Amini usiamini Marando ndo anabomoa CHADEMA

Amini usiamini Marando ndo anabomoa CHADEMA

Huku ni kukurupuka, huwezi kusema mtu afukuzwe halafu usitoe sababu ya kufukuzwa, kama ni kusema tu hata mi naweza kusema yeyote fukuzwe kama sina sababu ni sawa na kufukuza upepo

Ni kweli mkuu,mtoa mada yawezekana anajua kitu ila hajaweka bayana alichonacho moyoni.
 
naomba muelewe kwamba cdm ni taasisi kubwa haya ya ushushushu nao ni taasisi ndani ya cdm kama idara ya chama komavu,

Je nani anajua aliyekusanya na kutuletea data za wasaliti woote pamoja na jinsi walivyopokea malipo yao?

Naomba watu msijazwe mzimu wa usaliti na mawenge yao.kama mmeona cdm imewashinda tuachieni chama kistaarabu na mwende huko makohitajika pls!
 
Baada ya kugonga mwamba kuisambaratisha CHADEMA kwa kumutumia ZITTO sasa mnataka kumtumia MARANDO endeleni lakini nawaambia ukombozi huu unacheleweshwa tu lakini uko palepale muda ukifika hakuna wa kuzuia nguvu ya umma
 
na mtei je endeleeni kufukuzana jinamizi la ukabila linawala
 
toa uharo wako hapa,cdm ni chama makini kuliko.......???? kamanda Marando tunakukubali na kwa pamoja tunaijenga cdm!!!
 
Binafsi siwezi kupinga hilo inawezekana nikweli mana sioni anachokifanya Cdm na huenda akawa ndie M2
 
Habari wana jf....
Napenda kuwajuza kuwa kuwepo kwa mtu huyu ndani ya cdm ni hatari sana hata akifukuzwa leo cdm wamechelewa sana.

Marando alikuwa mshauri mkuu ikulu enzi za Mwl. Nyerere na anazijua siri kubwa za ukomboz kusini mwa Africa.

Wengi mkitizama umri wake mnaweza kuuliza au kupinga hoja yangu lakn mm nafahamu kinachoendelea...
Mabere ki umri ni mkubwa sana kuliko mdhanivo.

Nasema huyu ndo mbaya wa cdm...

Nawasilisha.

Kwa hiyo kwa hayo uliyoandika umemaliza na unataka tukuamini!? watakuamini vijana wa buku saba tu.
 
wangekua wamemjua siku nyingi sana,nawaamini cdm wanafanya kazi kuliko unavyodhani,kama zito tu simu zake zilifuatiliwa hadi akapatikana,why not this? Marando si msaliti
 
Mimi ninaweza kukubaliana kidogo na mleta mada kwani tumeshuhudia akiondolewa katika nafasi ya mwanasheria mkuu wa CDM huku tukiwa hatujafahamishwa nini kilichopelekea kuondolewa. Pili hadi sasa hatujaambiwa yule M2 katika ule waraka wa Usaliti ni nani kitu ambacho kila siku hufikiria M2 ni mabere Marando.
 
Marando ninamfahamu binafsi japo siyo kwa karibu sana. Alikuwa ni mmoja wa timu ya usalama wa taifa nyakati za Nyerere ambapo kulikuwa na timu kali sana ya akina Walingozi. Hata hivyo mwanzoni mwa mwaka 1987, ikiwa ni ndani ya mwaka mmoja tu baada ya Nyerere kuondoka madarakani, timu ya usalama wa Taifa pale Ikulu ilibaidilishwa sana ikiwa ni pamoja na kustaafishwa kwa Opiyo ambaye ndiye aliyekuwa mkuu wao. Marando akaanzisha kampuni yake ya sheria, kwa vile amesomea sheria, na ndipo pia alipoanzisha vuguvugu la kudai vyama vingi vya siasa kupitia ile mikutano yake ya NCCR; mimi nilihudhuria mikutano michache ya NCCR kabla hajaanzisha chama kilichopewa jina la NCCR-Mageuzi.

Sijajua lengo lake katika NCCR ile wakati huo kwani inawezekana ilikuwa ni preemetive tactics, ila kwa yeyote aliyekuwapo Tanzania mwaka 1995 enzi za NCCR-Mageuzi kabla haijachafuliwa na Mrema ni vigumu kuamini kuwa kweli Marando bado alikuwa akiitumikia serikali ya CCM wakati huo. Na iwapo alikuwa haitumikii CCM wakati huo, ninakuwa na ugumu kuamini kuwa atakuwa anaitumikia CCM leo
 
Back
Top Bottom