Watanzania kwenye ujinga wao, hii nchi bado sana maana watu asilimia kubwa hawana elimu kichwani na hawataki kijushughulisha, wanaamini kila wanachokiona mitandaoni, hizi story za 666 na mambo supernatural hua ni interesting ndio kwa kua ni fairy tales tu, binadamu kawaida tunapenda kusikia vitu ambavyo ni impossible vikitokea. Wengi mtaungana na mshanajr na group lake basi tu kwa kua wengi ndio story mnapenda kuzisikia.
Tafadhali msiturudishe nyuma, haya madudu yamewajaa sana watanzania mkishika kitu mnakishika ovyo, dini mnashika ovyo, haya nayo mnashika ovyo, unajua hii kazi nimeifanya sana miaka ya nyuma, enzi hizo tunatengeneza articles online za haya maujinga ya 666 tunadesign na picha tunajarivu kurelate na kila kitu na zilikua zinalipa sana matangazo sababu watu wengi wanapenda kusoma haya madudu, ila hakuna ukweli wowote ni story tulikua tunatunga tu ili kupiga hela, hilo swala bado tu bloggers wanaendelea kuandika, na walivo wajanja watatafuta vitu kibao kujarivu kuiframe evidence yao vizuri ili kuifanya ionekane very real, Sasa wajinga mnakuja humu na kuanza kusema mmefunguliwa na bwana kuuona ukweli, huko kufunguliwa ni kupewa internet na kusearch articles zilizotungwa na wapiga hela, basi ombeni mfungwe maana mmefunfuliwa pabaya, ndoo maana nawaambia mnashika mambo kijinga sana. Internet ina uongo zaidi ya 70%, huo wote umetungwa ili mfungue muangalie aliyetunga anaingiza hela ya matangazo period.
Sasa endeleeni kuamini madudu washa yenu mzungu anazidi kupiga hatua mbele, hili taifa kuja kufikia level nzuri sio leo, waamini madudu washa wapo zaidi ya 80%..