Young Tanzanian
JF-Expert Member
- Mar 10, 2012
- 1,736
- 293
Ha ha ha ha ha ha msando si mganga njaa kweli wakimfukuza msando tutajua saccos ya ufpa imeteketea....cdm ni chama cha kuweka na kukopa 2015 wenye roho za paka wataamia dp kwa mtkla
Yaani nyie CHADEMA mnakera sana siku hizi.
Why don't y'all just go away for sometime. Just take time out and disappear from the face of the earth and then come back after a month or two.
Mkuu Mimi ni mgeni hapa lakini TIMING misimamo yake naijua molemo kamkosea sana anapaswa amuombe radhiKuna wachangiaji humu inabidi nyie wasemaji wa CDM muwajue misimamo yao.
Unapiga risasi wrong target! Watch careful your aim!!
Msando nafikiri ni mtandao wa mafreemason, unakumbuka nyaga mawalla alivyowaua watu wengi sana
Wanasheria mnapenda sana kuchochea mambo, mpate ulaji weni. Why don't you go n talk with Mr. Mabere about Zitto. Zitto is two faces, please don't jump in this water,unless if you're one of them. It is friendly adviseMwaikenda,
1. Kutetea utawala wa Sheria na tafsiri sahihi ya Katiba yetu ni kubomoa chama? Ndio mimi ni Diwani lakini itakuwa ajabu sana kusema kwamba kumtetea Zitto lazima nijiuzulu kwanza. Mimi sio mjumbe wa Kamati Kuu, Baraza Kuu wala Mkutano Mkuu. Mgongano wa maslahi unatoka wapi? Naweza vipi kuathiri maamuzi ya vikao hivyo?
2. Je marekebisho ya Kanuni ya 2013 yalijumuisha kwamba kukiwa na dharura utaratibu uliotajwa kwenye kipengele (a) usifuatwe? Kwa nini kipengele kilichoongezwa cha (d) kilitaja utaratibu ambao hautafuatwa ni ule wa (b) na (c) peke yake? Hilo unalielezeaje?
3. Kikao cha Kamati Kuu kilikuwa kikao cha dharura? Waraka husika ulikamatwa siku hiyo hiyo ya kikao au jana yake kwa hiyo ikabidi maamuzi ya dharura yafanyike?
Kama ilikuwa ghafla hivyo kwa nini asingesimamishwa uongozi, apewe mashtaka kama Kanuni inavyosema halafu asikilizwe kwa dharura na adhabu itolewe ya kumvua uongozi? Dharura sio haraka kaka.
4. Kupewa taarifa rasmi kwa maandishi na mwenendo kupelekwa Baraza Kuu ni taratibu ambazo lazima zikamilike ili muadhibiwa aweze kukata Rufaa. Ndio maana taarifa ya nia imetolewa ili taratibu hizo zikamilike. Hakuna niliposema nataka mwenendo wa shauri. Tunachotaka ni taarifa rasmi ya maamuzi.
5. Mwenendo unatakiwa umefika Baraza Kuu ndani ya siku 14 toka tarehe 22/11/2013. Je umefikishwa?
Tusijadili kwa jazba na hasira. Mimi kueleweshwa kwa hoja ni mwepesi sana. Fanya hivyo na kama uko sahihi nitaconcede. Lakini sitaconcede kisa tu utasema akili au uelewa wangu mdogo.
Ahsante.
... Mkuu nashukuru umejitahidi kwa kiasi kikubwa sana kulifafanua hili.Nimesoma post zote toka mwanzo mpaka hapa naandika nimegundua mambo muhimu ambayo wengi hawayafahamu.
- Wengi wenu mmekariri sura ya sita kipengele (a) -(d) bila kujua nini kinaongelewa ndani yake.
- Kushindwa (akiwemo msando na zitto) kutoifautisha kati ya kufukuzwa uachama na uongozi.
UKWELI WA SURA YA SITA KANUNI ZA UENDESHAJI KAZI ZA CHAMA
Sura ya sita inahusiana na UANACHAMA (ADHABU ZA KINIDHAMU AU KUFUKUZWA CHAMA).
Nanukuu
"6.5 Taratibu zifuatazo lazima zizingatiwe katika kuchukua hatua za
kinidhamu:-
6.5.1 Kila tawi litaweka kumbukumbu/orodha ya wanachama wanaokoma kuwa wanachama wa tawi. Kumbukumbu itaonyesha jina kamili la mwanachama katika rejista ya wanachama tarehe aliyokoma kuwa mwanachama wa tawi na sababu za kukoma kuwa mwanachama.
6.5.2 Kwa mujibu wa ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza:
(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
(b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
(c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.
6.5.3 Mtu yeyote aliyepoteza uanachama wake kwa mujibu wa kifungu 5.4 cha Katiba atapoteza haki zake zote za uanachama na hatarudishiwa ada, zawadi au ruzuku yeyote aliyokwishaitoa kabla ya kupoteza uanachama wake.
6.5.4 Mwanachama aliyepewa adhabu na kikao kimoja cha kikatiba atakuwa na haki ya kukata rufani kwa kikao cha ngazi ya juu ya kile kilichompa adhabu.
6.5.5 Mwanachama aliyewahi kuachishwa ama kufukuzwa uanachama anaweza kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu za kutaka kurejea. Maombi yake yatachunguzwa kwenye ngazi hiyo na kutolewa maamuzi na vikao vya ngazi moja ya juu inayofuata. Aliyesimamishwa au kufukuzwa na Kamati Kuu ataweza tu kurejeshwa na Baraza Kuu. Watakaofukuzwa na Mkutano Mkuu hawatakuwa na chombo kingine chochote kitakachotengua uamuzi huo.
6.5.5.Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.
6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kuKata rufani au la.
6.5.9 Mwadhibiwa atakaye amua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu.
6.5.10 Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya
kikao cha maamuzi. " mwisho wa kunukuu
SASA TUONE IBARA YA 5.4.3 NA 5.4.4 INASEMAJE
Nanukuu
"5.4 Kukoma kwa UanaChama
5.4.1 Kwa kujiuzulu mwenyewe kwa hiari yake.
5.4.2 Kutokana na kufariki.
5.4.3 Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama, kwa mujibu wa katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo usioendana na Itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za Chama. Mwanachama atakuwa na haki ya kuKata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na adhabu hiyo.
5.4.4 Bila kuathiri kifungu 5.4.3 cha katiba, Kamati Kuu inaweza kumwachisha ama kumfukuza mwanachama yeyote kwa utaratibu utakaopangwa na kanuni za Chama.
5.4.5 Kukosa sifa za uanachama.
5.4.6 Kufukuzwa uanachama wa Baraza la Vijana au Wanawake au Wazee kwa utovu wa nidhamu."
Mwisho wa kunukuu
ANGALIZO KUHUSU UONGOZI NA KUKOMA KWAKWE KWA MUJIBU WA KATIBA
Nanukuu
"6.3.4 Kukoma kwa Uongozi
(a) Kwa kiongozi kujiuzulu kwa hiari yake
(b) Kwa kiongozi kuachishwa uongozi au kufukuzwa uanachama
(c) Kwa kiongozi kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya katiba, kanuni au maadili ya Chama.
(d) Kwa kufariki
(e) Ibara hii inahusu pia uongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ya Chama.
6.3.6 Mamlaka za Nidhamu na Uwajibishaji
(a) Kiongozi aliyechaguliwa na Mkutano Mkuu ataweza
kusimamishwa uongozi tu kama ifuatavyo:-
(i) Kiongozi ngazi ya Msingi na Kamati Tendaji ya Tawi
(ii) Kiongozi wa Tawi na Kamati ya Utendaji ya Kata/Wadi
(iii) Kiongozi wa Kata/Wadi na Kamati ya Utendaji ya
Jimbo/Wilaya.
(iv) Kiongozi wa Jimbo/Wilaya na Baraza la Mkoa
(v) Kiongozi wa Mkoa na Kamati Kuu.
(vi) Kiongozi wa Taifa na Baraza Kuu.
Kiongozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi ataweza
kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao kilichomteua.
(c) Bila kuathiri masharti ya vipengele (a) na (b) hapa juu, kiongozi yeyote anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao cha juu ya ngazi yake ya uongozi.
(d) Kiongozi aliyechukuliwa hatua za nidhamu na mamlaka yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya ile ya mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi hiyo utakuwa wa mwisho.
(e) Rufaa yoyote lazima ifanyike katika muda wa siku thelathini tangu tarehe ya kupokea rasmi kwa maandishi maamuzi ya mamlaka iliyotoa adhabu.
(f) Viongozi wa ngazi ya kitaifa waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wanaweza kusimamishwa uongozi endapo theluthi mbili ya wajumbe wa Baraza Kuu watapiga kura ya siri na kutokuwa na imani na kiongozi mhusika. Baraza Kuu litakuwa na wajibu wa kuteua atakayeshika nafasi hiyo kwa muda hadi uamuzi wa mwisho kufanywa na Mkutano Mkuu."
Mwisho wa kunukuu
HITIMISHO
- Kuhusu kuwavua au la uachama watuhumiwa , CHADEMA imefuata taratibu zote hapo ju. Zitto na wenzie wasubiri kuitwa na kamati kuu kwa mahojiano ya ana kwa ana. Baada ya hapo watapewa majibu ya maamuzi ya kamati kuu kwa maandishi ndani ya siku 14 toka mahojiano. Wanaweza kukata rufaa kama hawajaridhika na maamuzi
- Kuhusu kuvuliwa uongozi chadema walitumia katiba ibara ya 6.3.4 (c). Hili watuhumiwa waliitwa, wakahojiwa na kamati kuu, wote kwa pamoja wakakiri makosa kwa kuhusika na waraka wakaomba kujiuzuru nyazifa zao.
- Wanadai taratibu hazikufuatwa kuwapoka vyeo vyao. Ukivunja katiba na miiko ya uongozi hakuna cha taratibu, katiba iko wazi unapoteza wadhifa ulionao mara moja pamoja na kuchuliwa hatua zingine ikwemo kuvuliwa uanachama ambazo taratibu kwenye hili lazima zifuatwe kama ilivyoainishwa hapo juu.
MsandoAlbertoJF,
Issue sio Msando Albert ni nani au kwa nini anatetea.
Issue ni rahisi natetea nini na utetezi wangu uko based kwenye nini.
1. Utaratibu wa kumvua Zitto nyadhifa haukufuatwa.
2. Sababu zilizotolewa ni circumstantial. Hazijitoshelezi. Zote zinatokana na waraka wa Mwigamba
Kama kijana, mwanachadema mwenye taaluma ya Sheria nina wajibu kusema haya.
"wewe msando ni diwani wangu wa kata ya mabogini nakuomba uache kiherehere na shobo kwenye izo mambo ...njoo huku utekeleze ahadi zako....watu wamekuchoka huku toka tumekuchagua hujawai kuonekana katani....
Halafu nasikia unataka ubunge jimbo la moshi vijijini kwa taarifa yako umebuma"
by mpigakura wako
kata ya mabogini
Ebana eeh hao washkaji zako niaje bana? Mbona kutwa kucha wanatafuta kiki?
Tell them to get a life.
its surprises me a lot, Msando sijui imekuaje amevaa hii njuga
haina tija kwake wala kwa taifa, its just a bad lead kwa siasa za leo hasa vijana na hasa hasa vijana wa upinzani
we rukaruka tu lakini mwisho wa siku utamjua zitto kuwa ni nani kwenye hii dunia na chadema kwa ujumla.
Mteja wake anataka hivyo. Hapana umiza kichwa na fedha za magogoni...Why are you taking it public kama wewe ni mwanachama na mbali ya hapo ni diwani hujui taratibu za chama kweli? Serena Hotel imekuwa sehemu ya mamlaka za chama hadi ujitokeze kila siku kwenye hadhara
Unaonekana mtoto kweli aisee
Albert Msando kamgaragaza vibaya Tundu Lissu kwenye ulingo wa sheria.
Hillarious Indeed......!
So,Ukiulizwa kama Mwanasheria ni wapi nilipokutaja kweli utaleta majibu ya kuridhisha zaidi ya hisia na rhetoric hogwash!??
Huyo Msando sio Tatizo tu bali ni ZIGO ndani ya Chama,halafu ati ni Diwani anayetumia press kuwakilisha hoja zake dhidi ya CC ya Chama.....what a shame...!!!
Hivi hata kama ana hoja anazoamini kuwa ni sahihi kwa nini kukidhalilisha Chama yeye kama Diwani kwenda kwenye press inayolindwa na kuhudumiwa na maCCM..???
Ngoja tumalize hilo la mteja wao ZZK na yeye lake halitachukua zaidi ya nusu saa ndio utaijua Chadema iko vipi.......Siku zao zinahesabika,very shame.