DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 12,980
- 29,402
JMT!
Hivi karibuni kumetokea Sintofahamu baada ya mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo machachari sheikh Said issa mohamedi kufukuzwa uanachama na chama chake kwa madai mbali mbali..
hatahivyo baada ya kufukuzwa ameibuka na kudai kuwa ana uhalali wa kuendelea kuwa mwanachama kwa kuwa bado anahisi utaratibu haukufuatwa wa yeye lkutolewa uachama hapa chini nimekuandikia sababu halali za kikatiba kwanini kusimamishwa uanachama bila kufuata taratibu za kawaida.
Kama mwanadiplomasia au mfuatiliaji wa Maswala ya siasa na sheria naomba kuweka na kutia kijineno..
Kwanza tukirejea Uamuzi wa kumfukuza Ndugu Said Issa Mohammed kulingana na Taarifa kwa Umma ya tarehe 07 Juni 2026 iliyotolewa na Katibu wa Kanda ya Pemba, Abdulla Hassan, una uhalali kamili wa kikatiba.
Twende deep sasa Hapa chini za kikatiba na kikanuni zinazothibitisha kwanini hakuwa na sifa ya kupewa haki ya kusikilizwa ya kawaida (Natural Justice):
1. KUKIMBILIA MAHAKAMANI NI KUJIFUKUZISHA UANACHAMA
CHADEMA ina taratibu zake za ndani za kusikiliza na kutatua migogoro. Kitendo cha mwanachama kukimbilia mahakama za serikali kabla ya kumaliza ngazi hizo kinamnyang'anya sifa na haki zote za kulindwa na Katiba ya chama.
2. MAMLAKA YA DHARURA YA KULINDA CHAMA (DOCTRINE OF NECESSITY)
Kufungua kesi mahakamani na kusababisha hasara ama kukwamishaa uendeshaji wa shughuli za chama kinahesabika kuwa ni kosa kubwa la Usaliti na Hujuma.
Chini ya Mwongozo wa Maadili, Kipengele cha 3 (a)(i) na (vii) , matendo ya "kupanga njama za kuhujumu Chama" na "kuhujumu programu za Chama" yanatafsiriwa kama usaliti mkubwa unaoondoa haki ya kusubiri taratibu za kawaida.
Hatua hiyo iliyochukuliwa na Kamati Tendaji ya Kanda ya Pemba chini ya Mwenyekiti wa Kanda, Omar Nassor, tarehe 06 Juni 2026, inaendana na mgawanyo wa madaraka ya kinidhamu ndani ya chama.

- Ukisoma Katiba ya Chadema ya mwaka 2006 toleo la mwaka 2019 ,Mwongozo wa Kamati za Maadili ya Chama, Sehemu ya E (Hatua za Kinidhamu), Kipengele cha 2 (x) kiko wazi:
“CHADEMA itashughulikia matatizo ya viongozi na wanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo Mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za Chama hatavumiliwa na atakuwa amejifukuzisha uanachama.”
2. MAMLAKA YA DHARURA YA KULINDA CHAMA (DOCTRINE OF NECESSITY)
Kufungua kesi mahakamani na kusababisha hasara ama kukwamishaa uendeshaji wa shughuli za chama kinahesabika kuwa ni kosa kubwa la Usaliti na Hujuma.
Chini ya Mwongozo wa Maadili, Kipengele cha 3 (a)(i) na (vii) , matendo ya "kupanga njama za kuhujumu Chama" na "kuhujumu programu za Chama" yanatafsiriwa kama usaliti mkubwa unaoondoa haki ya kusubiri taratibu za kawaida.
- Katika mazingira ya hujuma ya wazi, Kanuni za Chama, Sura ya Sita, Kifungu cha 6.5.1 (d) inatoa mamlaka ya dharura:
“Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu wa kifungu (a) na (b) hapo juu [vya kupewa mashitaka ya maandishi na kusubiri wiki mbili za kujibu] kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa...”
Hatua hiyo iliyochukuliwa na Kamati Tendaji ya Kanda ya Pemba chini ya Mwenyekiti wa Kanda, Omar Nassor, tarehe 06 Juni 2026, inaendana na mgawanyo wa madaraka ya kinidhamu ndani ya chama.
- Chini ya Ibara ya 6.3.6 (a)(v), Kamati Tendaji ya Kanda ndiyo yenye Mamlaka ya Nidhamu kwa viongozi wa ngazi ya mkoa.