Tamaa imeniponza, nimeamua kujiachisha kazi

officialBossmtoto

JF-Expert Member
Jul 1, 2019
369
1,178
Nimeamua kuacha kazi na kuingia kwenye udalali huku bosi akinisaka na polisi Mbosso alisema mapenzi Gharama? Ufisi Gharama zaiiidi. Hii haikua kwa kupenda kwangu bali ni tamaa ya kupenda Uchi na hofu ya kupoteza maisha au Uanaume wangu.

Mimi ni kijana wa miaka 28 nilikua nimeajiriwa na nafanya kazi kama sales person kwa boss muhindi. Kuna deal nilisuka tarehe 29-01-2023 na malipo ikabidi yafanyike 30-01-2023. Kutokana na boss kupenda janja janja, hutaka malipo yafanyike kwenye account zetu alafu fedha itolewe na akabidhiwe cash (uzuri huwa hachukui yote anakuachia asilimia kadhaa 5 au 10 inategemea na ukubwa wa deal). Basi biashara hio ya milioni 16 ilifanyika jioni saa moja, sikua na namna ya kuweza kutoa pesa hio. Baada ya kuwasiliana na boss akanipa account moja niweke milioni 7, ingine tutaenda nae bank kesho kulipia kodi ya eneo la biashara.

Nikiwa nyumbani kijitonyama nacheki status kwenye sim nikakutana na status ya binti fulani ivi ambae mwezi wa kumi mwaka jana tulimpelekea bidhaa moja ambayo alinunuliwa na mzee fulani kama zawadi ya birthday. Kadada fulani kazuri sana. Nikajikuta nakatumia meseji na kuanza kuchat nako. Tulichat sana kwanzia hio saa mbili kasoro mpaka saa nne usiku. Nikaanza kumwaga uongo mwingi ikiwa ni pamoja na kumwambia kwamba ile kampuni ilioleta ile zawadi ni yangu mimi.

Tukaanza kuchat topic za usiku zikakolea akaanza kunitumia stickers zile za hovyo hovyo, nikamwomba mechi akasema kwake maji yalikatika ivo yupo hotelini tu mwenyewe kama vipi niende. Kidume huyo nikaoga nikatoka. Kama maelekezo yalivosema nikifika mbezi shamo tower nimpigie sim anielekeze zaidi nikafanya vile na akatuma live location. Chakushangaza nafika sio hotel bali ni nyumba ( zile apartment za kukodi) nikaingia nikafanya inspection ya haraka haraka nikagundua tuko wawili tuu mule ndani.

Ilikua mida ya saa sita kasoro tulivoanza mvurugano mpaka saa nane na nusu. Yule binti alikua na ushetani mwingi sana. Itoshe kusema kwamba kuna vitu mtu unaapa kabisa hutokaa kufanya ila ukiwekwa kwenye kitengo unajikuta unalamba asali . Sheria na kanuni zinanikumbusha kulala kwa mwanamke mwiko. Nikanyanyuka nikaoga nikaanza kuaga. Nikasema kimoyo moyo nijiandalie mazingira ya kupakua tena next time acha nimpe chochote kitu japo hatukua tumekubaliana.

Nikamuuliza kama namba yake inapokea pesa akasema ngoja nikupe account ya bank. Akanipa na mwanaume nilikua na 85,000 tu kwenye sim, nikamuwekea 82,000 alafu nikamwambia “hicho kidogo utapata supu asubuhi”. Akachukua sim akaangalia alafu akaniuliza kwa kejeli “kwa hio umeniona mimi mwanafunzi wa chuo?” Ehhhhh haraka haraka ikanijia picha ya mandonga inasema “UMEYAKANYAGA” duh nikakaa kimya kama sekunde kumi kisha nikamwambia “mbona hatukukubaliana hela mi nimetoa tu kama shukrani” akacheka kwa dharau, akatoa funguo mlangoni akazirusha nje ya nyumba alafu akasema “Unaonekana kabisa ushazoea K**ma za 20,000 mbwa wewe leo umeingia 5 star”

Nikajichekesha hapo kumtoa kwenye hasira maana kila nikiwaza kitafata nini sipati picha. Binti alikua mrembo sana ila ghafla nilianza kumuona MWAMBA HUYU HAPA. Nikamwambia “Haya mambo yanaongeleka bana em njoo kaa hapa tuongee” akanijibu kwa upole akawa amepoa akasema “ongeza pesa kwanza nitakuja hata ukitaka tena nitakupa”. Nikaona huu mtego huu. Acha niongeze hela alafu nisepe. Nikajiona sio kesi acha nipunguze laki kwenye faida ambayo ningepata kutoka kwa boss. Nikaingia App ya Bank Nikamsukumia laki nikamwambia, “Chukua pesa hio mama, mimi sio mchoyo tatizo napenda tujuane ndo utakula sana hela zangu” akaguna kisha akasema skia kaka angu “Vinyeg* vyako vitakuja kukuponza uvunjiwe heshima, sku ingine Nenda riverside au sinza, mbona unapata tuu kila kitu kwa bei yako ila sisi tuache kama tulivo. Tunajibrand”

Nikasema kimoyo moyo acha nikubali dharau niondoke nisimjibu wala nini. Kila nikijaribu kujiambia kimoyo moyo kwamba pisi yenyewe mbovu tuu, uhalisia unaniumbua. Huyu dada ni kifaa sio poaaa. Nikamwambia kwa sauti kavu isio na mashaka “basi sawa kama umeona ivo. Ila ningekupa vitu vingi sana. Kwa io sasa hapa tunatokaje na funguo umetupa nje”?

Akacheka afu akauliza “utoke uende wapi? Kwa io 180,000? Em kua serious, this is a very expensive p•ssy kaka, umeparamia bila kujipimia kama ni size yako” muda mwingi alikua na sim yake anachat hapo na mimi nikaona sasa dharau zimezidi nikaanza kufoka nikamsogelea nikamkoromea sana. Wakati naendelea kufoka nikaskia mlango unafunguliwa na ghafla wakingia washkaji watatu. Kuna ubaridi usio wa kawaida ulinipiga kwanzia miguuni mpaka kichwani. Sikumbuki nilifikaje kwenye kochi na kukaa maana nilikua katikati ya sebule nimesimama.

Kwa muda wa kama dakika tatu nilikua nimepigwa na bumbuwazi. Nilikua naona ila sielewi nachokiona. Mapigo ya moyo yakawa yanadundia kwapani. Jamaa wakasogea karibu kidogo. Wawili wakawa wanazungumza na dada pembeni mwingine akaja kusimama mbele yangu na kwa kejeli akauliza, “Unaonekana una Ny**ge sana wewe? Una Christmas ngapi hapa Dar?”
Midomo ilikua mizito sana, nilishindwa kujibu nikawa nakigugumizi. Wale wawili wakasogea. Jamaa moja likasema “mdogo etu, haya mambo yanawenyewe. Watu wanamwaga pesa ndefu, viwanja na magari ya maana. Wewe unakuja kuchota tu asali kwa laki na 80? Unataka kutaftia watu kesi za mauaji?” Nikazidi kuhofia maisha na utu wangu. Maneno ya huyu jamaa yakanikumbusha zawadi tulomletea dada siku ya birthday yake. Yule jamaa mmoja mpole akasema we jiongeze jumla ifike laki sita afu tunaweza ongea sasa. Kwa kutetemeka na kuona mwanya wa kujinasua nikaunlock sim haraka sana nikaingia app ya bank na nikaweka 430,000 fasta. Na wakafurahia kuiona. Wakahamisha kwenye sim yao wakitania anaweza akarejesha muamala huyu mpuuzi.

Hapo kichwani napiga mahesabu kwamba bado natumia faida yangu. Maana kwenye 14m yangu ni 1.4m. Basi wakaja wakasema sasa ile 600,000 ni ya kwao watatu watagawana. Hio ni hela ya kutetea wasinidhuru. Natakiwa sasa nimpe dada hela yake kwa sababu amefanya kazi yake tayari. Jasho lilinitoka, nilikua nimechanganyikiwa sijui nifanyeje. Nikiwaza kupiga kelele naona sitofanikiwa chochote maana mazingira ya mtaa sioni mtu yeyote akitoka nyumbani kwake kuja kunitetea kwani ni mitaa ya washua tuu.

Nikaomba kuongea na dada pembeni nikaruhusiwa nikamuita dada pembeni nikamshika mkono nikamtizama machoni, mwanaume hapo natia huruma nyingi sana, kamasi zinataka kutoka ni Pua tu zimekua ndogo, nikamwambia “Kusema ukweli sikujua kama ingekua hivi, saivi ni usiku mwingi, nimechoka na kuchanganyikiwa. Hapa nimeshatumia hela ambayo sio yangu na sijui nailipa vipi. Naomba kujua unataka bei gani kesho asubuhi nikutumie. Niko tayari kukupa hata Nida yangu ukae nayo”

Dada akasema kwa sauti na wapambe waskie “sitaki chochote ambacho sio hela kutoka kwako. Na hela iwe ya maana”. Kisha akanionyesha mwamala kwenye sim yake na meseji kuna kibaba Kimeiva, kimewaka kimetuma milioni tatu alafu kikasema ingine kitatuma siku wataonana. Kisha akasema tena “huyo mwenzio hajatia hata kidole kwenye K**MA YANGU wewe nimekupa vyote jiongeze toa hela ya kueleweka la sivo tunakurudishia laki sita yako na utajua mwenyewe. Uchovu na woga changanya hali ya hewa pale ndani ikazidi kua nzito. Nikiangalia huku na huku sioni pakutokea, nikasema liwalo na liwe, nikachukua sim yangu nikaingia tena kwenye app ya Bank nikaandika milioni, nikafuta, nikaandika mbili nikafuta, nikaweka tatu, ila nikakumbuka mwenzangu katoa tatu hajfanya chochote, nikampa dada sim nikamwambia andika kiasi unachotaka.

Dada akachukua sim akaandika akanirudishia sim. Chozi la uchungu lilinidondoka, chozi lilikua la moto linachoma shavu, maisha yangu yote sijawai tumia milioni sita kwa siku moja paap, yule dada nilimtizama nisimmalize, kila nikitaka kuweka password kidole kinakua kizito. Nikamalizana nae nikamuekea pesa yake. Dada yule baada ya kuona muamala akanikumbatia na kunipa busu shavuni, ila nilihisi kama ananiumiza au ananikera yaani nilikua na hasira mixer maumivu.

Basi kwenye wale jamaa lile limoja la mwanzo likasema nikusindikize utoke mpaka road huu mtaa una vibaka. Nikitaka kumjibu, “vibaka si ndo nyie”, ila nikaona nishaumizwa vya kutosha. Nikasema kwa unyonge “sina tena cha kuibiwa acha nikutane nao tuu nitawapa na hii sim” alafu nikaondoka. Jamaa akanifata akaniambia hapana twende wote. Nikamtaza kwa ukaribu ni kama mtu aliekua amepaka wanja na lipstick akafuta afu haijafutika vizuri nikaona huyu mbona kama reinbo. Nikamwambia sawa.

Jamaa likawasha pikipiki yake ilikua nje ya geti, likanipeleka mpaka barabarani na ilikua usiku mwingi, daladala zilikua chache sana jamaa likanipa 10,000 likasema panda bolt mwanangu alafu likasema “Sku ingine ukiwa na Ny**e nicheki nikupeleke chimbo lina watoto wakali bei kitonga sana.

Tangu skuio nafika home mpaka leo sijaenda kazini, sim za boss wala mtu yeyote kazini sipokei. Safari mpya ya udalali mjini Morogoro ni ngumu lakini nitayaweza yote kwa jina la aliye Hai.

Hefe.

_____________________________________________
NIMEFANIKIWA KUMPATIA BOSS HELA YAKE NA KUREJEA KAZINI.

NIMEREJEA KAZINI BAADA YA SEKESEKE LANGU KUPATA UTATUZI

Soma mrejesho: Mrejesho: Nimerejea kazini baada ya sekeseke langu kupata utatuzi
 
Aiseee bonge la kisa mzee. Nimevuta picha hapo demu alivyokubadilikia ghafla kuwa umempa 80,000 umemuona yeye denti wa chuo.

Umenikumbusha one time kuna sehemu tulikuwa na washkaji tunakula nyama, sasa jamaa mwingine akasuggest aje na mademu wa kuchangamsha party.

Kiukweli mimi na wadangaji ni vitu viwili tofauti. Hata huyo mwanamke awe mzuri kama malaika, the moment akionyesha yupo interested na kulipwa pesa ndipo akupe attention tena sio attention ya ukweli ni ya maigizo then hapo hapo naingia baridi na kukosa hamu nae.

Wale mabinti ni wazuri ukiwatazama na wamevaa vinguo vya mitego balaa. Ila wanakula balaa kama wanaume pale ndio nikaanza watoa dosari, nikaona kama wanakula hivi it means hawa walikuja na njaa hapa ili wale.

Haya baada ya hapo tukawa tunakunywa tu wao wanacheza mziki na kubambiana na kila kijana aliyekuwapo pale kwa mitego sana. Jamaa wakawa busy kuwa tunza 10,000 ili kuwahamasisha mimi natazama tu mchezo.

Vijana wanatoa hela wanaambulia kubambia tu. Muda wa kuondoka umefika mademu wakajikusanya wakaondoka kama walivyokuja yaani pamoja. Tena kwa kutumia usafiri wao. Nilicheka balaa nikasema vijana mnatoa hela kubambia tu. hizo hela mngewapa hata dada zenu au mama zenu si wangewashukuru sana leo?!

Aaaaah mimi mwanamke akishageuza mahusiano ni biashara stimu zinakata maana kichwa kinaniambia huyu anatumika na wengi wewe hapa unatafuta maradhi tu na hauna tofauti na mpiga punyeto.
 
JamiiForums-901207726.jpg
 
Nimeamua kuacha kazi na kuingia kwenye udalali huku bosi akinisaka na polisi Mbosso alisema mapenzi Gharama? Ufisi Gharama zaiiidi. Hii haikua kwa kupenda kwangu bali ni tamaa ya kupenda Uchi na hofu ya kupoteza maisha au Uanaume wangu.

Mimi ni kijana wa miaka 28 nilikua nimeajiriwa na nafanya kazi kama sales person kwa boss muhindi. Kuna deal nilisuka
Pole sana
 
Siwezi laumu sana, ila million 7 kasoro imeisha usiku mmoja, tena ukute umepiga goli moja. Alaf kibaya zaidi hujaenjoy maana umeondoka na stress, hata utamu wa hiyo K sidhani kama unaukumbuka

Kaka utamu siukumbuki. Namlaani yule dada ila wakati wa shughuli kwa kweli tulizungushana. Yule dada kuna laaana fulani anazo za mabibi zake. Itoshe kusema ana USHETANI mwingi sana. Amenifundisha mpaka vitu ambavyo sijawai vijua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom