Ushauri kwa vijana ambao hamjawahi kuajiriwa

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,679
12,249
Awali ya yote nawaomba wapambanaji wenzangu ambao kwa namna moja ama nyingine mmesoma au kusomeshwa na ndugu, jamaa ama mataasisi mbali mbali, wengi wetu tumekuwa na matarajio makubwa sana pindi tulipokuwa vyuoni, tulikuwa tunajiona kwa picha mbali mbali za kufikilika, unajiona ukiwa unazunguka kwenye kiti cha kuzunguka huku ukiwa unapigwa na kiyoyozi :oops::oops::oops::oops::oops::oops:

Mambo huanza kwenda mlama baada ya kutakiwa kwenda field hapo ndipo mapicha picha huanza kujitokeza na mtaa unaanza sasa kukuonyesha rangi yake halisi, kupata nafasi tu kwenye taasisi kwa wanafunzi wa chuo kwaajili ya mafunzo yao kwa vitendo huwa ni ngumu. kuna baadhi ya mikoa ni lazima ulipie ndipo unapata nafasi ya kufanya field kwenye taasisi yao.

huu ni ushauri wangu wa bure kwa vijana wenzangu mnaotafuta ajira na wengine mlio bahatika kupata ajira hivi karibuni.
1695976712779.png

kama unajijua wewe ni greatthinker ajira za Tanzania zozote hazikufai, watu wanao jielewa hawaitajiki kabisa kwenye ajira hapa nchini kwetu, ndio maana utashangaa dokta anapokea maagizo ya kumtibu mgonjwa kutoka kwa mwanasiasa utashangaa operation ya mguu mtu anafanyiwa kichwani ujue hayo ni maagizo kutoka juu ili huyo mgonjwa aisome namba.

ili umudu kudumu kwenye ajira hapa Tanzania yakupasa uwe mjinga tena mjinga haswa, thubutu kujifanya unazijua haki zako hakuna rangi ambayo utaacha kuiona kwenye hiyo ajira usipo fukuzwa utaacha mwenyewe kwa visanga utakavyo kutana navyo.

nimewahi kwenda wizara fulani, head wa hiyo department nilie mkuta alikuwa ni kituko kwa kweli hana lugha nzuri hata kidogo, nikajisemea kimoyo moyo huyu nafasi aliyo nayo hatoshi.

asilimia kubwa ya watendaji wazuri wapo mitaani ila walio bahatika kupata nafasi awana uzalendo wala uchungu hata kidogo...! hii inatokana na kuwekana kindugu au kihawala.

ipo wazi kuwa hivi sasa bila kuwa na mtu mwenye wadhifa mkubwa wizarani ajira hupati, lakini ajira yenyewe utakayo ipata ni lazima uwe chawa na muoga wa kufanya maamuzi ama pengine ukitaka kufanya maamuzi ya kiofisi ni lazima upate maelekezo kutoka juu sasa wewe jifanye mjuaji ujiamulie utajua kuwa hujui.

kama unaona kipimo chako cha Unyenyekevu ni kidogo, ajira za kitanzania zitakushinda. hakuna watu wanafanya kazi kwa mashaka na kunyenyekeana kama waajiliwa wa hapa nyumbani, wanajinyenyekeza hata kwa mambo ambayo hayahitaji kunyenyekewa. hivyo ili udumu kwenye ajira ni lazima uwe mnyenyekevu. unatakiwa unyenyekee kila kitu hilo mimi lilinishinda:eek::eek::eek:
1695976453595.png

Kuna taasisi ukiwaona wamevaa sare zao utawapenda na kutamani kuwa kama wao lakini nawaambia taasisi zote zenye uniformu hapa nyumba wafanyakazi wake wananyanyasika kisaikolojia sana na hawana cha kufanya maana wameikuta desturi ya unyenyekevu wa kijinga na wanaiendeleza na kujiondoa kwenye hiyo kadhia ina kuwa ngumu mithiri ya ile hadithi ya NANI ATAMFUNGA PAKA KENGERE...? sasa wa kumfunga paka Kengere hadi leo hajapatikana inahudhunisha sana kwakweli...!

1695977239090.png

Kama unatamani kuishi kwa msongo mkubwa wa mawazo Logwa uajiriwe. utafanya kazi kwa kiwango cha 5g na bado utatafutiwa sababu ufukuzwe ili nafasi yako apewe mwingine. utaishi maisha ya kulogwa au kuloga ili uinusuru nafasi yako. wafanyakazi wana hali ngumu sana maisha yao ni magumu wengi wanafanya kazi ndio hivyo tena awana cha kufanya maana madeni yamewaandama isinge kuwa madeni haki vile hakuna watu wanaoinjoi kufanya kazi wengi wao kazi wameichoka.

inafikia kipindi mtu anatamani kustaafu kazi ili pesa yake ya mafao imsaidie kupunguza ugumu wa maisha. na serikali ilivyokuwa na akili za kuwafanya watu wao waishi utumwani nyumbani ikaja na KIKOKOTOO. mtu unafanya kazi miaka zaidi ya 30 kwa shida sana umestaafu harafu mwanasiasa mmoja nakuja kukupangia jinsi ya kuchukua mafao yako. lifikilie hili kabla hujaamua kuajiriwa.
1695976322394.png

waajiriwa wa Tanzania awatakiwi kabisa kuzijua haki zao za msingi, na pengine ukijitahidi kuzitafuta ukaamua kuziishi hizo haki kwa kuzifuata itakula kwako. kutaka kufuata haki zako ni kupingana na matakwa ya muajiri wako na kwa nchi zetu hizi muajiri anayo haki muda wowote wa kusitisha mkataba kwa mbinu yoyote ya halali au haramu. utakuta kazi inayotakiwa kufanywa na wafanyakazi 10 hapa Tanzania inafanywa na mtu mmoja tena kwa masaa mengi ya kazi...thubutu kudai haki zako uone kitakacho kupata.
1695976236403.png

