Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 5,353
- 11,495
Inawezekana wana Chadema wakawa na sababu za msingi kuamini katika wanachama wote walionao na viongozi wote anayefaa ni Mbowe tu. Hamna mwingine.
Wale waliomo ndani walioamini wana uwezo mkubwa zaidi ya Mbowe wanakuwa wamepigwa kumbo, hawajaridhika fukuto linaendelea.
Prof. Safari kaamua kuachana na nafasi ya Umakamu Mwenyekiti. Hili mnaweza liona kama ni jepesi. Si jepesi kiasi hicho. Safari alikuwa muunganiko mwingine mzuri katika mambo fulani sasa msishangae akijiunga ACT/CCM au akaamua kunyamaa tu.
Mbowe kwanini uwachagulie watu Makamu awe Tundu Lissu? Je waliotaka kugombea maana yake wakitaka kugombea wanapingana na wewe Mwenyekiti? Anaadhibiwa.
Kwa nini usingewasiliana na Tundu Lissu huko aliko na kumwomba agombee nafasi hiyo? Au ukawatumia vijana wako kama walivyokuchukulia wewe form nao uwaambie wamchukulie na Lissu? Halafu wewe ukanyamaza kuacha sanduku liamue?
Waliotaka kugombea nafasi hiyo maana yake sasa watabaki na kitu rohoni. Pengine mnaweza mkawa hamguswi na wanaohamia CCM.
Kuna wanaoenda kwa sababu ya maslahi binafsi na kuna wanaoenda kwa hasira kuona hawatendewi haki ndani ya Chadema.
Kwanini kuna imani kuwa Mbowe pekee ndo anaweza iongoza chadema? Kwa nini iwe kutaka kumwondoa kwenye uongozi mbowe ni vita na CHADEMA?
hizi habari zinapojirudia rudia zinaleta ukakasi sana. Kumbukeni sakata la Chacha Wangwe, Zitto, Sumaye, Cecil nk.
Kutaka kugombea uenyekiti isiwe dhambi. Kuna watu wapo Chadema wameamua kususa wawaachie vijana wavuta bangi na wasiojielewa kupiga kelele.
Swali la kwanza. Mabere Marando amepatwa na nini ndani ya Chadema? Ni miaka sasa, e kuna jambo? Na wengine wengi watu wazima. Mbona kimya kingi?
Swali la pili. John Mnyika katika miaka hii 4 nini kimempata ndani ya Chadema? Ukimya wake unaleta maswali mengi kuliko majawabu. Huyu ni mmoja ya vijana wajuvi wa kujenga hoja na muelewa. Amepigwa ganzi gani?
Mbowe anataka abaki na vijana waganga njaa ambao hawataweza kumhoji. Watu wazima wote wanaonekana kushindwa kuendana naye. Chadema inajila yenyewe toka ndani.
Mnapoambiwa ukweli hamtaki. Mnakuwa wajeuri. Mnaamini kila anayewakosoa ni CCM na kila anayewasifu (praise and worship) ndiyo mwana Chadema bora.
Huku mkiwaandama CCM nao kwa kuendeleza nyimbo za Praise and Worship.
KAMBA HUKATIKIA PABOVU.