Enzi na Enzi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 888
- 821
Wapendwa wana JF,
Nadiriki kuandika uzi huu hapa nikiamini wataalam wa mambo ya SIASA wapo katika jukwaa pendwa la JF.
Mada yangu ni kuangazia makosa yaliyofanyika mpaka chama cha demokrasia na maendereo chadema kikafikia hatua hii mbaya kilipo kwa sasa.
Hili halina ubishi kuwa CHADEMA kina wakati mgumu kuliko nyakati zote katika siasa hapa Tanzania.
Hakuna ubishi kuwa, chadema kweli kilikuwa nichama cha demokrasia tukiacha maendeleo. Hili linathibitika wazi kuwa! CHADEMA ndo iliibua vijana wengi na kuwajenga kisiasa kitu kilichoperekea kuiamsha hata CCM.
MAKOSA WALIYOFANYA CHADEMA
1. Kiburi
Chadema walijawa na kiburi baada yachama kukubarika mpaka ngazi ya vijijini na raia wa kawaida ukiacha wenye heshima za utajiri, elimu, nk. Ni kweli ndani ya Chadema kulikuwa na kuheshimiana, umoja na kupendana, badala ya kuendeleza utamaduni huo, wakajawa na kiburi wakaanza kubaguana kwa kigezo cha elimu, umaarufu, ukwasi wa fedha na ukanda. Walikuja kushtuka baadae wakiwa wamechelewa, wakaanza kutoa vyeo kwa misingi ya usawa japo ilikuwa too late.
2. Tamaa
Walijawa na tamaa ya kutaka njia ya mkato kuchukua nchi nakuacha misingi mizuri iliyowajenga ! Pamoja na maonyo ya watu walioona mbari lkn hawakujari ! Hii inanikumbusha ajari mbaya ya meli ya Titainic iliyotokea baada ya Nahodha kudharau maonyo kwa sababu ya kiburi nakweli meli ilizama.
Nakumbuka DR. W. Slaa alionya kuwa E. N Lowasa asipokelewe na kukabidhiwa kugombea urais kwakuwa ilikuwa ni kazi ngumu kumsafisha uchafu ambao wao walimpaka, akaishia kuambiwa alitaka urais! Hata kama ilikuwa ndivyo, ni bora ya Dr. ambaye alikuwa zao la Chadema.
Chadema walisahau kuwa walikuwa ndani ya mapambano ambayo haikustahiri mateka mlie mteka apewe siraha na awe mshauri wenu huku akiwaongoza katika vita na maadui ambao yeye alikuwa upande wao.
Lakini haikutosha wakawachukua wana CCM wengi ambao hata kwa hakiri ndogo kwa hadhi waliyofikia hawawezi kufia chama tofauti nakinachowapa ridhiki wao na watoto wao kizazi na kizazi, *hii ilikuwa tamaa*
3. Siasa za uanaharakati
walisahau kuwa siasa ni siasa na harakati ni harakati, wakaingiza harakati za kuanza kutukana viongozi, ubabe, kupinga kila kitu! Wakashusha hadhi ya siasa nakujipambanua kuwa wao ni wanaharakati, tabia hii iliperekea kila ntu kuwashangaa!
Wakatuna mahakama, wakatukana police, wakatukana Rais na mawaziri, wakuu wa mikoa nk. Ikafika sehem kila mtu ndani ya chadema akawa msemaji simwanamke si mwanamme watanzania wakawashangaa. CCM wakakaa kimya, wakaandaa ntu mmoja wa kuwajibu kiuanaharakati nae ni MSIBA. Hoja za serikari zikajibiwa na Dr Abasi, Msemaji wa serikali, hoja za chama zikajibiwa na Polepole au Dr Bashiru Ally! Wao ikawa vurugu! Leo heche, kesho Msigwa, usiku Lema, mchana Ester Bulaya, asubuhi Halima Mdee, mara John Mrema, mara Mangi Kimambi, mara Fatma Karume na wengine; kifupi ikawa vurugu.
Chadema nahisi waliwadharau katibu mkuu Dr Mashinji, Prof. Baregu, Prof. Safari na wengine. Wakaingia mkenge wakujibishana na mkuu wa mkoa wa Dar P. Makonda, akawa anawajoki kwa kuwapa matamko ya kisiasa wanajaa hasira! Nahisi CCM ilikuwa imewasoma. Na kama kuna mtu kacheza nao Chadema, ni P. Makonda. Mi namuona anaijua siasa.
4. Chadema wakaanza kutetea wezi, wauza dawa za kulevya, wahujumu uchumi, vibaka na wanywa viroba!
Vyeti feki napo wakatetea, wakapinga utumbuaji mda huo wananchi wakifurahi. Nadhani ilifika hatua taarifa ya habari bila kusemwa magufuri haikunoga kwa watazamaji. Hili lilikuwa nikosa, wakawa wanashangilia ndege zetu kukamatwa, wakatamka bungeni na kwenye mitandao kuwa Barrick itaishitaki nchi matokeo yake rais wa Barrick akatia team kwa ndege binafsi. Hili nalo lilikuwa kosa kubwa kama chama kinachotaka kushika dola.
5. Covid19
Korona imewamaliza sana chadema, nabila aibu hawakutaka kujisahihisha mapema, kwani aliyetoa tamko ni ester bulaya baada ya malalamiko alitakiwa mbowe atengue hyo kauli mapema lkn wakashadidia kiasi kwamba mpaka wao kwa wao ikawala , na mbaya zaidi Dr john pombe magufuri akawa mshindi baada ya shirika ka afya WHO kukariri yaleyale aloyasemq mh. Rais, baadae marekani na nchi jirani nao wakaufyata mkia! Hapo napo walikurupuka.
Kelele zilizopigwa mda mlefu za rudhuku ya chama kuliwa na watu wachache zikashika kasi, utemi ndani ya chama ukashika kasi mambo ambayotulionya mapema, nahata wanapokuja na majibu hawajibu maswali ya wanachama kuhusu matumizi ya rudhuku, ujenzi wa ofice za chama mikoani na masrahi ya wanachama wengine.
NINI CHA KUFANYA
Chadema mkubari matokeo yakuwa chama mmekipasua kwa mambo niliyoyataja na mengine mengi ambayo sikuyaeleza humu!! Inabidi mtulie mrudi kuziba ufa japo nikazi ngumu, muachane na siasa za matusi na na siasa za kuvizia. Kama kweli mnataka kuchukua dola. Huwezi ukamtukana IGP ukamtukana TISS, ukatukana MAHAKAMA ukamtukana RAIS hasa asiye mwizi na ukafanikiwa.
Hata kama ni wabaya kwako cheka nao lakini si wema kwako! Siku wakiingia anga zako unawalipua. Lakini hizo siasa mnazofanya za kutegemea mataifa ya magharibi, na wanaharakati hazitawasaidia.
Yupo wapi Mabere Nyaucho marando? Yupo wapi Prof A. Safari? Yupo wapi Dr W. Slaa? Yupo wapi W. Lwakatare? Mmekaa mkajiuliza kwanini wabunge na wanachama wanahama chama? Je, wote wananunuliwa? Kama ndiyo, kwa nini wanunuliwe? Je, na nyie mlinunua wabunge na wana CCM waliohamia kwenu?
ANGALIENI MLIPO ANGUKA MKAPATENGENEZE MUENDELEE NA SAFARI
Enzi na enzi
Dar es salaam.