Katika kazi ambazo watu wake wanafanya kazi kwa kutumwa na kushinikizwa kufanya mambo yaliyo kinyume na utu, kinyume na taratibu, kinyume na haki ni hizi kazi za ULINZI hizi kazi hazifai ndio maana WALINZI wastaafu maisha yao huwa magumu sana. hivyo nisingependa kwa vijana tunaojitafuta kuangukia kwenye mikono ya kazi za ULINZI. hakuna mlinzi Tajiri labda uwe jambazi. hii kazi kwakweli kwa watu wanao penda haki haiwafai maana utatamani kudai haki zako huku sheria ikiwakataza vikali walinzi kubishana na mabosi zao. kiufupi walinzi wamezibwa midomo awana pa kusemea ndio maana unakuta kuna kesi nyingi sana za walinzi kujichapa au kuchapana Risasi.

Usijidanganye kuwa Kuna chama Cha kutetea wafanyakazi hapa Tanzania, ukifanyiwa kituko chochote kazi ujue utakabiliana nacho wewe mwenyewe ulisema uende kwenye vyama vya wafanyakazi. Hutopata msaada mwisho wa siku haki Yako utapoteza na kazi utafukuzwa.

Afisa kazi. Ni bosi lakini sio mtu atakae simama upande wako likitokea la kutokea...

😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭

TANZANIA SIO SEHEMU SALAMA KWA WATU WANAOJIELEWA​
 
Point kubwa sana Hii:

"kama unaona kipimo chako cha Unyenyekevu ni kidogo, ajira za kitanzania zitakushinda"

Hapa ndo palinifanya niache kazi yangu, na sijawahi kujuta kabisa.

Ila wa Bongo wengi ni wanafiki, waongo, washirikina, washenzy, na kujipendekeza.

Kama hauna hizo sifa hapo juu na unataka kudumu kwenhe ajira lazima uwe:

  • Mtu wa Mungu sana.
  • Mshirikina wa kutupa.

Ni jambo gumu sana mwanamke kuajiriwa, I cant imagine, wanawake wanapitia magumu sana.

Wanaume tutafute hela kwa bidii, hawa wake zenu vijana wafanye kazi kwa uchaguzi na sio vinginevyo.

Ma office yana wahuni, wabakaji, washenzy na wote wana vyeo, wake zenu vijana wataponea wapi?
 
hakuna penye uafadhali ndugu yangu kibwa uishi kama mjinga kama unatarget za kuajiriwa. waajiri wanapenda sana kunyenyekewa. ila target zako zikitimia unatimua vumbi unatengenezea vijana wenzako ajira kwa kujiajiri.
kwahyo magufuli alipunguza hii hali katika kipindi chake? Maana kwa maelezo yako inaonesha yote unayosema magufuli alikua anakemea japokuwa na yeye alikua kama ana ka udikteta fulani hvi, na vp kuhusu waalimu, wanapata tabu na wao za kutumikishwa?
 
kwahyo magufuli alipunguza hii hali katika kipindi chake? Maana kwa maelezo yako inaonesha yote unayosema magufuli alikua anakemea japokuwa na yeye alikua kama ana ka udikteta fulani hvi, na vp kuhusu waalimu, wanapata tabu na wao za kutumikishwa?
Huko ndio kabisa. Mwalimu anatumikishwa Hadi na mtendaji wa Kijiji. Ajabu ya mwaka Yani waajiriwa wote wanatunishiana misuli. Na kutokana na Kariba ya walimu wa zamani wale wa UPE. Waliopewa ualimu Kwa kujua kusoma na kuandika waliharibu sana tasinia ya elimu maana walikuwa wakiambiwa chochote wanafanya Kwa kuzingatia kwasababu waliopewa ualimu pasipo kuwa na vyeti stahiki
 
Popote alipo Mtanzania, Muhindi, Muarabu hapafai kufanya kazi. Nimeumizwaga sana kwenye ajira nikiwa kijana, Mungu anisaidie nisamehe.
Wewe unenielewa sana . Hali IPO hivyo Watanzania walioajiriwa wapo kwenye mateso makubwa sana. Harafu mbaya Zaidi hata serikalini wao pia wananyanyasika tena haswa kama ulivyo sekta binafsi tofauti ni pesa TU na mamlaka ila manyanyaso ni makubwa pande zote.🤣😭
 
kwahyo magufuli alipunguza hii hali katika kipindi chake? Maana kwa maelezo yako inaonesha yote unayosema magufuli alikua anakemea japokuwa na yeye alikua kama ana ka udikteta fulani hvi, na vp kuhusu waalimu, wanapata tabu na wao za kutumikishwa?
Kwake ndio ilizidi. Ikawa kufukuzwa ni rahisi sana ila kupata kazi ikawa ngumu japo alikuwa anaajiri Kila siku
 
Back
Top Bottom