Clouds FM inapoteza mvuto au imeshindwa kwenda sawa na mabadiliko na uwepo Radio nyingine?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
clouds-pic-data.jpg

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa vipindi vya Radio, utagundua kuwa kuanzia saa 12 asubuhi kipindi cha Good Morning kutoka Wasafi FM kinasikilizwa sana mitaani, kwenye madaladala, magari binafsi kuliko ilivyo Power Breakfast ya Clouds FM. Nimeshindwa kuelewa tatizo ni nini kwa Clouds kupoteza usikilizwaji kiasi hiko.

Kipindi cha Good Morning kinafanywa na Salma Dakota, David Rwenyagira, Oscar Kawau, Zungu, Charles William na Babu Zembwela wakati Power Breakfast inaanza na Matei, Khan then wanafuata Fatma (DJ Fetty), Masoud Kipanya, Ceazer, Sasali na Bonge. Tangu kuondoka kwa Gerald Hando ni kama hawajawahi kukaa sawa, bado wakamuondoa Barbara Hassan kumpeleka kwenye TV ndio kabisaaa.

Kwa kiasi kikubwa Clouds kwasasa inabebwa na Leo Tena, Amplifaya na Jahazi, ila PB, XXL, Sports Extra, Ala za Roho vyote vinakufa taratibu.
 
Mtoa mada umemtaja Sasali nimekumbuka kitu. Siku ya kwanza kumuona yule mchungaji wa kanisa la Neema juu ya Neema kina Sasali walimuita studio ktk kipindi chao cha Jumapili asubuhi.

Wakampa promo la maana. Leo namuona bwana yule katika video inayozunguka anasema eti AMRI 10 ZA MUNGU NI UPUUZI....NI MAHAMNA. NI UJINGA, Kweli?

Hivi vyombo vya habari viwe vinaangalia watu wa kuwapigia promo. Sio wanajibebea tu watu bila kungalia madhara yanayoletwa na watu hao. Hii ni nje ya mada lakini
 
Kwangu naona XXL ndo kama haina mvuto kabisa saivi. Yani tena kama siku hamna mgeni ndo hamna kitu kabisa
 
Ndio tatizo la kuajiri wau kwa sifa ya kuongea sana na kuropoka badala ya weledi.

Vijana waliosoma journalism na ni professionals wa kazi hiyo wapo kitaa hawana ajira halafu wao wanaajiri mwijaku, swebe, kingwendu kwasababu mtu ni maarufu au anaongea sana kutangaza matokeo yake wanaongea vitu vya ajabu humo redioni hadi mtu unajiuliza kwann nasikiliza hii redio muda huu.
 
Watanzania hebu tafuteni kazi za kufanya na muwe serious!! Hizo takataka za waandishi kanjanja bongo ndo mnakesha kusikiliza? Umaskini utawatoka lini? Stupid!!
"Stupid" Hii ni kama ya yule bibi anayesaidiwa kuendesha nchi na msoga!?
 
FM radio stations kwasasa hazina content yoyote zaidi ya matangazo ya Betting tu,yaani kipindi cha asubuhi Clouds mfano ndani ya saa moja content haizidi dk 10......najua matangazo ndiyo yanaleta hela ila mpangilio ni zero kabisa maana wanaweza kuwa na mgeni wanamuhoji ile anaanza kujibu tu matangazo yanaingia.

NB:Niliacha zamani kusikiliza Redio,saizi ni mziki tu
 
CLOUDS KWA SASA IMECHOKA KIONGOZI. WALISHINDWA KUBADILIKA KULINGANA NA WAKATI.
Kubadilika vipi wakati karibia wengine wote wanapita kwenye nyayo zao!? Hao Wasafi unaowasema "asubuhi ni kelele tupu, si ajabu nikipanda daladala yenye kelele zao huwa napachika earphones zangu nisikilize japo music tu."
 
Kwangu naona XXL ndo kama haina mvuto kabisa saivi. Yani tena kama siku hamna mgeni ndo hamna kitu kabisa
Naweza kuwa na miaka hata minne toka nikisikilize hiko kipindi mara ya mwisho.
 
FM radio stations kwasasa hazina content yoyote zaidi ya matangazo ya Betting tu,yaani kipindi cha asubuhi Clouds mfano ndani ya saa moja content haizidi dk 10......najua matangazo ndiyo yanaleta hela ila mpangilio ni zero kabisa maana wanaweza kuwa na mgeni wanamuhoji ile anaanza kujibu tu matangazo yanaingia.

NB:Niliacha zamani kusikiliza Redio,saizi ni mziki tu
Mimi pia Aisee. Redioni hamna kitu.
 
Redio nikisikiliza jahazi na Kibonde tu, toka afariki baaasii!! Wengi wamevamia studios uchambuzi mdogo hawana mvuto wanakera

Zaidi wanatutangazia MUDA "hivi sasa ni saa saba kamili kwa saa za afrika mashariki" hiv sasa ni saa saba na dk moja kwa saa za afrika mashariki ......
 
Back
Top Bottom