Ananikera hiki kitabia cha shagalabagala

Ananikera hiki kitabia cha shagalabagala

bbwaoy

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2015
Posts
466
Reaction score
468
Almost 5 years sasa niko kwenye relationship na dada mmoja, sawa kila binadamu ana mapungufu ila kiukweli hakuna kitu sipendi kama mtu kua disorganized hio ni sifa nambari 1 kwangu itayo fanya hata uwe mdogo wangu wa damu chumbani kwangu ntaku timua haraka sana. Napenda sana usafi, napenda kukaa au kutumia vitu vyenye usafi wa hali ya juu doa moja tu niki liona huwa nakata tamaa haraka sana.

Sasa basi huyu dada bwana yuko sooo disorganized yani, mara ukute vitu vime rushwa rushwa tu, nguo chafu zina kaa muda mrefu kwenye tenga, wakati mwingine akisha vaa nguo na jasho lote ana kunja ana rudisha kabatini, kama haitoshi hata mikoba yake tu ina vumbi usi ongelee viatu sasa.

Nilisha jitahidi sana kumwambia "bwana mimi hii tabia yau shagalabagala sipendi kwanini usifute vitu vyako vikae katika hali ya usafi una onekana kuto kujali hata vitu vyako ulivyo nunua kwa pesa yako?! "Na mengine kede wa kede.

Wadau pengine kuna njia mbadala ambayo inaweza saidia em tushirikishane hapa huwezi jua utakuja kutana na dada wa aina hio mbeleni na majibu ya uzi huu yaka kusaidia.

Nawasilisha bandugu!
 
Unapomwambia mwelekeze kwa mifano mkuu mfano mkoba una vumbi mwelekeze huku unafuta, nguo akikunja kabatini zina jasho zitie kwenye beseni la maji mwishowe atajua unakereka na atajistukia ataanza kubadilika
 
Five years of relationship??? Unamsomea nn mwenzio?? Sema nae atakuelewa Tu ILA fanya haraka umuoe
atamuoaje mtu mchafu?? ukichunguza sana hapo ni kwamba jamaa anabaki kwa ajili ya shida tu ya kiu... hana access na better options

Hebu imagine unakua na nguo chafu halafu unaweka kabatini?? does that make sense?
 
Almost 5 years sasa niko kwenye relationship na dada 1 hivi.... ni muhaya, sawa kila binadamu ana mapungufu ila kiukweli hakuna kitu sipendi kama mtu kua disorganized..hio ni sifa nambari 1 kwangu itayo fanya hata uwe mdogo wangu wa damu chumbani kwangu ntaku timua haraka sana. Napenda sana usafi, napenda kukaa au kutumia vitu vyenye usafi wa hali ya juu doa moja tu niki liona huwa nakata tamaa haraka sana... sasa basi huyu dada bwana yuko sooo disorganized yani, mara ukute vitu vime rushwa rushwa tu, nguo chafu zina kaa muda mrefu kwenye tenga, wakati mwingine akisha vaa nguo na jasho lote ana kunja ana rudisha kabatini, kama haitoshi hata mikoba yake tu ina vumbi usi ongelee viatu sasa... nilisha jitahidi sana kumwambia "bwana mimi hii tabia yau shagalabagala sipendi kwanini usi fute vitu vyako vikae katika hali ya usafi una onekana kuto kujali hata vitu vyako ulivyo nunua kwa pesa yako??!! "Na mengine kede Wa kede .. wadau pengine kuna njia mbadala ambayo inaweza saidia em tushirikishane hapa... huwezi jua utakuja kutana na dada wa aina hio mbeleni na majibu ya uzi huu yaka kusaidia...... na wasilisha bandugu!!!!

Mkuu pole!
Mnaishi pamoja?
Kabla ya hapo mlikuwa hamtembeleani ili kujua ndani kwake yuko vipi?
Nguo zikaa mda mrefu kwamba hata jmosi au Jpili hafui?
Ukimchunguza sana bata hutomla! Kama ktk vyote unavovitaka shida ni hicho tu basi mvumilie ukijua hakuna binadamu aliyekamilika ! Ukiona hajanya wewe fanya mwisho atajistukia na ataweza fanya mwenyewe! Ila uoaneni sasa! !
 
umeshachukua hatua ya kumwelekeza kwa staha? kama bado jaribu hivyo kisha sikilizia uone bàada ya Siku kadhaa!
 
Kabila hilo ndvyo walivyo, hapo usihangike hata kutafuta ushauri chagua moja kuvumilia tabia hiyo au kupiga chini mzigo.
 
Muache tu huyu hakufai akatafute wachafu wenzake maana uchafu kwake upo damuni!
Na hapo akizaa utahama mji huo kwa harufu za ajabu
 
atamuoaje mtu mchafu?? Ukichunguza sana hapo ni kwamba jamaa anabaki kwa ajili ya shida tu ya kiu... Hana access na better options

hebu imagine unakua na nguo chafu halafu unaweka kabatini?? Does that make sense?

ukimchunguza sana bata hauwezi uka mla
 
Haya ndo mahusiano yanayodumu miaka na Miaka ila Mkiingia kwenye Ndoa Miezi tu mmeachana...

Huyo Akiingia kwenye Ndoa Tegemea Mengine zaidi ... Akishajifungua utamkimbia
 
Mademu wa kihaya ndivo walivyo uchafu mwingi, sometimes mwanamke mpaka ananuka shombolololo, i faced the same problem nikapiga chini mapema sana sasa niko exceptional. Acha kuvumulia mapungufu ya kujitakia
 
Mademu wa kihaya ndivo walivyo uchafu mwingi, sometimes mwanamke mpaka ananuka shombolololo, i faced the same problem nikapiga chini mapema sana sasa niko exceptional. Acha kuvumulia mapungufu ya kujitakia


Hata mimi nilitaka sema hivyo nikaogopa kuambiwa mkabila ila wahaya na wagogo mmmh
 
Kwahy Braza wewe umempendea nn huyo binti miaka mitano yote hiyo, Maana me najua upendo upo kwenye tabia sababu sura hata mbuzi anayo, sasa kama tabia inakukera si umuache?
 
Kabila hilo ndvyo walivyo, hapo usihangike hata kutafuta ushauri chagua moja kuvumilia tabia hiyo au kupiga chini mzigo.

Sio wote bhana, me nina kitu changu kimoja kisafi balaa, si kwake si akija kwangu, yani nyumba inang'ara balaa
 
Muache tu huyu hakufai akatafute wachafu wenzake maana uchafu kwake upo damuni!
Na hapo akizaa utahama mji huo kwa harufu za ajabu

Wewe mbona kila uzi upo? Unatembeza ama? Au wewe ndo wale la 700,000 kwa mwezi? Watu mnakera mpaka basi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom