Hatima yangu
Member
- Dec 3, 2022
- 7
- 11
Naomba kujitambulisha
Mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 22 kutokea mkoani Mwanza. Kwa sasa ninaishi Manzese jijini Dar es salaam. Elimu yangu ni kidato cha sita. Sina familia na wala sijawahi wazia kutokana na ugumu wa kimaisha nilionao pamoja na kukosa uelekeo wa maisha yangu
Niko mbele yenu kuwaomba kwa mwanafamilia yeyote mwenye walau nafasi ya kazi katika kampuni / super market / duka / Hotel au assets nyingine kama hizo. Au mwenye connection za kazi viwandani au mahali popote ambapo ninaweza kujishikiza na kutengeneza future yangu anisaidie. Kwa sasa maji yamefika shingoni, napitia kipindi kigumu sana cha kimaisha. Sina mbele wala nyuma. Nina mzigo mkubwa sana nyuma yangu, bado umri unakwenda, majukumu yanaongezeka, napatwa na msongo wa mawazo, nakonda, nashambuliwa na "Sonona" kila uchao. Nina hali mbaya sana ya kimaisha
Naombeni walau nipate mahala pa kujishikiza ili kuwabeba wanaonitizama nyuma yangu, ili nami nitengeneze maisha yangu, nami nihame hapa kwa ndugu, si mnajua tena athari za kukaa kwa ndugu!
Natamani kurudi zangu nyumbani, lakini kule nitaenda kuwaongezea mzigo tu. Bora tuungane wana jamiiforums wenzangu, mnisaidie nami nipate maisha. Napitia kipindi kigumu sana cha kimaisha Kigumu mno
Nahitaji msaada. Mwenye kazi / connection yoyote walau kibarua kiwandani anisaidie
Niko tayari kufanya kazi mahali popote pale. Kuhusu kulala, hata nje nitalala. Kikubwa najua natengeneza kiasi kadhaa ambacho mwisho wa siku kitanisaidia kutengeneza maisha yangu, kupanga chumba changu, kujiendesha mwenyewe, kuwanyenyua wanaonitizama, kutengeneza future iliyo njema kwa familia yangu ijayo
Summary
Jinsia: ME
Umri: Miaka 22
Elimu: Kidato cha sita
Aina ya kazi: Yoyote ile itakayonitengenezea future yangu, hata kama ni kuwa kibarua viwandani, sawa tu
Hali ya kimaisha: Napitia kipindi kigumu sana cha kimaisha
====
UPDATES:
Niwashukuru wote mliokuwa bega kwa bega na mimi kwa mchango wenu wa hali na mawazo. Nipende kumshukuru member mmoja aliyeamua kujitolea kunipatia kazi
Shukhrani sana na Mungu awabariki