Ananikera hiki kitabia cha shagalabagala

nishawahi kuwa nae wa hivyo tulishindwana ,mimi kwanza nina kinyaa hata chakula chake nilikuwa naogopa kukila ,kuna wakati anajisahau ndoo ya kuogea anachotea maji ya kuosha vyombo huyo hakufai mwache atafute wachafu wenzake
 
Almost 5 years sasa niko kwenye relationship na dada mmoja, sawa kila binadamu ana mapungufu ila kiukweli hakuna kitu sipendi kama mtu kua disorganized hio ni sifa nambari 1 kwangu itayo fanya hata uwe mdogo wangu wa damu chumbani kwangu ntaku timua haraka sana. Napenda sana usafi, napenda kukaa au kutumia vitu vyenye usafi wa hali ya juu doa moja tu niki liona huwa nakata tamaa haraka sana.

Sasa basi huyu dada bwana yuko sooo disorganized yani, mara ukute vitu vime rushwa rushwa tu, nguo chafu zina kaa muda mrefu kwenye tenga, wakati mwingine akisha vaa nguo na jasho lote ana kunja ana rudisha kabatini, kama haitoshi hata mikoba yake tu ina vumbi usi ongelee viatu sasa.

Nilisha jitahidi sana kumwambia "bwana mimi hii tabia yau shagalabagala sipendi kwanini usifute vitu vyako vikae katika hali ya usafi una onekana kuto kujali hata vitu vyako ulivyo nunua kwa pesa yako?! "Na mengine kede wa kede.

Wadau pengine kuna njia mbadala ambayo inaweza saidia em tushirikishane hapa huwezi jua utakuja kutana na dada wa aina hio mbeleni na majibu ya uzi huu yaka kusaidia.

Nawasilisha bandugu!
Aisee.... yaani nilivyoona hii thread yako nimejikumbuka mimi. Yaani niko disorganised to the highest degree aisee!!! Nakumbuka nilivyokuwa nimeanza uhusiano na wife(kabla ya kuoana) alilalamika sana kuhusu hii ishu!! Maana wife anapenda sana organisation!! Mwisho wa siku nahisi aligundua kuongea sana haisaidii, tunaishia kugombana tuu; Akaanza kufanya kwa vitendo kujaribu kuweka order kila akikuta vitu viko hovyo hovyo!!
Nadhani ni zaidi ya tabia aisee, ni kitu fulani kama kinakuwa kwenye vinasaba hivi(genes); Ni ngumu sana kumbadilisha mtu wa hivi!! Mimi hata wife kipindi hicho hatujaoana alikuwa akilalamika kwanza yaani namshangaa yeye, kwamba huyu nae vipi?? Mbona ana mind vitu vidogo vidogo hivi?
Yaani mimi hata ukiniuliza my favourite colour; Sijui niseme sina au sijui!!!I just do not give a shit about vitu vimekaaje, vina rangi gani, vinatakiwa vikae vipi!! Hata wife anaweza akabadilisha order ya kupanga vitu sebuleni au chumbani; Na ikapita hata wiki nzima nisigundue hadi wife anishtue!!!!!!!
Unachotakiwa kufanya ni kujua kuwa hiyo ndiyo tabia ya mwenzi wako; Na kutafuta njia za jinsi ya kuishi nae in a way kwamba wewe utakuwa hukasiriki!! Otherwise bro kujipa moyo kwamba utambadilisha, ni kazi ngumu na ya muda mrefu, na unaweza ku end up with disappointment. bbwaoy The Boss Evelyn Salt
 
Last edited by a moderator:
Kuna ile unatoka job ukivua nguo unaiacha hapo hapo ulipovulia, soksi inapotea moja moja kwa sababu unaziweka bila mpango, ukitaka kula ukichukua sahani ukakaa sehemu unaiacha hapo hapo unaendelea na mishe zako.

Sasa wife alilalamika sana mwanzoni, ameshatenga kisehemu cha nguo chafu, cha kuweka vyombo ukimaliza kula, cha kutundika soksi zilizovuliwa, sijui chupi etc etc. Nikifanya kwa siku mbili tu naona kero, utaratibu una resume kama mwanzo.

Baadae ilifikia yeye mwenyewe ndo inabidi ajue nimeweka wapi ili apeleke mahali husika na maisha yanaendelea vizuri baada ya kuzoeana.

Haha mpaka sahani bro? Acha tu alalamike. Siwezi kuacha chombo nilichotumia na kuondoka.

Soksi ninazo pair 2 tu, so lazima nizitunze. Mi shida ni nguo kitandani na viatu chini ya kitanda. Kila nikijitahidi nipange, hata siku 2 hazizidi panarudi vile vile. Ni kama kuna mtu huwa ananifanyia uhuni. Nina mpango wa kufunga surveillance camera ili nimjue m'baya wangu.
 
Kabla sijaoa soksi zilikuwa zinapotea sana, unakuta nikivua viatu nje soksi naingia nazo ndani! Sasa unakuta asubuhi unataka kwenda job unaona moja ya pair hii haipo na ya pair nyingine haipo inabidi utinge soksi tofauti, dawa yake nilikuwa nanunua soksi nyingi zinazokaribia kufanana ili hata nikivaa tofauti hakuna shida.
 
akiwa na mtoto sipati picha maana hapa tangu asubuhi nmedeki mara5, shuka 2 kachafua nmetoa duuu
 
Kabla sijaoa soksi zilikuwa zinapotea sana, unakuta nikivua viatu nje soksi naingia nazo ndani! Sasa unakuta asubuhi unataka kwenda job unaona moja ya pair hii haipo na ya pair nyingine haipo inabidi utinge soksi tofauti, dawa yake nilikuwa nanunua soksi nyingi zinazokaribia kufanana ili hata nikivaa tofauti hakuna shida.
Hahaha. Kwa hiyo mzee, juu umekula suti, ndani soksi tofauti?

Mi kila nikivua viatu napitiliza na soksi zangu bafuni ili nizifue kwa ajili ya kesho kutwa. Discipline yangu kwenye hii issue ni 12/10.
 
Haha mpaka sahani bro? Acha tu alalamike. Siwezi kuacha chombo nilichotumia na kuondoka.

Soksi ninazo pair 2 tu, so lazima nizitunze. Mi shida ni nguo kitandani na viatu chini ya kitanda. Kila nikijitahidi nipange, hata siku 2 hazizidi panarudi vile vile. Ni kama kuna mtu huwa ananifanyia uhuni. Nina mpango wa kufunga surveillance camera ili nimjue m'baya wangu.
ha ha ha ha... we ni hatari asee!
 
mito njoo uone huyu anakaa na mwanamke miaka mitano bila kumuoa...
 
Last edited by a moderator:
Hahaha. Kwa hiyo mzee, juu umekula suti, ndani soksi tofauti?

Mi kila nikivua viatu napitiliza na soksi zangu bafuni ili nizifue kwa ajili ya kesho kutwa. Discipline yangu kwenye hii issue ni 12/10.

Safi sana, maana mimi pia nilianza kufikiria kuna hujuma kwenye soksi, ila baada ya kudhibitiwa na wife sasa hii siyo shida, pengine mwenyewe aibu inanishika tu, unakuta vitu vimepangwa kiasi ambacho inabiti ufuate utaratibu.

Na baada ya kuwa baba, ukifika dogo huyu kwa hiyo anajua soksi za baba zinakaa wapi, viatu anavipeleka mahali pake huku amevivaa.
 
Almost 5 years sasa niko kwenye relationship na dada mmoja, sawa kila binadamu ana mapungufu ila kiukweli hakuna kitu sipendi kama mtu kua disorganized hio ni sifa nambari 1 kwangu itayo fanya hata uwe mdogo wangu wa damu chumbani kwangu ntaku timua haraka sana. Napenda sana usafi, napenda kukaa au kutumia vitu vyenye usafi wa hali ya juu doa moja tu niki liona huwa nakata tamaa haraka sana.

Sasa basi huyu dada bwana yuko sooo disorganized yani, mara ukute vitu vime rushwa rushwa tu, nguo chafu zina kaa muda mrefu kwenye tenga, wakati mwingine akisha vaa nguo na jasho lote ana kunja ana rudisha kabatini, kama haitoshi hata mikoba yake tu ina vumbi usi ongelee viatu sasa.

Nilisha jitahidi sana kumwambia "bwana mimi hii tabia yau shagalabagala sipendi kwanini usifute vitu vyako vikae katika hali ya usafi una onekana kuto kujali hata vitu vyako ulivyo nunua kwa pesa yako?! "Na mengine kede wa kede.

Wadau pengine kuna njia mbadala ambayo inaweza saidia em tushirikishane hapa huwezi jua utakuja kutana na dada wa aina hio mbeleni na majibu ya uzi huu yaka kusaidia.

Nawasilisha bandugu!

Unapenda anavofanya na unampenda pia na unapenda huo urafu wake,5 years na bado umeshindwa kumrekebisha wala kumuacha?
Usitake watu wawe wanafiki hapa..
 
nishawahi kuwa nae wa hivyo tulishindwana ,mimi kwanza nina kinyaa hata chakula chake nilikuwa naogopa kukila ,kuna wakati anajisahau ndoo ya kuogea anachotea maji ya kuosha vyombo huyo hakufai mwache atafute wachafu wenzake

Duh mchafu mpk jikoni?? Hapan uyo amazidi buanaa
 
Safi sana, maana mimi pia nilianza kufikiria kuna hujuma kwenye soksi, ila baada ya kudhibitiwa na wife sasa hii siyo shida, pengine mwenyewe aibu inanishika tu, unakuta vitu vimepangwa kiasi ambacho inabiti ufuate utaratibu.

Na baada ya kuwa baba, ukifika dogo huyu kwa hiyo anajua soksi za baba zinakaa wapi, viatu anavipeleka mahali pake huku amevivaa.

The inspiration I needed bro, thanx. Soon natupia tangazo kule love zone. Nimechoshwa na hii hali.
 
Haujatuambia, Mkuu vipi kwa bibi mlandizi pako untidy pia!!!
 
Mim Nina tatzo LA kutokuja Nguo zangu jaman nakunja Leo kesho navurugua yan tangu Mdog,chuo mpk sas nimeolewa nimeshindwa kbs ila za Mr nakunja vzr tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom