Ambao hatukuitwa kwenda JKT tunapata wakati mgumu katika kuomba ajira, vigezo vinahitaji aliyepita JKT tunaomba ushauri tufanye nini?

Mr Nyau

JF-Expert Member
Oct 18, 2018
1,128
2,337
Ambao hatukuitwa kwenda JKT tunapata wakati mgumu katika kuomba ajira, vigezo vinahitaji aliyepita JKT tunaomba ushauri tufanye nini?

Miaka ya Nyuma baada ya kumaliza kidato cha sita katika shule nafasi zilitoka kwa kuchagua idadi fulani ya wanafunzi kwenda kwenye mafunzo ya JKT -Mujibu wa sheria ambao hatukupata nafasi hiyo ya kuchaguliwa
Sasa tunahangaika na kuomba nafasi za ajira , kila ukiona tangazo kigezo mojawapo ni Lazima awe amepitia mafunzo ya JKT

Tunaomba ushauri tufanye nini? Kulikua na ulazima gani wa kuweka kigezo hicho ilihali mnajua hakuweza kuwapa nafasi ya kuwapeleka wanafunzi wote huko?

Tunaomba ushauri na mapendekezo tufanye nini tunaopitia hali hii?
 
Ukiona kazi inahitaji uwe umepita JKT hizo ni kazi za kada za ulinzi na usalama.
Kwa sasa hivi kama kijana unataka kufanya kazi kwenye majeshi ya ulinzi au usalama mfano JWTZ, POLISI,MAGEREZA, UHAMIAJI AU ZIMAMOTO NA UOKOAJI hakikisha umepita JKT kwa kujitolea au kwa mujibu wa sheria japo kuwa kwa kujitolea nafasi inakuwa kubwa zaidi kwani asilimia kubwa majeshi yanachukua Form four leavers.
Kama hukubahatika kuchaguliwa mujibu wa sheria na unapenda kazi za majeshi fanya chap uwahi kuomba nafasi za kujitolea pindi zikitoka ukateseke miezi yako kadhaa then usubiri bahati yako, kigezo kikubwa kinachowaangusha wengi kwenye usahili wa majeshi ni JKT, UMRI NA PHYSICAL FITNESS so, kabla hajachukua maamuzi ya kwenda huko jiangalie au jipime kwanza kama unahizo sifa.
Kuhusu connection rafiki yangu labda anaye ku- connect awe ni mtu wa ngazi za juu sana au itokee zali kama la majaliwa mpiga mbizi (aliyeenda mafunzo ya jeshi la uokoaji baada ya kuokoa watu kwenye ajali ya ndege) uwe recommended kujiunga ndio unaweza kwenda bila kupitia JKT vinginevyo JKT ndio mlango wa kuchujia vipepeo wote kwa sasa.
Kama una swali lingine karibu.!
 
Ahsante, Umri wa mtu una mshauri aende JKT kwakuwa alikosa nafasi awali inabidi awe na miaka mingapi? Ili asiende kupoteza muda huko pia?
 
Unaweza kuwa na hicho cheti cha KJT na bado hata usiitwe kwenye usaili. Cha muhimu hizo nafasi za TAKUKURU kama sijakosea wewe omba tu hata wao ni binadamu wanaweza kukuita.
 
Ahsante, Umri wa mtu una mshauri aende JKT kwakuwa alikosa nafasi awali inabidi awe na miaka mingapi? Ili asiende kupoteza muda huko pia?
Kuhusu umri inategemea na level ya elimu yako.
Kwa mwenye cheti cha Form form four ( umri kuanzia miaka 18 - 23) ni bora zaidi
Kwa mwenye certificate na diploma( umri unakuwa kuanzia 18 - 25) ni bora zaidi.
Kwa degree mpka miaka 28 bado sio mbaya
Kwa master na PHd inaweza kwenda mpka miaka 35 bado sio mbaya.
Chakuzingatia ni kuwa unataka kwenda jeshi kwa kupitia level gani ya elimu au ujuzi gani ulionao maana hicho kita determine pia mshahara wako.
 
Bila shaka hizo ni ajira za majeshi na ni kweli huwezi ajiriwa huko kama hujapitia jkt, fanya kama kuachana nazo angalia upande mwingine
Ambao hatukuitwa kwenda JKT tunapata wakati mgumu katika kuomba ajira, vigezo vinahitaji aliyepita JKT tunaomba ushauri tufanye nini?

Miaka ya Nyuma baada ya kumaliza kidato cha sita katika shule nafasi zilitoka kwa kuchagua idadi fulani ya wanafunzi kwenda kwenye mafunzo ya JKT -Mujibu wa sheria ambao hatukupata nafasi hiyo ya kuchaguliwa
Sasa tunahangaika na kuomba nafasi za ajira , kila ukiona tangazo kigezo mojawapo ni Lazima awe amepitia mafunzo ya JKT

Tunaomba ushauri tufanye nini? Kulikua na ulazima gani wa kuweka kigezo hicho ilihali mnajua hakuweza kuwapa nafasi ya kuwapeleka wanafunzi wote huko?

Tunaomba ushauri na mapendekezo tufanye nini tunaopitia hali hii?
 
Hili jambo wenzetu huwa wanapeleka mahakamani.... either kila mtu apewe nafasi ya kwenda JKT au waondoe hicho kigezo
 
Back
Top Bottom