaongezeka pale vipaumbele vyenyewe anaamua mtu mmoja!! Kwa ubora gani aliokuwa nao? (ni rahisi kuhoji hivyo)
Mkuu, ebu fikiria vizuri. OK, umeongelea kwa kipindi kile, je unakumbuka idadi ya watu na uwiano wa mahitaji yao ya msingi.?
Leo Tanzania ina watu si chini ya milioni 45, je unahisi kuna uwiano wa mahitaji yao ya msingi, mfano kupata huduma bora za Afya, Malazi bora na Elimu bora.
Watu wanapanga foleni kila mahali siku hizi, sio hospital, kwenye mabenki, barabrani, baadhi ya maofisi ya umma.
Tuna matatizo mengi, sana na makubwa kuliko hata hilo la ndege.
Kwa mwando huu wa kuchagua vipaumbele vya maendeleo pasipo kufanya tafiti za kina na kutosha, tutabaki tunaruka sarakasi wakati bado tupo kwenye vazi la kanzu na msuli, kufaidisha wengine.