Amina Ally unaharibu kipindi cha Amplifier Clouds Fm

Mugabe Tz

Senior Member
Apr 6, 2016
196
215
Habari Wakuu, heri ya Sikukuu ya Mapinduzi...................

Awali ya yote napenda kusema mimi ni moja ya vijana wachache hapa mjini ambao bado tuko "very loyal" kwa radio hii maarufu ya Clouds Fm. Despite vipindi vya redio hii pendwa kwa vijana (kwa mujibu wa IPSOS 2015), kujaa matangazo ya biashara na content zisizo na tija kwa Taifa, ni nadra sana kwa mimi kukosa kusikiliza vipindi vya "Amplifier" by Millard Ayo, "Sports Extra" na "Nambie" kwa Zaidi ya miaka saba sasa, pengine sababu content ya vipindi hivi vinaendana na character yangu.

Ni kama wiki mbili au tatu zimepita tangu Dada huyu Amina Ally aliekuwa akifanya vizuri sana katika kipindi cha "Nambie" aanze kusika hewani katika kipindi cha Amplifier akiwa na Millard Ayo. Nilipomsikia kwa mara ya kwanza nilifurahi na kuhuzunika kwa pamoja. Nilifurahi nikijua kipindi kitakuwa kizuri Zaidi maana mafundi wawili wamekutana, na nilihuzunika na kuwa na hofu kidogo nikidhani pengine soon Millard Ayo atakiacha kipindi hiki na hivyo Amina Ally anaandaliwa kama replacement.

Cha ajabu tangu Dada huyu aingie kwenye kipindi hiki, amekua hovyo kweli, anacheka cheka bila msingi na kuleta stori zisizoendana na flow ya kipindi. Kwa kifupi amekuja kuiharibu Amplifier na kuifanya ishindwe kueleweka kwa wasikilizaji makini kama mimi. Nahisi Millard Ayo ameshaligundua hili ila anashindwa tu kumchana yule dada.

Nashauri program manager wa "Mawingu FM" kulitazama hili kwa jicho la tatu maana yule dada kawa kero kabisa na kipindi kinamshinda katika Nyanja zoote na ikiwezekana arudishwe kwenye kipindi chake cha zamani.

Nimewasilisha mawazo ya wengi ambao wanakerwa na uwepo wa dada huyu kweny kipindi hiki kupitia platform hii nikiamini taarifa hii itawafikia Clouds Media Group.
 
Nilitaka kulisema hilo lakini nikaona nikaekimya sababu mimi sio mpenzi wa clouds fm lakini kwa siku kadhaa sababu ya eneo nililo kuwepo haikuwa na namna ikawa nasikiliza tu,dada anaongea sana kushinda millard point chache anarukiarukia vitu mwenzie akiwa anataka kuelezea nadhani hii couple bado haija match labda kama ndio katika kipindi cha mpito kabla millard hajaachana na mawingu fm
 
Japo si shabiki wa mawingu kabisa nilikuwaga na hisi kipindi cha Ayo ndio kipindi serious pekee pale, ila toka yule sista aingie naye amekirejesha kwenye vipindi vya matani vile vile.
Ofcoz mi ndio nafurahia mawingu wakiwa wana fanya vibaya ila yule sista anatakiwa aweke u siriaz flan hivi at least unao endana na kipindi.
*sauti yake huwa naipenda though
 
Kitika vipindi bora kabisa vya clouds ukitoa cha michezo ni hicho Amplifier, kilikuwa kipindi kilichokuwa na habari bora na mtangazajia laikuwa serious, lakini sasa kimekuwa ni kipindi cha comedy, kimekufa kabisa maana yake

Huyo dada Amina Ally ana "boa" kuliko maelezo kazi ni kuchekacheka tu hata kama hakuna cha kuchekesha, pia kamzidi nguvu kabisa Ayo, Ayo amekuwa kama ni mtangazaji msaidizi tu, Clouds kama wanapita humu walifanyie kazi hilo,
Pia wasisahau kumpunzisha Adam Mchomvu ni mtu mwingine pia anaeharibu Kipindi cha XXL,
 
Yaan Millard Na amina hawajaendana kabisaaaa, yaan mama 1000 usikilize so so fresh ukutane Na many baby Na Adam mchomvu hawa watu, kipindi chao kingekua sio using mwingi wangepata mashabiki wengi, yaan kiukwel napenda SNA matan ya Adam Na many wananivutia sna
 
Sort mamy bby sio many
 
Jamaa big up sana uliyeleta kero hii! Mimi nikiri kuwa ni mpenzi sana wa amplifier na sports extra ukitoa vipindi hivyo sina time na vipindi vingine pale clouds. Mpaka mama yangu ambaye ana miaka 60's naye anakipenda sana kipindi hicho. Sasa kuingia kwa huyu dada/mama kumevuruga kabisa kipindi cha amplifier. Nina wiki sasa nimeacha kabisa kukifuatilia hata mama yangu kaacha Sasa. Clouds nadhani ujumbe mmeupata lifanyieni kazi hili
 
Kitika vipindi bora kabisa vya clouds ukitoa cha michezo ni hicho Amplifier, kilikuwa kipindi kilichokuwa na habari bora na mtangazajia laikuwa serious, lakini sasa kimekuwa ni kipindi cha comedy, kimekufa kabisa maana yake

Huyo dada Amina Ally ana "boa" kuliko maelezo kazi ni kuchekacheka tu hata kama hakuna cha kuchekesha, pia kamzidi nguvu kabisa Ayo, Ayo amekuwa kama ni mtangazaji msaidizi tu, Clouds kama wanapita humu walifanyie kazi hilo,
Pia wasisahau kumpunzisha Adam Mchomvu ni mtu mwingine pia anaeharibu Kipindi cha XXL,
Hahahaha
Yaan yule sista badala y a yeye kuendana na Millard sasa amefika stage ana taka Millard ndio aenda naye, halafu na kisaut kile akiongea tuu bas Millard ni kama anapotea
 
Back
Top Bottom