Albert Msando apotoka tena

Albert Msando apotoka tena

Na wewe usidandie hii kwa sababu unahisi atakua mpinzani wako huko Moshi Vijijini .Suala la idadi ya wanawake hapa halina mantiki.Jifunze debate acha ushamba wa Kisiasa.
sidhani fika kama unatambua kiudani maana ya neno "wadhifa" kamtafute leo Mh. mzee Clinton umuulize hayo kama pia panaweza kuwa mahala pake?? na je ni lini na wapi panaweza kuwa mahala pake???
 
kaa kitako uandike vzr wewe"mngevuviwa" ndiyo nini? Bora kuwa adui wa siku moja kuliko kuwa adui wa miaka52,tunakoelekea nitakukosea heshima bure acha ni obey rules za jf......salute kwako

bavicha huu ubabe mnajifunzia kwa lema. Mtaacha lini haya mambo?hivi vitisho ndio vinawafanya muonekane mnatetea msicho kijua.
 
NAOMBA NIKUJIBU KWENYE HIYO RANGI YA UGOLO yenye kuzungumzia udharula wa kuchukua maamuzi na haki ya kusikilizwa. Hizo hoja zingine ulizoziibua hazina mashiko na ziko kiushabiki zaidi kuliko "kweli"

a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.

b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.

c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.

d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.

Udharula wa kipengere "d" unauwezo na mamlaka ya kuvunja vipengere "b" na "c" iliyokwenye maandishi ya bluu, lakini kipengere "a" hakijatajwa kwenye kipengere "d" kama kinaweza kuvunjwa na hicho kipengere "d". hicho kipengere "a" ndio msingi wa haki ya kusikilizwa bila kipengere "a" hiyo katiba itakuwa inatoa fursa kwa watu wenye chuki binafsi kama Lema na Msigwa kufukuza wenzao hovyo kila wanapojisikia.

Tena tukizingatia wahusika waliomba kujiuzulu lakini Tundu Lissu kwa kujifanya anajua zaidi au huenda kwa kutumika kwake bila kujua akatoa hoja ya watuhumiwa kuvuliwa nyadhifa zao, basi kuvuliwa huko kwa nyadhifa kunahesabika ni adhabu au hatua za kinidhamu ambazo kwa kutii takwa la kifungu "a" ilibidi zichukuliwe mara baada ya wahusika kupewa mashtaka yao kwa maandishi na kisha wayajibu ndani ya wiki mbili.

Zitto kasomewa mashtaka badala ya kupewa kwa maandishi, lakini mbaya zaidi kasomewa mashtaka siku moja na siku hiyohiyo kajitetea na siku hiyohiyo hukumu ikatolewa kwa wahusika kuvuliwa nyadhifa zao. Hivi kweli huu ndio utawala wa sheria? au hii ni sheria ya wapi? hii ndio demokrasia ya chama chetu cha CHADEMA.

Mbowe kama Lipumba, kwa uongozi wake shupavu ameipaisha CUF na kwa kung'ang'ania madaraka kumeishusha CUF. Maamuzi haya ya kibabe ya kamati kuu kwa vyovyote vile ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Mbowe kubaki madarakani kwa kumvunja mbawa mtia nia. Kutangazwa kwa ratiba na tarehe ya uchaguzi siku chache mara baada ya maamuzi haya kibabe ni kiashiria tosha cha maamuzi yale ya kamati kuu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa mbowe kugombea bila kupingwa na Zitto. Sababu ni ajabu kwa Mwenyekiti na mwanademokrasia kubariki maamuzi haya ya kibabe na yenye kukiuka misingi ya kikatiba na ya haki ya kusikilizwa.

Nia njema huja sanjari na maumivu lakini nia ovu hukabiliwa kwa ustahamilivu, usishue chombo ili hali maji yajaa lakini unaweza kutengeneza kupwa kwa maji, kila jambo lina wakati wake lakini wakati unawezwa kutengenezwa pia, na kivuno cha mdudu chungu leo, kesho huenda ndio shibe yako, naomba haya Zitto Kabwe ayajue na yawe sehemu ya maisha yake.

Pole Zitto Zuberi Kabwe yote yana mungu, dunia ni hino hino, waja na ada zao ni wale wale tandu Adamu {a.s} hadi kwa Muhamad{s.a.w}, kwahivyo hayana budi kuwa midhali ungali chini ya jua. Tema mate chini ili waja waendelee kujilisha upepo kwa kudhani watashibisha matumbo yao yenye njaa ya tamaa, uchu na ung'ang'anizi wa madaraka wenye lengo la kufuta alama chafu za uongozi wao zilizochorwa kwa kalamu ya moto kwenye chuma cha pua.

Wakoloni waliwaita wapigania uhuru waahini na wachochezi, CCM inaimba wimbo kama huo wa kikoloni, lakini la ajabu baadhi ya viongozi wa CHADEMA, aidha kwakuwa watu walioshika mpini hulka zao hufanana au kigeugeu hakina mji wao, nao wameanza kuwaita wapinzani wao katika kuwania uongozi na wakosoaji wao kuwa ni wasaliti, mamluki na kubwa zaidi ni waahini kama vile CHADEMA ni dola kumbe ni chama tu cha siasa.

Njano5.
0655345394
Safi mkuu.
 
zitto kashaalibu ndoto za vijana wengi sana!

kama kuharibu ndoto za vijana basi chadema wanaongoza.
Godbless J Lema anawafundisha vijana kukataa amani na kutukana majukwaani.

Chadema kupitia redbragad wamewafunza vijana utekaji na uporaji. Refer kuburuzwa na kuibiwa kwa Ludo tsh 60000.
 
Last edited by a moderator:
ona sasa kumbe hata kiswahili hujui halafu eti unataka madaraka............rudi kwenye kamusi yako kasome neno VUVIWA lina maana maana gani.

yaani kama ndo memba wa CDM hawa ambao hata pa kukosoa hawajui basi nakupa pole sana .............halafu eti unapita kushabikia CDM viroba na BOSS hivi vitawaua msipokuwa makini

Hawa wanachojua ni matusi tuu si unaona walimu wao wakina lema msigwa kule bungeni?
 
kama kuharibu ndoto za vijana basi chadema wanaongoza.
Godbless J Lema anawafundisha vijana kukataa amani na kutukana majukwaani.

Chadema kupitia redbragad wamewafunza vijana utekaji na uporaji. Refer kuburuzwa na kuibiwa kwa Ludo tsh 60000.

Mwigulu Nchemba anafundisha vijana kutoa kucha, kuua, kumwagia tindikali, Nape anawabebesha mitutu watoto wadogo het kujifunza ukakamavu kwa jina green guard, Kinana yeye na tembo mpaka wanaisha saivi, Nchimbi yeye kutoa hongo vijana wanywe viroba yani kazi kweli kweli
 
Last edited by a moderator:
NAOMBA NIKUJIBU KWENYE HIYO RANGI YA UGOLO yenye kuzungumzia udharula wa kuchukua maamuzi na haki ya kusikilizwa. Hizo hoja zingine ulizoziibua hazina mashiko na ziko kiushabiki zaidi kuliko "kweli"

a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.

b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.

c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.

d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.

Udharula wa kipengere "d" unauwezo na mamlaka ya kuvunja vipengere "b" na "c" iliyokwenye maandishi ya bluu, lakini kipengere "a" hakijatajwa kwenye kipengere "d" kama kinaweza kuvunjwa na hicho kipengere "d". hicho kipengere "a" ndio msingi wa haki ya kusikilizwa bila kipengere "a" hiyo katiba itakuwa inatoa fursa kwa watu wenye chuki binafsi kama Lema na Msigwa kufukuza wenzao hovyo kila wanapojisikia.

Tena tukizingatia wahusika waliomba kujiuzulu lakini Tundu Lissu kwa kujifanya anajua zaidi au huenda kwa kutumika kwake bila kujua akatoa hoja ya watuhumiwa kuvuliwa nyadhifa zao, basi kuvuliwa huko kwa nyadhifa kunahesabika ni adhabu au hatua za kinidhamu ambazo kwa kutii takwa la kifungu "a" ilibidi zichukuliwe mara baada ya wahusika kupewa mashtaka yao kwa maandishi na kisha wayajibu ndani ya wiki mbili.

Zitto kasomewa mashtaka badala ya kupewa kwa maandishi, lakini mbaya zaidi kasomewa mashtaka siku moja na siku hiyohiyo kajitetea na siku hiyohiyo hukumu ikatolewa kwa wahusika kuvuliwa nyadhifa zao. Hivi kweli huu ndio utawala wa sheria? au hii ni sheria ya wapi? hii ndio demokrasia ya chama chetu cha CHADEMA.

Mbowe kama Lipumba, kwa uongozi wake shupavu ameipaisha CUF na kwa kung'ang'ania madaraka kumeishusha CUF. Maamuzi haya ya kibabe ya kamati kuu kwa vyovyote vile ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Mbowe kubaki madarakani kwa kumvunja mbawa mtia nia. Kutangazwa kwa ratiba na tarehe ya uchaguzi siku chache mara baada ya maamuzi haya kibabe ni kiashiria tosha cha maamuzi yale ya kamati kuu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa mbowe kugombea bila kupingwa na Zitto. Sababu ni ajabu kwa Mwenyekiti na mwanademokrasia kubariki maamuzi haya ya kibabe na yenye kukiuka misingi ya kikatiba na ya haki ya kusikilizwa.

Nia njema huja sanjari na maumivu lakini nia ovu hukabiliwa kwa ustahamilivu, usishue chombo ili hali maji yajaa lakini unaweza kutengeneza kupwa kwa maji, kila jambo lina wakati wake lakini wakati unawezwa kutengenezwa pia, na kivuno cha mdudu chungu leo, kesho huenda ndio shibe yako, naomba haya Zitto Kabwe ayajue na yawe sehemu ya maisha yake.

Pole Zitto Zuberi Kabwe yote yana mungu, dunia ni hino hino, waja na ada zao ni wale wale tandu Adamu {a.s} hadi kwa Muhamad{s.a.w}, kwahivyo hayana budi kuwa midhali ungali chini ya jua. Tema mate chini ili waja waendelee kujilisha upepo kwa kudhani watashibisha matumbo yao yenye njaa ya tamaa, uchu na ung'ang'anizi wa madaraka wenye lengo la kufuta alama chafu za uongozi wao zilizochorwa kwa kalamu ya moto kwenye chuma cha pua.

Wakoloni waliwaita wapigania uhuru waahini na wachochezi, CCM inaimba wimbo kama huo wa kikoloni, lakini la ajabu baadhi ya viongozi wa CHADEMA, aidha kwakuwa watu walioshika mpini hulka zao hufanana au kigeugeu hakina mji wao, nao wameanza kuwaita wapinzani wao katika kuwania uongozi na wakosoaji wao kuwa ni wasaliti, mamluki na kubwa zaidi ni waahini kama vile CHADEMA ni dola kumbe ni chama tu cha siasa.

Njano5.
0655345394
hujajua unenalo zaidi ya nahau, misemo, methali na tamathali zako za semi.
Heko mwana malenga kwa kukuza na kuitangaza lugha yetu hadhimu ya kaswahili. Barikiwa sana.
 
CDM malizeni hii issue tupumzike sasa na hizi story za ZZK!!
 
Kweli wewe ni Tatizo.Yaani huoni kuitisha Press na kuropoka mashtaka ya huyo msaliti wako umeivunjia heshima Kamati Kuu?

Huyo Msando sio Tatizo tu bali ni ZIGO ndani ya Chama,halafu ati ni Diwani anayetumia press kuwakilisha hoja zake dhidi ya CC ya Chama.....what a shame...!!!
Hivi hata kama ana hoja anazoamini kuwa ni sahihi kwa nini kukidhalilisha Chama yeye kama Diwani kwenda kwenye press inayolindwa na kuhudumiwa na maCCM..???
Ngoja tumalize hilo la mteja wao ZZK na yeye lake halitachukua zaidi ya nusu saa ndio utaijua Chadema iko vipi.......Siku zao zinahesabika,very shame.
 
albert msando kamgaragaza vibaya tundu lissu kwenye ulingo wa sheria.

hahaha makamanda wana hasira Tundu Lissu kagaragazwa. Sasa hivi hawana jinsi zaidi ya kumrushia tofali msando au wamfukuze kabisa.

Maana kwa hoja hawamuwezi kabisa na lazima utasikia wana sema kumchukulia hatua maana kamdhalilisha mwana sheria wa chama kuonekana amepitisha maamuzi yanayo kihuka katiba yao.

Yani lissu anatoa hukumu bila hata ya kusikiluza?nasikia kwenye kikao cha kamati kuu iliyotoa maamuzi ya kijuha Tundu Lissu alitaka wafukuzwe hata bila kusikilizwa maana kuandaa mtu kugombea uenyekiti ni uhaini hila mtei kumuandaa arfi si uhaini maana yeye ni chadema chumbani.

Fikiria mtu kama Tundu Lissu alivyo dikteta ndio mwanasheria wa chama chao.

Tundu Lissu alishindwa kumuwajibisha Godbless J Lema kwa kumpiga mwigamba tofali lakini ana jigamba ni mpigania haki.

Huyu Tundu Lissu ameshindwa kuwakemea redbragad kuacha utekaji na uporaji badala yake amejikuta ana kubali kuwa lwakatare alipanga tukio la utekaji hila alirekidiwa na ludo(kamsome kwenye maelezo yake kwenye tukio la ludo)alaf bado wana muita mtu makini.

Huyu tundu lissu na lema ndio wataichimbia kaburi chadema.
 
Last edited by a moderator:
Kama kweli we ni wakali ka unavyosema this is disgrace to all lawyers and advocates as a matter of fact it is unethical.
Wakili huwezi anza kudiscuss utetezi wa mteja wako kwenye media...Wakili hata ka we ni mwanasiasa hila hapa unamevaa kofia ya uwakili na unaongozwa na misingi ya uwakili.
Wanasiasa ndio upeleka case zao kwa wananchi waliowachagua au wanaowawakilisha to win publicity ila not lawyers.
Wanasheria tunabishania mahakamani au kwenye bodi iliyopewa mamlaka ya kimahakama (kama unakopeleka hili swala la mteja wako) na sio huku kwenye social networks.
Sasa umeingia kwenye majibishano yasiyonatija kwa mteja wako pili unabishana na watu wasio wanasheria kwenye mambo yanayohitaji legal skills...!!
Ebu revisit notes zako Legal Ethics na advocacy skills inawezekana ulipitiwa kidogo Wakili

Mwaikenda,

1. Kutetea utawala wa Sheria na tafsiri sahihi ya Katiba yetu ni kubomoa chama? Ndio mimi ni Diwani lakini itakuwa ajabu sana kusema kwamba kumtetea Zitto lazima nijiuzulu kwanza. Mimi sio mjumbe wa Kamati Kuu, Baraza Kuu wala Mkutano Mkuu. Mgongano wa maslahi unatoka wapi? Naweza vipi kuathiri maamuzi ya vikao hivyo?

2. Je marekebisho ya Kanuni ya 2013 yalijumuisha kwamba kukiwa na dharura utaratibu uliotajwa kwenye kipengele (a) usifuatwe? Kwa nini kipengele kilichoongezwa cha (d) kilitaja utaratibu ambao hautafuatwa ni ule wa (b) na (c) peke yake? Hilo unalielezeaje?

3. Kikao cha Kamati Kuu kilikuwa kikao cha dharura? Waraka husika ulikamatwa siku hiyo hiyo ya kikao au jana yake kwa hiyo ikabidi maamuzi ya dharura yafanyike?

Kama ilikuwa ghafla hivyo kwa nini asingesimamishwa uongozi, apewe mashtaka kama Kanuni inavyosema halafu asikilizwe kwa dharura na adhabu itolewe ya kumvua uongozi? Dharura sio haraka kaka.

4. Kupewa taarifa rasmi kwa maandishi na mwenendo kupelekwa Baraza Kuu ni taratibu ambazo lazima zikamilike ili muadhibiwa aweze kukata Rufaa. Ndio maana taarifa ya nia imetolewa ili taratibu hizo zikamilike. Hakuna niliposema nataka mwenendo wa shauri. Tunachotaka ni taarifa rasmi ya maamuzi.

5. Mwenendo unatakiwa umefika Baraza Kuu ndani ya siku 14 toka tarehe 22/11/2013. Je umefikishwa?

Tusijadili kwa jazba na hasira. Mimi kueleweshwa kwa hoja ni mwepesi sana. Fanya hivyo na kama uko sahihi nitaconcede. Lakini sitaconcede kisa tu utasema akili au uelewa wangu mdogo.

Ahsante.
 
HONGERA MsandoAlberto kwa kumgaragaza Tundu lissu.

Hongera Ludo kwa kumfanya LISU akubali kuwa lwakatare alikuwa ana panga tukio la utekaji.
 
Wewe ni mwanasheria wa kuandika affidavit na mauziano ya viwanja.. wewe ni mwepesi sana, lengo lako ni kujilikana, kuendeleza malumbano na kuchumia tumbo! Ningependa Chama kisijibu lolote kutokana na mipasho yako!
 
Hivi MsandoAlberto inamaana utaitwa kutoa utetezi wa wateja wako kwenye baraza kuu au kamati kuu, au wewe unaingiaje hapa na uwakili wako?
 
Last edited by a moderator:
kila mtu ameshajua chadema watafanya kila njia hili kumfukuza msando na msanso asirudi nyuma.

Chadema kuambiwa ukweli kwao ni kama kumkataza Dr.W.Slaa kukopa.
mwanzoni nilikuwa nakuelewa lakini kwa sasa naona na wewe unaelekea kufanana nao tu, rudi kwenye mstari
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom