Hivi wewe unazijua types of music videos? Unajua kama kuna Performance music videos, Narrative music videos na Conceptual music videos? Video ni taaluma jamani msiongee tu kwa kuwa ipo JF inayokupa nafasi ya kuongea.
Kilichofanyika kwenye video ya Mwana ni kitu kilicho kwenye taaluma kabisa, na ndivyo inavyokuwa Narrative music videos na imetendewa haki kama ambavyo imekuwa.
Producer haamui tu kuweka wimbo fulani kwenye video ya aina fulani, ila kutokana na urefu kisa chenyewe pamoja na mambo mengine ya kitaaluma. Kwa unavyofikiri kisa cha wazo la wimbo wa Mwana kinaweza kufanyiwa video na kutosha kwa dakika nne?
Nadhani Bob Marley angekuwa Mtanzania naye ungemshambulia kwa kufanya video ya wimbo No Woman No cry kwa aina ya Performance Music Videos, kwa sababu tu ni kwamba kuna mafunzo.
Unapaswa kuelewa kwamba hakuna wimbo usio na mafunzo duniani, ila kuna wimbo wa mafunzo mabaya na mafunzo mema.
Ova