Ali Kiba - Mwana Dar es Salaam (video)

Ali Kiba - Mwana Dar es Salaam (video)

Ile uliyowahi kuiona kabla hii haikua official video ile walitengeneza tu na kuunga vipande vya matukio ya nyimbo za watu wengine...angalia vizuri yale matukio ni ya nyimbo za wasanii wengine tofauti tofauti

Ok,asante kwa taarifa.
 
tusubirie Na Video Ya Ay Ft Seankingstone Itakuaje[/QUOTE]

duuuh!! kweli mashabiki maandazi wengi sana humu ndani...yaan hujui hata kuwa iyo video imetoka zaidi ya wiki moja iliyopita??!!
 
Wabongo tunashida sana.. assume wimbo huohuo ingetumika kizulu naamini wabongo wangeipenda hii video.
Tatizo mnajitengezea video zenu kichwani lakini yeye hajelenga soko la ndani tu yupo internationally..

Kweli kabisa mkuu. Ni kama video za nyimbo za Khona wa Mafikizolo, au Prakatatumba wa Cabo Snoop, zimebamba Africa nzima.
Ova
 
Safi sana...Hiyo ndo inaitwa kazi ya sanaa...Hapa watu walikuwa na mavideo yao kichwani ya maigizo....Jamaa amewacha waswahili wanashangaa....wanataka kuona maigizo eti binti katoka kijijini....

Big up Kiba....Video bombaaaa sans

Yaani kwa akili zao walitegemea kisa cha Mwana kingetosha kwenye video ya dakika nne? Kuna kilaza mmoja hapa eti alishauri ingekuwa anakutana na mateja njiani wakati anatembea, hajui kwamba tukio hilo lingeleta maana nyingine kabisa katika video.
Kwani wimbo wa Kipi Sijasikia umemalizwaje na video? Ni kwa kulazimisha maigizo kwenye video na ndio maana wakarudi studio kuongeza baadhi ya vitu kwenye audio, lakini hata hivyo bado haikuendana.
Ova
 
Ha ha ha haaaa. Sasa unadhan mashabiki wangapi wanayajua haya? Unaongea nn ww? He should deliver what we want na sio kutuletea huu ulimbukeni wa kujifanya unajua aina video... Kazingua. Video ya kawaida... Soon itapotea na kusaulika.

Hata mimi pia ni shabiki ujue, na nimeelewa. Navyojua shabiki wa muziki hutaka burudani tu toka kwa mwanamuziki. Ndio maana huwa tunafurahia nyimbo hata zilizo katika lugha zisizo zetu kama Khona, au Prakatatumba ambazo video zake nazo ziko kwa mtindo huu huu.
Ova
 
Yaani kwa akili zao walitegemea kisa cha Mwana kingetosha kwenye video ya dakika nne? Kuna kilaza mmoja hapa eti alishauri ingekuwa anakutana na mateja njiani wakati anatembea, hajui kwamba tukio hilo lingeleta maana nyingine kabisa katika video.
Kwani wimbo wa Kipi Sijasikia umemalizwaje na video? Ni kwa kulazimisha maigizo kwenye video na ndio maana wakarudi studio kuongeza baadhi ya vitu kwenye audio, lakini hata hivyo bado haikuendana.
Ova

Ha ha ha ha haaa. Team kiba at work. Video mbayaaaaaaaa.
 
Kuna watu walijitengenezea video zao za dakika kumi kichwani mwao.kama taarabu vile no way big up.The king Alli K video ni kali saana aiseee zile pamba ni noumaaa kamanda
 
Ila tambua mimi nilichokifanya ni benchmarking, sasa sijui ulitaka nimlinganishe na msanii gani hapa bongo?

Lakini upande wa videos lazima tukubali kuwa ame-improve. Hii ndo video yake bora kabisa na imezifunika baadhi ya video za Diamond. Kwa mtazamo wangu, video pekee ya Diamond ambayo naweza sema ina ubora na creativity nzuri ni number one remix.
 
Hussein machozi labda, Baba Levo...kidoogo Ommy Dimpoz
Diamond sio level yake...yani ni ile hakunagaaaa.....

Dada unaleta mahaba. Unaongelea upande wa kipaji cha kuimba au pesa au video bora?
 
Lakini upande wa videos lazima tukubali kuwa ame-improve. Hii ndo video yake bora kabisa na imezifunika baadhi ya video za Diamond. Kwa mtazamo wangu, video pekee ya Diamond ambayo naweza sema ina ubora na creativity nzuri ni number one remix.

Nakuunga mkono kamanda umenena vyema but vp upo powa lakini
 
video haina uhalisia, they ran short if ideas!!! director hakuwa na theme nzuri.
 
Kuna Dogo alifanya video ya "Kabla hajatoka Dayamondi" anaitwa Dogo S Kide kamfunika Kiba, unaimba Mwana DSM unashindwa kuonesha mitaa ya DSM, unashindwa kumwonyesha mtu yuko kwenye mishe mishe za Kimwana DSM, unashindwa kumwonesha alivyokuja kutaabika.

Inabidi Salam Jabir arudishe kipindi chake cha kuchambua video za wasanii wetu kama enzi zile za Planet Bongo!

Sasa ivyo vipande vyote c vitachukua Dk 20
 
Picha haiendani na stori nadhani anayeongelewa angeigiza hapo: i.e wazazi wakimlilia, kaanza kulewa, mademu, madawa. ....yule jamaa wa kibajaji angenogesha sana hii video

Kaja tofauti. Na ni vizuri sana kuwa unpredictable. Watu walishatengeneza video zao kichwani, hivyo kusingekuwa na haja ya video. Pia alishawahi toa ya maigizo Mack Mugan. Mwanzo mzuri Kiba. Kitaeleweka tu, na Kiba nae akatuwakilishe kimataifa sababu nina uhakika ANAWEZA kabisa.
 
Safi sana...Hiyo ndo inaitwa kazi ya sanaa...Hapa watu walikuwa na mavideo yao kichwani ya maigizo....Jamaa amewacha waswahili wanashangaa....wanataka kuona maigizo eti binti katoka kijijini....

Big up Kiba....Video bombaaaa sans

Kuwa unpredictable ni kitu moja safi sana. Watu waache kukariri. Naunga mkono hoja yako.
 
Kwa ambaye hajui kiswahili akiiangalia hii video, hatoweza ku-guess Kiba anaimba nini.

A ba ba ba ba a ba ba ba ba ba prakata kumba kumba kumba kumba!! Watu hawakuelewa ila waliserebuka mwanzo mwisho!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom