Amini usiamini wachawi wana kipindi kigumu sana

Amini usiamini wachawi wana kipindi kigumu sana

Shukrani kwa habari mzee wa Msata......nafuu tutalala kwa amani mzee wa busara kaenda likizo. Tulishachoka kujambiwa usoni kila siku mpaka tunaamka kama tuna hangover bureee kumbe mashuzi ya vigagula
Full mijambo!!
 
Mkuu mshana jr mbona hao hao wachawi inasemekana wanao uwezo wa kufunga mvua isinyeshe??!!

Mi nahisi kipindi cha mvua huwa wapo kwenye vikao vyao vya bunge la bajeti ndo maana inanyesha nyesha pasipo mipangilio!!
Ni kwa sehemu ndogo sana sana na hapa ndio unaweza kuamini kwanini iwe mvua na si jua wala mwezi
 
Unaweza ukadhani nazungumzia ukata wa kipindi hiki au pengine kupungua kwa wateja la hasha! Kuna sababu nyingine tofauti kabisa na hizi.

Mchawi na mitunguli yake yote na nguvu zake zote kiboko yake maji, yani hakuna tofauti na kitu cha umeme kisivyopatana na maji.

Tunguli na maji ni vitu viwili tofauti kabisa ndio maana hata siku moja ni ngumu sana kukuta tunguli zimefukiwa mtoni.

Kumbukeni ile mada ya uchawi hauvuki bahari kwahiyo kipindi hiki cha mvua ni kipindi kigumu kwa hawa ndugu zetu hasa kama tunguli zao sio zile water proof.

Kinachofanyika kwa sasa ni kufanya tu makafara ya damu lakini kule kulogwa ama kuchawiwa na kuwangiwa usiku graph imeshuka sana na anga limetulia mno.

Hizi mvua zikiendelea hivi hivi tutarajie mengi

Mkuu:
Unaposema wachawi wana kipindi kigumu kwa sasa (wakati wa mvua) una maana gani, kwani ni lazima wafanye huo uchawi wao, hawawezi kuishi bila hivyo au kungojea kiangazi.
 
Mbona vijijini kipindi cha mvua kunakuwa na vifo vingi vya vijana na inasadikika wanageuzwa misukule wakalime, kipindi cha kilimo ni kipindi cha mvua, hebu nidadavulie mshana jr
 
Mbona kama vile mi naonaga vinaendana na maji.Ndo maana kanda za ziwa wanasifikaga kwa uchawi.Nipe muongozo mshana.
Ukienda kisiwa cha ukara, mamba na viboko vinafugwa ndani ya maji, au unasemea maji ya mvua
 
Ahahaaaaa ni noma sana, kama vipi inyeshe mwaka mzima.
Kwahiyo mkuu mshana wataka kusema kipindi hiki cha mvua hizi zinazoendelea
warozi na wanga wako kwenye "Sabbatical leave"..?
 
Back
Top Bottom