Wasafi FM mmetia aibu leo katika kipindi cha Jana na Leo

xox

JF-Expert Member
Sep 23, 2018
1,398
6,515
Japo kuna baadhi watatetea kuwa kina Putin hawatumii kiingereza lakini ni fedheha kubwa mno kwa msomi ambae kasoma kwa kutumia kiingereza akashindwa kufanya mazungumzo yenye tija kwa lugha hiyo.

Leo kwenye kipindi cha Jana na Leo cha Wasafi Fm watangazaji wote watatu wameshindwa kuwahoji kina Prophet Lovy kwa kiingereza sahihi.

Adeliah alikuwa kama hayupo studio mbali ya siku zote yeye kujifanya mjuaji, Edo Kumwembe 'ze ze' zilijaa kiasi cha wanaohojiwa kutoelewa maswali. Kuja kwa kubwa lao baba mjua yote Oscar Oscar, huyo ndio kabisa, hata mtoto wa darasa la nne wa hizi academics anamtoa knock out.

Ifike wakati wa Tz tuache kuishi kwa mazoea kuwa kiingereza si muhimu. Kwa dunia ya leo, kiingereza kina umuhimu mkubwa mno kama lugha kuu ya mawasiliano duniani.

Enzi za uandishi wa habari wa kina Benjamin Mkapa, muandishi alikuwa na uwezo wa kufanya mahojiano ya debate kabisa na mtu mwingine kwa kiingereza fasaha. Lakini leo kila mjinga anajiita muandishi wa habari lakini maswali wanayouliza unaona aibu wewe msikilizaji.

Wasafi FM mmetia aibu leo.

Kuanzia Dk ya 53.


View: https://www.youtube.com/live/VGlaoWS4pUc?si=uWeFxTjB0Eivp0oQ
 
Nina hakika hao waandishi usiku wa kuamkia leo hawakulala wanahofia kiingereza.

Ila ni halali kwa wakenya kutuona wajinga. Hapo walikuwa wanahoji waafrika wenzao, ingekuwa wanahoji muingereza au mmarakeni halisi nahisi wote wangekacha kipindi.
 
Back
Top Bottom