stephot
JF-Expert Member
- Mar 1, 2012
- 17,840
- 27,419
Pole yake,sio kwamba alikosea kuoa ila asilimia 95 ya wanawake ukishakwama kwenye uchumi au akikuzidi kipato cha moto utakiona,though wapo wengine wanaojielewa sana...Rafiki yangu wa karibu alikuwa ananisimulia changamoto anazokutana nazo kwenye ndoa yake ambayo ina umri wa miaka mitatu anasema hivi karibuni mambo yake ya kiuchumi yameenda mraba sasa imepelekea dharau kubwa kuibuka kutoka kwa mke wake ambaye yeye ana kipato cha uhakika kwakuwa ni muajiriwa ,
Anasema wakigombana kidogo anamtolea kauli za kukera " sio bure nilikubalije kuolewa na mwanaume kama wewe lazma uliniroga haikuwa akili yangu [emoji3][emoji3][emoji3] halafu mwanamke anaanika habari zao kwa ndugu zake.
Jamaa anasema alikuwa tu anasikia ndoa ni ndoano lakini amejionea mwenyewe na pia anaona utofauti akilinganisha na kipindi cha uchumba jinsi mahaba yalivyokuwa mazito.