Albert Msando apotoka tena

mwaikenda

JF-Expert Member
Mar 26, 2011
903
0
Wana Jf,

Naomba ieleweke kuwa Katiba ya CHADEMA toleo la mwaka 2006 ndiyo msingi mkubwa wa kuendesha taasisi. Ufafanuzi uliotolewa leo kwa vyombo vya habari na Wakili Albert Msando ni upotoshaji mkubwa wa Katiba ya Chadema na hii inatokana na aidha uelewa mdogo wa Katiba hiyo na/ au ni makusudi kwa malengo ya huyo anayedai kumwakilisha.

Upotoshaji huo ni kama ufuatayo;

Mosi, hatua iliyochukuliwa Kamati Kuu kumsimamisha uongozi huyo anayedai kumwakilisha ilifikiwa kwa lengo moja tu la kunusuru Chama kama hatua ya dharura kwa mujibu wa ibara ya 6.5.2 ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama pamoja na marekebisho ya mwaka 2013 ili kuruhusu utaratibu wa kinidhamu wa kawaida kwa mujibu wa Katiba na Kanuni.
Itakuwa ni taasisi ya ajabu ambayo itasubiri madhara makubwa ya uharamia uliokuwa unataka kufanyika alafu Kamati Kuu kama chombo cha kusimamia utendaji wa Sekretarieti ikae kimya alafu wahaini waendelee kuutumia mwanya wa kikanuni kuharibu na kuathiri taasisi nzima. Hata hivyo Kanuni ipo kimya kuhusu dhana ya dharura, lakini kisheria dharura ni kutokana hali husika katika wakati huo au kutokana na mazingira yaliyopo (Prevailing circumstance).

Pili, kuhusu kupatiwa taarifa kamili ya mwenendo wa kikao cha Kamati Kuu kama ambavyo amedai kuwa mpaka sasa yeye na huyo anayemwakilisha hawajapokea, amepotoka kabisa. Kanuni aliyonukuu ambayo ni ibara ya 6.5.10 ya Kanuni za Uendeshaji kazi za Chama inatamka kuwa taarifa kamili ya mwenendo itawasilishwa kwenye kikao cha juu. Suala hapa ni je Msando amekuwa kikao cha ngazi ya juu pamoja huyo anayedai kumwakilisha?

Tatu, kuhusu anayedai kumwakilisha kutotajwa kwenye Waraka wa uhaini na hivyo kutokuwa na makosa ni jambo ambalo linaingia kwenye maudhui na hoja ambazo anayedai kumwakilisha anatakiwa kuzijibu katika muda aliopewa na kikao cha Kamati Kuu na hivyo hatua yake ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari ni aina ya utoto na kutaka msamaha/huruma ya umma (public sympathy) na kuendeleza mjadala usio na tija kwa vyombo vya habari.

Nne, Wakili Msando ameshindwa kutoa dhana ya anayedai kumwakilisha kupewa mashtaka na kutakiwa kujibu ndani ya siku 14. Je haikidhi matakwa ya kikanuni kama alivyoainisha?

Tano, anayedai kumwakilisha anakwepa kujibu tuhuma 11 zilizoainishwa katika hati ya mashtaka ili baada ya maamuzi, na kama hataridhika na maamuzi akate rufaa.

Sita, itakuwa ni taasisi ya ajabu ambayo inaona hujuma kubwa dhidi yake alafu iache kuchukua hatua za dharura kujinusuru.

Saba, Ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba ya Chama toleo la mwaka 2006 ikisomwa pamoja na marekebisho ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama ya mwaka 2013, vifungu vyote hivyo vinazungumzia hatua za kuvuliwa uanachama. Ikumbukwe kuwa hatua zilizochukuliwa ni za kiuongozi na sio kumvua uanachama huyo anayemwakilisha. Hata hivyo hati ya mashtaka pamoja na agizo la kujibu ndani ya siku 14 imekidhi utaratibu wa kikanuni kama anavyodai wewe.

Nane, ieleweke kuwa Wakili Msando ni Diwani wa CHADEMA katika akiwakilisha Kata ya Mabogini huko Moshi. Naomba arejee Kanuni za Madiwani ibara ya 5.0 (d) ambayo naomba kuinukuu "Diwani anawajibika kutumia hadhi, uwezo, wadhfa na nafasi aliyonayo kama Diwani kukijenga Chama ndani na nje ya Halmashauri". Kama Wakili naamini anajua hatua za kuchukua akiendelea kukomalia suala hili, nimkumbushe tu kuwa anatakiwa ajiuzulu hiyo nafasi ili kuondoa mgongano wa kimaslahi na afanye kazi yake ya uwakili kama anataka kuendelea na kushiriki kupinga maamuzi ya Kamati Kuu.

Naomba kuwasilisha.

Mwaikenda

=========================
Majibu kutoka kwa Albert Msando
=========================

Mwaikenda,

1. Kutetea utawala wa Sheria na tafsiri sahihi ya Katiba yetu ni kubomoa chama? Ndio mimi ni Diwani lakini itakuwa ajabu sana kusema kwamba kumtetea Zitto lazima nijiuzulu kwanza. Mimi sio mjumbe wa Kamati Kuu, Baraza Kuu wala Mkutano Mkuu. Mgongano wa maslahi unatoka wapi? Naweza vipi kuathiri maamuzi ya vikao hivyo?

2. Je marekebisho ya Kanuni ya 2013 yalijumuisha kwamba kukiwa na dharura utaratibu uliotajwa kwenye kipengele (a) usifuatwe? Kwa nini kipengele kilichoongezwa cha (d) kilitaja utaratibu ambao hautafuatwa ni ule wa (b) na (c) peke yake? Hilo unalielezeaje?

3. Kikao cha Kamati Kuu kilikuwa kikao cha dharura? Waraka husika ulikamatwa siku hiyo hiyo ya kikao au jana yake kwa hiyo ikabidi maamuzi ya dharura yafanyike?

Kama ilikuwa ghafla hivyo kwa nini asingesimamishwa uongozi, apewe mashtaka kama Kanuni inavyosema halafu asikilizwe kwa dharura na adhabu itolewe ya kumvua uongozi? Dharura sio haraka kaka.

4. Kupewa taarifa rasmi kwa maandishi na mwenendo kupelekwa Baraza Kuu ni taratibu ambazo lazima zikamilike ili muadhibiwa aweze kukata Rufaa. Ndio maana taarifa ya nia imetolewa ili taratibu hizo zikamilike. Hakuna niliposema nataka mwenendo wa shauri. Tunachotaka ni taarifa rasmi ya maamuzi.

5. Mwenendo unatakiwa umefika Baraza Kuu ndani ya siku 14 toka tarehe 22/11/2013. Je umefikishwa?

Tusijadili kwa jazba na hasira. Mimi kueleweshwa kwa hoja ni mwepesi sana. Fanya hivyo na kama uko sahihi nitaconcede. Lakini sitaconcede kisa tu utasema akili au uelewa wangu mdogo.

Ahsante.
 
Iramusm

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
454
250
Vipi kuhusu kupatiwa mashtaka kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu?
 
Kitaja

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
2,819
2,000
Hivi hizi pesa anazomwaga bwana zitto kwa watu kama hawa si angejiwekea hifadhi zikamsaidia baadae? au ndo sikio la kufa halisikii dawa?
 
gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,245
2,000
Yaani nyie CHADEMA mnakera sana siku hizi.

Why don't y'all just go away for sometime. Just take time out and disappear from the face of the earth and then come back after a month or two.
hahahahahha!!!!!!!!!!!!!
at least wewe umethubutu
 
don-mike

Member
Apr 3, 2011
50
0
mkuu, naomba u quote hivyo vifungu vya sheria hapa, unavyosema 6.5.2, then unaelezea bila kuandika hivyo vifungu hadithi yako inakuwa unbalanced.

"truth will set you free"
 
Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,491
2,000
Huyu Msando ni mchumia tumbo anajulikana na amekuwa akitukana viongozi wa Chadema kila siku kupitia FB wall yake!

