Amina Ally unaharibu kipindi cha Amplifier Clouds Fm

kumbe nawe umeona mkuu kipind kipo serious ila yeye hayuko sifa nyingi kanakera kinyama bora Ea radio
 
Huyo dada mbona yupo vizuri na ameendana na kipindi...

keep it up sister kitaa kinakuelewa
 
Duh kweli kibaya hakijifichi leo tu jioni tu amenikera na style yake ya kupayuka payuka na utani wa kulazimisha usiochekeshe. kwa kifupi hapo Ruge umekosea huyo Amina hawezi kipindi hicho kabisa amekiharibu halafu anaongea mfululizo hamuachii mr ayo nafasi.
 
Duh kweli kibaya hakijifichi leo tu jioni tu amenikera na style yake ya kupayuka payuka na utani wa kulazimisha usiochekeshe. kwa kifupi hapo Ruge umekosea huyo Amina hawezi kipindi hicho kabisa amekiharibu halafu anaongea mfululizo hamuachii mr ayo nafasi.
Design zile za kumpa rift mtu njian af anataka kukata kona na kupiga honi.......
 
Habari Wakuu, heri ya Sikukuu ya Mapinduzi...................

Awali ya yote napenda kusema mimi ni moja ya vijana wachache hapa mjini ambao bado tuko "very loyal" kwa radio hii maarufu ya Clouds Fm. Despite vipindi vya redio hii pendwa kwa vijana (kwa mujibu wa IPSOS 2015), kujaa matangazo ya biashara na content zisizo na tija kwa Taifa, ni nadra sana kwa mimi kukosa kusikiliza vipindi vya "Amplifier" by Millard Ayo, "Sports Extra" na "Nambie" kwa Zaidi ya miaka saba sasa, pengine sababu content ya vipindi hivi vinaendana na character yangu.

Ni kama wiki mbili au tatu zimepita tangu Dada huyu Amina Ally aliekuwa akifanya vizuri sana katika kipindi cha "Nambie" aanze kusika hewani katika kipindi cha Amplifier akiwa na Millard Ayo. Nilipomsikia kwa mara ya kwanza nilifurahi na kuhuzunika kwa pamoja. Nilifurahi nikijua kipindi kitakuwa kizuri Zaidi maana mafundi wawili wamekutana, na nilihuzunika na kuwa na hofu kidogo nikidhani pengine soon Millard Ayo atakiacha kipindi hiki na hivyo Amina Ally anaandaliwa kama replacement.

Cha ajabu tangu Dada huyu aingie kwenye kipindi hiki, amekua hovyo kweli, anacheka cheka bila msingi na kuleta stori zisizoendana na flow ya kipindi. Kwa kifupi amekuja kuiharibu Amplifier na kuifanya ishindwe kueleweka kwa wasikilizaji makini kama mimi. Nahisi Millard Ayo ameshaligundua hili ila anashindwa tu kumchana yule dada.

Nashauri program manager wa "Mawingu FM" kulitazama hili kwa jicho la tatu maana yule dada kawa kero kabisa na kipindi kinamshinda katika Nyanja zoote na ikiwezekana arudishwe kwenye kipindi chake cha zamani.

Nimewasilisha mawazo ya wengi ambao wanakerwa na uwepo wa dada huyu kweny kipindi hiki kupitia platform hii nikiamini taarifa hii itawafikia Clouds Media Group.
Mie nshaachana nacho kitambo...serious ana boa bi dada
 
Duh kweli kibaya hakijifichi leo tu jioni tu amenikera na style yake ya kupayuka payuka na utani wa kulazimisha usiochekeshe. kwa kifupi hapo Ruge umekosea huyo Amina hawezi kipindi hicho kabisa amekiharibu halafu anaongea mfululizo hamuachii mr ayo nafasi.
Kama Ruge amenogewa hata upige kelele haitasaidia. Ushauri wangu muda huo ukifika jaribu kusikiliza DW au BBC
 
Wanamuita Meena - Anyway ngoja nikuelezee kwanini walimuweka pale.. East Africa Radio wana The cruise kuna Queen Fifi na yule jamaa watu wengi sana ikifika mida ile huwa wanasikiliza sana East Africa Radio kutokana na Amplifier kupwaya na kua na matangazo 10000 ingawa ndipo hela inaingia wakaona wa mlete ili wawe kama Ea Radio..
2- Inasemekana Amplifire ilikuwa inafanyaka nyumbani kwa Ayo na kurekodiwa na kutumwa studio alafu Faraja (producer) akawa ana play vipande kuringana na news (Ayo yuko busy na ujenzi wa taifa ) katika station yoyote huwa kuna classfied adverts ambazo huwa zinasomwa hapo hapo wakati kipindi kinaendelea sasa zile zilishindwa kusomwa kwa sababu Ayo hayupo kwa io wakaona ni dharau hii kwa vile kijana ameona amefahamika kaanza dharau.. Wakamfuata Meena Bbc waka panda dau mazaga kede kede mkataba wakampa wakaja kumuweka hapo bila Ayo kufahamu siku ikafika akaambiwa utakua unafanya kipindi na uyu bidada wakampa na stress zingine.. Imebidi jamaa (ayo) avunje utaratibu wa zamani sa ivi kipindi kinafanyika studio (clouds) na hawezi kumuelekeza njia kuringana na maisha ya utangazaji yalivo
Huu uongo. Meena alikuwa anafanya kazi EaTV na amekuwa na Clouds muda mrefu Sana.
 
Hivi ni Amina Ally au MinaAlli,maana hata jina lake silielewi huyu dada.Hiyo Amplifaya akiwepo huyo Mina sijui Mc.Steve/muugiza sauti ni mpuyangooo tuu
 
Tangu haka kadada kaanze kutangaza nimeacha kusikiliza kanamshobokea Sana Millard halafu kana ingiza issue Za utani wa mapenzi Mara kajifanye kanamlilia Millard akatoe out kipindi kizima kujisifia yuko na millard yaan kanaboa sana
 
Huenda hao watangazaji ni Wapenzi, hivyo wameamua kuleta mapenzi yao studio.
Binafsi huwa siipendagi kabisa Clauds Fm, ni radio ya kinafiki, umbeya na ngono tu. Sinaga muda wa kuisikiliza.
 
Back
Top Bottom