Amenisaliti anang'ang'ania vitu vyangu

Amenisaliti anang'ang'ania vitu vyangu

Wana jamii wenzangu mimi ni mwanaume wa miaka 29 nimekuwa na uhusiano na msichana kwa miaka 3 mwishoni mwa mwaka niligundua kuwa ana uhusiano na mtu mwingine na nilipombana kwa maswali alikubali na kusema wamekuwa pamoja kwa miezi 8 ila wameachana wiki mbili zilizopita nimeumia sana maaana nilimwamini mno, nimeamua kuachana nae ila nilimpa laptop yangu ya gharama sana ya laki 9 kwa makubaliano nitamnunulia ya kwake ila baaada ya usaliti aliofanya nimeona anipe mali yangu .Cha ajabu anang'ang'ania kwa kusema anaitumia na kwa sasa hawezi kunipa,kipekee sipendi fujo nafikiria kutumia nguvu ila naona ni utoto na naweza kusababisha matatizo.Naombeni ushauri nifanyeje?

sikujua laptop ya laki 9 ni ya gharama sana. .....mwachie ni ujira wake wa kukuvulia kyupi kwa miaka mitatu mfululizo
 
Best jamaa aliahidi huyu kuwa bint atumie laptop ya jamaa mpaka atakaponunuliwa yake na jamaa,sasa jamaa hajatimiza ahadi ati!!!

Ukisoma vizuri utaona kuwa hayo makubaliano ya kununuliwa laptop yalitegemea status ya relationship yao!!

Hajatuambia lakini ndani ya miaka hiyo mitatu naye amepewa vingapi na bint na amerejesha vingapi baada ya kuachana!!!!

Usikimbilie kutaka kujua mengine ikiwa hili la laptop bado hujafanya hukumu ya haki...

Katika mahusiano ya ndoa, mtu hupaswi kubinafsisha mali za mpenzi mliyetengana...kesi kama hizi za dhuluma zimeshawaweka wengi matatizoni na huwa zipo sana mahakama za mwanzo
 
sasa ulimuachaje kabla kuchukua vya kwako kabisa...dah au ndo mihasira ilikuzidi...? wewe ungechukua laptop yako kimya kimya afu ndo umpige kibuti...
 
Haha haaaaaaaaa!
Sitaki hata like yake,ila ukweli lazima usemwe
Kwa hiyo unamuona yuko sahihi kuwa na mchumba ambaye amemvalisha pete huku akiwa na mwingne wa pembeni? au wewe umebase kwenye laptop peke yake?
 
Ukisoma vizuri utaona kuwa hayo makubaliano ya kununuliwa laptop yalitegemea status ya relationship yao!!

Usikimbilie kutaka kujua mengine ikiwa hili la laptop bado hujafanya hukumu ya haki...

Katika mahusiano ya ndoa, mtu hupaswi kubinafsisha mali za mpenzi mliyetengana...kesi kama hizi za dhuluma zimeshawaweka wengi matatizoni na huwa zipo sana mahakama za mwanzo

Msema peke yake muongo best,natamani bint naye angekuwa member humu atupe upande wa pili wa habari.
Inawezekana hata hiyo laptop alimuuzia!!!!
 
Kwa hiyo unamuona yuko sahihi kuwa na mchumba ambaye amemvalisha pete huku akiwa na mwingne wa pembeni? au wewe umebase kwenye laptop peke yake?
Hayo makosa mengine jamaa alishahukumu kwa kumuacha,mimi niko hapooo kwenye la laptop hapo
 
Mmechezeana miaka mi 3 leo unadai laptop kisa ya laki 9, laki tisa nini? hebu na wewe rudisha dhahabu uliyokuwa unachimba kwenye mgodi wake ndani ya miaka mitatu, ni ushamba, ni umaskini au ni nini?
 
sasa hata kama ni mimi sikupi.... kwa sababu naachana na wewe zaidi ya migegedo na starehe na outing nimebaki na kitu gani cha kwako amna sasa... mwachie bwana miaka mitatu ujamnunulia ya kwake mwachie tu bwana.... au kama kuna kitu kingine ulimpa sema ni haali yake kung'ang'ania kabisa nampa support nipe namba yake nimpe ujanja mwingine ...
Matatizo ya kugusa rafiki unayaona? Ukionja nyama ya mtu...... Umeniamini sasa?
 
Mmechezeana miaka mi 3 leo unadai laptop kisa ya laki 9, laki tisa nini? hebu na wewe rudisha dhahabu uliyokuwa unachimba kwenye mgodi wake ndani ya miaka mitatu, ni ushamba, ni umaskini au ni nini?
Kwani dhahabu alikuwa anachimba bila ridhaa ya mwenye mgodi?
 
Alimuazima aitumie mpaka atakapomnunulia ya kwake,akimnunulia atarudishiwa yake!!"!!!!

Sasa atamnunulia lini na kikombe cha kahawa kimeshavunjika? Bora aiache tu ili waendelee kuwa mbali .. Kudaidai vitu ni ulimbukeni
 
Pete kitu gani Daudi1? Tena siku hizi wanazibiana rizki tu,mtu anavalishwa pete mpaka inafubaa hakuna dalili ya ndoa.
Bint angekuja akaeleza yake story inge balance,wanaume wengi wanadanganya mabint na pete then wanaanza kuwahubiria uvumilivu huku street wanaendelea kufungua wallet kama kawa!!![/QUOTE
Kwa hili chukua tano ni kweli tena style yao mpyaa wanaenda kununua pete za kavungwe wanakuja na mbwembwe nyingii wanakupotezea mdaa baadae wanakutaftia sababu baada ya kukutumia kama toilet paper. Uliona wap uchumba miaka mitatu kama sio kuzibiana rizki za ndoa... Bora hata alivyojichukulia hako ka laptop ingawa hakana thamani juu ya mda alioupoteza
 
Last edited by a moderator:
Muachie utapata zaidi ya hiyo laptop kwani ndo anacho tumia uli muendelee kuwasiliana.
 
Msema peke yake muongo best,natamani bint naye angekuwa member humu atupe upande wa pili wa habari.
Inawezekana hata hiyo laptop alimuuzia!!!!

Ndio maana ushauri wangu kwa mleta mada ni kulipeleka hili jambo kwa wana usalama, huko ndio itajulikana nani mkweli...

Zaidi ya hapo basi asamehe tu na aendelee na maisha yake...
 
Kwani hiyo laptop aliiba? si alimpa kwa makubaliano ya kumnunulia nyingine amnunulie sasa, hawezi amwachiye yeye ndo anunue
Lakini si wameachana madam mbona unakuwa mkali jamani,Raisi muda wake unapoisha yale ambayo hakuyafanya atayafanya anayekuja yeye aruidishe tu hiyo laptop then atanunuliwa na mwingine atakayeshika madaraka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom