Albert Msando apotoka tena

Albert Msando apotoka tena

We Albert wewe ni ngazi ya uongozi na unapingana na maamuzi ya Kamati Kuu, huwezi cheza mpira mwenyewe na refa ukawa mwenyewe kwa hiyo JIUZULU UDIWANI halafu ndo ukomalie kumtetea ZZK, zaidi ya hapo unajaza maji kwenye gunia TUNAMFUKUZA.

Mungu alivyo mwema wasaliti na waasi wote wamejitokeza Peupe kabisa!
 
hivi mwanasheria na diwani inaishi nyumba za wanaume wezako kama demu inajisikiaje mwanaume kukuoa nyumba ukae bure na kukununulia magari ya kifahari au ni vipi Msando hatukuelewi yaani nyaga anakihudumia kuliko anavyoihudumia familia yake..

Mkuu una maanishaa huyu msando alikua ni mke wa Nyaga mawala?noma sana
 
Kile kikundi cha Wasaliti na Waasi kilichosambaratishwa na Kamati Kuu kilimuandaa Alberto Msando kuwa Mwanasheria Mkuu wa chama endapo wangefanikiwa kumpindua Mbowe.
 
Na huyo anayejiita msando kaenda kuzungumz na vyombo vya habari kwa lipi cha maana hapa. Unajua kuna watu huwa wakishindwa kufanya mazuri wakaonekana huwa wanafanya makosa au kinyume na utaratibu makusudi ili tu watu wamwone na yeye yumo. Namshauri akasimamie maendeleo kwenye kata yako sio kusimamia kesi isiyo na tija kwake mwenyewe, kwa anayemtetea, kwa chama na kwa taifa kwa ujumla
 
Msando is simply a bush lawyer. ZITTO naye of all the lawyers umemwamini huyu mzee wa affidavit na kesi za talaka?
 
Zitto anadhani bado anafanya siasa za daruso miaka ile yuko chuo.....
 
Nimesoma post zote toka mwanzo mpaka hapa naandika nimegundua mambo muhimu ambayo wengi hawayafahamu.
  1. Wengi wenu mmekariri sura ya sita kipengele (a) -(d) bila kujua nini kinaongelewa ndani yake.
  2. Kushindwa (akiwemo msando na zitto) kutoifautisha kati ya kufukuzwa uachama na uongozi.

UKWELI WA SURA YA SITA KANUNI ZA UENDESHAJI KAZI ZA CHAMA

Sura ya sita inahusiana na UANACHAMA (ADHABU ZA KINIDHAMU AU KUFUKUZWA CHAMA).

Nanukuu

"6.5 Taratibu zifuatazo lazima zizingatiwe katika kuchukua hatua za
kinidhamu:-

6.5.1 Kila tawi litaweka kumbukumbu/orodha ya wanachama wanaokoma kuwa wanachama wa tawi. Kumbukumbu itaonyesha jina kamili la mwanachama katika rejista ya wanachama tarehe aliyokoma kuwa mwanachama wa tawi na sababu za kukoma kuwa mwanachama.


6.5.2 Kwa mujibu wa ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza:

(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
(b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
(c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.

d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.

6.5.3 Mtu yeyote aliyepoteza uanachama wake kwa mujibu wa kifungu 5.4 cha Katiba atapoteza haki zake zote za uanachama na hatarudishiwa ada, zawadi au ruzuku yeyote aliyokwishaitoa kabla ya kupoteza uanachama wake.

6.5.4 Mwanachama aliyepewa adhabu na kikao kimoja cha kikatiba atakuwa na haki ya kukata rufani kwa kikao cha ngazi ya juu ya kile kilichompa adhabu.

6.5.5 Mwanachama aliyewahi kuachishwa ama kufukuzwa uanachama anaweza kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu za kutaka kurejea. Maombi yake yatachunguzwa kwenye ngazi hiyo na kutolewa maamuzi na vikao vya ngazi moja ya juu inayofuata. Aliyesimamishwa au kufukuzwa na Kamati Kuu ataweza tu kurejeshwa na Baraza Kuu. Watakaofukuzwa na Mkutano Mkuu hawatakuwa na chombo kingine chochote kitakachotengua uamuzi huo.
6.5.5.Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.

6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.

6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kuKata rufani au la.
6.5.9 Mwadhibiwa atakaye amua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu.


6.5.10 Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya
kikao cha maamuzi. " mwisho wa kunukuu





SASA TUONE IBARA YA 5.4.3 NA 5.4.4 INASEMAJE

Nanukuu

"5.4 Kukoma kwa UanaChama


5.4.1 Kwa kujiuzulu mwenyewe kwa hiari yake.
5.4.2 Kutokana na kufariki.
5.4.3 Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama, kwa mujibu wa katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo usioendana na Itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za Chama. Mwanachama atakuwa na haki ya kuKata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na adhabu hiyo.

5.4.4 Bila kuathiri kifungu 5.4.3 cha katiba, Kamati Kuu inaweza kumwachisha ama kumfukuza mwanachama yeyote kwa utaratibu utakaopangwa na kanuni za Chama.


5.4.5 Kukosa sifa za uanachama.
5.4.6 Kufukuzwa uanachama wa Baraza la Vijana au Wanawake au Wazee kwa utovu wa nidhamu."

Mwisho wa kunukuu


ANGALIZO KUHUSU UONGOZI NA KUKOMA KWAKWE KWA MUJIBU WA KATIBA

Nanukuu

"6.3.4 Kukoma kwa Uongozi

(a) Kwa kiongozi kujiuzulu kwa hiari yake
(b) Kwa kiongozi kuachishwa uongozi au kufukuzwa uanachama
(c) Kwa kiongozi kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya katiba, kanuni au maadili ya Chama.
(d) Kwa kufariki
(e) Ibara hii inahusu pia uongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ya Chama.

6.3.6 Mamlaka za Nidhamu na Uwajibishaji

(a) Kiongozi aliyechaguliwa na Mkutano Mkuu ataweza
kusimamishwa uongozi tu kama ifuatavyo:-
(i) Kiongozi ngazi ya Msingi na Kamati Tendaji ya Tawi
(ii) Kiongozi wa Tawi na Kamati ya Utendaji ya Kata/Wadi
(iii) Kiongozi wa Kata/Wadi na Kamati ya Utendaji ya
Jimbo/Wilaya.
(iv) Kiongozi wa Jimbo/Wilaya na Baraza la Mkoa
(v) Kiongozi wa Mkoa na Kamati Kuu.
(vi) Kiongozi wa Taifa na Baraza Kuu.
Kiongozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi ataweza
kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao kilichomteua.
(c) Bila kuathiri masharti ya vipengele (a) na (b) hapa juu, kiongozi yeyote anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao cha juu ya ngazi yake ya uongozi.
(d) Kiongozi aliyechukuliwa hatua za nidhamu na mamlaka yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya ile ya mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi hiyo utakuwa wa mwisho.
(e) Rufaa yoyote lazima ifanyike katika muda wa siku thelathini tangu tarehe ya kupokea rasmi kwa maandishi maamuzi ya mamlaka iliyotoa adhabu.
(f) Viongozi wa ngazi ya kitaifa waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wanaweza kusimamishwa uongozi endapo theluthi mbili ya wajumbe wa Baraza Kuu watapiga kura ya siri na kutokuwa na imani na kiongozi mhusika. Baraza Kuu litakuwa na wajibu wa kuteua atakayeshika nafasi hiyo kwa muda hadi uamuzi wa mwisho kufanywa na Mkutano Mkuu."

Mwisho wa kunukuu

HITIMISHO



  1. Kuhusu kuwavua au la uachama watuhumiwa , CHADEMA imefuata taratibu zote hapo ju. Zitto na wenzie wasubiri kuitwa na kamati kuu kwa mahojiano ya ana kwa ana. Baada ya hapo watapewa majibu ya maamuzi ya kamati kuu kwa maandishi ndani ya siku 14 toka mahojiano. Wanaweza kukata rufaa kama hawajaridhika na maamuzi
  2. Kuhusu kuvuliwa uongozi chadema walitumia katiba ibara ya 6.3.4 (c). Hili watuhumiwa waliitwa, wakahojiwa na kamati kuu, wote kwa pamoja wakakiri makosa kwa kuhusika na waraka wakaomba kujiuzuru nyazifa zao.
  3. Wanadai taratibu hazikufuatwa kuwapoka vyeo vyao. Ukivunja katiba na miiko ya uongozi hakuna cha taratibu, katiba iko wazi unapoteza wadhifa ulionao mara moja pamoja na kuchuliwa hatua zingine ikwemo kuvuliwa uanachama ambazo taratibu kwenye hili lazima zifuatwe kama ilivyoainishwa hapo juu.


Well said Mkuu!

Pamoja na BLUNDER hiyo Msando, Akumbuke yeye ni kiongozi wa Chama (DIWANI), Je? anaijua dhana ya
"COLLECTIVE RESPONSIBILTY?"

Kama anapenda kuwa Muasi, Angejiuzulu kwanza!
 
Mungu alivyo mwema wasaliti na waasi wote wamejitokeza Peupe kabisa!

Mlivyo vilaza mnadhani kila anayepingana au kuwakosoa ni msaliti. Hizi ndio tabia za kiCCM na mnafanya usaliti bila nyie kujua. Badala ya kujibu mnakimbilia kumuita mtu msaliti. fxxxx.
 
TIMING,

Wakati mchakato wa kuwajibishana ukiwa unaendelea kikanuni na kikatiba busara ni kuwa upotoshaji wowote wenye athari kichama ni lazima ujibiwe na mamlaka husika au wapenzi na wafuasi wa chama na hata wanataaluma ambao hawana chama .

Upotoshaji haupaswi kuendelea na kuharibu taswira ya chama kama CHADEMA ambacho kimebeba dhamaba kubwa ya watanzania katika kusukuma mabadiliko

Chama kikikaa kimya wakati shughuli ya kukichafua na kuzusha kila aina ya uongo basi hakitakua chama serious na hata dhamana waliyopewa hawatakua wameiheshimu

CDM bwana eti na wewe ni kichwa katika chama mwisho wenu utashangaza sana..

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Namshauri Msando jambo moja tu,Rejea gazeti la Nipashe la tarehe november 26,jumanne. Lenye kichwa cha habari RIPOTI YA SIRI ILIYOWAVUA MADARAKA ZITTO,DR.KITILA.Tafadhali kama haina ukweli wowote please take action to redress the status qua of your so called client,ama huna ubavu huo?vinginevyo yaliyoandikwa ni sahihi kabisa!!!.

Hili Gazeti si liliomba msamaha kesho yake au mwenzetu hukusoma hiyo pia?
 
Msando amedhalilisha kitivo cha sheria chuo kikuu cha Dar es Salaam
 
Hizi siasa za character assassination haziwezi kuisaidia CHADEMA na taifa kwa ujumla na kikubwa kabisa hii huwa ni dhambi kubwa sana katika siasa na haiwezi kuisha pindi ikitendwa. Ni sawa na kula nyama ya binadamu.

Kutaka kulazimisha mawazo na mitazamo ya watu wengine lazima iwe kama ya kwako ni dalili ya udikteta kwa kiwango cha juu kabisa.

Ni ukosefu wa fikra pevu na uduni wa mitazamo kuanza kumshambulia wakili kwa vile unamuwakilisha mteja ambaye mnapingana naye kisheria. Toka lini kwenye jamii yanye fikra pevu mjumbe akauwawa.

Kuna baadhi ya watu wangefurahi sana kama Mh. Zitto asingepata wakili katika shauri lake, kitu ambacho kinaenda kinyume na misingi ya demokrasia na usawa wa binadamu kama ulivyoainishwa katika katiba ya nchi kwenye kipengele cha 13(1-3).

Hawa hawa wanaosema Albert Msando anapingana na katiba, kanuni na itifaki za chama kwa kumtetea Mh. Zitto wanasahau kama Mh. Zitto bado ni mwanachama wa CHADEMA na kiongozi wa wananchi achilia mbali haki yake ya msingi kama raia inayolindwa na pia na Presumption of innocence katika macho ya sheria.

Kwa mawazo haya, hamuwezi mkasema mnasimamia misingi ya demokrasia na haki za binadamu wakati maamuzi ya kisheria na kikanuni mnataka/mnapenda yafanyike kwa mtindo wa kangaroo court.

Mbona conflict of interest inaonekana kwa Albert Msando tu wakati kuna viongozi kama Mabere Marando ambaye alikuwa anatetea mafisadi ambao chama kiliwataja na kusema ni maadui wakuu wa ustawi wa nchi lakini hakuna aliyepaza sauti kumkemea ili asiwatetee.

Mbona baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanatumia majukwaa ya kisiasa mikoani kuelezea hatua zinazochukuliwa na chama kuhusiana na sakata hili lakini Mh. Zitto akisema hatua anayochukua mbele ya wananchi kupitia press conference inakuwa ni nong'wa. Kwani mnataka na yeye aanze kufanya ziara za mikoani kwa kupitia njia ya "kuimalisha chama"

Mbona baadhi ya viongozi na wanachama wanaofahamika wa CHADEMA wanaanzisha thread hapa kila wakati kuhusiana na swala hili hakuna kiongozi au Mwanachama anayewanyoshea kidole.

Pambaneni katika hoja zinazohusiana na misuguano ya kikatiba, kikanuni na kiitifaki na siyo katika human character. Nje ya hapo ni dalili ya kushindwa katika hoja.

Of course hawa walioshikishwa akili hawataki kujadili hoja. Kwa uchambuzi huu tayari na wewe wameshakuingiza kwenye kundi la wasaliti. Yote hii ni kwa sababu walikuwa hawana hoja za msingi za kumfukuza Zitto zaidi ya chuki na wivu wa kisiasa ambao umewajaa akina Tundu Lissu na wenzake. Wanaona bora wamshambulie Zitto kulikoni kuwadhibiti CCM na NEC wanaojiandaa kuchakachua kura. Hawa hawana mpango wowote wa kukamata dola zaidi ya kutumiwa na wagombea urais wa CCM katika kufanikisha malengo yao. Hakuna hata kiongozi mmoja wa CHADEMA hawa waliomshikia bango Zitto ambaye sio wakala wa mgombea urais mojawapo wa CCM. Zitto anapigana vita kubwa mno ambayo wengi wetu hatuioni lakini tutaijua tunapoelekea 2015, lakini it will be too late.
 
Kile kikundi cha Wasaliti na Waasi kilichosambaratishwa na Kamati Kuu kilimuandaa Alberto Msando kuwa Mwanasheria Mkuu wa chama endapo wangefanikiwa kumpindua Mbowe.
Kweli wewe kilaza,nimesoma ule waraka hakuna mahali wamesema watampindua mbowe,ila waliandaa mtu ili agombee pindi uchaguzi utakapoitishwa.
 
Huyo Msando sio Tatizo tu bali ni ZIGO ndani ya Chama,halafu ati ni Diwani anayetumia press kuwakilisha hoja zake dhidi ya CC ya Chama.....what a shame...!!!
Hivi hata kama ana hoja anazoamini kuwa ni sahihi kwa nini kukidhalilisha Chama yeye kama Diwani kwenda kwenye press inayolindwa na kuhudumiwa na maCCM..???
Ngoja tumalize hilo la mteja wao ZZK na yeye lake halitachukua zaidi ya nusu saa ndio utaijua Chadema iko vipi.......Siku zao zinahesabika,very shame.

Kama kusema ukweli ni kudhalilisha acha chama kidhalilike. Mmezoea mambo ya kiCCM kufanya mambo kwenye giza. Hizo nyakati zimepita. Na bado mambo yatamwagwa hapa ili watu wajue nani ni msaliti.
 
Well said Mkuu!

Pamoja na BLUNDER hiyo Msando, Akumbuke yeye ni kiongozi wa Chama (DIWANI), Je? anaijua dhana ya
"COLLECTIVE RESPONSIBILTY?"

Kama anapenda kuwa Muasi, Angejiuzulu kwanza!

Mkuu wangu huyo naye ni Masalia na Muasi.Alitarajia kuwa mwanasheria mkuu endapo mapinduzi yangefanikiwa.
 
Kama kusema ukweli ni kudhalilisha acha chama kidhalilike. Mmezoea mambo ya kiCCM kufanya mambo kwenye giza. Hizo nyakati zimepita. Na bado mambo yatamwagwa hapa ili watu wajue nani ni msaliti.

Kwi kwi Kwi....Mfamaji wa Lumumba.

Vijana wa UVCCM jana walikuwa Imara kulinda mkutano Serena.
 
Back
Top Bottom