Ana sifa karibia zote ninazohitaji, ila tatizo elimu yake

Ana sifa karibia zote ninazohitaji, ila tatizo elimu yake

As long as mnapendana, anajitambua na Unaona Kabisa Ni Mtu anayekufaa kujenga naye familia, just marry her. Kuna watu wana elimu zao, ila ndo elimu zetu tu za makaratasi, Hana analolijua. Na kuhusu kushinda fb, insta, wasap etc Ni hulka tu ya Mtu, jitahidi kuongea naye ili apunguze hayo matumizi ya simu. Unaweza kumpeleka hata English course au akaenda akasomea ujuzi Fulani.., eventually mambo yatakuwa poa.

asante kwa mawazo yako!!
 
hivi unafikiri elimu itakupikia chakula itakufulia nguo italea watoto ?

kwanza huyo ndio mzuri hana kazi utampata muda wowote uhakika wa watoto kula na kwenda shule upo kwani unamuacha nyumbani
 
usichague mwanamke/mwanaume kwa sura. elimu. pesa n.k upendo wake kwako unatosha kuona anafaa au lah. kuna wasomi wazuri tu waliodumu kwenye ndoa zao and vs pia wapo std seven hawashikiki kila kitu wanajifanya wanajua yani fagio la chuma kwelikweli and vs is true. msikariri vitu maisha hayana fomula.

ila jiandae kuzaa vilaza coz kuishia std seven co sababu ya kumfanya mtu ashindwe kupambanua mambo kuna wengine hata drsn hawajaingia ila wanayajua maisha mwanzo mwisho japo kutema umeme km Nyani Ngabu hawawezi.
 
Last edited by a moderator:
Good, hapo Mkuu cha kufanya ni kumpeleka English Course tu japo ya mwaka mmoja ili awe updated kisasa, then unamfungulia Boutique au biashara yoyote kutokana na eneo husika if u can afford, chamsingi awe busy na pesa ila matumizi ya Mitandao ya kijamii yawe Limited.
 
kuna jamaa mmoja ashapost aboutI mkewe mwenye elimu kama hio,nmeshasahau jina la thread,
ila pia wanaume wenzio wengi humu JF wanapenda darasa la 7,kwa madai wa degree wasumbufu

STD 7 ndio habari ya mjini.
 
Elimu haipo kwenye sifa. Mwangalie mama yako. Shangazi na wengine
 
Mkuu elimu yetu zinafana hata Mimi nimeo std 7 mwezi wa 3 mwaka huu.maisha yanaendeleo ila tuna mikakati mingi tu ya maisha
 
Weka ndani ikiwa unampenda, mengineyo ni yakujadili nakupanga
 
Oa tu mkuu ni naswala ya muda,kadiri mnavyoendelea kuishi naye atarudi kwenye mstari na kuwa unavyotaka hasa kama ni wa umri wako ila kama mmepishana sana umri shughuli yake ni nzito
 
tindikalikali

Kwa maandiko yako hayo nnaona wewe ndiyo hujaelimika, labda umesoma lakini huna elimu.

Hivi hiyo shule ulienda kusomea ujinga?
 
Last edited by a moderator:
tindikalikali

una elimu ya? mwambie aje jamii forums julwaa la siasa,uchumi na biashara na jukwaa la tech, mtafutie na mwalimu wa ingilishi kozi�� na mbona hapa umeandika kwa kiswahili kizuri tu kitumie kwa mupenzi wako
 
Last edited by a moderator:
kuna jamaa mmoja ashapost aboutI mkewe mwenye elimu kama hio,nmeshasahau jina la thread,
ila pia wanaume wenzio wengi humu JF wanapenda darasa la 7,kwa madai wa degree wasumbufu

Muache aoe mwenye degree aone timbwilitimbwili lake
Atapangiwa adi mda wa kula papuchi
 
Mkuu kwanza shukuru umepata mwanamke anaekupenda na kukujali, HILO NDIO LA MSINGI, haya mengine ya elimu ni vikorombwezo tu ambavyo unaweza kuvirekebisha. Usiwe na mawazo ya ready made wife, mtengeneze mwenyewe na atakuheshimu sana. Hao ambao wameshasoma wengi wao ni pasua kichwa asikwambie mtu, watu wanajikaza tu kwa vile tayari wapo kwenye ndoa.

Unachotakiwa kufanya ni kumueka chini na kumuelewesha kuwa dunia ya sasa elimu ni muhimu hivyo hana budi arudi shuleni, hii yote ni kutafuta willingness yake mana kwenye kusoma hakuna kuforce!Anza kwa kumsajili QT, Mpe sapot ya tuitions, materials na mjali kihisia ili elimu ya utu uzimani asije akaiona kama adhabu! Mpe moyo! Naamini atafanikiwa. Akimaliza tu form four mtaftie hata certificate inayoendana na interest yake.

Kama una uwezo wa kufungua biashara then msomeshe hata certificate ya accounts ili aweze kusimamia vizuri biashara yake kwa upende wa pesa. Mjenge katika kujikomboa na sio asome ili aajiriwe. Muwezeshe elimu ambayo itamsaidia katika kujiajiri au kusimamia miradi ya familia. Nina mfano hai wa staff mate wangu ambaye mkewe amepita katika mchakato kama huu na sasa yuko vizuri sana ukiambiwa aliunga unga elimu huwezi amini
 
Mi nikushauri hivi...Kama unampenda msaidie walau akapate elimu kdogo hata kama ni Certificate au koz ambayo walau itainua kiwango chake kielimu. Trust me Elimu ni nzuri sana...na usikae ukaridhika na elimu yake eti kisa ana vigezo vyote.

Si mbaya kwa upande mwingine maana si wote walioishia std 7 walipenda...ni maisha tu. But msaidie pia kama umepata nafasi hiyo...maana mafanikio yake ni mafanikio yenu na wanenu.

Kwa upande wangu hata mm std 7 kwa dunia ya sasa hivi..wengi upeo wao ipo chini. Jaribuni kufatilia hili...u can't compare akili ya at least mtu wa form 4 na std 7 ...kuna utofauti. ( najua sio wao mtakubaliana na hilo).
Yangu ni hayo.
 
Back
Top Bottom