Sijui Chadema iliokota wapi mamluki hawa na kuwapatia uongozi.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
87,597
2,000
hahahahahha!!!!!!!!!!!!!
at least wewe umethubutu

Imekuwa kama mashindano ya kujipatia publicity.

Leo hicho kiwakili Msando kimeitisha presser...hamna lolote la maana kilichozungumzia. Hakuna jipya zaidi ya kutafuta kiki.

Kesho ama keshokutwa akina Mnyika nao wataitisha presser. Hamna ya maana watakayoongea.

Ili mradi ni vurugu tu na nani anapata airtime.

I'm so sick of them.
 
NKUU SINDE KWETU

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
831
0
Huyu Msando ni mchumia tumbo anajulikana na amekuwa akitukana viongozi wa Chadema kila siku kupitia FB wall yake!

Sijui Chadema iliokota wapi mamluki hawa na kuwapatia uongozi.

Muulize Idadi ya wanawake alionao!! Siasa kavamia tuu huyu, na ndio maana yuko chadema.
 
naumbu

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
4,710
2,000
dah hii bongo bwana kwa hiyo Alberto naye amekua bonge la mwanasheria na watu kupoteza muda kumjadili no wonder hadi viazi wanakua MP
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
21,998
2,000
Wamekuwa kama vi-teenybopper vya junior high school vinavyogombania vivulana.

Shameful. Hivi na huyo Msando kakosa vijikesi vingine huko uraiani?

its surprises me a lot, Msando sijui imekuaje amevaa hii njuga

haina tija kwake wala kwa taifa, its just a bad lead kwa siasa za leo hasa vijana na hasa hasa vijana wa upinzani
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,979
2,000
Asante sana Mkuu@mwaikenda, sasa nyie badala ya kwenda serena nyookeni jangwani kwenye mahakama ya umma.

Zitto tupa kule!!
 
Albert Msando

Verified Member
Nov 2, 2010
1,019
0
Mwaikenda,

1. Kutetea utawala wa Sheria na tafsiri sahihi ya Katiba yetu ni kubomoa chama? Ndio mimi ni Diwani lakini itakuwa ajabu sana kusema kwamba kumtetea Zitto lazima nijiuzulu kwanza. Mimi sio mjumbe wa Kamati Kuu, Baraza Kuu wala Mkutano Mkuu. Mgongano wa maslahi unatoka wapi? Naweza vipi kuathiri maamuzi ya vikao hivyo?

2. Je marekebisho ya Kanuni ya 2013 yalijumuisha kwamba kukiwa na dharura utaratibu uliotajwa kwenye kipengele (a) usifuatwe? Kwa nini kipengele kilichoongezwa cha (d) kilitaja utaratibu ambao hautafuatwa ni ule wa (b) na (c) peke yake? Hilo unalielezeaje?

3. Kikao cha Kamati Kuu kilikuwa kikao cha dharura? Waraka husika ulikamatwa siku hiyo hiyo ya kikao au jana yake kwa hiyo ikabidi maamuzi ya dharura yafanyike?

Kama ilikuwa ghafla hivyo kwa nini asingesimamishwa uongozi, apewe mashtaka kama Kanuni inavyosema halafu asikilizwe kwa dharura na adhabu itolewe ya kumvua uongozi? Dharura sio haraka kaka.

4. Kupewa taarifa rasmi kwa maandishi na mwenendo kupelekwa Baraza Kuu ni taratibu ambazo lazima zikamilike ili muadhibiwa aweze kukata Rufaa. Ndio maana taarifa ya nia imetolewa ili taratibu hizo zikamilike. Hakuna niliposema nataka mwenendo wa shauri. Tunachotaka ni taarifa rasmi ya maamuzi.

5. Mwenendo unatakiwa umefika Baraza Kuu ndani ya siku 14 toka tarehe 22/11/2013. Je umefikishwa?

Tusijadili kwa jazba na hasira. Mimi kueleweshwa kwa hoja ni mwepesi sana. Fanya hivyo na kama uko sahihi nitaconcede. Lakini sitaconcede kisa tu utasema akili au uelewa wangu mdogo.

Ahsante.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom