Tanzania bado tuna tatizo la upangaji vipaumbele vyetu, baada ya Elimu, Afya na kilimo, ilipaswa ije nishati!. Ni aibu na hatari kupikia kuni na mkaa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,550
Wanabodi,
Hii ni Makala yangu ya Nipashe Jumapili
Nishati 1.png
Nishati 2.png

Tanzania tulipopata Uhuru ile Desemba 9, 1961, sisi Tanzania tukiwa na rasilimali lukuki, lakini sasa hapa tulipo, tukijilinganisha na baadhi ya wenzetu nchi tulizopata nazo uhuru, wengi with nothing compared, kiukweli kabisa, sisi tumeachwa mbali!,

Nikijiuliza tatizo ni nini, ndipo nimekuja na conclusion yangu, sisi Tanzania tuna tatizo katika upangaji wa vipaumbele vyetu!.

Tangu enzi za Nyerere, tumepata uhuru, tukiwa na maadui wakubwa watatu ambao ni adui Ujinga, Umasikini na Maradhi, leo baada ya miaka 60 sio tuu maadui watatu hao bado wapo, bali tumeongeza na maadui wengine wawili wa Rushwa na Ufisadi!.

Falsafa ya Maendeleo ya Mwalimu Nyerere "Ili tuendelee, tunahitaji vitu 4, Watu, Aridhi, Siasa Safi na Uongozi Bora", hivi vyote vinne tulikuwa navyo, sasa tulikwama wapi?.

Falsama hiyo hiyo ilikuwa na makosa, kwa kukinzana na Adam Smith kwenye Land, Labor, Capita na Interprenaship. ilikuwa na omission ya Capital.

Ile Siasa Safi na Uongozi Bora ni kitu kimoja, tulihitaji Capital, uwekezaji mkubwa.

Kwenye upangaji wa vipaumbele vyetu, Mwalimu alikosea, Mwinyi akakosea, Mkapa akakosea, JK akakosea, JPM akakosea, na sasa Samia, asiposaidiwa kwenye hili la upangaji vipaumbele vyetu, pia Samia atakosea, hivyo natoa wito, tumsaidie ili asikosee kwa kuangazia maeneo ya vipaumbele ambavyo huko nyuma yalipuuzwa.

Moja ya maeneo haya ni eneo la sekta ndogo ya umeme.

Ungana nami katika mfulilizo wa makala hizi za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo hutoka kila Jumapili kwenye gazeti la Nipashe, sasa zitakuwa zinaandamana na kipindi cha TV, ambacho kwa kuanzia, kitakuwa kinarishwa na TBC na ITV kuanzia wiki hii.

A 5 min short version
. A full 30 min Prog.

Makala yenyewe ni Hii

MAENDELEO NI NISHATI, NI KOSA KUBWA NISHATI KUTOKUWA KIPAUMBELE
Kama kawaida, safu ya Kwa Maslahi ya Taifa, inaangazia mada anuwai kuhusu Taifa Letu Tanzania, ikijikita kwenye mada za kisiasa, kiuchumi na kijamii, na kwa mudamuda mrefu “Kwa Maslahi ya Taifa, imekuwa ikitokea kwenye makala Magazetini na mitandao ya kijamii pekee, kuanzia wiki hii, makala hizi za kwa Maslahi ya Taifa, pia zitaanza kuonekana kwenye luninga zetu, kwa kipindi cha TV kiitwacho “Kwa Maslahi ya Taifa” na kwa kuanzia, kitaanza kuonekana TBC na ITV, mambo yakienda vizuri, pia kitarushwa Star TV, Channel Ten na Azam TV, kwa lengo lile lile la kulisaidia taifa letu.

Si wengi wanafahamu kuwa ukiondoa uhai, tuliopatiwa na Mwenyeenzi Mungu, hewa tuyayovuta, na maji, kitu muhimu kuliko kitu kingine chochote ni Nishati. Bila hewa, maji na nishati ya jua, hakuna mmea wowote unaoweza kuota, hivyo dunia kuangamizwa kwa baa la njaa.

Mimi ni miongoni mwa wale waumini wa falsafa ya maendeleo ya Mwalimu Nyerere, aliyoiandika kwenye kitabu chake cha “Binadamu na Maendeleo”, kuwa ili tuendelee, tunahitaji vitu vine, Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora, “fedha si msingi, fedha ni matokeo tuu”. Sisi Tanzania, toka ile tunapata uhuru, miaka ya 60, vitu hivyo vyote vine tunavyo, jee tunakwama wapi?.

Japo mimi sio mchumi, ila kwa maoni yangu, Tanzania tunakwama kwenye kupanga vipaumbele vyetu.

Kwa muda mrefu nchi wafadhili, mashirika fadhili, nay a misaada ya kimataifa, ndio yanatupangia vipaumbele vyetu watakavyo fadhili, hivyo kupata misaada ya kimaendeleo na mikopo yenye masharti.

Kwa vile sisi watu wa media, sio wachumi, kazi yetu ni kusikiliza tuu wachumi na wakubwa wakipanga, na sisi kazi yetu ni kuripoti, kuandika kilichosemwa na wakubwa hawa, hivyo kujikuta, hatulisaidii taifa.

Mimi naamini kabisa kwa dhani ya moyo wangu kuwa Rais Samia, ana nia ya dhati, ya kulisaidia Taifa, lakini ili afanikiwe, ni lazima asaidiwe kuelezwa ukweli maeneo yenye udhaifu, yaliyotukwamisha, ni eneo la upangaji vipaumbele vyetu, moja ya maeneo hayo ni eneo nishati, kiukweli kabisa, licha ya Tanzania kugundua gesi asili, kuwa na maporomoko ya Mto Rufiji, tuna jua la kutosha kuzalisha solar energy, tunaupepo wa kutosha kufunga windmills, na chini ya ardhi tuna geothermal ya kutosha kuzalisha umeme, mpaka sasa ni nchi kubwa yenye watu milioni 60, lakini umeme wetu ni Megawatt 1,600, ni aibu!.

Japo tuna wataalamu na wataamuna, wachumi waliobobea, wanaopanga vipaumbele vyetu, kiukweli kwenye baadhi ya vipaumbele, wanazidi tuu kumuingiza chaka Mama Samia, namshauri mama Samia, aendelee kuwasikiliza Wataalamu wake wa uchumi, lakini pia asipuuze sauti zetu sisi akina hohehahe, kuna vitu tunaona tunakwenda ndivyo sivyo, tunashauri tunapuuzwa, nashauri pia tusikilizwe, huwezi jua, tunaweza kusaidia. Vipaumbele vikuu vyetu view, 1. Elimu, 2. Kilimo, 3. Afya 4. Nishati, 5. Miundombinu.

Wiki iliyopita katika siku ya Tanzania Day, kwenye Maonyesho ya Expo Dubai 2020, Wizara ya Nishati, pia ilifanya Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji kwenye Sekta ya Nishati ambalo lilihutubiwa na Waziri wetu wa Nishati, Mhe. January Makamba.

Hivyo mara tuu baada ya kurejea, nchini, nilimtafuta Mhe. Januari

Makamba amesema “Moja ya Changamoto kubwa sana ya sub sector ya umeme ni uwekezaji usiotosheleza , Nchi yenye ukubwa kama yetu, inayokuwa kwa kasi kama yetu, na ongezeko la idadi ya watu, kuwa na Megawati 1600 ni aibu kubwa, au kuwa na mtandao mdogo wa usafirishaji umeme kama tulionao ni aibu” Amesema “ tumezungumza na wawekezaji wengi, wakubwa wenye uwezo, na nia njema ambao wako tayari kuja nchini kwetu na kuwekeza katika maeneo hayo”

Makamba amesema, kufuatia hali ya nishati nchini kwetu, na fursa zilizopo Tanzania katika umeme, mafuta na gesi, Tanzania imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa ni kitovu cha biashara ya Nishati ukanda huu wa Afrika Mashariki, kati na Kusini”

Makamba amesema, “Tanzania imedhamiria kufanya mapinduzi makubwa ya nishati, kwa kuifanya nishati ya kupikia, kupatikana kwa wingi na kwa urahisi zaidi, kufuatia asilimia 70 ya nishati yote Tanzania, kutumika kwa kupikia, ikifuatiwa na mafuta na umeme. Nishati kubwa inayoongoza kutumika n kupikia, ni nishati ya Tungomotaka (biomass).

Makamba ameusema ukweli mchungu kuwa “Hali ya nishati ya nchini Tanzania, sio nzuri, watu 22,000 wanapoteza maisha, kila mwaka kutokana na magojwa ya upumuaji yanayosababishwa na moshi wa kupikia kwa kuni na mkaa, hivyo kufuatia hali hiyo, kipaumbele cha kwanza kwenye sekta ya nishati, ni kuhakikisha gesi inapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu na inafika kwenye kila nyumba, hivyo kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Pia Makamba, amezungumzia hali ya nishati ya Umeme nchini sio nzuri, kutokana na ukuaji mkubwa wa uchumi, na ongezeko la idadi ya watu, usiokwenda sambamba na uwekezaji kwenye sekta ya umeme, hivyo kinachofanyika sasa ni kutafuta fedha, za kufanya uwekezaji mkubwa kwenye umeme, kuweza kukidhi mahitaji.

Kwa upande wa Tanesco, Waziri wa Nishati, January Makamba, amesema Tanesco inahitaji transformes mpya zaidi ya 20,000 nchi nchi nzima ili ku stabilize umeme, kuacha kukatika katika mara kwa mara kutokana na transformers zilizopo kuelemewa.

Moja ya kero kubwa kwa Watanzania ni kero ya kukatika katika kwa umeme, Waziri January Makamba amesema, kunachangiwa na ukuaji wa ghafla wa uchumi wa mtu mmoja mmopja, watu wengi zaidi sasa wanatumia vifaa vya umeme ukilinganisha na kule nyuma, hivyo peak demand ya matumizi ya umeme kwa wakati mmoja, kuongezeka maradufu, na kusababisha instability.

Waziri Makamba, amemalizia kwa kuwahakikishia Watanzania, serikali ya awamu ya 6, chini ya Rais Samia, imedhamiria kwa dhati, kukabiliana na changamoto zote zinazoikabili sekta ya nishati, miradi ya kupeleka umeme vijijini, iko pale pale, Tanesco iko kwenye mageuzi makubwa ya kiutendaji kuboresha huduma zake.”

Shida zilizopo tunazijua, changamoto tunazijua, majawa tunayajua, kinachohitaji ni subra na uvumilivu, na baada ya muda sii mrefu, kukatika katika umeme, kutakuwa ni historia”

Hili tatizo la Upangaji wa Vipaumbele Vyetu, litajirudia very soon, baada ya nishati ya kupikia na umeme majumbani nishati muhimu sana ni mafuta ya petrol na dizeli. Kufuatia vita vya Ukraine, mafuta yatapanda tena bei kwenye soko la dunia kama enzi za vita vya ghuba, watu wanaojua kupanga Vipaumbele kupitia kufanya SWOT and PEST Analysis by now tungeishajua mafuta yatapanda sana bei na kuanza kujipanga kwa mitigation steps kabla hayajapanda ili kuzuia kupanda bei, na sio kusubiri yapande, yazue taharuki ndipo msikie vikao vya kukutana ku mitigate, ndipo itolewe ruzuku bei ya mafute ishuke.

Paskali
 
Alafu kupikia kuni mkaa sio hata tatizo,sijui unaongea nini.

Huelewi hata vyakula vinatoka humo ni organic na very tasty.

Namkumbuka bibi yangu Tunsume akipika mbalagha ni michozi tu inatutoka kwa moshi wa kuni.

Msosi ukiiva mnateremsha na mtindi na matakapela kisha mbonji.

Yule ilikua hata upeleke mkaa gunia ngapi utazikuta hapo ulipoziacha.

Ye ni kuni tu.

Mama gesi,umeme vipo pia lakini No.

Yuko comfotable akipika na mkaa.

Vitu vingine ni leisure tu si lazima
 
Kabisa...

Nishati ni suala nyeti na muhimu sana. Ni wazi serikali ya Tanzania hailichukulii suala la Nishati nchini kwa uzito unaotakiwa.

Serikali ya Tanzania inachukulia nishati kama chanzo cha mapato badala ya huduma muhimu kwa wananchi ili kuendesha uchumi wa nchi.

Mfano nusu ya bei ya Mafuta ni kodi na tozo mbali mbali za serikali. Mchanganuo wa kodi na tozo mbali mbali za serikali kwa kila lita moja ya mafuta ni kama ifuatavyo:

1625678586027.png


Hii sio afya kwa uchumi wa nchi, matokeo yake ni mfumuko mkubwa wa bei.

Serikali inatakiwa kuacha mara moja kufanya mafuta ni chanzo cha mapato ili kuleta unafuu wa bei kwenye bidhaa ya mafuta nchini. Matokeo yake bei ya mafuta Tanzania ni kubwa kuliko nchi kama Zambia ambazo zinapitisha mafuta yake hapa hapa Tanzania.

Na hili "kosa" limejirudia kwa mara nyingine tena kwenye eneo la Internet Data. serikali ya Tanzania badala ya kuchukulia data kama huduma muhimu kwa maisha na Dunia ya sasa, wao wameona ni chanzo cha mapato. Matokeo yake Data rates zimekuwa very high sababu ya makodi mengi yaliyowekwa humo.
 
Kutotaja kabisa sera ya taifa ya nishati ya mwaka 2015! Ni kutotendea haki mjadala juu ya nishati nchini. Vinginevyo, hiyo makala niwe nimeipitia kwa spidi kali kiasi cha kuiruka.
 
Tulipopata uhuru, kulingana na hali tuliyokuwa nayo wakati huo, tulijitangazia maadui wakubwa watatu: ujinga (elimu), umaskini (uchumi), na maradhi (afya). Hiyo maana yake ni kwamba hivyo ndivyo vilikuwa vipaumbele vyetu vya kushughulikia wakati huo.

Katika kushughulikia vipaumbele hivi siyo rahisi kuelekeza resources zote kwenye moja kati ya hivyo na kuviacha vingine nyuma, inabidi ku-deal navyo vyote simultaneously maana vyote ni muhimu na vinategemeana.

Katika utekelezaji wa hivyo vipaumbele kuna mambo mengine ambayo hujitokeza na kuonekana pia yanahitaji kushughulikiwa kwa haraka ili yaendane na development ya hivyo vipaumbele. Mfano, miaka si mingi sana iliyopita kulitokea ukame huko Shinyanga kiasi cha watu kuwa hatarini kufa kwa njaa, lakini wakati huo huo huko Rukwa na Ruvuma kulikuwa na mahindi mengi yanaoza magharani, shida usafiri -barabara ni mbovu hazipitiki.

Ili kuondoa tatizo kama hilo inabidi kuelekeza resources kwenye ujenzi wa barabara pia. Na kwa kuwa resources zetu ni chache kutokana na kuwa na uchumi duni, basi inabidi kugawanya kidogo kwenye maeneo mengi!

Sasa kwa kuwa hali yetu ni afadhali kuliko wakati tulipopata uhuru, inatupa nafasi ya kuviangalia upya na hata kuvipanga vipaumbele vyetu upya.
 
Tulipopata Uhuru itulikwa na rasilimali lukuki, tukijilinganisha na baadhi ya wenzetu nchi tulizopata nazo uhuru, wengi with nothing compared, kiukweli kabisa, sisi tumeachwa mbali!, Nikijiuliza tatizo ni nini, ndipo nimekuja na conclusion yangu, sisi Tanzania tuna tatizo katika upangaji wa vipaumbele vyetu!.
Nakubaliana nawe na hili limekuwa donda ndugu!
Tangu enzi za Nyerere, tumepata uhuru, tukiwa na maadui wakubwa watatu ambao ni adui Ujinga, Umasikini na Maradhi, leo baada ya miaka 60 sio tuu maadui watatu hao bado wapo, bali tumeongeza na maadui wengine wawili wa Rushwa na Ufisadi!.
Nakubaliana pia
Falsafa ya Maendeleo ya Mwalimu Nyerere "Ili tuendelee, tunahitaji vitu 4, Watu, Aridhi, Siasa Safi na Uongozi Bora", hivi vyote vinne tulikuwa navyo, sasa tulikwama wapi?. Falsama hiyo hiyo ilikuwa na makosa, kwa kukinzana na Adam Smith kwenye Land, Labor, Capita na Interprenaship. ilikuwa na omission ya Capital. Ile Siasa Safi na Uongozi Bora ni kitu kimoja, tulihitaji Capital, uwekezaji mkubwa.
Hatukuhitaji Capital, tulitakiwa tusiifanye serikali iendeshe shughuli za umma.
Siasa ya ujamaa ilikuwa tatizo kubwa sana. Kwanini tulitaifisha mashamba ambayo leo ni mapori?
Kwanini tulikuwa na STC na RTC? n.k.
Kwenye upangaji wa vipaumbele vyetu, Mwalimu alikosea, Mwinyi akakosea, Mkapa akakosea, JK akakosea, JPM akakosea, na sasa Samia, asiposaidiwa kwenye hili la upangaji vipaumbele vyetu, pia Samia atakosea, hivyo natoa wito, tumsaidie ili asikosee kwa kuangazia maeneo ya vipaumbele ambavyo huko nyuma yalipuuzwa.
Hapa naomba kumtetea Mwalimu Nyerere.
Mwalimu hakuwa na choice wakati tunapata Uhuru. Mwl hakuweza hata kupata msomi wa kumteua kuwa katibu mkuu ilikuwa mbinde.

Shule hazikuwa za kutosha, hatukuwa na vyuo vya elimu, Hospitali za kutosha au vyuo vya afya. Tulikuwa na matatizo ya nishati, mawasiliano na kila aina ya miundo mbinu. Mwalimu alibeba vyote kwa kuchagua kipi kina afadhali si kipaumbele

Mafanikio ya Mwalimu kwa miaka 23 magogoni ni kubwa kuliko Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli kwa pamoja. Hawa ndio wa kuuliza vipaumbele si Nyerere
Mfano, nionyeshe mita moja ya reli iliyojengwa na Mwiyi, Mkapa, Kikwete au Magufuli

Moja ya kero kubwa kwa Watanzania ni kero ya kukatika katika kwa umeme, Waziri January Makamba amesema, kunachangiwa na ukuaji wa ghafla wa uchumi wa mtu mmoja mmopja, watu wengi zaidi sasa wanatumia vifaa vya umeme ukilinganisha na kule nyuma, hivyo peak demand ya matumizi ya umeme kwa wakati mmoja, kuongezeka maradufu, na kusababisha instability.

Waziri Makamba, amemalizia kwa kuwahakikishia Watanzania, serikali ya awamu ya 6, chini ya Rais Samia, imedhamiria kwa dhati, kukabiliana na changamoto zote zinazoikabili sekta ya nishati, miradi ya kupeleka umeme vijijini, iko pale pale, Tanesco iko kwenye mageuzi makubwa ya kiutendaji kuboresha huduma zake.” Shida zilizopo tunazijua, changamoto tunazijua, majawa tunayajua, kinachohitaji ni subra na uvumilivu, na baada ya muda sii mrefu, kukatika katika umeme, kutakuwa ni historia”

Paskali
Hili tatizo lipo miaka zaidi ya 20 kama lile la Maji wakati wa Sumaye hadi sasa

Viongozi si tatizo, wananchi ni tatizo. Ukiwa na choice haya hayawezi kutokea.

Nchi za wenzetu utasikia leo chama hiki kesho kile.
Serikali za vyama zinashindana ku 'deliver' si kukabidhiana matatizo kama Tanzania.

Mfumo wetu unaruhusu haya kutokea .

Watu wanaposema tukae tuandike taratibu zetu na kusahihisha makosa maana yake ni hii.

Miaka 60 tuna matatizo yale yale na watu wale wale bado tunategemea matokeo tofauti.

Kule kwa malkia wanaita ''Insanity''
 
Paskali, Raisi Nyerere alifanya makubwa practically kwenye nishati ya kupata umeme nafuu kwa matumizi ya nyumbani hadi viwandani labda kuliko raisi mwingine hadi leo.

1973 mara baada ya Opec kudhibiti upatikanaji wa mafuta rahisi. Mwalimu alijenga Hydro electric power plants Kidatu,Mtera,na akiwa ameishapanga kujenga bwawa kubwa Stigler gorge huko mto Rufiji,lakini ukata uliotokana na vita vya Kagera ulisimamisha ujenzi huo.
Hata hivyo alijenga kiwanda cha majiko ya umeme madhubuti na yenye bei nafuu ya TANLEC huko Arusha.

Nakumbuka miaka ya 80 watu wengi walivutiwa na matumizi ya majiko hayo,na bei ya umeme ilikuwa chini sana hadi awamu ya Mzee Ruksa ndipo Mabwawa "yalikaushwa"ikawa mwisho wa umeme nafuu hadi leo.

Lakini Raisi Nyerere huyo huyo ndie alianzisha TPDC kwa lengo la kutafuta mafuta na gesi asilia na kusomesha vijana wa Kitanzania fani ya Nishati katika nchi mbalimbali. By 1976 alikuwa amepata gesi asilia pale Songo Songo. Licha ya kugudua gesi nyingi mno miaka iliofuata,hadi leo TPDC ameshindwa kusambaza gesi hiyo majumbani.

Kibaya zaidi serikali inakataza utumiaji wa mkaa na kuni wakati haiwapi nishati mbadala. Kama haitoshi serikali imeshindwa kabisa kuja na mbinu za kusambaza na kuutumia mkaa wa mawe majumbani.Tanzania kuna na hazina kubwa ya mkaa wa mawe.

Mwisho kabisa Paskali kama ujuzi au elimu ya nishati ipo.
Kama upatikanaji wa vyanzo vya kufua umeme nafuu vipo.
Kama ni visima vya gesi asilia, visima kibao.
Upatikaji wa mkaa wa mawe Tanzania ina zaidi ya 297 million MT,ikichukuwa nafasi ya 50 duniani.
Labda Tanzania tuna upofu wa utashi kuliko upofu wa macho.
 
Wanabodi,
Hii ni Makala yangu ya Nipashe Jumapili
View attachment 2158659View attachment 2158660
Tanzania tulipopata Uhuru ile Desemba 9, 1961, sisi Tanzania tukiwa na rasilimali lukuki, lakini sasa hapa tulipo, tukijilinganisha na baadhi ya wenzetu nchi tulizopata nazo uhuru, wengi with nothing compared, kiukweli kabisa, sisi tumeachwa mbali!...
Kila awamu inakuja na mikakati yake katika kutatua suala la umeme. Awamu ya tano umeme wa maji Awamu ya sita umeme wa Gesi kweli mkuu hatuwezi kufika.
 
Umuhimu wa nishati naona wanautambua tatizo hawajui wafuate njia au aina ipi, kila awamu inayokuja inakuja na mradi wake tofauti na ule wa mtangulizi wake matokeo yake hatusogei mbele tunabaki kushangaa tu na hasa ukizingatia pesa za hiyo miradi mpaka tukaombe kwa wazungu.
 
Hii gesi iliyopo kwa kuanzia tu wananchi wangegaiwa majiko ya gas na mitungi yake bure, kwa wale wenye uwezo mdogo, na wakulima vijijini.

Wengine hawatumii gas kwasababu hawajaizoe , wengine wanaogopa kulipukiwa, kuna sababu nyingi ambazo wangejaribu kuitumia wangeona umuhimu wake.

Njia hii itawaongezea wauzaji wa gas wateja wengi na tutatunza misitu yetu.
 
Hii gesi iliyopo kwa kuanzia tu wananchi wangegaiwa majiko ya gas na mitungi yake bure, kwa wale wenye uwezo mdogo, na wakulima vijijini.

Wengine hawatumii gas kwasababu hawajaizoe , wengine wanaogopa kulipukiwa, kuna sababu nyingi ambazo wangejaribu kuitumia wangeona umuhimu wake.

Njia hii itawangezea wauzaji wa gas wateja wengi na tutatunza misitu yetu.

Hiyo gas unayoiona kwenye mitungi ya kupikia ni imported 100% , Watanzania tunadanganywa sana kuna watu wanaamini kabisa akienda kununua gesi kwenye mtungi ni Gesi ya Kusini Tanzania, siyo kweli tuna import hivyo haya mambo ya uchumi wa gesi wa akina Makamba ni uongo na wizi kwani hiyo gesi siyo mali ya Serikali ya JMTZ Serikali itanunua kutoka kwa mmiliki ambaye ni foreigner ingawaje anaichimbia Tanzania, got it ?
 
Hiyo gas unayoiona kwenye mitungi ya kupikia ni imported 100% , Watanzania tunadanganywa sana kuna watu wanaamini kabisa akienda kununua gesi kwenye mtungi ni Gesi ya Kusini Tanzania, siyo kweli tuna import hivyo haya mambo ya uchumi wa gesi wa akina Makamba ni uongo na wizi kwani hiyo gesi siyo mali ya Serikali ya JMTZ Serikali itanunua kutoka kwa mmiliki ambaye ni foreigner ingawaje anaichimbia Tanzania, got it ?
Wazo langu ni kuwafahamisha watu wengi zaidi matumizi ya gas, haijalishi ni ya ya kutoka wapi lakini lengo kuu ni kupunguza watumiaji wa kuni na mkaa na kulinda misitu yetu.
 
Wazo langu ni kuwafahamisha watu wengi zaidi matumizi ya gas, haijalishi ni ya ya kutoka wapi lakini lengo kuu ni kupunguza watumiaji wa kuni na mkaa na kulinda misitu yetu.

Hilo linakwenda sambamba na income ya watu, Tanzania watu ni low income hata Dar tu matumizi ya Gesi hayawezi kufikia hata tu 20% na Dar ndio mji tajiri Tanzania, hivyo watu wanaotumia kuni au mkaa siyo kwamba hawajui kuna gesi bali hawawezi kumudu hivyo bado mkaa/ kuni ni cheaper kwa matumizi ya kila siku.

Kwa kifupi hakuna kitu hii Serikali inafanya na wala haina plans zozote na kuongeza income za watu, kilichopo ni fitina, majungu na wizi, baaasi !
 
Hilo linakwenda sambamba na income ya watu, Tanzania watu ni low income hata Dar tu matumizi ya Gesi hayawezi kufikia hata tu 20% na Dar ndio mji tajiri Tanzania, hivyo watu wanaotumia kuni au mkaa siyo kwamba hawajui kuna gesi bali hawawezi kumudu bado mkaa/ kuni ni cheaper kwa matumizi ya kila siku.
Wewe isiombe uwe kijijni ma mvua imenyesha, huna akiba ya kuni, ukitoka nje kuni zimenyeshewa na mvua ndani watoto wanalia njaa.

Kipato cha Watanzania ni duni kwakua kilimo na mifugo ambayo ni ajira ya wengi hakijapata masoko stahiki.

Hii ni agenda nyingine kabisa inabidi nitoke kwenye gesi, mkaa na kuni. Hiki kilimo cha jembe la mkono hakitatufkisha popote. Kila mwananchi anatetaka kulima angepewa ekari mbili za kulima mazao ya chaguo lake ili kulisha familia, ardhi nyingine tukaribishe wawekezaji wenye mitaji mikubwa ili walime kilimo cha biashara. Hawa watatoa ajira kwa wengi na kama watalipa kima cha chini cha mshahara kwa watu wenye ekari mbili za kilimo na wanaishi kwenye nyumba zao hawalipo kodi basi kipato cha wengi kitaingezeka.
 
Back
Top Bottom