Amenisaliti anang'ang'ania vitu vyangu

Mlanje

Senior Member
May 16, 2013
139
225
Wana jamii wenzangu mimi ni mwanaume wa miaka 29 nimekuwa na uhusiano na msichana kwa miaka 3 mwishoni mwa mwaka niligundua kuwa ana uhusiano na mtu mwingine na nilipombana kwa maswali alikubali na kusema wamekuwa pamoja kwa miezi 8 ila wameachana wiki mbili zilizopita nimeumia sana maaana nilimwamini mno, nimeamua kuachana nae ila nilimpa laptop yangu ya gharama sana ya laki 9 kwa makubaliano nitamnunulia ya kwake ila baaada ya usaliti aliofanya nimeona anipe mali yangu .Cha ajabu anang'ang'ania kwa kusema anaitumia na kwa sasa hawezi kunipa,kipekee sipendi fujo nafikiria kutumia nguvu ila naona ni utoto na naweza kusababisha matatizo.Naombeni ushauri nifanyeje?
 
MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
5,549
2,000

Ni ushamba kudai vitu mlivyopeana wakati wa uhusiano.... Akianza kudai vitu vyote alivyokupa, utaweza kurudisha??
 
Luv

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
1,789
2,000
Huo ni ushamba! Na wewe akikudai "alivyokupa" utaweza kurudisha?
 
Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
20,724
2,000
Wallah kama ulikua kwenye akili yangu nilivyosoma tuu huo mstari ukanijia kichwani khaaa....si amwachie laki 9!!
Kanunua cmu kampa demu alipoachana kamnyanga'anya ahahahaha kifuta jasho hicho babu wewe sio asili ya mwanaume kudai dai ulivyotoa laki 9 tu wengine wanahonga nyumba na wanaachwa na hawatii mguu kudai lol
 
mountain

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
756
500
Hata mm yashankuta ...nkaona haina kelele nkamwachia ...bora umwacchie utapata zaid ya hivyo..alafu moyon utakuwa na aman ....kama anakupenda kweli atakurudishia mali yako ....asiporudsha shukuru maana ungemwoa ungeipata kali zaid endappo mngeingia kwenye mzozo
 
mohamed18

Member
Sep 19, 2013
57
70
hapo utata... inawezekana anavyong'ang'ania lapt0p yako anahic ndi0 njia pekee ya kukuweka KARIBU kama ameshakaa sawa malizen mrudiane tu..
 
mohamed18

Member
Sep 19, 2013
57
70
hapo utata... inawezekana anavyong'ang'ania lapt0p yako anahic ndi0 njia pekee ya kukuweka KARIBU kama ameshakaa sawa malizen mrudiane tu.. UJUE miaka mi3 ming labda alikua haoni dalili yeyote ya mapenZ kwenda step ingine.. funguka bhana.
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,113
2,000
Dah, inauma sana basi ndio hivyo tena achana nae mwache aende nayo tu laki si pesa bhana milioni deni ati!!! Utapata mwingine Mpwa usiumie sana hakuwa wako huyo. Jifanye kama vile umepoteza, mbona huwa tunapoteza vingi???
 
Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,384
1,250
Kanunua cmu kampa demu alipoachana kamnyanga'anya ahahahaha kifuta jasho hicho babu wewe sio asili ya mwanaume kudai dai ulivyotoa laki 9 tu wengine wanahonga nyumba na wanaachwa na hawatii mguu kudai lol

Ila inaumaje?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom