Amenisaliti anang'ang'ania vitu vyangu

Amenisaliti anang'ang'ania vitu vyangu

Wana jamii wenzangu mimi ni mwanaume wa miaka 29 nimekuwa na uhusiano na msichana kwa miaka 3 mwishoni mwa mwaka niligundua kuwa ana uhusiano na mtu mwingine na nilipombana kwa maswali alikubali na kusema wamekuwa pamoja kwa miezi 8 ila wameachana wiki mbili zilizopita nimeumia sana maaana nilimwamini mno, nimeamua kuachana nae ila nilimpa laptop yangu ya gharama sana ya laki 9 kwa makubaliano nitamnunulia ya kwake ila baaada ya usaliti aliofanya nimeona anipe mali yangu .Cha ajabu anang'ang'ania kwa kusema anaitumia na kwa sasa hawezi kunipa,kipekee sipendi fujo nafikiria kutumia nguvu ila naona ni utoto na naweza kusababisha matatizo.Naombeni ushauri nifanyeje?

tatizo na wewe unaliia lia sana.hivi hujui kudai?kama hujui nikodishe mimi kwa buku 50 tu uone kama haijarudi kwa siku mbili.

dah laki tisa kubwa.asikuone mtu mjinga ndugu yangu ili hali hajui ulilala njaa siku ngapi ili ujichange hiyo kilo 9 ya laptop
 
acha hizo wewe unajua ndani ya mahusiano yao waliahidiana nini?
 
Wana jamii wenzangu mimi ni mwanaume wa miaka 29 nimekuwa na uhusiano na msichana kwa miaka 3 mwishoni mwa mwaka niligundua kuwa ana uhusiano na mtu mwingine na nilipombana kwa maswali alikubali na kusema wamekuwa pamoja kwa miezi 8 ila wameachana wiki mbili zilizopita nimeumia sana maaana nilimwamini mno, nimeamua kuachana nae ila nilimpa laptop yangu ya gharama sana ya laki 9 kwa makubaliano nitamnunulia ya kwake ila baaada ya usaliti aliofanya nimeona anipe mali yangu .Cha ajabu anang'ang'ania kwa kusema anaitumia na kwa sasa hawezi kunipa,kipekee sipendi fujo nafikiria kutumia nguvu ila naona ni utoto na naweza kusababisha matatizo.Naombeni ushauri nifanyeje?
Youngman akiirudisha na yeye atarudi Moyo mwako.... wee mwachie na ndiyo mwisho wake!!
 
kwanza utaanzia wapi kunibana wakati najua namana ya kukupanga unasahahu yote
Kuna muda technique zote zinayeyuka kuna watu wako serious kwenye haya mambo hawataki ujinga ukishikiwa bastola hizo tekiniki unazitoa wapi zinakuwa zimeyeyuka hapo kilichobaki ni kutapika ukweli tu!
 
Kama yapi best?

Naona wengi mwashabikia dhuluma na kuona ni sawa kabisa...

Ingelikuwa ni ndoa huyo dada yamkini angelikuwa sahihi, lakini gelofrendi arudishe mali za watu...

Mimi namshauri huyu mleta mada kama anazo stakabadhi halali za hiyo dadavuzi mpakato, peleka huyo dada kwenye vyombo vya dola...
 
Hii siyo mada ya kuleta humu jf timiza ahadi yako kwakuwa ulikwisha muhaidi huna ujanja naye kumbe ana akili umeisha umia amua aidha umwachie hiyo ama umnunulie uliyomwahidi
 
Ila inaumaje?

Ni kweli inauma sana lakini ukitaka kupata amani haraka dawa ni kupotezea vitu ulivyompa msaliti wako. Kwa sababu hata ukipewa vitu vyote moyo hautaridhika maana hutapata hasa kile ulichopoteza yaani uaminifu wa mpenzi wako na hilo ndilo linalouma sana. Uaminifu katika mapenzi hauna replacement. Ni ama kusamehe au kuchapa lapa bila kudai kitu. Halafu ukimwachia vitu ulivyompa yaani vitamuumiza kwa sababu vitabakiza kumbukumbu ya uhusiano wenu kila akiviona na kuvitumia.
Nilimsifu jamaa yangu mmoja huku ninakoishi, alikuwa na mpenzi wake na jamaa alimpenda sana. Wakiwa na miezi kadhaa ya uhusiano akagundua msichana wake anatoka na mwanaume mwingine. Akimuuliza anakataa katakata. Jamaa akafanya uchunguzi akawaona wakiwa sehemu fulani na mtu wake. Akamtumia sms kuwa amemuona sehemu fulani na mwanaume. Bibie akajua sasa mambo yalishaharibika kwa hiyo ikawa ndio kuachana.
Kilichonifurahisha ni kwamba bibie alikuwa anachukua bidhaa sehemu fulani jamaa anaenda kulipa. Na wakati wanatibuana kulikuwa na deni halijalipwa, jamaa alienda kujua anadaiwa kiasi gani akalipa deni lote na kumweleza muuzaji kuwa akichukua vitu vingine atalipa mwenyewe.
 
Naona wengi mwashabikia dhuluma na kuona ni sawa kabisa...

Ingelikuwa ni ndoa huyo dada yamkini angelikuwa sahihi, lakini gelofrendi arudishe mali za watu...

Mimi namshauri huyu mleta mada kama anazo stakabadhi halali za hiyo dadavuzi mpakato, peleka huyo dada kwenye vyombo vya dola...

Best jamaa aliahidi huyu kuwa bint atumie laptop ya jamaa mpaka atakaponunuliwa yake na jamaa,sasa jamaa hajatimiza ahadi ati!!!
Hajatuambia lakini ndani ya miaka hiyo mitatu naye amepewa vingapi na bint na amerejesha vingapi baada ya kuachana!!!!
 
Alijua jamaa king'ang'anizi,asipoambiwa wana share hakubali kuachwa
Hahahahaaaa haya bwana sasa amejikuta anang'ang'ania yeye si ampe laptop yake ataenda kupata kwa huyo mwenye uelekeo wa ndoa
 
Hahahahaaaa haya bwana sasa amejikuta anang'ang'ania yeye si ampe laptop yake ataenda kupata kwa huyo mwenye uelekeo wa ndoa
Bidada alijipanga na hiyo laptop alishaiweka kwenye list ya anavyomiliki kihalali.
Kazi kwake jamaa aliyefunga mlango mwenyewe halafu analalamika kafungia wallet yenye nauli,aamue safari ife au ajongee mdogo mdogo aone miguu itamfikisha wapi
 
Dah unamtetea kwa udi na uvumba aisee angekuwepo humu nadhani hata vocha ungepata aisee
 
Dai mali yako arifu, achana na hawa wanaokwambia eti unaweza kurudisha alivyokupa? Kwani kakupa nini? mijitu ina dhana eti kwenye uhusiano mwanamme ndo anapewa wakati mnapeana. Logically haukumpatia laptop ila ulimuazimisha, ukiamua kuidai hakuna kosa wala ushamba hapo. Unless uridhie mwenyewe kusahau na kumuachia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom