Anaitwa Roma: Wimbo mpya wa Roma Mkatoliki

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,708
45,072
Roma Mkatoliki amerudi upya jamani.
Ametoa wimbo mpya unaitwa "Anaitwa Roma".

Ni Roma yule tuliyemzoea enzi za Mrisho akitamba na vibao vyake matata. Je Basata watauacha huu wimbo? Utafute mapema kabla hawajauchukulia hatua.

Katika wimbo huo mimi nimependa mstari fulani hivi unasema;
"Kwetu bima ya afya ni bora kuliko ndege"

Ibrahim Musa maarufu Roma Mkatoliki amerudi tena na tungo zilizoamsha hisia za mashabiki wa muziki na kuwa gumzo mitandaoni.

Wimbo mpya wa msanii huyo unaitwa ‘Anaitwa Roma’.

Wimbo huo aliouachia kwenye mtandao wa YouTube ukiwa ni saa 18 tangu uwekwe ulikuwa umesikilizwa na watu 174,000 .

Wimbo huo amemshirikisha msanii One Six umekuwa gumzo kwenye mitandao huku watu wakihofia unaweza kumtia matatani wakihusisha na tukio la kutekwa kwake la mwaka 2017.

Aprili 7, 2017 msanii huyo akiwa na wenzake watatu walichukuliwa na watu wasiojulikana wakiwa kwenye studio ya Tongwe Records iliyopo Masaki Dar es Salaam wakifanya kazi ya kurekodi nyimbo.

Msanii huyo na wenzake walikaa mikononi mwa watu hao kuanzia siku ya Jumatano na kuachiwa Ijumaa.

Tukio hilo lilihusishwa na aina ya nyimbo anazoimba na ndiyo maana alipotoa wimbo huu umezua mjadala.

Watu wengi waliokuwa wakiujadili walikuwa wanamsifia na kumuonya kwa pamoja.

Kwenye mtandao wa Instagram waliousikiliza wimbo huo walisema:

onkolonkonchwa: kwani mzee haujaitwa basataa wanakusubiri ujee ila hongeraa ni bonge la ngomaa…

streetboyz509: Roma utekwi tena mzee bb ushaaga UK huko…

emanuelmadale7: ngoma kali kichiz sema nawaza sjui kama imepita Basata.

abelianpaul: Oyaa tulia kwanza huko Marekani waxije wakakuteka tena

tuwabin: Huyuuuu ndo romaa tunaye mjuwaa.

otanaely: Roma hizo tungo kali la waraka wa waebrania

noshadymangule: Nimeshaipakua brother goma lipo sawa kbs yn ni Dua brother

namungofcsupporters: Mnapiga Bomu Monchwari alafu mnajisifu mmeua

kassumbi: Safari hii wakikukamata kaka haurudi kabisa angalia wahuni sio watu wazuri aisee…

ozil_mattarjr: hii nyimbo imenigusa sana nyimbo imegusa maisha yetu halisi…

the_ceo: Hivi huyu jamaaa kaenda Marekani kaenda nafamilia yake au...

skak_wiz_tz: Tuwekee namba kaka tuanze kabisa kuchanga hela ya dhamana..

Roma mwenyewe alipowasiliana na Mwananchi kujua alilenga nini kutunga mashairi hayo na anachukuliaje onyo analopewa na mashabiki wake licha ya kupongezwa pia alijibu kwa kifupi.

“Nitakujibu sipo sehemu rafiki kwa mazungumzo hayo, ” alijibu Roma.

======

MASHAIRI

Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha Roma Roma Nani wa kunyamazisha Roma Roma Kazi kuongea ongea kesho yake on air Kesho kutwa wamepotea

Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha Nani wa kunyamazisha Roma Roma Kazi kuongea ongea kesho yake on air Kesho kutwa wamepotea

Wanauliza siku hizi Roma huimbi za kiharakati Huku wakisema ununio ndo kumbukumbu iliyo baki

Ahh sasa hamtaki mbona hamkumsapoti Mange Nyinyi mtakuwa wanafki

yaani sijui mlikwama wapi Walivunja dole la mwisho wakaliacha dole la kati(Mmh)

Eeeh hii si ni nchi ya demokrasi mkimind basi mnajua Sa mbona kamati(Mmmm)

Tuiache hayo Vipi korosho za Mtwara Maana wapiga kura wengi wakulima wafanya biashara

Kumnyima mpinzani ajenda, tendetu yaliyo mema Sio kumpelekea defender mtaani tutie vilema

Chozi ya waTanganyika hayatawaacha salama Na damu zilizo mwagika milele zitawaandama

Serikali imewapa nafasi wanawake pongezi ifike Najiona mwenye bahati nikimtazama mwanangu wa kike

Akikuwa akiuliza wale waloniteka nani aliwatuma Mjibuni mmemzaa mpare ila asiwachukie wasukuma

Najua atanuna najua ya nyuma yatamtia huruma Asilipe kisasi ashtaki kwa Mungu aipate suna

Na nikiitwa kwa Mungu Baba nikafa Sijamuona mtoto, mmpe shada la msalaba Aliweke upande wangu wa kushoto

Na mtapo imaliza ibada iwe ni padi ya paroko Nguo zangu azipige mnada mmpe albino ama uroko

Mi ni soja niko vitani Nikipona unikiss silaha nawaachia maishani Ibebeni mkomboe taifa
maana nchi yenu itaangamia Viongozi hawana maarifa na hawataki wakosolewe Wanafanya kazi kwa sifa

Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha Roma Roma Nani wa kunyamazisha Roma Roma Kazi kuongea ongea kesho yake on air Kesho kutwa wamepotea

Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha Nani wa kunyamazisha Roma Roma Kazi kuongea ongea kesho yake on air Kesho kutwa wamepotea

Yuda usimharibie Dani ili ufurahishe mtukufu Sisi wote wanao kwanini unapenda sana Yusufu?

Yakobo, baba pesa madaraka umaarufu Wanaomwapata vijana wanakosa hekima na utu

Wapunguzie vifungo wafungwa wasio na hatia Wengine walifuata mkungo kiukweli hawakuwa na nia

Naskia jimbo la Ubungo kuna mtu amelipania We umezitungo ni zaidi ya waraka wa Waibrania

Chama kilisha watimua na siasa mlowanunua Mnapiga bomu mortuary mnajisifu mmeua

Tuliombee taifa tuombee viongozi wetu Nchi ina miiba so tuwavishe viatu walioko peku

Tusilete uchama kwenye issue za kitaifa Uongozi ni kuacha alama chanya na kuajibika

Kutekana kuuana sio sifa ya MTanganyika Ubora ndama ndio unalipa zizi la ng'ombe uhakika

Hongera baba kwa ukusanyaji wa mapato kedekede Ya kodi na flyover ndio hizo kanyaga twende

Kwetu huduma ya afya ni bora kuliko ndege

Atafanya yote tumuombee na tuimbe Yesu nibebe

Watu wametumbuliwa mwezi mmoja kabla ya kustaafu Walimu wamesahauliwa mapato yao halafu Mapolisi mishahara yao bado twapiga tafu Hospitali boresha tupunguze idadi ya wafu

Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha Roma Roma Nani wa kunyamazisha Roma Roma Kazi kuongea ongea kesho yake on air Kesho kutwa wamepotea

Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha Nani wa kunyamazisha Roma Roma Kazi kuongea ongea kesho yake on air Kesho kutwa wamepotea

Sijawai kuona mpga kinanda wa kanisa akitoa sadaka Cameraman akianguka ndani ya misa kwa pepo kaka

Na sadaka halali ni ile utaitoa kwa uchungu Tafta pesa wee siku hizi hulijali sio ukubwa rungu

Na nyota mshale we bishoo segera Ukuki na kulenga tokea hale Nenda kalete mamluki

karoge mambo iko huku Roma anaiteka show, kafara unamchinjia kuku? Mi namchinja naichinja kondoo

Andaa show alafu mmlete mkali wenu tafta venue Baada ya dakika mbili mpige mziki ya maiti yenu Eti unarap? Huwa unarap wewe? Unarap nini?

Ni wanakubeba na hautaamini usiku wakikupiga chini Sa we kamatia chini mi nakamatia ndinga Na ukikamatia mpini si utakamatia mimba

Alafu kizazi nakwacha unang'aza sharubu Kula nganzi mi kisirani nina gubu Na elfu mbili na ishirini si tumwombe Mungu Wewe na mimi na wote wasaka tonge watao rudi vitini Watuepushe na hiki kikombe mwaskizisha nguma pini Mjengoni wasikae kinyonge

Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha Roma Roma Nani wa kunyamazisha Roma Roma Kazi kuongea ongea kesho yake on air Kesho kutwa wamepotea

Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha Nani wa kunyamazisha Roma Roma Kazi kuongea ongea kesho yake on air Kesho kutwa wamepotea
 
Roma Mkatoliki ni ameamua kujilipua ama? Binafsi sijamuelewa au labda amepewa go ahead na system.

Wimbo mzima ukiusikiliza kwa umakini ni kama ameamua kumnanga "prince".

Pale anaposema "mjibuni mmemzaa Mpare ila siwachukii Wasukuma."

Naendelea kuamini, aidha Roma ameamua potelea mbali liwalo na liwe ama amepewa kinga na wasiojulikana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom