NAOMBA NIKUJIBU KWENYE HIYO RANGI YA UGOLO yenye kuzungumzia udharula wa kuchukua maamuzi na haki ya kusikilizwa. Hizo hoja zingine ulizoziibua hazina mashiko na ziko kiushabiki zaidi kuliko "kweli"
a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.
Udharula wa kipengere "d" unauwezo na mamlaka ya kuvunja vipengere "b" na "c" iliyokwenye maandishi ya bluu, lakini kipengere "a" hakijatajwa kwenye kipengere "d" kama kinaweza kuvunjwa na hicho kipengere "d". hicho kipengere "a" ndio msingi wa haki ya kusikilizwa bila kipengere "a" hiyo katiba itakuwa inatoa fursa kwa watu wenye chuki binafsi kama Lema na Msigwa kufukuza wenzao hovyo kila wanapojisikia.
Tena tukizingatia wahusika waliomba kujiuzulu lakini Tundu Lissu kwa kujifanya anajua zaidi au huenda kwa kutumika kwake bila kujua akatoa hoja ya watuhumiwa kuvuliwa nyadhifa zao, basi kuvuliwa huko kwa nyadhifa kunahesabika ni adhabu au hatua za kinidhamu ambazo kwa kutii takwa la kifungu "a" ilibidi zichukuliwe mara baada ya wahusika kupewa mashtaka yao kwa maandishi na kisha wayajibu ndani ya wiki mbili.
Zitto kasomewa mashtaka badala ya kupewa kwa maandishi, lakini mbaya zaidi kasomewa mashtaka siku moja na siku hiyohiyo kajitetea na siku hiyohiyo hukumu ikatolewa kwa wahusika kuvuliwa nyadhifa zao. Hivi kweli huu ndio utawala wa sheria? au hii ni sheria ya wapi? hii ndio demokrasia ya chama chetu cha CHADEMA.
Mbowe kama Lipumba, kwa uongozi wake shupavu ameipaisha CUF na kwa kung'ang'ania madaraka kumeishusha CUF. Maamuzi haya ya kibabe ya kamati kuu kwa vyovyote vile ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Mbowe kubaki madarakani kwa kumvunja mbawa mtia nia. Kutangazwa kwa ratiba na tarehe ya uchaguzi siku chache mara baada ya maamuzi haya kibabe ni kiashiria tosha cha maamuzi yale ya kamati kuu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa mbowe kugombea bila kupingwa na Zitto. Sababu ni ajabu kwa Mwenyekiti na mwanademokrasia kubariki maamuzi haya ya kibabe na yenye kukiuka misingi ya kikatiba na ya haki ya kusikilizwa.
Nia njema huja sanjari na maumivu lakini nia ovu hukabiliwa kwa ustahamilivu, usishue chombo ili hali maji yajaa lakini unaweza kutengeneza kupwa kwa maji, kila jambo lina wakati wake lakini wakati unawezwa kutengenezwa pia, na kivuno cha mdudu chungu leo, kesho huenda ndio shibe yako, naomba haya Zitto Kabwe ayajue na yawe sehemu ya maisha yake.
Pole Zitto Zuberi Kabwe yote yana mungu, dunia ni hino hino, waja na ada zao ni wale wale tandu Adamu {a.s} hadi kwa Muhamad{s.a.w}, kwahivyo hayana budi kuwa midhali ungali chini ya jua. Tema mate chini ili waja waendelee kujilisha upepo kwa kudhani watashibisha matumbo yao yenye njaa ya tamaa, uchu na ung'ang'anizi wa madaraka wenye lengo la kufuta alama chafu za uongozi wao zilizochorwa kwa kalamu ya moto kwenye chuma cha pua.
Wakoloni waliwaita wapigania uhuru waahini na wachochezi, CCM inaimba wimbo kama huo wa kikoloni, lakini la ajabu baadhi ya viongozi wa CHADEMA, aidha kwakuwa watu walioshika mpini hulka zao hufanana au kigeugeu hakina mji wao, nao wameanza kuwaita wapinzani wao katika kuwania uongozi na wakosoaji wao kuwa ni wasaliti, mamluki na kubwa zaidi ni waahini kama vile CHADEMA ni dola kumbe ni chama tu cha siasa.
Njano5.
0655345394