Umasikini na aibu

Umasikini na aibu

Liana N

Member
Joined
Jul 27, 2024
Posts
25
Reaction score
89
Ndugu zangu, mimi nakabiliana na changamoto kubwa ya maisha yangu, ambayo sijawahi kuhisi kama ipo siku itanifikia. Ni kama nimechanganyikiwa, na ukweli nimechanganyikiwa. Najiona kabisa akili yangu haina uwezo wa kufikiri.

Tatizo langu la kwanza ni umaskini. Sidhani kama nishawahi kuishi katika hali ya kiumaskini. Nilikuwa na maisha yaliyokuwa yanaendelea kawaida, lakini sasa ndiyo nagundua kuwa mimi ni maskini na sina cha kujisaidia kabisa zaidi ya matumaini. Hata jana na mwaka jana nilijikuta nimemtukana Mungu na nimejikatia tamaa, nikitamani anipe adhabu yangu ya dhambi ambayo ni kifo. Namjaribu ili tu afanikishe suala lake.

Mimi ni mwanamke mwenye miaka 30. Hapo awali, nilivyomaliza chuo nilipata kazi na nilikuwa napata kama laki moja kwa mwezi. Trainings ndogo zikitokea tulikuwa tunalipwa, hivyo pesa zilikuwa zinaongezeka ila mpaka trainings zitokee.

Baadaye nikaja kupata kijikazi fulani nikawa nalipwa laki tano kwa mwezi, hapo nikiwa na miaka kama 25 hivi. Ila siyo laki tano tu, kuna programs ambazo zikitokea take home inakuwa laki tano, lakini muda mwingine account inaweza kusoma zaidi ya milioni mbili.

Kwa kweli nilikuwa natumia tu pesa zangu na kusomesha watoto wa dada yangu. Nina dada yangu ambaye alipata changamoto za maisha zilizompelekea mpaka kujiua.

Kwa hiyo nilikuwa natumia pesa zangu tu. Nilikuwa najiona bado mdogo na kwamba lazima ntaolewa na tutafanya vitu pamoja.

Basi nikaja kupata mwanaume wa Australia anayefanya kazi Geita kwenye migodi. Huyo mwanaume alikuwa mkubwa kidogo kwangu, zaidi ya miaka 20.

Nilivutiwa naye, lakini mara ya kwanza sikuona kama huyu mtu nitafika naye popote. Sikuwahi kumuomba chochote, lakini alidanganya kwamba familia yake ilifariki kwenye ajali. Basi nikawa interested na nikaanza kumzingatia zaidi kuliko zamani.

Akanambia ananipenda, hapo nikiwa na miaka 26, na mimi nikaona nimepata mwanaume, nikatulia naye kabisa.

Sikuwahi kwenda Australia. Tulikuwa tunakutana tu akipata muda hapa Tanzania, halafu yeye anarudi Australia.

Sikuwahi kumuuliza chochote. Nilijua kama mtu ananipenda, yeye ndiye atasema kitu.

Basi ilibidi nianze kwenda kwenye camp anakofanyia kazi. Ujinga uliniingia niachane na kazi, maana promises alizonipa ni kwamba tutaenda wote Australia akihamishwa kikazi.

Pia alikuwa ananihudumia zaidi ya pesa niliyokuwa naingiza kwa mwezi. Kingine, nilikuwa nadanganya sana kazini kwa sababu ya kwenda kuonana naye. Kila akiwa Tanzania tulikuwa tunaonana kama mara mbili kwa mwezi, hotelini na camp kwake.

Niliacha kazi, akaanza kuniudumia zaidi, kisha nikaenda Dar kwa sababu sote tulikuwa tunapenda kukutana Dar.

Basi ndugu zangu, siku zilivyozidi kwenda, mwanaume hafikirii kuja nyumbani kujitambulisha. Hatufanyi plans zozote za maisha. Nikimwambia ninunue kiwanja, anasema hawezi kununua huku.

Ila pesa ya kodi na matumizi alikuwa ananipa. Tatizo ni kwamba akili yangu ilikuwa imefungwa. Nilijua siku moja tutaenda Australia au nchi nyingine, hivyo nilikuwa naogopa kuanzisha kitu nitakachokuja kuuza baadaye.

Kwa hiyo nilikuwa nafikiria kazi ambayo nitatoa huduma tu, siyo kuuza vitu.

Kadri siku zilivyozidi kwenda, niligundua kwamba familia yake ipo hai. Akanambia ana watoto wawili wa kike na mama yao wametengana (separated). Pia anasema ana cancer na anasubiri apone ndipo waachane kabisa, halafu sisi tuje kuoana.

Akanipa pete ya promise ring, tukaendelea na mapenzi yetu.

Siku zilivyozidi kwenda, nikagundua kwamba anapendana na mwanaume mwenzake. Ila nilikaa kimya kwa sababu tayari tulikuwa kwenye mahusiano zaidi ya mwaka mmoja, nilishampenda na sikuwa na kazi, hivyo nilimtegemea.

Akaanza kutaka tufanye mapenzi kinyume na maumbile. Nilikuwa nakataa, lakini baadaye nikamwambia tukishazaa ndipo tutaanza kufanya hivyo, maana nilikuwa naogopa aibu nikiwa labour kwa sababu nilikuwa nimesikia story nyingi.

Basi akaendelea kunikumbusha sana. Nikaona nimridhishe mpenzi wangu kwa sababu niliamini tunapendana na sitakuwa na mwanaume mwingine zaidi yake. Hata kama alikuwa na shida zake, nilijua ananipenda. Nilijichanganya sana.

Mwaka 2024 ulikuwa mgumu sana kwangu. Dada yangu alifariki, mama yangu akafariki, na bibi yangu naye akafuata. Nafikiri mama yangu alipata mshtuko baada ya dada yangu kufariki, akaja kufariki miezi kama minne baadaye.

Nilikuwa na mawazo sana. Nilinenepa sana na nikaanza kunyonyoka sana nywele mpaka nikapata kipara karibu kichwa kizima. Nilinyoa kumuenzi mama yangu, na uzuri wangu nikahisi umepotea kabisa.

Pia nilikuwa najihisi mpweke zaidi kwa sababu mtu wangu akiwa Australia alikuwa ananiambia tu “good morning” na “usiku mwema”. Hakuwa anachati ndani ya siku kwa sababu anakuwa busy sana.

Nikajikuta nachat na baadhi ya wakaka ili tu niwe occupied. Siku moja alikuja, nikasahau kufuta message kwa sababu sikuwa naona kama ni jambo kubwa.

Kama kawaida yake, huwa anaangalia simu yangu. Huwa naiacha kwa sababu sina kitu cha ajabu. Lakini baada ya kuona zile message akaanza kubadilika, ingawa bado alikuwa ananiambia ananipenda.

Siku moja muda wake wa kuondoka Australia ulipokaribia, akanambia kwamba ataenda nyumbani moja kwa moja kwa sababu kuna msiba wa rafiki yake. Ila maelezo yake hayakuwa yanaeleweka na nilijua ananidanganya.

Baadaye akaniambia yupo anapanda ndege kuondoka, lakini alijichanganya na akanitumia picha ambazo aliwahi kunitumia zamani. Nikajua ananidanganya.

Nikampigia simu, akaniblock. Hakuni-unblock mpaka alipofika Australia.

Baadaye nikamuona amejicommentisha kwenye picha za msichana mwingine kwa comments za lover vibes. Wamefollowiana, nikamuuliza kama huyo ndiye demu wake. Akaniblock, na huyo msichana naye akaniblock papo hapo.

Basi nikakaa nikasubiri siku atakaporudi.

Madereva waliokuwa wanatujua waliinishangaa kwa sababu sikuwa naye tena. Mmoja akanipigia simu, nikajua tu yupo naye.

Basi huyo bwana akampa huyo mwanamke namba yangu anipigie. Akanipigia, baadaye akaniblock. Nilipompigia hakupokea, ila yule mwanaume akapokea.

Wakiwa pamoja, walikuwa wanacheka na kusema, “Huyu ni mbibi amechakaa. Huyo bwana haendani naye kabisa. Kachakaa, ni mrembo wa zamani. Sasa ni muda wetu sisi watoto wa 2000. Bwana tunae na tunatamba naye.”

Nikajiuliza walinitafuta kwa sababu gani, wakati sikuwa hata na muda wa kuwatafuta.

Basi huyo bwana naye akaniblock kabisa.

Nikapauka sana. Sina mtu wa kumkimbilia. Mama yangu keshadondoka kaburini. Nilijihisi nimechanganyikiwa na nikawaza mambo mengi. Niliumia sana kwa sababu ya aibu na kwa sababu ya watoto, hasa mmoja ambaye yupo English medium school.

Nikaona niyaachie yote kwa Mungu, lakini hasira zilinijaa.

Nilipomtafuta, akanambia kwamba aliniona nachat na wanaume na kwamba hanipendi. Hilo limenijaza hasira mpaka leo.

Naona kabisa anamfanyia huyo mwanamke vitu ambavyo hakuwahi kunifanyia mimi. Ni TikToker, wanakutana airport, wanapost picha, na sasa amembebesha mimba. Wanaendelea kucommentiana na wakati mwingine nashikwa na kichaa mpaka natamani kuwavurugia.

Sasa hivi naishi maisha ya umaskini na sina pa kukimbilia. Kama walivyosema, mimi sasa ni mbibi. Sijui nifanye nini na nianzie wapi.

Sikuwahi kutegemea maisha yangu yatakuwa hivi. Vitu nilivyokuwa naogopa zaidi maishani mwangu vimenitokea.

Ila namshukuru Mungu kwa sababu ndugu zangu wengine wamechukulia kwa uzito suala la kuwasomesha watoto.

Lakini sasa hivi nimekuwa mtu mwenye hasira sana. Najihisi nina roho mbaya na chuki kubwa.

Nilirudi kuishi kwenye nyumba ya mama yangu pamoja na watoto. Ninaishi na dada yangu mkubwa ambaye anaangalia nyumba. Hana kipato chochote, ila Mungu anasaidia tunaishi.

Kama kweli Mungu yupo, ndugu zangu, mniombee kwa sababu naona maisha yangu yanaporomoka na nahisi nitaendelea kuishi maisha ya umaskini.

Marafiki zangu wote siwasiliani nao kwa sababu ninaona aibu. Zamani tulikuwa wote tunapambana, lakini sasa mimi ni maskini asiye na mbele wala nyuma.

Ila bado nina hasira na hao watu. Sijui naachaje kuwachukia. Sitaki kuendelea kuhisi hivi, lakini nahisi haya maumivu yataendelea kuwa nami maisha yangu yote.

❤️
 
Achaana na mitandao ya kijamii.
Jitoe huko Kwa muda,futa acc zako deactivate
Tafuta kazi ya kufanya ikuweke bize
Utasahau yote
Kazi nimefanya zakujitolea na zakuwa busy sana…..ata mda wakupumzka nakosa…ila ata ndani siku nimebadlka nimekua kama zezeta imeniathiri mpk ki saikologia.. kuna kpnd nilkua naaibu ya kuangalia watu usoni..ni kitu tuu kinanitokea automatically najhs kama mtu hafai kuniangalia……na nikienda kulala navifikilia, mda wote mpk napitiwa na usingz ata kuota sazngn namuota kwnye mazingira kama nina gombana na uyo mbwana…au nipo kwnye mazingira mngn tofuati sizkmbk ndoto ila kuna namna kama uwa nipo kwnye mazingira yakupishana nae kwnye ndoto..yaan ni kama nina ile sonona yankweli kweli (severe depression) hainitoki ata nikiwa busy..….akili yangu ikiwa imesahau mwili wangu hausahau na watu wakiwa karbu ndo inajiactivate kabsa…..
 
Ndugu zangu, mimi nakabiliana na changamoto kubwa ya maisha yangu, ambayo sijawahi kuhisi kama ipo siku itanifikia. Ni kama nimechanganyikiwa, na ukweli nimechanganyikiwa. Najiona kabisa akili yangu haina uwezo wa kufikiri.

Tatizo langu la kwanza ni umaskini. Sidhani kama nishawahi kuishi katika hali ya kiumaskini. Nilikuwa na maisha yaliyokuwa yanaendelea kawaida, lakini sasa ndiyo nagundua kuwa mimi ni maskini na sina cha kujisaidia kabisa zaidi ya matumaini. Hata jana na mwaka jana nilijikuta nimemtukana Mungu na nimejikatia tamaa, nikitamani anipe adhabu yangu ya dhambi ambayo ni kifo. Namjaribu ili tu afanikishe suala lake.

Mimi ni mwanamke mwenye miaka 30. Hapo awali, nilivyomaliza chuo nilipata kazi na nilikuwa napata kama laki moja kwa mwezi. Trainings ndogo zikitokea tulikuwa tunalipwa, hivyo pesa zilikuwa zinaongezeka ila mpaka trainings zitokee.

Baadaye nikaja kupata kijikazi fulani nikawa nalipwa laki tano kwa mwezi, hapo nikiwa na miaka kama 25 hivi. Ila siyo laki tano tu, kuna programs ambazo zikitokea take home inakuwa laki tano, lakini muda mwingine account inaweza kusoma zaidi ya milioni mbili.

Kwa kweli nilikuwa natumia tu pesa zangu na kusomesha watoto wa dada yangu. Nina dada yangu ambaye alipata changamoto za maisha zilizompelekea mpaka kujiua.

Kwa hiyo nilikuwa natumia pesa zangu tu. Nilikuwa najiona bado mdogo na kwamba lazima ntaolewa na tutafanya vitu pamoja.

Basi nikaja kupata mwanaume wa Australia anayefanya kazi Geita kwenye migodi. Huyo mwanaume alikuwa mkubwa kidogo kwangu, zaidi ya miaka 20.

Nilivutiwa naye, lakini mara ya kwanza sikuona kama huyu mtu nitafika naye popote. Sikuwahi kumuomba chochote, lakini alidanganya kwamba familia yake ilifariki kwenye ajali. Basi nikawa interested na nikaanza kumzingatia zaidi kuliko zamani.

Akanambia ananipenda, hapo nikiwa na miaka 26, na mimi nikaona nimepata mwanaume, nikatulia naye kabisa.

Sikuwahi kwenda Australia. Tulikuwa tunakutana tu akipata muda hapa Tanzania, halafu yeye anarudi Australia.

Sikuwahi kumuuliza chochote. Nilijua kama mtu ananipenda, yeye ndiye atasema kitu.

Basi ilibidi nianze kwenda kwenye camp anakofanyia kazi. Ujinga uliniingia niachane na kazi, maana promises alizonipa ni kwamba tutaenda wote Australia akihamishwa kikazi.

Pia alikuwa ananihudumia zaidi ya pesa niliyokuwa naingiza kwa mwezi. Kingine, nilikuwa nadanganya sana kazini kwa sababu ya kwenda kuonana naye. Kila akiwa Tanzania tulikuwa tunaonana kama mara mbili kwa mwezi, hotelini na camp kwake.

Niliacha kazi, akaanza kuniudumia zaidi, kisha nikaenda Dar kwa sababu sote tulikuwa tunapenda kukutana Dar.

Basi ndugu zangu, siku zilivyozidi kwenda, mwanaume hafikirii kuja nyumbani kujitambulisha. Hatufanyi plans zozote za maisha. Nikimwambia ninunue kiwanja, anasema hawezi kununua huku.

Ila pesa ya kodi na matumizi alikuwa ananipa. Tatizo ni kwamba akili yangu ilikuwa imefungwa. Nilijua siku moja tutaenda Australia au nchi nyingine, hivyo nilikuwa naogopa kuanzisha kitu nitakachokuja kuuza baadaye.

Kwa hiyo nilikuwa nafikiria kazi ambayo nitatoa huduma tu, siyo kuuza vitu.

Kadri siku zilivyozidi kwenda, niligundua kwamba familia yake ipo hai. Akanambia ana watoto wawili wa kike na mama yao wametengana (separated). Pia anasema ana cancer na anasubiri apone ndipo waachane kabisa, halafu sisi tuje kuoana.

Akanipa pete ya promise ring, tukaendelea na mapenzi yetu.

Siku zilivyozidi kwenda, nikagundua kwamba anapendana na mwanaume mwenzake. Ila nilikaa kimya kwa sababu tayari tulikuwa kwenye mahusiano zaidi ya mwaka mmoja, nilishampenda na sikuwa na kazi, hivyo nilimtegemea.

Akaanza kutaka tufanye mapenzi kinyume na maumbile. Nilikuwa nakataa, lakini baadaye nikamwambia tukishazaa ndipo tutaanza kufanya hivyo, maana nilikuwa naogopa aibu nikiwa labour kwa sababu nilikuwa nimesikia story nyingi.

Basi akaendelea kunikumbusha sana. Nikaona nimridhishe mpenzi wangu kwa sababu niliamini tunapendana na sitakuwa na mwanaume mwingine zaidi yake. Hata kama alikuwa na shida zake, nilijua ananipenda. Nilijichanganya sana.

Mwaka 2024 ulikuwa mgumu sana kwangu. Dada yangu alifariki, mama yangu akafariki, na bibi yangu naye akafuata. Nafikiri mama yangu alipata mshtuko baada ya dada yangu kufariki, akaja kufariki miezi kama minne baadaye.

Nilikuwa na mawazo sana. Nilinenepa sana na nikaanza kunyonyoka sana nywele mpaka nikapata kipara karibu kichwa kizima. Nilinyoa kumuenzi mama yangu, na uzuri wangu nikahisi umepotea kabisa.

Pia nilikuwa najihisi mpweke zaidi kwa sababu mtu wangu akiwa Australia alikuwa ananiambia tu “good morning” na “usiku mwema”. Hakuwa anachati ndani ya siku kwa sababu anakuwa busy sana.

Nikajikuta nachat na baadhi ya wakaka ili tu niwe occupied. Siku moja alikuja, nikasahau kufuta message kwa sababu sikuwa naona kama ni jambo kubwa.

Kama kawaida yake, huwa anaangalia simu yangu. Huwa naiacha kwa sababu sina kitu cha ajabu. Lakini baada ya kuona zile message akaanza kubadilika, ingawa bado alikuwa ananiambia ananipenda.

Siku moja muda wake wa kuondoka Australia ulipokaribia, akanambia kwamba ataenda nyumbani moja kwa moja kwa sababu kuna msiba wa rafiki yake. Ila maelezo yake hayakuwa yanaeleweka na nilijua ananidanganya.

Baadaye akaniambia yupo anapanda ndege kuondoka, lakini alijichanganya na akanitumia picha ambazo aliwahi kunitumia zamani. Nikajua ananidanganya.

Nikampigia simu, akaniblock. Hakuni-unblock mpaka alipofika Australia.

Baadaye nikamuona amejicommentisha kwenye picha za msichana mwingine kwa comments za lover vibes. Wamefollowiana, nikamuuliza kama huyo ndiye demu wake. Akaniblock, na huyo msichana naye akaniblock papo hapo.

Basi nikakaa nikasubiri siku atakaporudi.

Madereva waliokuwa wanatujua waliinishangaa kwa sababu sikuwa naye tena. Mmoja akanipigia simu, nikajua tu yupo naye.

Basi huyo bwana akampa huyo mwanamke namba yangu anipigie. Akanipigia, baadaye akaniblock. Nilipompigia hakupokea, ila yule mwanaume akapokea.

Wakiwa pamoja, walikuwa wanacheka na kusema, “Huyu ni mbibi amechakaa. Huyo bwana haendani naye kabisa. Kachakaa, ni mrembo wa zamani. Sasa ni muda wetu sisi watoto wa 2000. Bwana tunae na tunatamba naye.”

Nikajiuliza walinitafuta kwa sababu gani, wakati sikuwa hata na muda wa kuwatafuta.

Basi huyo bwana naye akaniblock kabisa.

Nikapauka sana. Sina mtu wa kumkimbilia. Mama yangu keshadondoka kaburini. Nilijihisi nimechanganyikiwa na nikawaza mambo mengi. Niliumia sana kwa sababu ya aibu na kwa sababu ya watoto, hasa mmoja ambaye yupo English medium school.

Nikaona niyaachie yote kwa Mungu, lakini hasira zilinijaa.

Nilipomtafuta, akanambia kwamba aliniona nachat na wanaume na kwamba hanipendi. Hilo limenijaza hasira mpaka leo.

Naona kabisa anamfanyia huyo mwanamke vitu ambavyo hakuwahi kunifanyia mimi. Ni TikToker, wanakutana airport, wanapost picha, na sasa amembebesha mimba. Wanaendelea kucommentiana na wakati mwingine nashikwa na kichaa mpaka natamani kuwavurugia.

Sasa hivi naishi maisha ya umaskini na sina pa kukimbilia. Kama walivyosema, mimi sasa ni mbibi. Sijui nifanye nini na nianzie wapi.

Sikuwahi kutegemea maisha yangu yatakuwa hivi. Vitu nilivyokuwa naogopa zaidi maishani mwangu vimenitokea.

Ila namshukuru Mungu kwa sababu ndugu zangu wengine wamechukulia kwa uzito suala la kuwasomesha watoto.

Lakini sasa hivi nimekuwa mtu mwenye hasira sana. Najihisi nina roho mbaya na chuki kubwa.

Nilirudi kuishi kwenye nyumba ya mama yangu pamoja na watoto. Ninaishi na dada yangu mkubwa ambaye anaangalia nyumba. Hana kipato chochote, ila Mungu anasaidia tunaishi.

Kama kweli Mungu yupo, ndugu zangu, mniombee kwa sababu naona maisha yangu yanaporomoka na nahisi nitaendelea kuishi maisha ya umaskini.

Marafiki zangu wote siwasiliani nao kwa sababu ninaona aibu. Zamani tulikuwa wote tunapambana, lakini sasa mimi ni maskini asiye na mbele wala nyuma.

Ila bado nina hasira na hao watu. Sijui naachaje kuwachukia. Sitaki kuendelea kuhisi hivi, lakini nahisi haya maumivu yataendelea kuwa nami maisha yangu yote.

❤️
Pole sana. Kisa chako kinatukumbusha kuwa tusichezee wakati.
 
Nilijua tu story ya wazungu mwisho ni kuruka ukuta, wazungu washenzi sana sijui kwanini mnawapapatikia

Kutoka kwenye trauma ni kutokujihusisha nayo kubali kila kitu kwa sasa dharau, matusi, misonyo, mateso, masimango nk vyote viwe kawaida kwako utafanya mishe zako na utakuwa poa kabisa

NB, Usigawe namba ya tigo tena acha kabisa hiyo laana
 
Pole sana, wewe ni mdada wa pili sasa kusema kuwa ulifanya kinyume na maumbile kisa kumridhisha, mwingine rafiki yangu aliniambia alifanya kinyume na maumbile na mchumba wake kutoka Uspania kisa kumridhisha....sijui inakuaje unamridhisha mtu kwa kumfanyia kitu cha namna hiyo.

Ushauri wangu: Rudisha akili yako nyuma kabla ya kukutana na huyo jamaa aliyekuumiza then anzia hapo kwenda mbele.
 
Wazungu washenzi sana hiyo kwao ni kama tamaduni wengi wenye mabwana wa kizungu wote wanapinduliwa ni vile hawasemi
 
Bahati nzuri hajaambukizwa ukimwi tena hao wa migodini geita wameua sana dada zetu wengi, naongea kama mwana geita napajua vizuri
Hajasema kama amepima au lah, wanawake wetu hawa wakiona ngozi nyeupe wanaweweseka sana

Kuna siku katika pitapita zangu nawaona wanafunzi wa kike wanawafukuzia wazungu huku wakitoa sifa kede kede kwa wale jamaa vinajichekesha chekesha na kujitongozesha
 
Back
Top Bottom